Uzalo Special Thread

Its Pancho

JF-Expert Member
Sep 21, 2018
14,176
22,577
Wakuu kwa wale wapenzi wa Isidingo tuliipenda sana lakini hakuna kisicho na mwisho. Hivyo kwa sisi wafuatiliaji wa ITV wameamua kutuletea tamthilia mpya ya Uzalo, japo sina hakika kama ni mpya kabisa, ni ya muda kidogo. Kama mwaka juzi

Hivyo uzi huu ni wa kupeana sasisho kwa wale watakaokosa na ikiwezekana kuweka mkeka wote kiufupisho kidogo hapa. Imeanza ina kama mwezi, uzuri waigizaji wa Isidingo wapo humu humu. Kuna Lungi wa Isidingo yupo humu kacheza kama Sindi.

Kuna yule aliyekuwa mzee wake Sechaba kacheza kama Inspector Dhlomo.

Ni balaa hii!
eb65b8d55eb9456994a89386adf029aa.png

58a7b6453a26d9ab5308f272620aa72a.png
c967ee4d9446309b68a7c43e7ae94327.png

c3e78006221d652d441887fc914d2948.png
 
Kuwa na mama mchungaji kama yule ni kisanga dakika mbili anakuzingua

Ayanda nae hataki kuimba kwa mzee wake kanisani
Sema dingi ni kama vile anaheshimu ndoto za mwanae[Ayanda] za kuwa DJ ila mke wake ndio anamzingua.

Mastermind naye kamchana sbu kwamba wanajua yeye ni snitch anashilikiana na police.
 
Sema dingi ni kama vile anaheshimu ndoto za mwanae[Ayanda] za kuwa DJ ila mke wake ndio anamzingua.

Mastermind naye kamchana sbu kwamba wanajua yeye ni snitch anashilikiana na police.
Dingi yuko peace toka mwanzo alishasena wajarbu kumsapoti ayanda kimbembe kipo kwa mama sasa utaskia "You selling alcohol at tavern?"
😀😀😀
 
Sema dingi ni kama vile anaheshimu ndoto za mwanae[Ayanda] za kuwa DJ ila mke wake ndio anamzingua.

Mastermind naye kamchana sbu kwamba wanajua yeye ni snitch anashilikiana na police.
Mastermind kashaharibu aseeh sijui leo atamwambia nini bosi wake
 
UZALO.. Friday. 11 Jun.

Xulu akiwa na mkewe wanataniana kidogo kuhusu mambo yao jikoni, mkewe anagusia swala la xulu kwenda wote kanisani familia nzima kwa nia ya kumuaga kijana wao mxolisi anayerudi joburg kufanya kazi..

Pastor mdleshe na mkewe pamoja na mtoto wao nkosinathi, wakijiandaa kwenda kanisani huku wakimsubiri ayanda aliyekwenda mazoezini.

Njiani ayanda akiwa anarudi kutoka mazoezini huku akikimbia anamparamia sindi, kisha anamuomba samahani na kuendelea na Safari,
Sindi anakutana na kijana mmoja na kumuulizia ni wapi kwa pastor mdleshe ili akatoe ukweli kuhusu watoto wawili ayanda na mxolisi kuwa walibadilishwa na na mama yake alipokuwa nesi miaka ya 90, hivyo ayanda ni mtoto wa xulu na si pastor mdleshe na mxolisi ni wa pastor na sio xulu.

Mastermind baada ya kulikoroga anakutana na mfanyakazi mwenzie wa gereji kisha anampanga kuwa watamfute sbu na kumuua kwani ni snitch anashirikiana na polisi, kutoa taarifa zao, lakini anamuonya jamaa huyo kuwa asimwambie mtu

Sindi anafika nyumbani kwa pastor na kukaa sana getini hadi anapopita mamlambo anayesali kanisani kwa pastor na kumwambia sindi kuwa pastor na family yake wamekwisha kwenda kanisani hivyo kama ana shida naye waende kanisani huko huko atampata, wanaondoka.

Kanisani kwaya inaimba kabla ya ibada sindi anaelekezwa kwa pastor, lakini pastor yuko bize na ibada inaanza,anaambiwa amfuate pastor baada ya huduma kisha pastor anakuja kutoa neno kidogo

Sbu anaonekana akila unga wake (cocaine)

Inspector dhlomo anampigia sbu simu na kumwambia achague lililo jema either waendelee kufanya kazi au arudi jela

halafu anaacha kwaya iimbe tena kisha anaanza kutoa neno,
Kisha anaomba ushuhuda au kwa wenye kutubu, hapo anasimama mke wa xulu na kwenda kwa mbwembwe sana na kuanza kusifia pesa zao familia yao na kuanza kumsifia kijana wake mxolisi kuwa ana akili hajawahi kuwa hata wa tano ila anakuwaga wa kwanza au wapili 😀😀
Watu wanaonekana kuboreka.

Kisha kwa mara nyingine tena pastor anauliza kama kuna mwengine basi anasimama sindi kisha anaenda mbele na kujitambulisha kuwa ni mgeni, anasema kaja kutoa ukweli ambao anajua utawaumiza wahusika lakini ndio njia pekee ya kuujua ukweli.kisha anaenda kukaa kwanza

Kwaya inarudi tena kuimba.
Wakiwa hapo kanisani ghafla anaingia sbu akiwa kachafuka usoni koti liko wazi anafyatua risasi tatu akiwa na bastora mkononi, zinaskika kelele humo ndani

Mpka jumatatu hiyo..
 
kavuruga sana...,staki kuamini kama sbu kamshoot mxolis
Inawezekana kamshoot mxolisi au xulu au alipiga hovyo hovyo tu
Mastermind alitakiwa kuwa kimya sbu angefanyiwa kitu mbaya sana
 
Inawezekana kamshoot mxolisi au xulu au alipiga hovyo hovyo tu
Mastermind alitakiwa kuwa kimya sbu angefanyiwa kitu mbaya sana
kweli mastermind hakutuliza akili..hasira na wivu juu ya sbu ndo vilikua vinamuendesha,kaaribu mchezo mzima wa mxolisi juu ya sbu..aaagh!
 
kweli mastermind hakutuliza akili..hasira na wivu juu ya sbu ndo vilikua vinamuendesha,kaaribu mchezo mzima wa mxolisi juu ya sbu..aaagh!
Xulu alipanga plan vizuri kabisa akamwambia master kuwa wafanye kama hawajui sbu ni snitch.
Lakini master wivu unamuendesha na pombe zilichangia,

Halafu haonekani akipigiwa simu haipatikani.. Lile li sbu noma sana kumbe likila unga limeingia kama shetani vile kanisani 😀😀😀😀
 
aseh nilishtuka sana apo kha ni hatari kaibuka ka jini vile😅
 
Back
Top Bottom