ZeMarcopolo
Platinum Member
- May 11, 2008
- 14,017
- 7,220
Nauliza haraka ya nini? Mboni tuko mbioni?
Kuyafukua madini, mwaka huu si mwakani?
Ukifuatilia mijadala inayozunguka uwekezaji kwenye mafuta na gesi, utagundua kuwa wapo watanzania (tena wasomi) ambao hawajatambua kuwa rasilimali tunayoizungumzia ina uwezo wa kubadilisha kabisa hali ya maisha ya watanzania.
Rasilimali hii ni Game Changer...
Kama kwenye mpira wa miguu, ni sawa na kupewa penalt dakika ya 90.
Sasa hivi tumepewa penalt, halafu tumeshaonyesha dalili za kumpa penalt hiyo beki apige. Striker wetu tunasema akae pembeni! Hili ni kosa. Yatatukuta kama Yanga walivyofanywa na David Mwakalebela...
Hoja kubwa inayozunguzwa ni kwamba watanzania hawana uwezo wa kuwekeza kwenye sekta hii.
Tuko watanzania zaidi ya milioni 45. Watu milioni 45 tunashindwa vipi kuwekeza kwenye uchimbaji mafuta na gesi?
Jibu ni kwamba hatushindwi. Ila maamuzi ya haraka haraka yanafanya ionekane kama vile tunashindwa.
Kuna hoja zinaongelewa kama vile tunalazimika kuchimba mafuta mwaka huu, mara moja. Kama vile mafuta yatakimbia.
Mafuta yalikuwepo, yapo na yataendelea kuwepo. Tunachohitaji sisi ni mkakati wa jinsi ya kuyavuna kwa faida zaidi.
Ingefaa tuwe na mkakati wa miaka kumi (10) wa kujijengea uwezo wa kuchimba mafuta na gesi.
Katika kipindi hicho cha miaka 10 tupeleke vijana wakasome ujuzi wa kiufundi, kisheria, kiuchumi, kibiashara na kimazingira wa uchimbaji mafuta na gesi. Vijana 60 katika ufundi na wengine 10 katika fani nyingine, jumla vijana 100. Vijana hawa wangesoma kwa wastani wa miaka mitatu degree ya kwanza.
Baada ya hapo, tukawapeleka vijana hawa miaka miwili internship kwenye makampuni ya uchimbaji mafuta na gesi katika fani walizosomea. Paid intenship.
Baada ya miaka hiyo miwili tukawapeleka kusoma masters degree katika fani zitakazowekewa malengo maalum. Masters itakuwa kwa wastani wa muda wa miaka miwili.
hapo itakuwa imeisha miaka saba (7). Tutakuwa na wataalam wenye uelewa wa kutosha kuhusu uchimbaji mafuta na gesi, tuliowaandaa kwa malengo maalum. Wapo ambao hawatamaliza masomo lakini iwapo uchaguzi utafanyika vizuri, ambao hawatamaliza watakuwa wachache sana.
Wataalam hawa baada ya kumaliza masters degree warudi nyumbani kwa ajili ya kuanzisha masomo ya elimu ya uchimbaji mafuta na gesi kwa ngazi ya diploma na degree. At the same time watumiwe katika uwekezaji huu.
Je, pesa zitatoka wapi?
Miaka kumi inatosha kubuni mfuko wa kukusanya pesa za mtaji wa kuwekeza kwenye uchimbaji toka kwa wananchi.
Ili nchi za Africa ziendelee, kwanza kabisa inabidi zitambue kuwa haziwezi kufanikiwa iwapo zitakuwa zinaiga jinsi nchi zilizoendelea zinavyotatua masuala yao. Nchi zilizoendelea zina mifumo inayoziwezesha kutabili matokeo ya maamuzi wanayofanya. Sisi mifumo hiyo hatuna. Maamuzi yetu mengi ni trial and error.
Kwahiyo, inabidi tubuni utaratibu ambao uko customised kulingana na mazingira yetu.
Serikali inaweza kuhamasisha wananchi kujiunga na mfuko wa ukusanyaji mitaji. Kwa kipindi cha miaka saba nchi ifanye kazi ya kukusanya mitaji tu na kuhifandhi fedha hizo. Ukiangalia pesa zinazochangwa kwenye harusi, utakuwa shahidi wa kuwa uwezo tunao - kinachokosekana ni organisation tu. Ndio maana hata kwenye familia inayofanya harusi ya shilingi milioni tano si ajabu kukuta kuna mtoto anayekosa ada ya shilingi laki mbili!
Wakati haya yakifanyika serikali inaendelea na uboreshaji wa TPDC kimfumo, kisera na kimiundombinu ili iwe tayari kwa kazi hii. Hii ni pamoja na kuanzicha chuo cha TPDC chenye lengo la kuzalisha wataalam wa ngazi mbalimbali za ujuzi katika sekta ya mafuta na gesi.
Kwa utaratibu huu, katika kipindi cha miaka saba nchi inakuwa na wataalam pamoja na pesa na TPDC inakuwa standby. Inabaki miaka mitatu ya wataalam hao kushirikiana na wale wachache ambao tayari wapo na watendaji wa serikali kutengeneza utaratibu rasmi wa uchimbaji kutokana na utaalam waliojifunza. Pale tunapopungukiwa tunaweza kuajiri washauri wenye uzoefu zaidi, lakini wanakuja kama waajiriwa wanaosikiliza mahitaji ya mwajiri ambaye ni sisi.
Haraka ya nini? Mbona kama kuna kitu kinakimbiliwa kabla jambo fulani halijatokea? Je, ni nini future ya miradi hii baada ya jambo hilo kutokea? - kwa sababu ni lazima litokee.
Nchi yetu imejiendesha zaidi ya miaka 50 bila mafuta na gesi, inaweza kuvumilia miaka mingine kumi bila mafuta na gesi wakati tukijiandaa.
Tufikirie vizazi vijavyo. Hakuna mwingine wa kuwaandalia mazingira bora watanzania wa kesho ila ni sisi.
Kupanga ni kuchagua...