Jaguar
JF-Expert Member
- Mar 6, 2011
- 3,437
- 1,025
Mchungaji akawaambia waumini wa-kiume kwamba kila mmoja atoe sadaka kubwa kwa kadiri ya uzuri wa sura ya mkewe.Watu wakatoa viwango tofauti tofauti,wengine laki mbili,laki tano,laki nane na hata wengine walitoa milioni na zaidi isipokuwa bwana mmoja tu.Huyu jamaa alijisachi kwa muda mrefu then akatoa sh.100 akaweka kwenye kapu la sadaka.Mchungaji alimuona,akaanza kumhoji kwa hasira;"we kwanini umetoa sh.100 tu?".Jamaa akajibu;nimetoa hii sh.100 kwa sababu sina chenji,vinginevyo ningetoa sh.50,ndugu mchungaji,ukimwona mke wangu,hata hii sh.100 utanirudishia chenji!