Uyahudi na Watu weusi

sony23

Member
Mar 27, 2018
11
19
Je ulishawahi kuwaza kuwa labda jamii ya watu ambayo ilikuwa na watu maarufu duniani kama Yesu, mfalme Daudi na mfalme Sulemani walikuwa na ngozi nyeusi?

nakuletea taarifa kuwa jamii ya Wayahudi walikuwa na ngozi nyeusi na mpaka leo wayahudi ni watu weusi na kwa maana hii wewe unayesoma uzi huu unaweza ukawa Myahudi

Naanza na historia fupi ya Wayahudi, kipindi cha mfalme Rehoboamu taifa la Israeli liligawanyika kwenye falme mbili ulikuwa mwaka 930 kabla ya kristo ilikuwa ni kipindi baada utawala wa mfalme Sulemani.. hizo falme mbili ni ufalme wa Israeli (shekemu na Samaria) ufalme huu ulikuwa na makabila kumi kwanzia kabila la Rubeni mpaka kabila Efraimu na ufalme wa kusini ambao ni ufalme wa Yuda ufalme huu ulikuwa na makabila matatu ambayo ni kabila la Yuda, Benjamin na Lawi.... huu ufalme wa Yuda ndo Wayahudi...

mnamo mwaka 587 kabla ya kristo mfalme Nebukadneza alivamia Yerusalemu kipindi hicho ufalme wa Yuda ulikuwa China ya mfalme Sedekia, mfalme Nebukadneza aliiteka Yerusalemu na akawachukua Wayahudi wengi walikuwa na vyeo vya juu na pia wakazi wengine ndani ya mji na kuwapeleka Babeli kama watumwa na kisha akawaacha Wayahudi wachache sana Yerusalemu ambao walikuwa ni manikini aliwaacha chini ya uangalizi wa amiri jeshi wake aliyeitwa Nebuzaradani.. miaka kadhaa baadae hawa Wayahudi wachache masikini waliokuwa wamebaki Yerusalemu waliamua kukimbilia Misri hiyo ndo safari ya kwanza ya Wayahudi kulowea Misri na hapo ndo tunaanza kupata ule uhalisia wa kuwa wayahudi ni watu weusi.....

baada ya hapo mnamo mwaka 167 kabla ya kristo mfalme wa ugiriki aliyetawala Syria alitambulika kwa jina la Antiochus (IV) Epiphanes alivamia Jerusalem na kuingia hadi kwenye hekalu la Mungu wa Israeli na kuweka sanamu la mungu zeus na kutoa kafara ya nguruwe kipindi hiki Wayahudi wengi sana pia walikimbilia Africa na kulowea huku nia yao ilikuwa ni kukimbia kuwa watumwa wa wagiriki na kipindi hiki wayahudi walikimbilia Libya, Morocco na Algeria na wakajenga himaya kubwa sana huko Africa ya kaskazini iliyoitwa Carthage, hii himaya ya kiyahudi ilikuwa na mfalme maarufu aliyeitwa Hannibal
Huyu jamaa alikuwa maarufu kwa sababu ya mbinu yake ya kupigana vita kwa kutumia tembo, alipigana vita nyingi na Roman empire na warumi walimjua vizuri na kumuogopa sana Hannibal.

