Uwekezaji huu wa Dangote uangaliwe upya

MTANGANYIKA M

Member
Mar 19, 2014
8
19
Watanzaia wengi na hata nchi jirani mtakuwa mmewahi kusikia pambio za sifa kutoka kwa wanasiasa na uongozi wa awamu ya nne, hasa wa kutoka mrengo wangu wa kulia, juu ya uwekezaji wa kiwanda cha saruji cha tajiri namba moja wa Afrika, Mnigeria Aliko Dangote mkoani mtwara. Binafsi niliposikia baadhi ya wanasiasa na hasa mkuu wa kaya enzi hizo akiimba na kusifu ujenzi wa kiwanda hicho cha saruji, nilitaka kuingia kwenye mtego wa kuwaamini watu wa mrengo wangu wa kisiasa, hususani tulipoambiwa kwamba kiwanda hicho kikikamilika kitaweza kutoa ajira takribani elfu kumi 10,000 kwa watanzania. Nilishituka sana, lakini kwa akili ya haraka haraka nikajiongeza kufikiri kwamba aaah hiyo idadi si inajuisha wafagiaji wa magodown ya mawakala watakaokuwa pale wilayani kwetu kasulu? Nikajiongeza kuvuta kumbukumbu ya ahadi ya ajira millioni moja kwa vijana iliyotolewa mwaka 2005, na hatimaye majibu yaliyotolewa baadaye kwenye hotuba ya mwanasiasa namba moja mwaka 2010 wakati akiomba ridhaa tena ndipo nilipofunguka akili zaidi na kuona katika fikra, binamu yangu ambaye aliishia darasa la saba akibeba mfuko wa saruji kumpelekea mnunuzi nyumbani kwake nikajua tayari nayeye amejumuishwa kwenye idadi ya ajira elfu kumi. Hilo halikunisumbua sana, nilijua siasa inafanya kazi yake ingawa niliamini kwa sehemu kwamba uwekezaji huo utatunufaisha watanzania kwa kutoa ajira na hata kujenga uwezo wa kiteknolojia na uzoefu kwa wale watakaopata fursa ya kufanya kazi na uwekezaji huo.

Mwishoni mwa mwaka jana 2015 nilipata neema ya mwenyezi Mungu ya kusogea karibu na uwekezaji huo. Kabla sijaanza kuchunguza namna Watanzania hasa wananchi wa Mtwara wanavyonufaika na uwekezaji huu, nilipigwa na butwaa kwa mwenendo ambao sikuuelewa uliohusu ukaribu wa mkuu wa kaya na wanasiasa wake wateule na waandamizi kwa mradi huu. Mara kwa mara niliona magari ya serikali na wakuu mbalimbali wakipishana kwenye geti la mradi kana kwamba ndio mahali pao pa kazi ( ikulu Fulani hivi). Kwakweli naamini msisimko wa jamii uliotokana na kelele za kisiasa kuhusu mradi huu, ulichangia mabadiliko makubwa kiuchumi, ikiwa ni pamoja na kupanda kwa gharama za maisha hususani nyumba, mavazi na maeneo ya kufanyia biashara kusiko na ulazima matokeo yake maumivu yameegemea kwa maskini wa hali ya chini.

Kilichonisukuma kuandika Makala hii, si kutaka kukosoa uhusika wa mrengo wowote wa kisiasa katika mchakato wa uanzishwaji wa mradi huu, wala si usaliti kama ambavyo tumezoea kuambiwa huko nyuma sisi watu wenye mawazo huru ndani ya taasisi zetu za kisiasa, katika hili nalazimika kuamini katika usemi wa kila zama na kitabu chake, kwa sababu hata nikisema kwamba, kwa udhaifu wa uwekezaji huu ambao nitauzungumzia hapa chini waliohusika kutufikisha hapa hawachomoi, wao watakuja na majibu ya mzaha na matusi bila kujali hadhira, umri na nafasi zao kwamba ‘’aaaah sijachomeka popote bwana!’’.

