Uwekezaji wa majengo haulipi

Ukijenga na kuuza sawa, ila ukitaka upangishe ili uweze kujilipa, fedha ulioiwekeza hutoipata.
Ndio maana kuna uwekezaji wa mda mrefu na wa mda mfupi. Ww unataka faida za haraka haraka wekeza kwingine kwenye nyumba za kupangisha ni uwekezaji wa mda mrefu na huchukua mda kurudisha pesa yako ila faida yake ni nyumba itakua na thamani mara mbili ya faida ama fedha uliyo wekeza
 
Mkuu, kama nyumba umejenga sehemu nzuri na umejenga kitaalam una haki kusema ni faida. Umewekeza eg bilioni 1 , unakula faida ya ya eg milioni 5 kila mwezi na mtaji unabaki pale pale. Watu wengi wanakosea kuwekeza kwenye nyumba kwa sababu anataka kurudisha fedha alizojengea kwa muda mfupi afanye shughuli nyingine zizalishe tena. Uwekezaji wa nyumba siyo wa namna hiyo, yaani siyo una fedha ya ngama halafu unawekeza kwenye nyumba. NB: unaweza kutumia hati ya nyumba yako kukopa fedha na ukafanyia shughuli nyingine.
 
Ni kama social security yako

Ova
 
Chukulia nyumba uliyojenga ndio mtaji wako na hela ya pango unayopata ndio faida siku ukitosheka na faida unauza nyumba/ardhi unarudisha mtaji wako kibindoni kwishaa
 
Sawa, HIYO PESA YA KUWEKEZEA KWENYE MAJENGO WAWEKEZE KWENYE NINI? MAANA WEWE UNAJUA MATUMIZI YA PESA NA UWEKEZAJI KULIKO WAO, WAFUNDISHE BROO USIISHIE HAPO WAAMBIE NA KIPI CHA KWENDA KUWEKEZA PESA
Si sahihi kumpangia mtu matumizi, ila ni muhimu kutathmini faida na hasara ya kila uwekezaji.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…