Chosen Rich
JF-Expert Member
- Jan 7, 2019
- 1,565
- 1,118
Unahitaji elimu ili upate maarifa ya kutosha, Utakua na taarifa sahihi juu ya uwekezaji wa namna hii na utabadilisha mtazamo wakoKuwekeza kwenye majengo ni sawa na fedha zako kuzifukia sehemu, na kuanza kuila kidogo kidogo mpaka iishe.
Na kula huko unakuwa hauli faida zaidi ya kula mtaji (fedha ulioiwekeza). Wengi ukimbilia kujenga nyumba za kupanga, 'apartment', hoteli, nyumba za kulala wageni n.k huku wakijipa matumaini majengo hayo yatawalipa na kupata faida zaidi na zaidi.
Kwa ujumla majengo hayo uwapa hasara, vinginevyo mmiliki hatonufaika zaidi ya kizazi chake kijacho ambacho ndio kitakuwa kinakula faida baada ya miaka kadhaa kupita.
Ukitaka kuamini hili, tembelea nyumba za kupanga, 'apartment', hoteli, nyumba za kulala wageni n.k zipe miaka mitano alafu ukazitembelee tena, utazikuta zimechoka na kama hakutokuwa na hela ya ziada ya ukarabati, ndio hivyo biashara inakuwa imekufa.
Kwa nini majengo ya zamani yamechoka kama kweli uwekezaji huo unalipa?Unahitaji elimu ili upate maarifa ya kutosha, Utakua na taarifa sahihi juu ya uwekezaji wa namna hii na utabadilisha mtazamo wako
Sio kwa Nyumba za wageni,,aise wanapiga peza we jiulize show time elffu 10 na lodge ina vyumba 30+
Unahamisha risk?Na huyo atakayenunua yeye ndio pesa yake itarudi kwa haraka?
Ni kweli kabisa na hakuna haja ya kwenda shule/vyuo kujifunza mawazo ya watu wengine kwenye vitabu.Kila mtu Aamiin anachokiamini
Kama mtu alishawekeza huko, lazima ajifariji kwa sababu hawezi tena kurudi nyuma.Hawa watu sasa hivi tunawaacha na hizi thread zao maana hata ukiwapa mifano hai wanaumia watabaki kusema unajimwambafai. ASIEJUA MAANA HAAMBIWI MAANA.
Inawezekana wewe utakuwa una jengo unakusanya 30,000 kwa mwezi.Chai
Pesa uliojengea ilisharudi?Kuna mdau anakwambia nyumba inakaa miezi sita bila wapangaji,mimi kusema kweli nyumba zangu akitoka mpangaji madali wameshagombania kesho anaingia mwingine.Location ni muhimu
Hiyo unayoiita faida utakuja kuitumia kwenye ukarabati mkubwa, mbaya zaidi hizo fedha huwa hatuziweki, baada ya miaka kadhaa jengo linakuwa limechoka na mabati kuwa na rangi kama jezi ya simba.Biashara hii inategemea na wapi umewekeza, jengo la aina ile ile ubora ule ule, kodi inatofautiana sehemu na sehemu, __cpLocation ndio jambo kubwa zaidi kwenye biashara nyingi.
na ubora wa ujenzi ulioufanya.. miaka mi5 ukarabati tena mkubwa hayo ni maajabu mkuu.
Nimefanya sehemu kwa udogo, naona faida yake, ningekuwa na uwezo ningefanya kwa ukubwa zaidi, ni biashara nzuri, haina stress na inalipa vizuri.
Mfano mie nijenge frem za biashara 5 kwa milioni 30, kodi ni laki 2 kwa mwezi,hapo nakuwa nakunja milioni kila mwezi, kodi ya miezi 6 ni milioni 6.. nakunja hiyo pesa wakati jengo(milioni 30) lipo, yaani hizo milioni kila mwezi ni faida.
Pesa uliojengea ilisharudi?
Selling information through technologyNi biashara ipi unaiamini zaidi kwenye kuwekeza mkuu, kwa miaka hii ya sasa???
Itarudi nikitaka hata kesho na faida kubwa tu.Pesa uliojengea ilisharudi?
Ni kwa sababu unataka kujenga kwa cash, matajiri hutumia madeni so ile cash flow ni ela mpya kwakeKuwekeza kwenye majengo ni sawa na fedha zako kuzifukia sehemu, na kuanza kuila kidogo kidogo mpaka iishe.
Na kula huko unakuwa hauli faida zaidi ya kula mtaji (fedha ulioiwekeza). Wengi ukimbilia kujenga nyumba za kupanga, 'apartment', hoteli, nyumba za kulala wageni n.k huku wakijipa matumaini majengo hayo yatawalipa na kupata faida zaidi na zaidi.
Kwa ujumla majengo hayo uwapa hasara, vinginevyo mmiliki hatonufaika zaidi ya kizazi chake kijacho ambacho ndio kitakuwa kinakula faida baada ya miaka kadhaa kupita.
Ukitaka kuamini hili, tembelea nyumba za kupanga, 'apartment', hoteli, nyumba za kulala wageni n.k zipe miaka mitano alafu ukazitembelee tena, utazikuta zimechoka na kama hakutokuwa na hela ya ziada ya ukarabati, ndio hivyo biashara inakuwa imekufa.
Itarudi kwa kudunduliza kila mwezi au kwa kuuza hilo jengo?Itarudi nikitaka hata kesho na faida kubwa tu.
Hapa logic ipoNi kwa sababu unataka kujenga kwa cash, matajiri hutumia madeni so ile cash flow ni ela mpya kwake
Ukarabati mkubwa upi huo mzee, bati zinachoka baada ya muda gani, milango ya fremu baada ya muda gani, wiring ni muda gani, sioni, hapo ni kuomba mungu tu aepushe ajali za moto, tetemeko na mengineyo kama hayo..Hiyo unayoiita faida utakuja kuitumia kwenye ukarabati mkubwa, mbaya zaidi hizo fedha huwa hatuziweki, baada ya miaka kadhaa jengo linakuwa limechoka na mabati kuwa na rangi kama jezi ya simba.
Ni jengo lipi lenye miaka 10 ambalo ukilitazama leo, bado lina mng'ao ule ule wa upya?Ukarabati mkubwa upi huo mzee, bati zinachoka baada ya muda gani, milango ya fremu baada ya muda gani, wiring ni muda gani, sioni, hapo ni kuomba mungu tu aepushe ajali za moto, tetemeko na mengineyo kama hayo..
Makadirio ni miaka 20 mbele huko, wakati huo thamani ya eneo inapanda, kodi inaongezeka, sasa ishu ya wiring kwa mimi, si kodi ya mwezi mmoja tu nimerekebisha. Na sio leo wala kesho, mpaka sasa jengo lina miaka mi5, mie kwa mahesabu yangu nakula faida, sababu ujenzi wake naona pesa isharudi mkuu.
Je marekebisho yake hayo ni sawa na kujenga jengo upya? Marekebisho yanachukua hata 25%? Jibu hapana.Ni jengo lipi lenye miaka 10 ambalo ukilitazama leo, bado lina mng'ao ule ule wa upya?