kukukakara
JF-Expert Member
- Jul 31, 2012
- 496
- 164
Mchambuzi,Tutamjadili Zitto Kabwe kugombea urais wa Tanzania atakapofikisha umri ambao kikatiba unamruhusu, kwa sasa katiba haimruhusu Zitto Kabwe kugombea urais kwa vile yuko chini ya umri wa miaka 40. Hata 2015 kama kifungu cha katiba kuhusu umri wa kugombea urais Tanzania usipofanyiwa marekebisho bado hatakuwa na nafasi hiyo.
Bora Zitto na wanamwunga mkono wangehangaikia Katiba mpya kufanyiwa marekebisha badala ya kuhangaikia kitu ambacho kikatiba ni ukiukwaji.
Hiyo ni hoja nzito ambayo inagusa Katiba ya nchi kuhusu umri wa mgombea Urais
Jingine zaidi ya hapo zitto amekosa adabu mbele chama kwa kujitangazia uamuzi mkubwa bila kuhusisha chama labda kama anamaanisha kuwa rais hata kama sio kupitia cdm, kitu ambacho wengi tunaamini ndio chanzo cha'jeuri yake.
Inakuwaje afanye unilateral declaration wakati chama kipo na viongozi wenzake wapo? Tayari ameshaonyesha udhaifu mkubwa sana kuweza kuwa kiongozi wa nchi, hana ushirikiano na viongozi wenzake, atatawwala vipi bila wenziwe ambaye hakujali hata kutumia vikao vya ndani kujadili kama ni muda mwafaka kutoa tamko na pengine kwa staili gani kwa manufaa ya ushindi wa chama na taifa.
Wenye critical thinking wanahitimisha kuwa Zitto kalewa sifa zifuatazo: mosi, utetezi wake wa raslimali bungeni ambazo kawida sio'effort zake kama yeye bali ni chama, pili; kuchukulia advantage ya propanganda za kuwa cdm ni chama cha wakristo na ukanda kwa hiyo yeye kama muislamu ana support ya waislamu wote, tatu yeye as under 40 vijana wooootte na hasa wanamziki wa kibongo ni maswahiba ambao watamuunga mkono, mwisho ni uswahiba kwenye watawala. Hizi ni ndizo pillar za zzk kuvimba kichwa hadi kudharau chama. Je tuzipime ni misingi hii ambayo ndio mtaji wake wa kuupta urais ni wa maslahi kwa taifa na hasa wanyonge? Au ushabiki wa kuharibu na kugawanya tu kura kwa faida ya wengine. Cdm ingependa kupata rais wa wananchi sio wa mtandao fulani ndio maana ya harakati za m4c kwanza!!
Nashauri ZZK aache mambo hayo atangaze kufuta nia na awaambie wafuasi aliyojitengenezea warudi kujenga chama. Yeye atapata uwaziri kama kijana atatumia miaka kadhaa kujenga uzoefu wa uongozi na hatimae miaka ijayo inshallah mwenyeezi mungu atamshushia ndoto yake hyio. Demokrasia isiwe ticketi ya kuifanya taasisi ya Urais ikawa kama cm ya mchina kila mtu anauwezo wa kuinunua!