UZI MAALUM WA WATANI

Uta Uta

JF-Expert Member
Feb 2, 2016
3,687
8,600
Habari wanajamvi?
Tanzania imebahatika kuwa na makabila mengi sana zaidi ya 100. Mababu zetu huko zamani walianzisha utani kati ya kabila moja na lingine ili kudumisha mahusiano mazuri pindi uwapo nje ya mipaka ya eneo lenu, maana zamani kulikuwa na koo au kabila ndio iliyoyoamua mipaka ya eneo moja au lingine. Baadhi ya utani uliokuwa ukifanyika ni pamoja na watani wakifika katika kijiji chenu aidha katika misiba au shughuli nyingine basi huchinja mnyama yeyote anaefugwa eneo hilo kama kuku, mbuzi, kondoo au ng'ombe. Na ikitokea mnyama aliechinjwa si wa watani basi wale watani wenyeji huwajibika kumlipa yule aliechinjiwa mnyama wake. Pia baadhi ya watani huwa wanazuia mwili wa marehemu usizikwe mpaka wapate fidia, wengine huchukua wanawake na kuondoka nao kwao kwend kuwafanya wake zao bila hata kuozeshwa. Huo ni baadhi tu ya utani. Baadhi ya makabila watani
Wngoni watani zao ni wangindo, waluguru, wamatumbi, wamakonde nk
Wasukuma watani zao ni wandengereko, wamasai nk
Waluguru watani zao ni wanyakyusa, wamakonde, wayao, wamatumbi, wazaramo nk
Wanyamwezi watani zao ni wangoni, wandengerko, waluguru nk
Hayo ni baadhi tu ya makabila kwa uchache na watani zao. Je vijana wa leo wanaujua huu utani wa jadi au wanaujua wa simba na yanga na man u na chelsea? Hivi wachaga nao wana watani? Hebu tiririka hapa watani zako ni kabila gani na utani gani hasa huwa unafanyika
 
Mtani wa man u ni arsenal...hao wajomba hawaivii kabisa hata huko vibanda umiza

Wachaga vs waparee
 
wapare mupooo ati nasikia mnakulaga ugali kwa picha ya samaki.
au samaki mmoja atapikiwa mchuzi hadi aishe, ani ni hivi akipikwa sasa hivi baba anamtoa anamweka pembeni anakuja kupikwa tena na tena .,
hii taabia mshaachaga ?????
 
Back
Top Bottom