Mkereketwa_Huyu
JF-Expert Member
- Feb 19, 2011
- 10,586
- 7,976
Yaani ufe kisa kugombania mwanamke? No way jose!
Mkuu usishangae. Hata mimi na kiburi changu cha kutopigania mwanamke siku moja yalinikuta haya ila sikuuwawa wala kuua bali nilijikuta tu bila kuetegemea napigana na mwenzangu kisa demu wake. Yule demu alikuwa kibaka kwani hakuniambia kuwa ana mtu wake japo walikuwa siyo official (yaani wanapigana miti tu kishikaji). Tukawa tumekaa sehemu hivi tunapata moja moto moja baridi huku tukipanga ya baadaye, jamaa akanivizia na kunipiga chupa kisogoni😕. Nilipogeuka nikaona jamaa anadamu kwenye t-shirt yake (damu yangu) huku akinitukana na kunisanifu kuwa ataniua. Ndipo nikatumia karate zangu za mwalimu Hamidu, nikamrukia kwa tikitaka ya usoni. Jamaa akaanguka chini nikamrukia tumboni mpaka akajinyea kidogo nimuue ila jamaa waliopo pale wakamwokoa kwa kunishika mimi. Kumuuliza yule binti kulikoni ndipo akaniambia kuwa yule kaka ni jamaa yake tu wa kiushikaji ila hayuko serious naye. Nikajifanya mnyonge ila nikamwambia sijisikii kukutana naye kimwili ile siku na nikamkatia mawasiliano moja kwa moja. Matukio mengine yanatokea tu bila kuyapanga mkuu.