SoC01 Uwezeshaji Sera za kilimo kwa vijana

Stories of Change - 2021 Competition

_Angel

New Member
Jul 14, 2021
2
1
Kilimo ni taaluma inayojulikana na pia ni mwajiri mkubwa wa wananchi wengi katika taifa hususani kwenye nchi zinazoendelea mfano; Tanzania. Japokua watu wengi wanaojishughulisha na kilimo Kama njia moja wapo ya maisha Mara nyingi ni watu wa makamo(aged) pamoja na wale wasio na elimu, ingawa katika kipind cha sasa vijana wamekua na idadi kubwa nchini ambayo inaweza kuchangia katika kuchochea maendeleo ya taifa, lakini idadi kubwa ya Sera za kilimo na mipango zilizobuniwa hazikuchochea maslahi ya vijana hivyo kupelekea vijana kutafuta ajira katika sekta nyingine za kiuchumi ili kuweza kujikwamua kiuchumi na kuacha kilimo kwa watu wa makamo(aged).

Moja
Ikiwa lengo kuu la uchumi Tanzania ni viwanda, wakati kilimo kikiwa ni hafifu na ushiriki wa vijana kwenye kilimo ni wale wasio na elimu pamoja na walio shindwa shule hii hufanya vijana kuona kilimo ni kitu duni, hakina faida yoyote, kisicho timiza malengo na ngumu sana hivyo kutokuweka nia katika kilimo. Kuna haja ya kushughulikia hili kubadili mtazamo hasi wa vijana kupelekea kilimo pamoja na kushiriki wito katika maendeleo Kama zilivo sekta nyingine katika maendeleo zinavotegemea vijana.

Mbili
Kutokushiriki kwa vijana katika shughuli za kilimo Tanzania imekua ni suala linaloleta utata mkubwa kati ya watafiti na wataalamu wa kilimo pamoja na wasimamizi ikiwa ni pamoja na kupungua kwa idadi ya wanafunzi wanaoingia katika mafunzo ya kilimo imekua ikiongezeka zaidi ya miaka hivyo kupelekea wasomi kukidharau kilimo.

Tatu
Uhamasishaji wa vijana katika maendeleo ya kitaifa ni Jambo la msingi katika nchi zinazoendelea, kwa kuwashirikisha vijana katika shughuli za kiuchumi kupitia programu ya vijana utachangia kwa kiasi kikubwa katika maendeleo ya kilimo pamoja na kuwezesha wananchi na vijana kwa ujumla kupata mahitaji kamili ya kujitosheleza katika uzalishaji wa mazao biashara na chakula kwa sababu vijana ni mustakabali na muhimili muhimu katika nchi yoyote.

Mwisho, mabadiliko ya kilimo hayawezi kufanyika katika nchi zinazoendelea mfano Tanzania bila ya kuwa na nguvu kazi (vijana) wengi katika kilimo isipokua tu Kama kutakua na teknolojia bora pamoja na utayari wa vijana kushiriki katika nyanja za kilimo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom