Migogoro mingi ya ardhi inasababishwa na Madiwani na Wenyeviti wa mitaa

Kimwakaleli

JF-Expert Member
Apr 16, 2018
3,897
5,354
Ni usiku mwema kwa wote wana jf,

Nimeona ni jambo jema na la kufanyiwa kazi hasa kwa Wizara ya ardhi. Ili kuepusha migogoro na malumbano yasio na tija kwa eneo husika hasa wananchi kwenye swala la ardhi ni vyema hawa viongozi wetu tajwa hapo juu wachaguliwe kulingana na tabia nzuri zisizo na tamaa za kijinga!

Nimekuwa nikishuhudia migogoro mbalimbali ya ardhi hasa hapa Dodoma, mingi utakuta wamo waliosababisha migogoro hiyo ni wenyeviti wa mitaa pamoja na madiwani!

Kama vile uvamizi wa maeneo ya wazi, utakuta mwenyekiti wa mtaa nae anaeneo kajimegea pamoja na Diwani baadhi.

Hivyo kabla ya kuchukulia hatua wananchi tuanze na hawa madalali Chama!
 
Kwa bahati mbaya au nzuri hao viongozi wote wanapatikana kwa njia ya kupigiwa kura na sio kwa kuteuliwa labda tungeilaumu serikali moja kwa moja.

Kwa mfumo wa Tanzania unaogubikwa na viongozi wanaoyanunua madaraka ili wapate nafasi za uongozi uadilifu ni changamoto mana nafasi za uongozi wao wanabadilisha kuwa ni fursa ya ajira na wanatoa pesa(kama mtaji) ili wapate nafasi.

Wanachowaza ni namna ya kunufaika na uongozi wao, uadilifu ni zero, tatizo hili linazalishwa na wananchi wenyewe ambao ndiyo wanaoziuza kura zao wenyewe na haya ndiyo matokeo ya kile walichokitenda.

Ila naamini wananchi kwa kushirikiana na maafisa ardhi pamoja na wakuu wa wilaya au mikoa wanaweza kutatua changamoto hizi.
 
Ina gharama mkuu,kuna maeneo hadi watu wanapoteza maisha kwa sababu ya migogoro!Ukiiangalia kiundani unaambiwa mwenyekiti wa mtaa nae yuko upande flani badala ya kusimamia sheria na Haki!
 
Kwann awe upande wa fulani badala ya kusimamia haki?
Rushwa ndiyo adui wa haki siku zote na katika ulimwengu wa rushwa maskini hana haki, ni sawa na kuwa na hakimu fisi mshtakiwa awe mbuzi alafu utegemee haki.
Ni kweli migogoro ya ardhi huleta maafa makubwa inayogharimu hadi uhai wa watu.

Kunapotokea suala kama hili kwa ukubwa ni vyema kwenda kwa viongozi wakubwa wa ngazi ya juu kama DC au RC kama kutakuwa na mashaka kwenye ngazi zote hizo ndy watafutwe viongozi wa juu kama mawaziri.

Ila cha muhimu ni wananchi kipindi cha uchaguzi njaa isifanye tuuze kura zetu kwa watu wasiokuwa waadilifu maana sisi ndiyo tutakuwa kwenye dimbwi la mateso kwa muda wa miaka mitano, tuchague viongozi kufuatana na sera pamoja na mienendo yao ya kitabia pamoja na kuangalia historia zao na familia zao wanazotokea.
 
Kuna haja ya kuweka vipengere vya wasie madaalali!
 
Back
Top Bottom