uwiii Elizabeth Michael tena!!!!!

uwiii Elizabeth Michael tena!!!!!

vivian

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2009
Posts
1,825
Reaction score
1,307


mwili wa marehemu daniel mwasalemba 30 ukiwa umelala kwenye majani baada ya kutolewa ndani marehemu amechomwa visu kisa ni ugomvi wa kugombania mwanamke aitwae elizabeth michael

mnamo tarehe 08.02.2013 majira ya saa 06:30hrs huko katika mtaa wa itiji kata ya itiji jiji na mkoa wa mbeya. Daniel s/o mwasalemba,miaka 18,kyusa,mkulima mkazi wa itiji alikutwa akiwa ameuawa kwa kuchomwa kisu kifuani upande wa kushoto na peter s/o bosco,miaka 25,mfipa,mpiga debe,mkazi wa itiji. Mwili wa marehemu ulikutwa ukiwa uchi kando ya barabara. Chanzo ni wivu wa kimapenzi baada ya marehemu na mtuhumiwa kumgombea mwanamke elizabeth d/o michael, miaka 18,kyusa,muuza pombe za kienyeji katika kilabu kiitwacho musoma mkazi wa itiji. Kabla ya tukio marehemu na mtuhumiwa ambao wote walikuwa na mahusiano ya kimapenzi na elizabeth d/o michael walipigana kilabuni hapo tarehe 07.02.2013 majira ya saa 21:00hrs wakimgombea mwanamke huyo kisha kuamuliwa na wateja wengine na mtuhumiwa aliondoka na mwanamke huyo hadi nyumbani kwa mwanamke na kuanza kumpiga.



hata hivyo elizabeth d/o michael alifanikiwa kukimbia na kurudi kilabuni ambapo alikutana na marehemu na kumweleza tukio hilo ambaye walikubaliana kurudi wote nyumbani kwa mwanamke huyo. Majira ya saa 01:30hrs mtuhumiwa peter s/o bosco alirudi nyumbani kwa elizabeth d/o michael na kumkuta mwanamke huyo akiwa na marehemu chumbani hivyo aliwafungia mlango kwa nje na kwenda kutafuta kisu na aliporudi alivunja mlango kisha ugomvi baina ya marehemu na mtuhumiwa ulianza upya na mtuhumiwa alimchoma marehemu kisu kifuani upande wa kushoto na kusababisha marehemu kudondoka chini huku damu nyingi zikimtoka na mtuhumiwa kutoweka.


mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya rufaa mbeya kwa uchunguzi zaidi. Mtuhumiwa peter s/o bosco amekamatwa kwa ushirikiano baina ya polisi na wananchi wa eneo hilo. Taratibu za kisheria zinafanywa ili afikishwe mahakamani kwa kosa la mauaji. Aidha mwanamke anayedaiwa kugombewa elizabeth d/o michael anaendelea kuhojiwa polisi kuhusiana na tukio hili. Kamanda wa polisi mkoa wa mbeya kamishna msaidizi wa polisi diwani athumani anaendelea kutoa wito kwa jamii kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi. Aidha anatoa rai kwa wenye ndoa/mahusiano ya kimapenzi kuwa waaminifu kwa wenzi wao ili kuepusha matatizo yanayoweza kuepukika na pindi wanapokuwa na migogoro/matatizo watumie njia ya mazungumzo kumaliza/tatua matatizo/migogoro yao.
 
Poleni sana akina Elizabeth Michael kwa haya mambo yaliyowasibu.
 
Hivi kigombewacho hadi kuuana ni hii hii FIRIGISI tuijuayo au kuna kitu kingine tofauti jamani?
 
Heshimuni marehemu ... kuweka picha za maiti ni uncooth.
 
Yaani ufe kisa kugombania mwanamke? No way jose!

Nyani Ngabu unadhani ni rahisi kiasi hicho kwa watu waliochoka na kukata tamaa ya maisha kama hawa jamaa zetu wa kijiji cha Itiji Mbeya?
Watu wanakesha kwenye mataputapu unadhani kuna mtu anawazia kufa? Lazima mmoja aonekane kidume kwa kumdhibiti mwenzake...
 
Last edited by a moderator:
Mungu aninusuru na balaa hili,Kama rizki imekwisha basi ...
 
Wanawake walivyo wengi na warembo bado mnauwana? Shame on you
 
Yaani ufe kisa kugombania mwanamke? No way jose!

kaka yawezekana asilimia kubwa ya wanaouawa au kuua ktk kesi za mapenzi kinachosababisha mtu kuuua au kuuawa siyo mapenzi moja kwamoja(-sina takwimu, ni speculation tu). ni kama leo kindimbajuu na nyani ngabu tumekutana kwa mwanamke tukaanza kuzozana. kindimbajuu nikajibu namna ambavyo ikakufanya wewe uhame kwenye mawazo ya mwanamke ukabaki na yale niliyo yasema, hapo waweza ku-react vyovyote vile, hiyo reaction yaweza either msababishia kifo kindimbajuu au kindimbajuu aka over- counter reaction ya nyani ngabu, na nyani ngabu kwishnehi... tuombe tu hekima itawale ktk matendo yetu ya kila siku
 
Kuna mzee mmoja mwenye busara alinidokeza kua; kitakacho maliza watu wengi wa rika hili (akimaanisha vijana) ni ngono kwa namna tofauti..... sasa naanza kuamini.... R.I.P Barlow.:confused2:
 
mapenzi matamu sana, kifo kibaya sanaaaa.
kuwahi kifo kibaya ukaacha mapenzi matamu, kisa "elizabeth michael" ni uhayawani wa hali ya juu, huyu ibilisi anayeleta mawazo kama haya ashindwe na ...... kwa jina la ....
 
Back
Top Bottom