Uzuri sio urembo ni tabia

Uzuri sio urembo ni tabia

Blue G

JF-Expert Member
Joined
Jun 20, 2012
Posts
5,339
Reaction score
3,674

Habarini wana MMU,

Kuna usemi usemao uzuri sio urembo au mwonekano wa nje ila ni tabia,usemi huu una maana yake na kuna ukweli ndani yake,lakini swali linakuja,unawezaje kuanza kumchunguza mtu tabia pasipo kuvutiwa naye kwanza? yaani kupata sababu inayoweza kukufanya ukaanza kumchunguza mtu tabia yake?

Kwa binafsi yangu nafikiri mwonekano huwa wa kwanza,na hicho ndicho humfanya mtu akaanza kuchunguza tabia ya mtu fulani.
Wengine huvutiwa na nywele,kifua,sauti,kucha,pua,rangi,macho,lipsi,tembea au jinsi tu mtu huyo alivomchunguza tabia moja kwa moja bila kuvutiwa na kitu chochote kutoka kwake.

Wale ambao bado mnatafuta wenzi wenu wa maisha kwa sasa unaweza kuanza tu ilimradi kila mmoja ana kipimo cha kitu kinachomfurahisha binafsi kuwa anafaa kuwa naye na ikiwa hafai hata licha ya mwonekano mzuri ambao umemvutia mtu huyo anaamua hawezi kuishi naye. Hapo ndo ule usemi uzuri sio mwonekano wa nje bali ni tabia unatimia, lakini ni baada ya kuvutiwa na mtu fulani kwa nje kisha kuona kuwa kimwonekano anavutia lakini kitabia si mzuri.

Wengine mnasemaje juu ya hili?

kuna yeyote aliyewahi kuanza kumchunguza mtu wa jinisa tofauti ambaye leo hii ni mume/mke wake tabia yake ilhali hajavutiwa na kitu chochote kutoka kwa mtu huyo?

Na kwa wale ambao hawajafunga ndoa bado je mchumba uliyenaye kwa sasa,ulianza kuhunguza tabia ya mtu wa jinsia tofauti bila kuvutiwa na chochote kutoka kwake?

Hapa naongelea ule uhusiano unaopelekea kwenye ndoa na sio uboyfriend na ugilfriend karibuni wana mmu.

Uzuri na tabia huwezi kuvitenganisha ni kama kidole na kucha sana sana inategemea na mtu kipi anakipa uzito kati ya hivyo.
 
^^
Inawezekana kabisa! Jamii nyingi za zamani za Kiafrika walifanya jambo hilo kwa niaba ya vijana wao, na ndoa zilidumu.
Tofauti ya sasa na kale ni kuwa, kuna jambo fulani ambalo linakubalika katika ulimwengu wa roho lilifanyika ila sasa halifanyiki..yaani kuanza mahusiano na mtu mmoja na kuishi nae huyo huyo!
Ila uzao wa sasa, unakutana na mtu ana uzoefu wa kusifika zaidi ya wapenzi kumi, basi upatanisho unabaki mvuto tu

uko sawa kaisa mkuu,lakini wewe binafsi unaweza kutuambia ni nini unakipa uzito kati ya hivyo viwili?mke uliyenaye kwa sasa ikiwa umeoa ilikuwaje kuwaje mpaka ukaamua awe mwenzi wako?
 
Macho yangu yameona mabinti wengi wazuri, wenye mivuto, maridadi, ni kama watakatifu walioshinda tuzo ya sayari ya Venus lakini tabia zao hata shetani anazivulia kofia
^^
 
katika kutafuta mwanamke mi ninaangalia zaid ananivutiaje,kwa sababu ukimchukua tu sijui unaingalia tabia inayorekebishika wakati wowote baadae unakutana na visura vya ajabu unaanza kutafuta mchepuko,na unakuta na tabia ulioingalia mwanzon na kubadilika ilishabadilika.mi naangalia uzuri bwana mengine hata kwa maombi yanabadilika,,
 
nimekupata vilivyo mkuu,lakini nina maswali machache kwako,hapo kwenye red mkuu unafikiri ndoa zilidumu kwa ajili tu ya kuridhishwa na tabia za wenzi wao?au kwa kuwa tu kulikuwa na maadili ya hali ya juu hivi kwamba watoto wasingeweza hata kusema neno lolote la kuwakatalia wazazi wao?unaamini ndoa hizo zilidumu kwa ajili ya upendo uliokuwepo baina ya waliiooana au ni kwa kuwa watoto walikuwa tayari kufanya yote kwa ajili ya wazazi wao na maadili ya hali ya juu yaliyokuwepo kwa wakati huo?

