Habarini wana MMU,
Kuna usemi usemao uzuri sio urembo au mwonekano wa nje ila ni tabia,usemi huu una maana yake na kuna ukweli ndani yake,lakini swali linakuja,unawezaje kuanza kumchunguza mtu tabia pasipo kuvutiwa naye kwanza? yaani kupata sababu inayoweza kukufanya ukaanza kumchunguza mtu tabia yake?
Kwa binafsi yangu nafikiri mwonekano huwa wa kwanza,na hicho ndicho humfanya mtu akaanza kuchunguza tabia ya mtu fulani.
Wengine huvutiwa na nywele,kifua,sauti,kucha,pua,rangi,macho,lipsi,tembea au jinsi tu mtu huyo alivomchunguza tabia moja kwa moja bila kuvutiwa na kitu chochote kutoka kwake.
Wale ambao bado mnatafuta wenzi wenu wa maisha kwa sasa unaweza kuanza tu ilimradi kila mmoja ana kipimo cha kitu kinachomfurahisha binafsi kuwa anafaa kuwa naye na ikiwa hafai hata licha ya mwonekano mzuri ambao umemvutia mtu huyo anaamua hawezi kuishi naye. Hapo ndo ule usemi uzuri sio mwonekano wa nje bali ni tabia unatimia, lakini ni baada ya kuvutiwa na mtu fulani kwa nje kisha kuona kuwa kimwonekano anavutia lakini kitabia si mzuri.
Wengine mnasemaje juu ya hili?
kuna yeyote aliyewahi kuanza kumchunguza mtu wa jinisa tofauti ambaye leo hii ni mume/mke wake tabia yake ilhali hajavutiwa na kitu chochote kutoka kwa mtu huyo?
Na kwa wale ambao hawajafunga ndoa bado je mchumba uliyenaye kwa sasa,ulianza kuhunguza tabia ya mtu wa jinsia tofauti bila kuvutiwa na chochote kutoka kwake?
Hapa naongelea ule uhusiano unaopelekea kwenye ndoa na sio uboyfriend na ugilfriend karibuni wana mmu.