Uwekezaji huu wa Dangote uangaliwe upya

Uwekezaji huu wa Dangote uangaliwe upya

Wikileaks Expose The Bitter-truth About Secret Of Aliko Dangote Wealth - Business - Nigeria

Nime i copy hupo juu

The named Alike Dangote, in nigeria, African
and the rest of the world means entrepreneur
and commodities tycoon. Recently released of
Forbes world most richest person in the world
rank nigeria entrepreneur among the 40th
richest man in the world. Richer than Russian
wealthiest man and Indian richest man.
About few days ago pan African magazine
Ventures African ranked him 1st richest black
man in African continents over others 54
billionaires in African. But the truth about it
success secret was recently exposed by
International online, non-profit organisation
which publishes secret information, news leaks,
and classified media from anonymous sources —
WikiLeaks which is owned by Julian Assange.
WikiLeaks describe Alike Dangote, as person
operating a “Beggar-thy-countrymen” ie- get
rich by turning Nigerians into beggars, business
model. Furthers says that the government
enforced and encourage monopolies and the
destruction of all competition. Aliku Dangote,
the embodiment of corruption itself, establishes
himself in unimaginable wealth, and then buys
press to placate the masses by making them
believe that a few ‘slave-labor’ employments
and charities define him as different, patriotic
and benevolent. Contrary to popular narration,
Dangote did not invest in Nigeria, Dangote uses
Nigeria. Nigeria’s governments deposited the
nations resource in Dangote.

Nahis kabla ya kumruhusu muwekezaji tuwetunatafuta profile yake. Watu kamahawa sio wazuri. Kwasababu ukisona sana ni kwemba anaua competition kwenye market. Sasa na tanzania yetu hii ivi tanga cement, mbeya cement na twiga zikafa kisa mtu moja utakuwa ni upuuzi. Kwan mtu mwenyewe yawezekana ata kodi halip. Alafu kampuni yenyewe ata kwenye soko la hisa la tanzania haipo. Na article ingine nimesoma ya dangote cement ya zambia ni shidah sana. Ambapo ameshusha bei ya cement nusu ya soko la dunia nakupelekea makampuni mengine kushindwa kuoperate na kupeleka watungikupoteza ajira. Hatukatai kushusha bei lakin inabidi tuangalie upande wa pili.
 
Last edited:
Yaaani viongozi wetu ni wapuuzi sana, yani swala dogo kama hili Mpaka Magufuli aingilie Kati, Mkuu wa Mkoa, mkuu wa wilaya, Afisa utawala, Viongozi wa kisiasa huko Mtwara wamekaa kimya tu wanaangalia, inexperienced individuals coming all the way from India to Mtwara and grab opportunities which Tanzanians can successfully manage. These issues and others of sort promote the hate of ones own country,
 
Bila shaka serikali inapaswa kufatilia kwa ukaribu sana hili swala na kuhakikisha hizo kero zinaangaliwa...aliye andika ni nahakika anaweza kuwa ni mfanyakazi wa pale! Hapo ndipo watu wakifukuzwa kazi kwa kushindwa kusimamia mambo serikali inaonekana mbaya!

Hivi serikali ya mkoa wa Mtwara inafanya nini hadi haya yanatokea? Nafikiri kabisa serikali ya mkoa wa mtwara inapaswa kuwajibika kwenye haya na kutoa maelezo ya kina! Hakika huu ni upuuzi kweli..!
 
Wikileaks Expose The Bitter-truth About Secret Of Aliko Dangote Wealth - Business - Nigeria

Nafikiri kwenye hili pengine mwekezaji hana kosa bali kosa linaanza kwenye uongozi wa kiwanda mpaka wasimamizi na bado sifikirii kama Dangote ana watuma wafanye wanayo yafanya!

Hiki kiwanda kina msimamizi anatakiwa awe wa kwanza kuwajibika kwenye haya yote...!

Hata ukwepaji wa kodi uliofanya na maofisa sidhani kama Dangote ana ufahamu...!

Walipewa jukumu la kusimamia shughuli za kiwanda hiki ndio tatizo na bila shaka Serikali ita wamulika....

Nime i copy hupo juu

The named Alike Dangote, in nigeria, African
and the rest of the world means entrepreneur
and commodities tycoon. Recently released of
Forbes world most richest person in the world
rank nigeria entrepreneur among the 40th
richest man in the world. Richer than Russian
wealthiest man and Indian richest man.
About few days ago pan African magazine
Ventures African ranked him 1st richest black
man in African continents over others 54
billionaires in African. But the truth about it
success secret was recently exposed by
International online, non-profit organisation
which publishes secret information, news leaks,
and classified media from anonymous sources —
WikiLeaks which is owned by Julian Assange.
WikiLeaks describe Alike Dangote, as person
operating a “Beggar-thy-countrymen” ie- get
rich by turning Nigerians into beggars, business
model. Furthers says that the government
enforced and encourage monopolies and the
destruction of all competition. Aliku Dangote,
the embodiment of corruption itself, establishes
himself in unimaginable wealth, and then buys
press to placate the masses by making them
believe that a few ‘slave-labor’ employments
and charities define him as different, patriotic
and benevolent. Contrary to popular narration,
Dangote did not invest in Nigeria, Dangote uses
Nigeria. Nigeria’s governments deposited the
nations resource in Dangote.

Nahis kabla ya kumruhusu muwekezaji tuwetunatafuta profile yake. Watu kamahawa sio wazuri. Kwasababu ukisona sana ni kwemba anaua competition kwenye market. Sasa na tanzania yetu hii ivi tanga cement, mbeya cement na twiga zikafa kisa mtu moja utakuwa ni upuuzi. Kwan mtu mwenyewe yawezekana ata kodi halip. Alafu kampuni yenyewe ata kwenye soko la hisa la tanzania haipo. Na article ingine nimesoma ya dangote cement ya zambia ni shidah sana. Ambapo ameshusha bei ya cement nusu ya soko la dunia nakupelekea makampuni mengine kushindwa kuoperate na kupeleka watungikupoteza ajira. Hatukatai kushusha bei lakin inabidi tuangalie upande wa pili.
 
Bila shaka serikali inapaswa kufatilia kwa ukaribu sana hili swala na kuhakikisha hizo kero zinaangaliwa...aliye andika ni nahakika anaweza kuwa ni mfanyakazi wa pale! Hapo ndipo watu wakifukuzwa kazi kwa kushindwa kusimamia mambo serikali inaonekana mbaya!

Hivi serikali ya mkoa wa Mtwara inafanya nini hadi haya yanatokea? Nafikiri kabisa serikali ya mkoa wa mtwara inapaswa kuwajibika kwenye haya na kutoa maelezo ya kina! Hakika huu ni upuuzi kweli..!

kweli kabisa mkuu, nimesikitika sana niliposoma thread hii, nimeshawishika kuamini kilichoandikwa kwa jinsi mletaji alivyojieleza, ni wakati wa Magu kufukuza hawa wakuu wa mikoa na wilaya wasiojua hata wajibu wao,
 
Kuajiri wageni kwenye nafasi ambazo wabongo wanaweza kufanya sio sawa!lakini inawezekana na sisi tuna matatizo pia!haya makampuni watu wamewekeza hela zao au pengine mikopo,wanahitaji zirudi na wapate faida.Bila hiyo faida au hata kubreak even hizo kampuni hazitaendelea kuwepo na hata hizi ajira tunazozungumzia hazitakuwepo pia!sasa tatizo letu mtu akipewa nafasi hawazi kufanya mambo yatakayoifanya kampuni iwe prosperous na kuendelea kuwepo(maana uwepo wake ndo uwepo wa ajira yako na ya wengine na ya vizazi vijavyo),asilimia kubwa ya wabongo watafikiria njia za kupiga wajinufaishe wao binafsi na familia zao na kula bata za kibabe mtaani!ukifikiria kupiga fikiria na njia za kuiwezesha kampuni kumake profit kubwa zaidi ili hata hako kamrija kako ka kupiga kaendelee kuwepo basi!lakini sisi hatuko ivyo tunawaza kupiga tu!nimeona mtu ameandika hata Bonite ya Mengi imejaa wahindi,mi siamini kama Mengi hapendi kuwapa kazi watanzania wenzake,yani hataki kuwapa hizo ajira hata ndugu zake wachaga???kwanini??labda ni kwasababu anajua akiwapa hizo nafasi watamfilisi.kwaiyo na sisi tukipata izo nafasi tubadilike,tufanye kazi vizuri.hata wahindi na wazungu wanapiga sana tu,lakini hawafilisi kampuni na wanafanya vitu vinavyoipeleka kampuni mbele.sasa kwa mbongo inakua kama kumkabidhi fisi bucha.inasababisha tuonekane hatufai,matokeo yake wanapewa kazi wahindi,wazungu,wachina..e.t.c ambao wengine hawana sifa wala uwezo!
 
kweli kabisa mkuu, nimesikitika sana niliposoma thread hii, nimeshawishika kuamini kilichoandikwa kwa jinsi mletaji alivyojieleza, ni wakati wa Magu kufukuza hawa wakuu wa mikoa na wilaya wasiojua hata wajibu wao,
Bila shaka viongozi wa serikali wa pale mtwara wanatakiwa kuwa wa kwanza kuwajibishwa kwa madudu haya...! Haya madudu yanafanyika chini ya uongozi wa serikali ya mkoa wa Mtwara na haiwezekani hawafahamu haya....
 
Haya Waziri wa viwanda pamoja na waziri wa kazi na ajira njooni huku muone ya dangote jamaniiiii!!!!

Nadhani hiyo ni msogadangote; wee acha tu tembelea malaika hoteli huko mwanza yaani watz ni mawaiter na waitress lakini supervisor wote ni wahindi tuuu, sasa hapo eti tunamaofia wa uhamiaji, hehheheeeeeeeeeeeeee!!!!!!!! uuuuuuuuuuwiiiiiii, nchi yetu tunashida MUNGU tuokoe tunaangamia

Je hivi JPM naye huwa anaingia humu?
 
Watanzaia wengi na hata nchi jirani mtakuwa mmewahi kusikia pambio za sifa kutoka kwa wanasiasa na uongozi wa awamu ya nne, hasa wa kutoka mrengo wangu wa kulia, juu ya uwekezaji wa kiwanda cha saruji cha tajiri namba moja wa Afrika, Mnigeria Aliko Dangote mkoani mtwara. Binafsi niliposikia baadhi ya wanasiasa na hasa mkuu wa kaya enzi hizo akiimba na kusifu ujenzi wa kiwanda hicho cha saruji, nilitaka kuingia kwenye mtego wa kuwaamini watu wa mrengo wangu wa kisiasa, hususani tulipoambiwa kwamba kiwanda hicho kikikamilika kitaweza kutoa ajira takribani elfu kumi 10,000 kwa watanzania. Nilishituka sana, lakini kwa akili ya haraka haraka nikajiongeza kufikiri kwamba aaah hiyo idadi si inajuisha wafagiaji wa magodown ya mawakala watakaokuwa pale wilayani kwetu kasulu? Nikajiongeza kuvuta kumbukumbu ya ahadi ya ajira millioni moja kwa vijana iliyotolewa mwaka 2005, na hatimaye majibu yaliyotolewa baadaye kwenye hotuba ya mwanasiasa namba moja mwaka 2010 wakati akiomba ridhaa tena ndipo nilipofunguka akili zaidi na kuona katika fikra, binamu yangu ambaye aliishia darasa la saba akibeba mfuko wa saruji kumpelekea mnunuzi nyumbani kwake nikajua tayari nayeye amejumuishwa kwenye idadi ya ajira elfu kumi. Hilo halikunisumbua sana, nilijua siasa inafanya kazi yake ingawa niliamini kwa sehemu kwamba uwekezaji huo utatunufaisha watanzania kwa kutoa ajira na hata kujenga uwezo wa kiteknolojia na uzoefu kwa wale watakaopata fursa ya kufanya kazi na uwekezaji huo.

Mwishoni mwa mwaka jana 2015 nilipata neema ya mwenyezi Mungu ya kusogea karibu na uwekezaji huo. Kabla sijaanza kuchunguza namna Watanzania hasa wananchi wa Mtwara wanavyonufaika na uwekezaji huu, nilipigwa na butwaa kwa mwenendo ambao sikuuelewa uliohusu ukaribu wa mkuu wa kaya na wanasiasa wake wateule na waandamizi kwa mradi huu. Mara kwa mara niliona magari ya serikali na wakuu mbalimbali wakipishana kwenye geti la mradi kana kwamba ndio mahali pao pa kazi ( ikulu Fulani hivi). Kwakweli naamini msisimko wa jamii uliotokana na kelele za kisiasa kuhusu mradi huu, ulichangia mabadiliko makubwa kiuchumi, ikiwa ni pamoja na kupanda kwa gharama za maisha hususani nyumba, mavazi na maeneo ya kufanyia biashara kusiko na ulazima matokeo yake maumivu yameegemea kwa maskini wa hali ya chini.

Kilichonisukuma kuandika Makala hii, si kutaka kukosoa uhusika wa mrengo wowote wa kisiasa katika mchakato wa uanzishwaji wa mradi huu, wala si usaliti kama ambavyo tumezoea kuambiwa huko nyuma sisi watu wenye mawazo huru ndani ya taasisi zetu za kisiasa, katika hili nalazimika kuamini katika usemi wa kila zama na kitabu chake, kwa sababu hata nikisema kwamba, kwa udhaifu wa uwekezaji huu ambao nitauzungumzia hapa chini waliohusika kutufikisha hapa hawachomoi, wao watakuja na majibu ya mzaha na matusi bila kujali hadhira, umri na nafasi zao kwamba ‘’aaaah sijachomeka popote bwana!’’.

Katika kichwa cha habari nimeomba uwekezaji huu uangaliwe kwa sababu ya mienendo inayondelea katika kiwanda hiki ambapo bila serikali kuingilia kati nchi yetu itaendeleaa kudharaulika na kuwa shamba la bibi miaka yote, na pia watanzania wataendelea kutawaliwa na wakoloni wa ki Assia wakati serikali ikichangia uangamizaji wa taifa kwa kutetea na kuaminisha watu kwamba huu uwekezaji una tija kwa taifa. Mathalani, nitazungumzia maeneo makuu manne yenye msukumo muhimu ambayo ni, nafasi za ajira, masrahi, unyanyasaji na usalama kazini kwa watanzania.

NAFASI ZA AJIRA.

Katika idara takribani kumi na mbili ambazo ni: Rasilimali watu, Manunuzi, stores, usafirishaji, Fedha, Mechanical, Electrical, Uchakataji, Instrumentation, uchimbaji(mines), ulinzi na karakana, ni idara mbili tu kati ya hizo ndio zinaongozwa na watanzania ambazo ni idara ya Ulinzi na Rasilimali watu, ambapo hata hivyo hii ya rasilimali watu inaongozwa na Mzee mmoja ambaye hana tofauti na raia wa Assia kwa uongo, Rushwa na ujanja ujanja. Pia katika idara zote hizo unaweza kukuta wasaidizi mpaka wa nafasi ya nne kushuka chini ni wahindi, maana yake ni kwamba kila idara inaongozwa na wahindi kwa mtiririko hadi wanapoisha ndipo Mtanzania anafuata. Kitu cha ajabu ni kwamba, hawa wahindi katika idara unaweza kumkuta mmoja tu mwenye taaluma husika, wengine ni ndugu zao tu ambao hawana vigezo, kuna watu pale wametoka India wamekuja kutunza kumbukumbu za motor reading na data entry ambazo hata mtu aliyepitia veta mtanzania anaweza kuzifanya kwa ufasaha kabisa, hawa wanajumuishwa na kuitwa wataalam (experts) pindi afisa wa kazi anapokwenda kukagua. Sitaki kuzungumzia sana vibali vyao maana nasikia pale TIC ukienda unatoa hela tu unapewa, nashukuru sasa kazi hiyo imerudi kwa mamlaka moja . Wapo watanzania wenzetu kama yule mzee anayejiita senior HR na mwenzake mwarabu, wanaotumika kuwapa mbinu na kuwaficha hawa wahamiaji haramu wa kihindi kwa malipo.

Katika kiwanda hiki huwezi kupata Mtanzania mwenye uzoefu au mhandisi mwenye uzoefu, na wao hawadhubutu kuajiri watanzania wa namna hiyo maana hizo ni nafasi za wahindi, hata wakitangaza nafasi hizo wanaweka vigezo ambavyo viko India tu (mfano mtu awe na uzoefu wa miaka kumi na tano kwenye kiwanda cha saruji) na hata ikitokea mtu amepatikana kutoka viwanda vingine vya saruji hapa Tanzania wanamwambia wampe mshahara ambao ni mdogo ambao hawezi kukubali ili kuonyesha kwamba watanzania hawataki kazi, mfano engineer ana uzoefu wa miaka kumi anaambiwa apewe laki tisa kwa mwezi,wakati alipotoka alikuwa anafanya kazi hizo hizo kwa ufasaha na analipwa vizuri. Hata hivyo, ajira zenyewe zimegubikwa na mazingira ya Rushwa na magumashi ya hali ya juu. mfano Zipo nafasi zimetangazwa wiki kama mbili zilizopita, ikiwemo nafasi ya stores manager, lakini kabla hata watu hawajaitwa kwenye usaili kuna mhindi kutoka India ameshaanza kazi wiki iliyopita kwenye nafasi hiyo.

Kiwanda kiliwachukua vijana wa kitanzania kutoka vyuoni (fresh graduates) wa uhandisi kwa ahadi ya kuwapeleka kwenye mafunzo kwa miezi sita katika nchi ya Nigeria, kwa kuwalipa posho kidogo, na baada ya hapo wakimaliza mwaka wataajiriwa kama wahandisi kiwandani vijana walihangaika kutafuta passports kwa kasi na kujiunga na kampuni ambapo baada ya kufika kiwandani zile posho zikageuka kuwa mishahara na safari ya mafunzo ikawa haipo tena zikaanza figisu figisu za kihindi nyingi, baada ya kelele nyingi wakaamua kuwachukua vijana hao wahandisi 20 kati ya 100 waliosemwa kwenye ripoti, kuwapeleka Nigeria kwenye kiwanda cha saruji kufanya kazi kwa miezi miwili na hiyo ndiyo ikawa imetoka, na hiyo habari ya mafunzo haipo tena hapo kiwandani na hata baada ya mafunzo hao ishirini waliohudhuria Nigeria hawashirikishwi hata kwenye mikutano ya kiufundi wao wanaagizwa kwenda kusimamia usafi na kurekodi data kwenye substatations.

Siku zote hapo kiwandani wahindi wanafanya kazi ya kuhakikisha watanzania hawajifunzi kitu ili mwisho waonyeshe kwamba watanzania hawawezi, nilishangaa sana kuona kwamba hata wachina walioko kiwandani kwa ajili ya kuendesha kiwanda kwa guarantee ya miaka miwili hawaruhusiwi kuwafundisha Watanzania, wanazuiliwa na wasimamizi wa mradi ambao ni wahindi.

Najiuliza, nini faida ya uwekezaji huu katika taifa, maana mwekezaji amepewa maeneo ya kuwekeza bure, mpaka eneo la kujenga bandari amepewa bure kwa kushirikiana na seriakli iliyokuwepo madarakani kurubuni wananchi kwa kuwaambia kwamba watafaidika na uwekezaji wa Dangote. Pia amepewa msamaha wa kodi kwa miaka mitano, ni nini fadhila yake kama haikuwa kuwaajiri na kuwajengea uwezo watanzania ? hatua gani zinachukuliwa na usalama wa taifa kuhusu hili? Naamini wapo pale, je wanapeleka taarifa hizi?

MASRAHI

Ni dhahiri kwamba mtanzania yeyote au hata mtu wa nje ya nchi akisikia mtu unafanya kazi kwa Dangote Tanzania, picha inayokuja kichwani kwa mtu huyo ni kwamba masrahi yako ni mazuri maana unafanya kazi na kampuni ambayo kwanza ni ya kimataifa na kwa sababu ya jina lenyewe basi ataamini kwamba uko vizuri tofauti na viwanda vingine vya ndani. Lakini mambo sivyo, yalivyo baada ya kufuatilia maisha na masrahi ya watu pale ninaamini kwamba huyu ndugu yetu mwafrika mwenzetu anapaswa kuitwa mafia, wafanyakazi wake wanalipwa ujira mdogo sana kiasi kwamba ni vigumu kuamini wakati mwingine kama wanafanya kazi kwa Dangote.

Lakini kubwa Zaidi ni tofauti kubwa iliyopo ya kimasrahi kati ya wahindi na watanzania, wahindi wote wamepewa usafiri, allowances nyingi na wanaishi hotelini muda wote kwa gharama ya kampuni, kila kitu na bima ya afya ya kiwango cha juu na mishahara yao hakuna mtanzania anayejua inalipwa kwenye akaunti zipi, lakini watanzania kila kitu wanafanya kwa shida, wanasafiri kwa kugombania daladala na kuning’inia kama maembe. Watu wanapewa bima ya afya AAR iliyoandikwa kwenye vikaratasi ya mwezi mmoja, hata hivyo wakienda hospitali hazikubaliwi. Mikataba inayotolewa ni mwaka mmoja mmoja kinyume na sheria ya Tanzania, Hakuna huduma yoyote ya motivation kwa mfanyakazi, hata maji ya kunywa unayapata kwa kuhonga rushwa ya salamu kwa mhindi, akijisikia anazuia watu kunywa maji. Watu wanakula kwenye vibanda vya mama ntilie mazingira amabyo si salama kabisa, ukipita Dangote barabani mchana unaweza kuona kundi kubwa la watu kwenye vibanda umiza kwa akina mama ntilie ukafikiri labda hao ni vibarua kumbe kuna maafisa rasilimali watu, fedha, manunuzi na wahandisi ndani ya vibanda hivyo wakati wahindi wana wapishi wao maalumu wanaowapikia nyumbani kwao na kuwaletea huduma kazini kwa gharama ya kampuni.

Wapo madereva kama mia tatu walifanyiwa usahili, kwa ajili ya kuendesha malori ya saruji, tena walikuwa wanaitwa baada ya kutoa rushwa, na baada usaili walipoambiwa mshahara hakuna hata mtu mmoja aliyebaki, wote waliondoka na kampuni ikaajiri wakala mwingine mhindi mtanzania anayeleta madereva vibarua pale kazi inapojitokeza.

Tujiulize, huu ndio uwekezaji tunaoruhusu uje kuuwa viwanda vingine vya saruji vinavyoa ajira zenye tija kwa watanzania?

UNYANYASAJI

Katika hili watanzania wanapata shida sana kwenye kiwanda hiki, watu wanaishi kama watumwa, si ajabu sana kuona Mtanzania mfanyakazi wa hali ya chini mfano wafanya usafi wakifukuzwa kazi kwa kosa la kucheka, mikataba yao wengi ni ya mwezi mmoja mmoja na hawalipwi kwa muda wakidai wanafukuzwa wanaletwa wengine, si watanzania wana shida?

Wapo vijana wanafukuzwa kazini bila sababu za msingi nilishangaa sana hivi majuzi niliposikia mtu(operator) amefukuzwa kazi na bosi wake mhindi anayeitwa Mr. Manoj kwa kupata pancha ya tairi eneo la mining, wakati huo ikiwa hakuna afisa usalama alieajiriwa ambaye ndio mwenye mamlaka ya kuthibitisha kosa hilo kuwa la maksudi au la, na mwingine ameitwa na huyo mhindi akamuangalia kwa kuwa anafuga ndevu akasema wewe unafanana na alshabaab sikutaki kazini na akamfukuza kazi, vilevile hata ukifukuzwa hupewi barua wakiishakupa taarifa kwa maneno tu ukiendelea kubaki kazini unapoteza muda maana mshahara hutauona. Hapo Kiwandani kila mhindi bila kujali nafasi yake ni bosi popote alipo kwa mtanzania hata kama mtanzania anamzidi elimu, wahindi hapo wana living certificates za sekondari,wengine mafundi Umeme wa grade ya chini kabisa hawajui chochote lakini wanaitwa wataalamu na wanaambiwa wasimamie wahandisi watanzania wenye shahada. Mhindi huyo Akisema yeye hakutaki HR anasema ndiyo bosi na anakufuta kwenye payroll haraka.

Yapo mambo mengi sana ambayo ukiyatazama hautofautishi na mahusiano kati ya mabwana na watumwa ambayo tuliyasoma katika vitabu vya historia zamani tukiwa mashuleni, wakati najiuliza haya nilipata kuzungumza na vijana waliokwenda Nigeria kufanya kazi kwenye kiwanda cha Dangote OBAJANA kilichopo Lagos. Kule wafanyakzi wahindi ni karibu asilimia themanini na wazawa ni kama ishirini tu ,Wahindi wanapewa upendeleo sana kwa sababu wakuu wa kampuni ni wahindi, ndhani hayo ndiyo mambo ambayo mkuu wetu wa kaya awamu ya nne alikuwa analenga yafanyike hapa kwetu hii ndiyo sababu mpaka sasa hawa wahindi hawaamini kwamba wako wachache sana hapa Dangote ya Tanzania hivyo wanataka kuonyesha watanzania hawawezi ili waletwe wengi.

USALAMA KAZINI

Mazingira ya kazi ni magumu sana kwa kuwa ndugu zetu hawa nadhani kwa sababu ya kubana matumizi hawataki kabisa kusikia kwamba kuwekeza katika usalama kazini ni jambo muhimu, vifaa vya kazi (PPEs) wanavyotumia wafanyakazi wa Dangote ukiwaangalia ni kofia tu na viatu ndivyo vinazofanana maana vifaa vingine unajinunulia mwenyewe ukiona vina umuhimu kwako, hata viatu tu ubora wake si wa kudumu miezi mitatu au mitano lakini unaambiwa ukae navyo mwaka mzima. Hakuna alama za tahadhari ya usalama kiwandani, magari yanaendeshwa kwa spidi inayofurahisha madereva na kila kitu kwenye usalama ni cha hovyo hovyo, wahindi wana dharau sana wakiambiwa kuhusu usalama wanawaambia watu waondoke waende wakafanye kazi maeneo salama kwenye viwanda vingine Tanzania, hii yote ni kujaribu kuonyesha kwamba watanzania hawako tayari kufanya kazi. Hakuna maafisa usalama wala mtaalamu wa mazingira hapo, kila kitu kinaendeshwa kienyeji kwa utaratibu wa India.

Nimeandika waraka huu nikiwa na masikitiko makubwa sana kama mtanzania wa kawaida, najua serikali yetu ya awamu ya tano imeanza kushughulikia matatizo haya kwa kasi nzuri, naiunga mkono seriklai na kuipongeza kwa hatua iliyofikia, kwa hapa tulipofikia na kwa jinsi tunavyoendelea nashawishika kuamini kwamba tunaelekea kupata heshima kama binadamu wenye taifa lao. Naiomba serikali iendelee kufanya operations za kuwarudisha hawa wahamiaji haramu makwao, najua ni wabishi sana na wengi wao wanaamini kwamba serikali ya Tanzania haijawahi kuwa na haitakuwa serious kiasi hicho ndiyo maana wengi wanaonekana kugoma goma na kuokuwa na mpango wakuondoka.

Ninamini, watanzania wana uwezo mkubwa wa kufanya mambo makubwa na kuleta maendeleo katika nchi yetu, iwapo taifa likiwekeza katika kuwaendeleza wasomi tulionao, hakuna taifa lililoendelea kwa kutegemea kuendelezwa na watu wa mataifa mengine kama viongozi wavivu wa kufikiri walivyoamini, Serikali iliyopita ililewa madaraka na kuamini katika uzembe, ukarimu wa kijinga pamoja na wizi wa ujanja ujanja, hakuna taifa linaloendelea kwa kujenga msingi wa maendeleo yake katika wizi na ujanja ujanja na matanuzi. Lazima tukubali kuanza kuumia ili kujenga taifa lenye heshima, leo hii ukienda kutafuta Mtanzania anayefanya kazi India humpati, kwanza nani atamruhusu, nenda Kenya, Rwanda na China kama utakuta mtanzania anakalia nafasi ya wazawa, lakini kwetu hapa limekuwa shamba la bibi na sisi tunalia hakuna ajira hata pale tunapopata ajira tunakuwa chini ya raia wa nchi nyingine na tunachekelea tu, Hatuwezi kuwa taifa lenye watu wenye akili timamu tukakubaliana na haya.

Mkuu sitasahau nilipoenda kufanya interview ya process engineer pale...Niliwajibu maswali yote ikaja wakati wa kukubaliana mshahara,daaaah!!! nilichoka ,waliniomba salary slip yangu waangalie jinsi ninavyolipwa current,walah cabinet nzima ilishangaaa,nanukuu maneno yao,"ooh my friend why do you want to leave this company? you are paid extremely even in India no one is paid like this" niliishiwa nguvu zooote,eti walishtuka na kamshahara kangu ka million moja,wao wakataka wanipe laki 6!!! wahindi wajinga sana.
 
Wakitoka huko waende na madepo ya mafuta kurasini kuanzia oilcom,camel oil, oryx, engine na gbp etc ni mwendo wahindi tu na wazungu uchwara na baadhi ya waarab sio raia. Yaan unakuta kazi ya kuhesabu gari pia afanya raia wa kigeni hana elimu wala nn huku wabongo kazi yao kufagia tu
 
Uwepo wa idad ya zaidi ya watu 360 kufanya kazi kwenye kampuny hiyo ni ishara tosha kuwa kampuni hiyo inawanufaisha watu wachache (vigogo) na s watanzania. Hivyo serikali ya JPM iichunguze uozo uliopo huko tujue JK kafanya nin!?
 
pale dangote kuna jipu kubwa linaitwa UCC (unique consulting). hao ndiyo wamepewa tenda ya kuajiri kwa niaba ya dangote. asee, utawaonea huruma vijana walioajiriwa pale. tatizo ni kwamba watu walikuwa na matumaini makubwa sana, na siasa zilizopitiliza!

Wafanyakazi 360 wa Dangote
wakamatwa kwa vibali vya kazi
Wafanyakazi zaidi ya 360 wa kiwanda cha
saruji cha Dangote mkoani Mtwara,
wamekamatwa kwa kufanya
Waziri wa Mambo ya Ndani, Charles Kitwanga
Mtwara. Wafanyakazi zaidi ya 360 wa
kiwanda cha saruji cha Dangote mkoani
Mtwara, wamekamatwa kwa kufanya kazi
nchini bila kuwa na vibali vya Uhamiaji.
Kamatakamata hiyo imekuja baada ya agizo la
Waziri wa Mambo ya Ndani, Charles Kitwanga
la kuwakamata wahamiaji haramu na wageni
wanaofanya kazi bila vibali.
Jana, ofisi ya Uhamiaji ya mkoa ilifanya
operesheni katika kiwanda hicho, lakini
haikupewa ushirikiano na uongozi.
Ofisa Uhamiaji wa mkoa, Zakayo Mchele
alisema walifika kiwandani hapo kufanya
ukaguzi, lakini walikosa ushirikiano kutoka
kwa Meneja Mkuu aliyefahamika kwa jina la
Vidya Digixt.
Mchele alisema kutokana na meneja huyo
kutotoa ushirikiano, wanamshikilia ili
kusaidiana na Uhamiaji kuwabaini
wafanyakazi wanaoishi bila uhalali na pia
watamfikisha mahakamani.
Alisema licha ya kukosa ushirikiano,
wafanyakazi 117 wa kiwanda hicho
walipeleka maombi ya kutaka kupewa vibali
vya kazi.
 
Uwepo wa idad ya zaidi ya watu 360 kufanya kazi kwenye kampuny hiyo ni ishara tosha kuwa kampuni hiyo inawanufaisha watu wachache (vigogo) na s watanzania. Hivyo serikali ya JPM iichunguze uozo uliopo huko tujue JK kafanya nin!?
mkuu mbona tunalishupalia sana swala la DANGOTE, kuna mbona hatuulizi tanga , cement, IPP mbona watu wamelalamika sana hapa kuwepo kwa idadi kubwa ya wahindi kwenye cola jobs , huku wazawa wakiambulia vibarua tu .tena kwa ujira kiduchu hilo mbona hatulisemi
 
Ni vyema ukaazisha mada nyingine kujadili hayo mambo!Swala tunalo lijadili hapa ni swala la Dandoge na linapewa umuhimu hapa kwakuwa ndio kwanza uwekezaji unaanza kwa hiyo ni vyema watu wakawai mapema kabla ya kuchelewa....
 
mkuu mbona tunalishupalia sana swala la DANGOTE, kuna mbona hatuulizi tanga , cement, IPP mbona watu wamelalamika sana hapa kuwepo kwa idadi kubwa ya wahindi kwenye cola jobs , huku wazawa wakiambulia vibarua tu .tena kwa ujira kiduchu hilo mbona hatulisemi
Hivi wewe unaona unacho kiandika? kwa hiyo unataka waache kushupalia kwakuwa kuna wengine wanafanya makosa yanayo fanywa na uongozi wa Dangote?
 
Uwepo wa idad ya zaidi ya watu 360 kufanya kazi kwenye kampuny hiyo ni ishara tosha kuwa kampuni hiyo inawanufaisha watu wachache (vigogo) na s watanzania. Hivyo serikali ya JPM iichunguze uozo uliopo huko tujue JK kafanya nin!?
Haya makosa yanafanywa na watendaji wa serikali tena wachini kabisa maana hiki kiwanda kina msimamizi kutoka serikali na hata afisa rasilimali watu sasa kama haya kweli yanatokea hawa wanapaswa kuwajibika!

Tena tujiulize serikali ya mkoa wa mtwara ndio imekuwa karibu sana na kiwanda hiki ina maana hawafahamu haya?

Muda mwingine serikali ikihamua kufukuza watu kazi watu wanaanza kusema ooooh ni visasi na uonevu sasa angalieni haya.....
 
Wageni wote waondoke nadhani kuna haja ya kuitosha maandamano juu ya hili...hata kwenye mahotel nako waondoke...
Sio swala la wageni kuondoka hapa kinacho paswa kuangali ni kama uwepo wao una ulazima au tija kwa watanzania na kiwanda husika! Kama wanafanya kazi ambazo watanzania wanaweza kufanya na wapo wengi basi sheria bila shaka hiko wazi...
 
pale dangote kuna jipu kubwa linaitwa UCC (unique consulting). hao ndiyo wamepewa tenda ya kuajiri kwa niaba ya dangote. asee, utawaonea huruma vijana walioajiriwa pale. tatizo ni kwamba watu walikuwa na matumaini makubwa sana, na siasa zilizopitiliza!
Ninacho jiuliza ina maana watendaji pale mkoani mtwara hawafahu haya mpaka serikali ije au waziri aingilie hili swala?
 
Dangote Muundo wake kama kiajira ni shida kwa wazawa.Wizara ya kazi bado ina nafasi ya kurekebisha tofauti hizo
Hapa umenena ni vyema wizara ikaliangalia swala hili mapema maana wana nafasi hiyo!
Bado najiuliza serikali ya mkoa wa mtwara inafanya kazi gani hadi haya yanatoke? walishindwa kusimamia? Bila shaka kuna watu wanapaswa kuwajibika!
 
Kuna tatizo kubwa sana na jinsi mambo yalivyoenda awamu ya nne. Kila kitu kina walakini! Kwanini? Haiwezekani wakasema cement itauzwa bei ya chini kama kodi zote zitafuatwa inavyotakiwa...tofauti itakuwa ya kawaida na siyo ile ya mbingu na nchi.

Ngoja tuone ila kama hata kufuata sheria ni tatizo basi kuna matatizo mengi yatakayokuja.
 
Back
Top Bottom