baada ya himaya ya wagiriki kuanguka warumi walianza kutawala dunia, mpaka kipindi cha Yesu na baada kufa kwa Yesu warumi walikuwa wakitawala dunia, na warumi walitawala mpaka Yerusalemu na Yudea na mmoja kati ya magavana wa kirumi ndani ya Yudea na Yerusalemu alikuwa ni Pontio pirate, kabla Yesu hajafa aliwapa unabii Wayahudi kuwa Yerusalemu ungezungukwa na majeshi ya Roman empire... twende kwenye huo unabii wa Yesu Luka 21: 20- 21 "lakini, hapo mtakapoona mji wa Yerusalemu umezungukwa na majeshi, ndipo jueni ya kwamba uharibifu wake umekaribia"
"Ndipo walio katika Uyahudi na wakimbilie milimani, na walio katikati yake wakimbilie nje, na walio katika mashamba wasiuingie" huu unabii aliotoa Yesu ulitimia mwaka 70 AD ambapo majeshi ya Roman empire yalivamia Yerusalemu chini ya Jenerali wa jeshi la kirumi aliyeitwa Vespasian na mwanae Titus kipindi cha military campaigns za huyu jenerali Vespasian kuanzia mwaka 68AD hadi mwaka 70 AD... kwenye kitabu kiitwacho From Babylon to Timbuktu professor Rudolf Windsor anasema kuwa takribani Wayahudi milioni moja walikimbilia Afrika ...itaendeleaa
 
WAISLAMU WEUSI
WARUSI WEUSI
WAMAREKANI WEUSI
WAKRISTU WEUSI
WAYAHUDI WEUSI
WAHINDI WEUSI
WAAFRIKA WEUSI
😂😂😂😂

MWEUSI NI MWEUSI TU HIZO CATEGORIES NI KAMA UBABAISHAJI TU WA UTU WA MTU
 
Nothing new.

IMG-20220326-WA0010.jpg
 
Kudumane jokisabe ndivo alivo itwa MWEUSI tiii . Alafu Annunak Wanasemaje jombaá.
Annunak walirudi kwao Nibiru zamani za kale baada ya kumaliza mission Yao ya Gold mining kukamilika,
Zipo nadharia zao za kurudi kwao na Moja ya tales ni Ile ya masihi Heru/Horus/Jesus Christ/Zeus kurudi Tena na kundi la Malaika au watchers wakitokea mawinguni Maana walizicopy huko Watu wa dini za Abraham!
 
Annunak walirudi kwao Nibiru zamani za kale baada ya kumaliza mission Yao ya Gold mining kukamilika,
Zipo nadharia zao za kurudi kwao na Moja ya tales ni Ile ya masihi Heru/Horus/Jesus Christ/Zeus kurudi Tena na kundi la Malaika au watchers wakitokea mawinguni Maana walizicopy huko Watu wa dini za Abraham!
Ngoja tuwasubiri tuone Kama wata Rudi.
 
Uzi huu unaendelea tulipoishia jana.. jana nilitoa historia fupi ya wayahudi na jinsi gani walivyolowea Afrika,.. ila leo natoa maelezo ya wasomi wengi walioingia Africa na kuona jamii za wayahudi weusi ndani ya hili bara na pia nitatoa historia ya wayahudi wengi weusi walioletwa Afrika kutokea Ureno

Naanza na kutoa ushahidi wa msomi na mwanahistoria mmoja aliyetembelea Afrika ya kaskazini aliyeitwa Maurice Fishburg aliyetembelea miji ya Algiers, constantine iliyopo Algeria pamoja na mji wa Tunis uliyopo Tunisia aliwaona wayahudi wengi ambao walikuwa ni "Negroid type" maana ni weusi sana kama Negroes......