inaonyesha kwa upande wako uzuri ndio jambo la maana zaidi,si vibaya lakini nafikiri yote yanapaswa kuchukuliwa kwa uzito kwani kuna msemo usemao sikio la kufa halisikii dawa na pia tabia haina dawa,hasa kuzingatia point yako kuhusu tabia hapo kwenye red unasemaje pia kuhusu misemo hiyo miwili?je ni kweli mara zote inawezekana kubadilisha au kurekebisha tabia ya mtu?au umeona wangapi waliowahi kufanikisha kumrekebisha mtu tabia yake?

katika kutafuta mwanamke mi ninaangalia zaid ananivutiaje,kwa sababu ukimchukua tu sijui unaingalia tabia inayorekebishika wakati wowote baadae unakutana na visura vya ajabu unaanza kutafuta mchepuko,na unakuta na tabia ulioingalia mwanzon na kubadilika ilishabadilika.mi naangalia uzuri bwana mengine hata kwa maombi yanabadilika,,
 
uko sawa kaisa mkuu,lakini wewe binafsi unaweza kutuambia ni nini unakipa uzito kati ya hivyo viwili?mke uliyenaye kwa sasa ikiwa umeoa ilikuwaje kuwaje mpaka ukaamua awe mwenzi wako?

Mkuu mimi nilitumia kanuni ya neno la Mungu kuwa mwanamke mwenye busara/hekima/tabia njema mtu hupewa na Bwana,so cha kwanza ni tabia,nilifanya maombi ya kuatamamia nikiwa nimeambatanisha utashi wangu kwa Mungu...maana imenenwa haja zenu na zijulikane na Bwana,niliomba sana Mungu pamoja na tabia nilihitaji mwanamke mzuri kwa kweli.....maana imenenwa mtakula mema ya nchi hahaha.

Waswahili husema Mungu si ng`wana ong`wa kulwa nilikutana na huyo mke wangu ana sifa zaidi ya nilivyomuomba Mungu japo sikuwa namfahamu kabisa.Hivyo watu wasiogope kumuomba Mungu wakihofu kuwa watapewa wasiowataka.".........ikiwa ninyi mlio waovu mnajua kuwapa watoto wenu vilivyo vema si zaidi sana baba yenu aliye mbinguni..........."

nimekupata vilivyo mkuu,lakini nina maswali machache kwako,hapo kwenye red mkuu unafikiri ndoa zilidumu kwa ajili tu ya kuridhishwa na tabia za wenzi wao?au kwa kuwa tu kulikuwa na maadili ya hali ya juu hivi kwamba watoto wasingeweza hata kusema neno lolote la kuwakatalia wazazi wao?unaamini ndoa hizo zilidumu kwa ajili ya upendo uliokuwepo baina ya waliiooana au ni kwa kuwa watoto walikuwa tayari kufanya yote kwa ajili ya wazazi wao na maadili ya hali ya juu yaliyokuwepo kwa wakati huo?

^^
Ukimuuliza binti yeyote, ni taswira ya ipi ya mwanaume hataisahau, atasema ni yule aliyemtoa BIKRA,, hapa ndipo kuna maagano ya kiroho yaliyofanya ndoa nyingi zidumu. Pia upo ukweli usiosemwa, mwanaume pia humkumbuka mwanamke wake wa kwanza!
Kama mapatano hayo yalidumu, pia jamii ikaongeza sheria kali za kulinda ndoa basi mivuto lilikuwa jambo la mwisho kutazamwa, ila sasa ni la kwanza huku tabia ikiwa ya mwisho
^^
 
BmUE9Y0IMAA31SW.jpg
 
^^
Macho yangu yameona mabinti wengi wazuri, wenye mivuto, maridadi, ni kama watakatifu walioshinda tuzo ya sayari ya Venus lakini tabia zao hata shetani anazivulia kofia
^^

kweli mkuu hata mimi tabia naipa uzito zaidi mwenye tabia mbovu anaweza kuku fedhehesha sana hata ukachukia wanawake wote........hata hivyo si wazuri wote wana tabia mbaya......mwanamke amchaye Bwana ndiyo atakayesifiwa"

katika kutafuta mwanamke mi ninaangalia zaid ananivutiaje,kwa sababu ukimchukua tu sijui unaingalia tabia inayorekebishika wakati wowote baadae unakutana na visura vya ajabu unaanza kutafuta mchepuko,na unakuta na tabia ulioingalia mwanzon na kubadilika ilishabadilika.mi naangalia uzuri bwana mengine hata kwa maombi yanabadilika,,

