#COVID19 Uwepo wa COVID-19 umesababisha migogoro ya ajira kuongezeka

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,011
9,879
Tumeya Usuluhishi na Uamuzi wa Migogoro ya Ajira imesema baada ya kuibuka kwa mlipuko wa ugonjwa wa COVID-19 imepokea migogoro inayofi kia 18,222 kuanzia mwaka jana hadi mwaka huu.

Kaimu Msemaji wa tume hiyo, Nahshon Mpula alisema hayo alipozungumza na televisheni ya Azam.

Alisema ongezeko la migogoro hiyo ni kubwa ikilinganishwa na kipindi cha nyuma na sehemu kubwa ni kuhusu kusimamishwa na kupunguzwa kazi.

“Kwenye sheria hakuna sehemu inakosema kuwa Covid- 19 ni sababu ya kumpunguza mtu kazi. Unachopaswa uthibitishwe ni kwa namna gani umeathirika na ugonjwa huo kwamba labda uchumi umeshuka au pato la mwajiri limeathirika kwa hiyo siwezi kulipa wafanyakazi 1,000 naweza kubaki na 200,” alisema Mpula.

Akaongeza: “Muhimu ni kufahamu taratibu za kisheria za haki ili mtu ajue ametendewa haki.” Alisema zaidi ya migogoro 6,000 imeongezeka katika kipindi ambacho mlipuko wa ugonjwa huo umeibuka nchini.

Mpula alisema tume ilitoa uamuzi wa migogoro 14,468 ndani ya kipindi hicho na kati yake ya usuluhi ni 8,814 na ya uamuzi ni 9,408.

Alisema migogoro ya usuluhishi ni ile ambayo mfanyakazi na mwajiriwa wanafikia mwafaka wa mgogoro huo na ya uamuzi ni ile ambayo pande zote zinashindwa kuafikiana na hivyo tume kutolea maamuzi.

Mpula alisema katika migogoro hiyo sekta iliyowasilisha migogoro mingi kwa tume hiyo katika kipindi hicho ni ya ujenzi ikifuatiwa na ya ulinzi binafsi, vyakula na hoteli.

Alisema Mkoa wa Dar es Salaam uliongoza kwa kuwasilisha migogoro hiyo ya ajira, ukifuatiwa na Arusha (sekta ya utalii iliongoza) na Mwanza

Chanzo:
HabariLeo
 
Back
Top Bottom