uwiii Elizabeth Michael tena!!!!!

uwiii Elizabeth Michael tena!!!!!

Wanawake walivyo wengi na warembo bado mnauwana? Shame on you

Jogoo wenyewe waishaacha kugombana waligundua kuwa mbona tetea wengi? Huyu akifukuzia tetea huyu mwenzake anafukuzia mwingine maisha yanaenda.
 
Sasa mbona eliza ni jina zuri tu,ila labda mtu mwenyewe ndio tatizo
 
Najua siku tukianza kufunguka hapa, hakuna mwanaume hajawahi kuingia katika mgogoro wa level tofauti na mwanaume mwingine sababu ya mwanamke. Actually mi mwenyewe kwa sasa niko kwenye mgogoro na mlugaluga Fulani. Hope hatutachomana visu...lol
 


mwili wa marehemu daniel mwasalemba 30 ukiwa umelala kwenye majani baada ya kutolewa ndani marehemu amechomwa visu kisa ni ugomvi wa kugombania mwanamke aitwae elizabeth michael

mnamo tarehe 08.02.2013 majira ya saa 06:30hrs huko katika mtaa wa itiji kata ya itiji jiji na mkoa wa mbeya. Daniel s/o mwasalemba,miaka 18,kyusa,mkulima mkazi wa itiji alikutwa akiwa ameuawa kwa kuchomwa kisu kifuani upande wa kushoto na peter s/o bosco,miaka 25,mfipa,mpiga debe,mkazi wa itiji. Mwili wa marehemu ulikutwa ukiwa uchi kando ya barabara. Chanzo ni wivu wa kimapenzi baada ya marehemu na mtuhumiwa kumgombea mwanamke elizabeth d/o michael, miaka 18,kyusa,muuza pombe za kienyeji katika kilabu kiitwacho musoma mkazi wa itiji. Kabla ya tukio marehemu na mtuhumiwa ambao wote walikuwa na mahusiano ya kimapenzi na elizabeth d/o michael walipigana kilabuni hapo tarehe 07.02.2013 majira ya saa 21:00hrs wakimgombea mwanamke huyo kisha kuamuliwa na wateja wengine na mtuhumiwa aliondoka na mwanamke huyo hadi nyumbani kwa mwanamke na kuanza kumpiga.



hata hivyo elizabeth d/o michael alifanikiwa kukimbia na kurudi kilabuni ambapo alikutana na marehemu na kumweleza tukio hilo ambaye walikubaliana kurudi wote nyumbani kwa mwanamke huyo. Majira ya saa 01:30hrs mtuhumiwa peter s/o bosco alirudi nyumbani kwa elizabeth d/o michael na kumkuta mwanamke huyo akiwa na marehemu chumbani hivyo aliwafungia mlango kwa nje na kwenda kutafuta kisu na aliporudi alivunja mlango kisha ugomvi baina ya marehemu na mtuhumiwa ulianza upya na mtuhumiwa alimchoma marehemu kisu kifuani upande wa kushoto na kusababisha marehemu kudondoka chini huku damu nyingi zikimtoka na mtuhumiwa kutoweka.


mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya rufaa mbeya kwa uchunguzi zaidi. Mtuhumiwa peter s/o bosco amekamatwa kwa ushirikiano baina ya polisi na wananchi wa eneo hilo. Taratibu za kisheria zinafanywa ili afikishwe mahakamani kwa kosa la mauaji. Aidha mwanamke anayedaiwa kugombewa elizabeth d/o michael anaendelea kuhojiwa polisi kuhusiana na tukio hili. Kamanda wa polisi mkoa wa mbeya kamishna msaidizi wa polisi diwani athumani anaendelea kutoa wito kwa jamii kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi. Aidha anatoa rai kwa wenye ndoa/mahusiano ya kimapenzi kuwa waaminifu kwa wenzi wao ili kuepusha matatizo yanayoweza kuepukika na pindi wanapokuwa na migogoro/matatizo watumie njia ya mazungumzo kumaliza/tatua matatizo/migogoro yao.

