Uzazi wa mpango: Nafikiri ni wakati muafaka sasa kwa Serikali kutupangia idadi ya watoto

kwenda21

JF-Expert Member
Mar 11, 2014
3,422
3,393
Nafikiri ni wakati muafaka sasa kwa serikali kutupangia idadi ya watoto na siyo kuzaana zaana tu, tukiendelea na tabia hii, nchi itashishwa kujiendeleza na kufanya kazi ya kujenga mashule na mazahanati, lazima kuwe na limit, ili pesa inayopatikana ikafanye maendeleo mengine.
 
Vietnam wasingekua na idadi kubwa ya watu,na uduni wao wa silaha uko maporini

Ile Vita yao na USA wangeshafutika uso wa dunia, Ila marekani alichokutana nacho uwanja wa vita hatosahau maishani.

Unapiga unadhan umemaliza,
wanakuja wengi zaidi ya wale ulioua,
Ilibidi ile Vita aachane nayo maana inazidi kumtia hasara na watu hawaishi Wala kurudi nyuma japo walikua na silaha duni

Sent using JamiiForums mobile app
 
Acha ushamba
Watu Ni mtaji mkuu
Watu Ni nguvu Kazi ya taifa
Watu Ni jeshi la taifa
Watu Ni soko la ndani
Hakuna mtu atakubabaisha pa kuuza bidhaa yako, utauza soko la ndani maisha yataenda.
We mwenyewe ukizaa watoto wengi kuwasomesha na kuwatibu unashindwa,watoto watashindwa kupata malezi bora
 
Acha ushamba
Watu Ni mtaji mkuu
Watu Ni nguvu Kazi ya taifa
Watu Ni jeshi la taifa
Watu Ni soko la ndani
Hakuna mtu atakubabaisha pa kuuza bidhaa yako, utauza soko la ndani maisha yataenda.

Nchi kama tz inahitaji mipango thabiti hasa inshu za population control mana hii nchi wajinga wengi na wanazidi kuzaa wajinga tupu,china haikifika hapo ilipofika bila kuweka mikakati maalaumu juu ya population ya watu wake.
 
We mwenyewe ukizaa watoto wengi kuwasomesha na kuwatibu unashindwa,watoto watashindwa kupata malezi bora
Jukumu la kusomesha
Na kuwapa malezi Bora watoto sio lako,
Ni jukumu la serikali yako unayoilipa Kodi

Nchi zinazojali raia wake,
Mtoto Ni tunu na hazina ya taifa
Zinasomesha,kutibu na kutoa huduma mbalimbali za kiljamii kwa watoto bure.

Jpm alishaanza hizo harakati kwa kutoa elimu bure na kuhamasisha Watu wazae sana.

Zaman tulihisi elilmu bure Kama ni ndoto,
Sahv tumegundua kumbe inawezekana,
Ukifuatilila Hata Afya kwa watoto chini ya miaka 5 Sasa Ni bure vituo vyote vya serikali

Kumbe kila jambo linawezekana tukiacha woga wa kijinga jinga.

Sent using JamiiForums mobile app
 
Athar ya watu wachache Kwny taifa,
Imewakuta wajapan kipind Cha world war

Yale mabomu 2 ya Hiroshima na Nagasaki
Yaliwakata Nguvu wajapan kuendelea na Vita,

Maana on the single bomb strike,
walikufa maelfu ya wajapan, wakajua huyu USA hatanii na akipiga mengine mawili taifa letu zima linafutika ktk uso wa dunia.

Bora kunyoosha mikono juu.
Na Kweli walinyoosha mikono juu
Mpk leo Japan kaufyata mkia na Hana Tena Nguvu Wala influence yoyote ile kijeshi Asia Wala dunian kokote

Sent using JamiiForums mobile app
 
We mwenyewe ukizaa watoto wengi kuwasomesha na kuwatibu unashindwa,watoto watashindwa kupata malezi bora
Mvulana ni Mvulana tu, mara ngapi Ke huzalishwa Mtoto mmoja tu na Mvulana na kutelekezwa akiwa single mother?

Acha Watu wafyatue Watoto kadri walivyobarikiwa.

Pia maisha hayana kanuni, huoni kuna familia zenye Watoto wawili tu na familia nyingine zina Watoto zaidi ya wanne lakini kiuchumi zinaweza kwenda sambamba au wakati mwingine familia zenye Watoto zaidi ya wanne kuwa juu zaidi kiuchumi?

Ninyi ndiyo mnaoeneza upuuzi wa "Kataa ndoa" ilihali unanuka uzinzi mwili mtupu sababu kila kona ya mtaa una demu.

Maisha hayana kanuni wala kukariri, acha uwoga wa maisha Kijana sababu hakuna kizuri kinachopatikana bila jasho, Me tukazeni tuache kuwa walaini laini tukilia lia kila wakati kama Ke.
 
Back
Top Bottom