Uzi maalumu wa kupongeza Watu walioinua Wengine

Uzi maalumu wa kupongeza Watu walioinua Wengine

Mstahiki Mea

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2018
Posts
6,519
Reaction score
12,448
Ni jambo bora sana kuwapa maua yao watu waliowainua wengine iwe nikwakujua au kutokujua. Wale waliotazamwa kama njia kwa wengine, wale walio washika wwngine mkono wakafanikiwa .

Kazi kwenu wakipita waone umuhimu wao naanza na wachache

1. Mkubwa Fela
2. Naseeb Abdul Diamond
3. Ruge Mutahaba
4. Millard Ayo

Idadi nikubwa sana na nadhani wanafahamika wapeni maua yao.
 
swed mungu akubariki.
kumpa mtu connection ya kazi ambaye sio ndugu yako inataka moyo
 
Siku moja nilialikwa na mshikaji wangu wa damu alikuwa na jubilee ya miaka 20 ya ndoa ni shukran kwa Mungu, sasa katika vitu vilinifanya nikatafakar jamaa wadogo zake na ndugu walimshukuru sana kwa jins alivyosimama nao mpaka wote wametoka. Nikakumbuka mi ni wa la saba lakin nimehangaika na wadogo zangunwore saba na wote ni wasomi wazur wenye kaz zao tena zenye kipato kizur lakin hakuna hata aliyewah kutoka kusema bro nakushukuru. Nimelala minadan nimejibana nimepambqna miaka hiyo. Ila leo hata mzee. Life sometimes ukilifikiria ni ushenz tu. Kikubwa ni uhai hakuna jambo bora kama kushukuru. Hasa mtu ambae bila yeye usingetoka hilo eneo. Nina mshikaji mmoja mmisri nilimsaidia tukiwa hongkong miaka ya 2002 huyu jamaa aliwah kuja mpaka kilimanjaro na mkewe kunishukuru na kujua kwetu.
 
Kuna jamaa mmoja ni mwenzetu humu aliwahi kuleta uzi wake miaka kama mitano au sita iliyopita, kubwa alikuwa akielezea mapito aliyowahi kupita akiwa kama mtoto wa mitaani jijini Mwanza mpaka kufanikiwa kumaliza masomo kwa ngazi ya Shahada. Wengi tuliguswa na maisha yake ila kuna wakubwa humu ninaamini walimshika mkono na huko aliko bila shaka alishayatengeneza maisha yake vizuri.

Kubwa nililojifunza kutoka kwa jamaa na huwa ninamshukuru kila siku ni kuwa na maisha huru yaliyojawa nuru na furaha, mustakabali wa maisha yako utakuwa mtamu tu! Acha kulalamika ama kunung'unikia wengine kisa kutokusaidiwa na wao
 
Back
Top Bottom