Mkuu kubadilisha tabia ya mtu si jambo rahisi angalia mastar wangapi wenye sura/maumbo mazuri wameachika,unafikiri nini kiliwafanya waachike?
 
mmmmh tabia na uzuri ni vitu viwili tofauti

kama unaona uzuri ni muhimu basi kila mwanamke angeolewa ...tofautisha kutamani na kupenda

uzuri wake utakusaidia nini katika kulea familia???tunajidangnya vijana wengi wa siku hizi kutokan na kukua kwa sayansi na kuiga na ndo mana ndoa hazidumu...wazee waliangalia tabia zaid yauzuri ndo mana ndoa zimedumu
 
asante mkuu kwa kushare expirience yako pamoja na sisi,na hongera kwa kupata mke mwema,na nafikiri mwonekano wa mtu una nafasi sana kabla hujaamua kumchunguza tabia,kwani licha ya kumwomba Mungu akupe mwenye tabia njema,je ulipomwona tu ukaanza kumchunguza tabia yake tu bila chochocte kukuvutia kutoka kwake?
Mkuu mimi nilitumia kanuni ya neno la Mungu kuwa mwanamke mwenye busara/hekima/tabia njema mtu hupewa na Bwana,so cha kwanza ni tabia,nilifanya maombi ya kuatamamia nikiwa nimeambatanisha utashi wangu kwa Mungu...maana imenenwa haja zenu na zijulikane na Bwana,niliomba sana Mungu pamoja na tabia nilihitaji mwanamke mzuri kwa kweli.....maana imenenwa mtakula mema ya nchi hahaha.

Waswahili husema Mungu si ng`wana ong`wa kulwa nilikutana na huyo mke wangu ana sifa zaidi ya nilivyomuomba Mungu japo sikuwa namfahamu kabisa.Hivyo watu wasiogope kumuomba Mungu wakihofu kuwa watapewa wasiowataka.".........ikiwa ninyi mlio waovu mnajua kuwapa watoto wenu vilivyo vema si zaidi sana baba yenu aliye mbinguni..........."

ukiipenda tabia yake utamwona mzuri tu hata aweje....sasa sijui ukimpenda sura yake kama lazima utaipenda tabia yake
 
naunga mkono juu ya agano mkuu Himidini lakini ninachojaribu kuwaza na kufikiria,si ule mtazamo walio nao vijana wengi wa leo,wa kuufanya uzuri kuwa ndo kila kitu,mkuu unawezaje kuanza tu kumchunguza mtu bila kupenda chochote juu yake hata iwe ni kucheka kwake,kutembea kwake au chochote?inawezekanaje?hata hilo agano nafikiri huja baada ya jinsia hizi mbili kuwa zimevutiana .
^^
Ukimuuliza binti yeyote, ni taswira ya ipi ya mwanaume hataisahau, atasema ni yule aliyemtoa BIKRA,, hapa ndipo kuna maagano ya kiroho yaliyofanya ndoa nyingi zidumu. Pia upo ukweli usiosemwa, mwanaume pia humkumbuka mwanamke wake wa kwanza!
Kama mapatano hayo yalidumu, pia jamii ikaongeza sheria kali za kulinda ndoa basi mivuto lilikuwa jambo la mwisho kutazamwa, ila sasa ni la kwanza huku tabia ikiwa ya mwisho
^^
 
Last edited by a moderator:
^^
Macho yangu yameona mabinti wengi wazuri, wenye mivuto, maridadi, ni kama watakatifu walioshinda tuzo ya sayari ya Venus lakini tabia zao hata shetani anazivulia kofia
^^

waambie huo uzuri watautumia kwa kipi???Tabia ndo kila kitu hekima,upendo,kumcha MUNGU,mwanamke anayejitambua,upole n.k....
watu wanataman then wanasema wamependa na ndo mana mahusiano na ndoa hazidumu..
mke mwema atoka kwa MUNGU...
 
Tabia mwisho chalinze huku mjini ni urembo tu

mwekundu baba si vibaya kutamani mume/mke wako awe na mwonekano mzuri,lakini kwa mke/mme uzuri au urembo utakusaidia nini katika kufanya familia bora na yenye kudumu?unweza kutuelezea jinsi unavyofikiria wewe uzuri una nafasi gani katika kujenga familia nzuri yenye umoja upendo na amani?au hapa wewe unaongelea ugf na ubf?
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom