Uzi maalumu kwa ajili nyimbo za injili za zamani(Old school Gospel songs) za Tanzania!

Aisee kuna wimbo unaimbwaga kipindi cha majilio...
Unaimbwa " nii yohana alia nyikani
Tengee.. tengeneza njia ya bwana apitee
Bwana apite apitee
Mungu apite apitee.. tengeneza njia ya bwanaa apiteee"
Mwenye nao naomba autupie

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi natafuta wimbo wenye maneno..ndugu zangu mnaishi dunia yenye dhiki, jipeni moyo.....kibwagizo "jenga imani yako, kwenye mwamba imaraaa, mwamba wetu ni Yesu..Alfa na Omega"...sijui uliimbwa na kwaya gani zamani kweli
 
kama kuna mtu ana toleo la hii Kwaya lile la zamani. Naona sasa hivi wamebadlisha wameondoa vionjo vuake asilia
 

Attachments

  • kazaliwa emmanuel.mp4
    9.3 MB · Views: 123
Huu wimbo ulinipaga moyo sana kama sijakosea miaka hiyo 1998 nikiwa sekondari nimetoka kupokea ugali maharage yenye wadudu
Dah basi kuna mtoto mmoja wa tajiri alifanikiwa kumiliki radio
Ukawa unapugwa radioni


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanazidi kumchochea jamaa wa korea ya kaskazini hawa uficheni huu wimbo wasije fanyia majaribio huku

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanazidi kumchochea jamaa wa korea ya kaskazini hawa uficheni huu wimbo wasije fanyia majaribio huku

Sent using Jamii Forums mobile app

Waimbaji huwa wanaujumbe wa kila aina ''Silaha za Maangamizi'', ''Nuclear'' - Kwaya Mabalozi wa Yesu au ''Msiabudu America''- Faustin S. Munishi n.k ni kama vile wanauangalia ulimwengu na kufikiri scenario zilizopo na zinazokuja kufuata na Maandiko juu ya siku za mwisho kama zilivyo ktk imani.
 
Kuna wimbo nausaka ila siukumbuki jina na nimejitahidi kupitia huu uzi sijaupata naomba kama kuna mtu anaufahamu anitajie au aniwekee hapa nitashukuru sana..

Kwenye huo wimbo kuna maneno kama haya nadhani kwenye kiitikio hutamkwa ''Yesu aliteswaa msalabani watu wote tuwe huru,huru kweli kweli*2"....halafu ''haleluya aah haleluya aaah*4''
 
Ni wa upendo kwaya kijitonyama
 
Hao ni AIC Kambarage, enzi zile kesho nitakuwekea hapa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…