Itigi ipo wilaya ya Manyoni na sio mbeya. Asante kwa taarifa.
 
Mkuu,mimi nipo Mbeya,na jana asubuhi nimeshuhudia kwa macho yangu mwili wa marehemu huyo ukipelekwa hospitali,huku huyo binti na jamaa yake muuaji wakiwa wanapelekwa polisi.

Asante kwa taarifa mkuu. Ila maana yangu ya kumuuliza mrembo vibie ni hilo swali ni kwa njinsi alivyoandika hayo maelezo.
 
Kijana wa watu maskini, miaka 18 si ndio kwanza kabalehe
 
Dah! Mshikaji umenichekesha sana. Shukrani tele.

Ila hiyo ya kwako mbona inakubalika na kueleweka kabisa...manake wewe hukukianzisha hicho kitimtim. Jamaa alikushambulia na wewe ulikuwa na haki zote za kujihami kwa kumpa kisago kitakatifu na inavyoelekea ulimpa alichostahili.

Ambacho mimi siwezi kukifanya ni kwa mfano nikimkuta tuseme mke wangu au mpenzi wangu yuko na njemba sehemu na labda wanafanya wasiyopaswa kufanya, kwa kweli siwezi kulianzisha. Nilianzishe ili iweje? Nimpiganie mwanamke ambaye hata haniheshimu? Hapana aisee. Ninajipenda sana kiasi cha kutoweza kumpigania mtu aliyenidharau na kunidhalilisha.

Katika muktadha wa mapenzi na mahusiano, nitajipigania (kama nimeshambuliwa kwanza) mwenyewe na yule tu anayeniheshimu na kunipenda kweli. Zaidi ya hapo hapana, sitoki ngeu isiyo na sababu ya msingi.


Mkuu Nyani Ngabu nimekupata kisawasawa baada ya kusimulia kwa kina. Ni kweli inauma sana kuona demu wako yuko anapapaswa na jibaba lingine kwani hii inahashiria kuwa kakuchoka. Hata mimi kwa mantiki hii tu siwezi kumpigania demu hata iweje. Tupeane pole.
 
Last edited by a moderator:
Najua siku tukianza kufunguka hapa, hakuna mwanaume hajawahi kuingia katika mgogoro wa level tofauti na mwanaume mwingine sababu ya mwanamke. Actually mi mwenyewe kwa sasa niko kwenye mgogoro na mlugaluga Fulani. Hope hatutachomana visu...lol

muache, wanawake wapo wengi, sijawahi kugombea mwanamke ila kuna watu walitaka kugombana na mimi kisa wanawake nilikaa nao mbali kwa sababu mwanamke akiwa na msimamo hawezi kugombewa.
 
Gazeti la kipuuzi sana hili. Unaliwa hela yako ivi ivi kweupe barabarani.
FRONTWIKIENDA.jpg
 
HATA MI HUWA NAJIULIZA SANA BILA KUPATA MAJIBU SAHIHI!!!!!!:confused2::confused2::confused2::confused2::confused2:
Hivi kigombewacho hadi kuuana ni hii hii FIRIGISI tuijuayo au kuna kitu kingine tofauti jamani?
 
Hivi kigombewacho hadi kuuana ni hii hii FIRIGISI tuijuayo au kuna kitu kingine tofauti jamani?
Tatizo siyo FIRIGISI, Tatizo utamu na ladha uipatayo pale, ni tofauti kabisaaaaaaaaaaaaaa!!!!!!!!!!!!!!
Kuna zingine zinaladha ya ndimu, zingine ladha ya sukari, basi alimradi ladha tofauti ndiyo maana unaweza kutana na moja ukadata kutokana na ladha.
 
Might it be a cursed name?

Possible, kuna majina baadhi ni balaa. Kama haya ya akina Elizabath( Liz),Beatrice,Lilian ni balaa.Tujihadhari na majina ya kuita watoto pia na majina ya kurithi kwa wazee.
 
Back
Top Bottom