Msomi mwingine kwa jina la Nahum schoulz aliwatembelea hawa wayahudi weusi waliokuwa Algeria na akakusanya ushahidi ya uwepo wa hawa wayahudi weusi Afrika ka kaskazini kupitia njia tatu, ya kwanza ni kupitia rekodi za kihistoria za waarabu, ya pili kupitia oral traditions za watu wa Afrika ya kaskazini na ya mwisho ni kupitia archeological remains za himaya za kiyahudi zilizo kuwepo huko Afrika ya kaskazini kabla ya ujio wa waarabu hasa kwenye jangwa na Sahara na nchi ya Sudan ambazo zilikuwa zina date kwenye Karne ya 13 AD.. anasema Nahum schoulz kuwa about half away down the border of Algeria kulikuwa na mji ulioitwa Wargla anasema kuwa Wayahudi walikuwepo huko toka mwaka 620 AD.. kutokana na msomi na mwandishi mwingine wa kihistoria aliyeitwa Godbey anasema kuwa kwa umbali wa takribani maili 350 kutoka bahari ya Mediterranean kulikuwa na ufalme wa kiyahudi uitwao Wargla ambao ulikuwa na Wayahudi weusi ambao ni Negroes..... Godbey anaendelea kusema kuwa kwenye sehemu ya Libya iliyoitwa Gharia kulikuwa na Wayahudi wanaishi huko ambao walikuwa wanasema walikimbia uvamizi wa warumi na waarabu, katika hilo eneo anasema Godbey kuwa hawa wayahudi weusi walijenga makazi yao underground na walifanikiwa kujenga strongholds ambazo zilikuwa na compartments ambazo zilienda three to four stories underground, anasema Godbey kuwa hizo stories zilikuwa ni makazi ya hawa wayahudi weusi waliokuwa huko Gharian, Libya anasema tena kuwa msafiri aliyeitwa Hesse wartegg alifanikiwa kutembelea haya makazi ya hawa wayahudi weusi wa Gharian ambayo yalikuwa ni Ben-Abbas, Jebel Neffussa, Yehud Abbas, Tigrena na Jebel iffren... Godbey anasema kuwa alivyowakuta hawa Wayahudi weusu walikuwa wanafuata sabato na kuishika torati na pia walikuwa wanafahamu asili yao ya uyahudi na pia alikuwa anasema kuwa kwa kipindi hiko alipokuwa Afrika ya kaskazini alikutana na makabila mengi ambayo ni watu weusi waliokuwa waislamu lakini walifahamu asili yao ya uyahudi... lakini baada ya kuona ushahidi huu wa wana historia kuwa kulikuwako na Wayahudi weusi wengi Afrika ya kaskazini, ila miaka mingi sana baadae kutokana na wimbi kubwa la ungezeko la vita ya jihad wayahudi wengi sana walikimbilia Afrika magharibi na hapa tutaona ushahidi wa wana historia juu ya hawa wayahudi weusi waliokimbia Afrika ya kaskazini na kushuka Afrika ya magharibi na mambo walioyafanya huko..

Anasema professor Rudolf Windsor kwenye kitabu chake cha From Babylon to Timbuktu kuwa wayahudi weusi wengi walihama kutoka Sudan kuja Niger River au West Africa, tukumbuke kuwa nilisema kwenye uzi uliopita kwamba wayahudi weusi wengi walikimbila Misri baada ya kutoka Yerusalemu,.. Sasa Misri ya kale iliitwa Kemet au Mitzarayam kwa lugha ya kiebrania cha zamani au unaweza ukasema Paleo-Hebrew na Sudan ilikuwa ni sehemu ya Kemet, so Wayahudi wengi walihama from Sudan to West Africa na wengine walihama kutoka North Africa kuja Niger river amabapo ni West Afrika na wakakutana hapa makundi haya yote mawili.... Professor Rudolf Windsor kwenye hichi kitabu chake anasema kuwa Wayahudi weusi walikuwepo Afrika miaka 1500 kabla ya Uislamu haujaingia Afrika na kila mahala ambapo waislamu walikanyaga Afrika wayahudi weusi walikuwepo hapo,.. pia anatujuza kuwa wayahudi weusi ndo ambao waliwaongoza waislamu ambao walikuwa ni waarabu na watu walioitwa moors ambao wana asili ya Morrocco kuingia Spain na hawa wayahudi weusi walikuwa kama ni ma interpreters... professor Rudolf Windsor anatuambia kuwa kipindi waislamu waarabu wanaingia North Afrika waliwakuta Wayahudi weusi wanatawala trade route zote za maeneo hayo from Morrocco to Sudan the black jews were dominant kabla ya ujio wa waarabu...

Kutokana na maandishi ya mwandihi mmoja, kwa jina la Leo Africanus he was a Moorish writer anatupa information kuwa kulikuwa na himaya ya wayahudi weusi kaskazini mwa senegal river iliyoitwa Kanuria, iliyokuwa na miji miwili mikubwa amabayo ni Kamnuri na Naghira... pia kuna moorish writer mwingine aliyeitwa El idrisi yeye aliishi Andalusia, Spain anatupa informations kuhusu himaya ya wayahudi weusi iliyoitwa Lamlam ambayo ilikuwa kama maili 200 kabla hujafika timbuktu, hii himaya ya Lamlam ilikuwa na Wayahudi weusi tupu na ili control trade routes haya maeneo yote ya timbuktu... anasema El Idrissi kwamba hawa wayahudi weusi hawakuwa na makazi ndani ya interior of Africa pekee ila pia walikaa kwenye coast ya Africa kwanzia Morrocco hadi Angola....

Sio hivyo tu wayahudi weusi hawakuja Afrika kwa kupitia ardhi peke yake ila walikuja kwa njia ya maji.. miaka hii ya karne ya 15 wayahudi weusi wengi sana walikuwepo wakiishi Ureno (kuhusu kwamba hawa wayahudi weusi walifikaje Ureno hilo ni somo la siku nyengine),.. Professor Rudolf Windsor anasema kuwa mnamo mwaka 1484 mfalme John wa Ureno aliwa deport wayahudi weusi wengi sana kwenye kisiwa cha Sao Thome kilichopo karibu na Gabon, anasema Professor Rudolf Windsor kuwa hawa wayahudi weusi waliletwa kwenye kisiwa cha Sao Thome walihama hapo Sao Thome na kwenda Angola kwanzia mwaka 1484 hadi mwaka 1499.. hawa wayahudi weusi waliotokea Ureno walikuwa wakiitwa Black Portuguese kwa kuwa wengi walizaliwa na kukulia Ureno ila leo wote hao ni waafrika, mnamo oktoba mwaka 1497 mfalme manuel wa ureno alitoa amri kuwa wayahudi weusi wote wanoishi Ureno wabatizwe na wawe wakatoliki na endapo watakataa inabidi wauwawe, kanisa katoliki hapo Ureno lilikuwa likitumia njia waliyoita Inqusition ambayo walifanya kuwachoma moto watu wote waliokataa kuwa wakatoliki, hii amri ilitolewa kwa wote ila iliwalenga haswa wayahudi weusi ambao walikuwa hawataki kuacha tamaduni za babu zao yaani torati, hichi kitu kiliwafanya Wayahudi weusi wengi kukimbia Ureno na kwenda kwenye kisiwa cha Sao Thome huko West Africa, professor Rudolf Windsor anasema kuwa wayahudi weusi wachache waliobaki Ureno walilazimika kuwa wayahudi kwa siri na kuwa wakristo kwa nje tu, wayahudi walikatazwa kuishika sabato, walilazimishwa kuto kuwatahiri watoto wao wa kiume na pia walilazimishwa kula nyama ya nguruwe, mambo ambayo ni kinyume na torati, kipindi hicho huko Ureno wayahudi wengi walikuwa wakristo kwa sababu ya uoga, wakawa wanaitwa secret jews kwa sababu walikuwa wana practice torati kwa siri,

Professor Rudolf Windsor anatoa pia majina ya Wayahudi maarufu sana miaka hiyo wayahudi weusi walivyokuwa wanaishi Spain.. wayahudi hao ni wanafalsafa maarufu ambao ni Baruch spinoza na Moses maimonides hawa jamaa walikuwa ni wayahudi weusi maarufu sana Spain na pia ni majina maarufu sana kwenye falsafa..... nitakuja na details zao kwenye muedelezo wa huu uzi pamoja na wayahudi weusi walivyojenga Ghana, Songhay na Mali empires.. itaendelea
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom