Uwepo, biashara na Uwekezaji

Hundred_sisters

New Member
Oct 5, 2023
3
16
UWEPO
MWENYE ENZI MUNGU akaiumba DUNIA. Hakika katika Dunia MWENYE ENZI MUNGU akawaweka VIUMBE wengi sana na akampa mamlaka makubwa ya UFAHAMU kiumbe Mmoja tu BINADAMU.

Binadamu wamepita wengi sana huko nyuma na leo hii UPO WEWE na ndo maana hukuwepo mwaka 500 upo SASA hivi 2023.

Sasa kila binadamu anayo hii NGUVU ya UWEPO ambayo akishaigundua kuwa YEYE YUPO basi huanza kugundua baadhi ya mambo ambayo YAPO na yana vipaumbele sana kwenye hii DUNIA yenye UWEPO. Moja ya mambo hayo ni

BIASHARA.
Ukiona upo katika hii DUNIA aliyo iumba MWENYE ENZI basi Huna budi kugundua pia katika KIZAZI ulicho zaliwa Kuna UWEPO wa BIASHARA kama ambavyo wewe UPO, hivyo Huna budi kui Kuifahamu biashara ni kitu gani ambacho mtu unazaliwa unakuta watu wako busy, kila unamuona ni kama anatafuta PESA ambayo pesa io imetoka katika mfumo wa UWEPO wa BIASHARA

BIASHARA
Biashara ni shughuli au mchakato wa KUNUNUA na KUUZA mali au vitu kwa LENGO la kupata faida.
Inaweza kufanywa na mtu binafsi au kwa ushirikiano na jamii au nchi kwa lengo la kupata PESA.
Popote pale unapopita utaona BINADAMU wana shughuli au hizi michakato za KUNUNUA au KUUZA. hapo ujue hio ni BIASHARA.

ukiona io shughuli inatokea popote unapoona tambua io ni BIASHARA na unatakiwa ui FAHAMU sio kuilewa tu.
Unapoona michakato kama io tambua BINADAMU anatafuta PESA, kwa hivyo kinachotokea pale ni kwamba mtu mtu anauza na Kununua Ili tu apate io PESA

PESA & BIASHARA

Pesa ni nini?

Pesa ni kitu kinachotumika kufanya mabadilishano Yani mtumiaji wa anakupatia PESA we unampatia mali au vitu. Kinachotokea ni kwamba PESA ilichaguliwa kama kifaa kitachotumika katika BIASHARA pale mtu anataka KUNUNUA au KUUZA Mali, ilichaguliwa kama THAMANI ambayo inaweza kutumika kubadilishana kwa bidhaa au huduma yoyote Ile ambayo BINADAMU kaianzisha, ikumbukwe zamani PESA haikuwepo lakini tafsiri ya PESA ilikuwepo Yani watu walikua wanabadilishana bidhaa kwa bidhaa katika BIASHARA ( BARTER TRADE ) na kwa hivyo pesa sio Ile karatasi, pesa ni kile kitendo cha KUBADILISHANA.

Sasa kabla hujawa mwenda wazimu na kutafuta PESA inakubidi uitambue Ili ujue thamani ya UWEPO wako kabla yenyewe haija shusha UWEPO wako.

UJASIRIAMALI & BIASHARA
kama ushawai kusikia neno ujasiriamali basi ndo kitu cha kwanza kwanza kabisa unachotakiwa kuanza kabla hujawa MFANYA BIASHARA, hii ni hatua ya kwanza kabisa ya kuanza biashara.
Hatua hii inakufanya uanze kujua nini huwa kinaendelea kuhusu biashara.

UJASIRIAMALI ni nini?
Ni mchakato wa kuzitambua Fursa na kuzitumia katika shughuli za kijamii, kiuchumi, kitaifa.

Mfano una shilingi 100,000 na unataka kuanza biashara, hapo tunasema utaanza kuwa MJASIRI na MALI kwanza kabla ya kuwa mfanya BIASHARA, una 100,000 na unataka kwa mwezi uwe na faida ya 100,000 nyingine

MFANO: Utaanza Kununua mchicha na kupitisha kwenye nyumba za BINADAMU
utanunua mafungu 40 utapisha na utauza fungu 10 tu.

utagundua hujauza na Kutakua na sababu ambayo inabidi uzujue ukiwa kama kiumbe MWENYE UFAHAMU na utakua ushakula LOSS, lakini UWEPO wa BIASHARA unasema KUTOUZA ndo kujua namna ya KUUZA.

kesho utaongeza ujazo wa fungu na utauza fungu 20 utagundua tena mzigo haujaisha. na umekula LOSS.

Siku inayofata utagundua mpinzani wako ndo anafanya huuzi sana, utaanza Kununua vitunguu vidogo vidogo na Kila fungu kuweka kitunguu kimoja

Baadae utagundua Wateja ni wengi na pesa ya mtaji haitoshi, hapo sasa utakua kwa kidgo sana umeanza kuuelewa ujariamali kwani ulikutana na changamoto na ukazitatua yani (ujari na Mali) kwa kutumia UFAHAMU.

Utapata MTAJI MKUBWA na utaanza kulima matuta ya MCHICHA na KUUZA
baada ya mda flaani utaanza kupata PESA.

Utagundua unapata pesa lakini
MTAJI HAUKUI KABISA pesa inaisha na hujui Nini kinaendelea, hapo sasa Unaanza kuingia kujifunza BIASHARA vizuri.

TUENDELEE..

Utaanza KUSOMA vitabu Ili kujua Nini kinaendelea kuhusu BIASHARA na mambo ambayo utagundua Kuhusu Siri ya biashara ni..

sio Kila biashara ni yako japo unaweza kupata PESA nyingi, yani katika DUNIA hii we haujaja kufanya tu Kila jambo, Kuna jambo lako ambalo inabidi ulifanye Ili sasa uanze kuuona UFALME.

pesa ya biashara sio yako kabisa tena haikuhusu yani pesa ya biashara ni kitu kingine na wewe ni kitu kingine kabisa, umemgawia MR. BIASHARA sh 5,000,000 hivyo hiyo pesa sio yako ila Asilimia kadhaa inayotoka kwenye faida ya huwo MZUNGUKO WA PESA TASLIMU ndiyo yako ukiwa kama msimamizi wake.
Usimdhurumu BIASHARA pesa yake.

MWANZO WA MAFANIKIO YAKO YA UWEPO NA BIASHARA
Ukifika hatua zote hizo Katika biashara utaanza Kutaka kujua mambo, na kuna mambo ambayo utajikuta unayafahamu kwani tayari MUNGU ameshaiona Ile NIA yako NJEMA ya KUJITAFUTA kitu cha kwanza kabisa utatakiwa Kukifahamu ni

WEWE NI NANI?
Hii ndo Siri ya kwanza kabisa ya BINADAMU yani kama hujawai kuitambua hii SIRI, ndugu yangu bado upo kwenye upotevu, Yani kwa tafsiri nyingine unatembea ila HAUPO.

INAENDELEA....


Inasemekana na watu waliofanikiwa kuwa KUJITAMBUA WEWE NI NANI ndo hatua ya kwanza kabisa ya kufanikiwa katika ZAMA ZA MAARIFA NA TAARIFA ( information age).
Kujitambua ni SOMO ambalo linafundishwa kwenye Vitabu vya wakuu , semina mbali mbali za makampuni ya wakuu.,
KUJITAMBUA ndo fungua ubongo ya mwanzo wa safari baada ya kutoka kwenye mafundisho ya UJASIRIAMALI na BIASHARA.
Kujitambua kunakufanya uache kuchukua kila biashara na uchukue pale kwenye UPEKEE wako, pia kujitambua kunakufanya Ugundue kuwa hatutafuti pesa kama kitu muhimu sana ila tunatafuta UHURU WA KIFEDHA,
pia utagundua kuwa BINADAMU inatakiwa atafutwe na pesa kwasababu yeye ni MKUU kwenye DUNIA hii.,





UWEKEZAJI & BIASHARA

Tunatafuta pesa Ili tuwe na UHURU wa KIFEDHA, na unapoanza biashara ukiwa umeshajitambua inaanza kukua kwa haraka sana, kwani unakua ushajitambua wewe ni nani, unapenda nini, unataka nini, na nini hutaki.


Kijana Mmoja alisomea kilimo akapata na kazi, akaanza kazi na akawa anapata pesa lakini moyo wake haukua unalidhika. Baadae akasoma vitabu vya KUJITAFUTA na akagundua yeye ana HAMASA na FASHION & INTERTAINMENT , akaamua kutafuta njia za kuingia huko na akaanza taratiiibu kupata MAARIFA yanayohusu MAVAZI, akapata WAZO ambalo hili wazo lilikua linamsubili muda mwingi, wazo likakamilika na akaanza kuliishi kwakua ndo hamasa yake. akaanza kufanikiwa haraka sana.

Yani alikua yupo kwenye sekta ya kilimo na ndio taaluma yake lakini alikua anapenda Fashion & intertainment.

anaitwa FRED VUNJABEI

Fred anaaanza kupata PESA nyingi kwenye mavazi Kisha faida anazipeleka Shambani.

analima mashamba.
anaweka store gunia za nafaka.
anapanda miti katika mashamba

Faida anayopata kutoka kwenye
MAVAZI & SHAMBA ana WEKEZA kwenye kununua VIWANJA na kujenga MAJENGO ya kukodisha (Mali zisizo amishika ), ana WEKEZA kwenye HISA na HATI FUNGANI

Kisha GAWIO na KODI ZA MAJENGO Zinamlipia MAISHA YAKE kama vile

kodi ya maduka yake.
kodi za mijengo yake.
mafuta ya Gari zake.
@Wafanya kazi wake.
pamoja na Bill zingine

na sasa tayari pesa inamtafuta popote kwani alishaacha kutafuta pesa anaishi katika HAMASA yake, kutokana na kuishi anavopenda yeye, pesa inamfata.



Vijana wengi sana wapo njiani wanakuja kwani mambo yameshabadilika, mwenye Maarifa na Taarifa ndiyo mwenye nafasi.



ukiwa unatafuta maisha usiache K UJITAFUTA kwani Ile siku umejipata we ni nani, unapenda nini, unaweza nini sana kuliko vyote na ukaanza kuongeza ujuzi, maarifa na taarifa basi baraka huwa zinaanza kumwagika kuliko kawaida.

KUNA UHUSIANO WA KUFANIKIWA KWA KASI KUBWA SANA ENDAPO UTATAMBUA HAMASA YAKO NA KUIGEUZA IKUINGIZIE PESA KWA KUIGEUZA KAMA WAZO LA BIASHARA.
 
Back
Top Bottom