Katika kichwa cha habari nimeomba uwekezaji huu uangaliwe kwa sababu ya mienendo inayondelea katika kiwanda hiki ambapo bila serikali kuingilia kati nchi yetu itaendeleaa kudharaulika na kuwa shamba la bibi miaka yote, na pia watanzania wataendelea kutawaliwa na wakoloni wa ki Assia wakati serikali ikichangia uangamizaji wa taifa kwa kutetea na kuaminisha watu kwamba huu uwekezaji una tija kwa taifa. Mathalani, nitazungumzia maeneo makuu manne yenye msukumo muhimu ambayo ni, nafasi za ajira, masrahi, unyanyasaji na usalama kazini kwa watanzania.

NAFASI ZA AJIRA.

Katika idara takribani kumi na mbili ambazo ni: Rasilimali watu, Manunuzi, stores, usafirishaji, Fedha, Mechanical, Electrical, Uchakataji, Instrumentation, uchimbaji(mines), ulinzi na karakana, ni idara mbili tu kati ya hizo ndio zinaongozwa na watanzania ambazo ni idara ya Ulinzi na Rasilimali watu, ambapo hata hivyo hii ya rasilimali watu inaongozwa na Mzee mmoja ambaye hana tofauti na raia wa Assia kwa uongo, Rushwa na ujanja ujanja. Pia katika idara zote hizo unaweza kukuta wasaidizi mpaka wa nafasi ya nne kushuka chini ni wahindi, maana yake ni kwamba kila idara inaongozwa na wahindi kwa mtiririko hadi wanapoisha ndipo Mtanzania anafuata. Kitu cha ajabu ni kwamba, hawa wahindi katika idara unaweza kumkuta mmoja tu mwenye taaluma husika, wengine ni ndugu zao tu ambao hawana vigezo, kuna watu pale wametoka India wamekuja kutunza kumbukumbu za motor reading na data entry ambazo hata mtu aliyepitia veta mtanzania anaweza kuzifanya kwa ufasaha kabisa, hawa wanajumuishwa na kuitwa wataalam (experts) pindi afisa wa kazi anapokwenda kukagua. Sitaki kuzungumzia sana vibali vyao maana nasikia pale TIC ukienda unatoa hela tu unapewa, nashukuru sasa kazi hiyo imerudi kwa mamlaka moja . Wapo watanzania wenzetu kama yule mzee anayejiita senior HR na mwenzake mwarabu, wanaotumika kuwapa mbinu na kuwaficha hawa wahamiaji haramu wa kihindi kwa malipo.

Katika kiwanda hiki huwezi kupata Mtanzania mwenye uzoefu au mhandisi mwenye uzoefu, na wao hawadhubutu kuajiri watanzania wa namna hiyo maana hizo ni nafasi za wahindi, hata wakitangaza nafasi hizo wanaweka vigezo ambavyo viko India tu (mfano mtu awe na uzoefu wa miaka kumi na tano kwenye kiwanda cha saruji) na hata ikitokea mtu amepatikana kutoka viwanda vingine vya saruji hapa Tanzania wanamwambia wampe mshahara ambao ni mdogo ambao hawezi kukubali ili kuonyesha kwamba watanzania hawataki kazi, mfano engineer ana uzoefu wa miaka kumi anaambiwa apewe laki tisa kwa mwezi,wakati alipotoka alikuwa anafanya kazi hizo hizo kwa ufasaha na analipwa vizuri. Hata hivyo, ajira zenyewe zimegubikwa na mazingira ya Rushwa na magumashi ya hali ya juu. mfano Zipo nafasi zimetangazwa wiki kama mbili zilizopita, ikiwemo nafasi ya stores manager, lakini kabla hata watu hawajaitwa kwenye usaili kuna mhindi kutoka India ameshaanza kazi wiki iliyopita kwenye nafasi hiyo.

Kiwanda kiliwachukua vijana wa kitanzania kutoka vyuoni (fresh graduates) wa uhandisi kwa ahadi ya kuwapeleka kwenye mafunzo kwa miezi sita katika nchi ya Nigeria, kwa kuwalipa posho kidogo, na baada ya hapo wakimaliza mwaka wataajiriwa kama wahandisi kiwandani vijana walihangaika kutafuta passports kwa kasi na kujiunga na kampuni ambapo baada ya kufika kiwandani zile posho zikageuka kuwa mishahara na safari ya mafunzo ikawa haipo tena zikaanza figisu figisu za kihindi nyingi, baada ya kelele nyingi wakaamua kuwachukua vijana hao wahandisi 20 kati ya 100 waliosemwa kwenye ripoti, kuwapeleka Nigeria kwenye kiwanda cha saruji kufanya kazi kwa miezi miwili na hiyo ndiyo ikawa imetoka, na hiyo habari ya mafunzo haipo tena hapo kiwandani na hata baada ya mafunzo hao ishirini waliohudhuria Nigeria hawashirikishwi hata kwenye mikutano ya kiufundi wao wanaagizwa kwenda kusimamia usafi na kurekodi data kwenye substatations.

Siku zote hapo kiwandani wahindi wanafanya kazi ya kuhakikisha watanzania hawajifunzi kitu ili mwisho waonyeshe kwamba watanzania hawawezi, nilishangaa sana kuona kwamba hata wachina walioko kiwandani kwa ajili ya kuendesha kiwanda kwa guarantee ya miaka miwili hawaruhusiwi kuwafundisha Watanzania, wanazuiliwa na wasimamizi wa mradi ambao ni wahindi.

Najiuliza, nini faida ya uwekezaji huu katika taifa, maana mwekezaji amepewa maeneo ya kuwekeza bure, mpaka eneo la kujenga bandari amepewa bure kwa kushirikiana na seriakli iliyokuwepo madarakani kurubuni wananchi kwa kuwaambia kwamba watafaidika na uwekezaji wa Dangote. Pia amepewa msamaha wa kodi kwa miaka mitano, ni nini fadhila yake kama haikuwa kuwaajiri na kuwajengea uwezo watanzania ? hatua gani zinachukuliwa na usalama wa taifa kuhusu hili? Naamini wapo pale, je wanapeleka taarifa hizi?

MASRAHI

Ni dhahiri kwamba mtanzania yeyote au hata mtu wa nje ya nchi akisikia mtu unafanya kazi kwa Dangote Tanzania, picha inayokuja kichwani kwa mtu huyo ni kwamba masrahi yako ni mazuri maana unafanya kazi na kampuni ambayo kwanza ni ya kimataifa na kwa sababu ya jina lenyewe basi ataamini kwamba uko vizuri tofauti na viwanda vingine vya ndani. Lakini mambo sivyo, yalivyo baada ya kufuatilia maisha na masrahi ya watu pale ninaamini kwamba huyu ndugu yetu mwafrika mwenzetu anapaswa kuitwa mafia, wafanyakazi wake wanalipwa ujira mdogo sana kiasi kwamba ni vigumu kuamini wakati mwingine kama wanafanya kazi kwa Dangote.

Lakini kubwa Zaidi ni tofauti kubwa iliyopo ya kimasrahi kati ya wahindi na watanzania, wahindi wote wamepewa usafiri, allowances nyingi na wanaishi hotelini muda wote kwa gharama ya kampuni, kila kitu na bima ya afya ya kiwango cha juu na mishahara yao hakuna mtanzania anayejua inalipwa kwenye akaunti zipi, lakini watanzania kila kitu wanafanya kwa shida, wanasafiri kwa kugombania daladala na kuning’inia kama maembe. Watu wanapewa bima ya afya AAR iliyoandikwa kwenye vikaratasi ya mwezi mmoja, hata hivyo wakienda hospitali hazikubaliwi. Mikataba inayotolewa ni mwaka mmoja mmoja kinyume na sheria ya Tanzania, Hakuna huduma yoyote ya motivation kwa mfanyakazi, hata maji ya kunywa unayapata kwa kuhonga rushwa ya salamu kwa mhindi, akijisikia anazuia watu kunywa maji. Watu wanakula kwenye vibanda vya mama ntilie mazingira amabyo si salama kabisa, ukipita Dangote barabani mchana unaweza kuona kundi kubwa la watu kwenye vibanda umiza kwa akina mama ntilie ukafikiri labda hao ni vibarua kumbe kuna maafisa rasilimali watu, fedha, manunuzi na wahandisi ndani ya vibanda hivyo wakati wahindi wana wapishi wao maalumu wanaowapikia nyumbani kwao na kuwaletea huduma kazini kwa gharama ya kampuni.

Wapo madereva kama mia tatu walifanyiwa usahili, kwa ajili ya kuendesha malori ya saruji, tena walikuwa wanaitwa baada ya kutoa rushwa, na baada usaili walipoambiwa mshahara hakuna hata mtu mmoja aliyebaki, wote waliondoka na kampuni ikaajiri wakala mwingine mhindi mtanzania anayeleta madereva vibarua pale kazi inapojitokeza.

Tujiulize, huu ndio uwekezaji tunaoruhusu uje kuuwa viwanda vingine vya saruji vinavyoa ajira zenye tija kwa watanzania?

UNYANYASAJI

Katika hili watanzania wanapata shida sana kwenye kiwanda hiki, watu wanaishi kama watumwa, si ajabu sana kuona Mtanzania mfanyakazi wa hali ya chini mfano wafanya usafi wakifukuzwa kazi kwa kosa la kucheka, mikataba yao wengi ni ya mwezi mmoja mmoja na hawalipwi kwa muda wakidai wanafukuzwa wanaletwa wengine, si watanzania wana shida?

Wapo vijana wanafukuzwa kazini bila sababu za msingi nilishangaa sana hivi majuzi niliposikia mtu(operator) amefukuzwa kazi na bosi wake mhindi anayeitwa Mr. Manoj kwa kupata pancha ya tairi eneo la mining, wakati huo ikiwa hakuna afisa usalama alieajiriwa ambaye ndio mwenye mamlaka ya kuthibitisha kosa hilo kuwa la maksudi au la, na mwingine ameitwa na huyo mhindi akamuangalia kwa kuwa anafuga ndevu akasema wewe unafanana na alshabaab sikutaki kazini na akamfukuza kazi, vilevile hata ukifukuzwa hupewi barua wakiishakupa taarifa kwa maneno tu ukiendelea kubaki kazini unapoteza muda maana mshahara hutauona. Hapo Kiwandani kila mhindi bila kujali nafasi yake ni bosi popote alipo kwa mtanzania hata kama mtanzania anamzidi elimu, wahindi hapo wana living certificates za sekondari,wengine mafundi Umeme wa grade ya chini kabisa hawajui chochote lakini wanaitwa wataalamu na wanaambiwa wasimamie wahandisi watanzania wenye shahada. Mhindi huyo Akisema yeye hakutaki HR anasema ndiyo bosi na anakufuta kwenye payroll haraka.


Yapo mambo mengi sana ambayo ukiyatazama hautofautishi na mahusiano kati ya mabwana na watumwa ambayo tuliyasoma katika vitabu vya historia zamani tukiwa mashuleni, wakati najiuliza haya nilipata kuzungumza na vijana waliokwenda Nigeria kufanya kazi kwenye kiwanda cha Dangote OBAJANA kilichopo Lagos. Kule wafanyakzi wahindi ni karibu asilimia themanini na wazawa ni kama ishirini tu ,Wahindi wanapewa upendeleo sana kwa sababu wakuu wa kampuni ni wahindi, ndhani hayo ndiyo mambo ambayo mkuu wetu wa kaya awamu ya nne alikuwa analenga yafanyike hapa kwetu hii ndiyo sababu mpaka sasa hawa wahindi hawaamini kwamba wako wachache sana hapa Dangote ya Tanzania hivyo wanataka kuonyesha watanzania hawawezi ili waletwe wengi.

USALAMA KAZINI

Mazingira ya kazi ni magumu sana kwa kuwa ndugu zetu hawa nadhani kwa sababu ya kubana matumizi hawataki kabisa kusikia kwamba kuwekeza katika usalama kazini ni jambo muhimu, vifaa vya kazi (PPEs) wanavyotumia wafanyakazi wa Dangote ukiwaangalia ni kofia tu na viatu ndivyo vinazofanana maana vifaa vingine unajinunulia mwenyewe ukiona vina umuhimu kwako, hata viatu tu ubora wake si wa kudumu miezi mitatu au mitano lakini unaambiwa ukae navyo mwaka mzima. Hakuna alama za tahadhari ya usalama kiwandani, magari yanaendeshwa kwa spidi inayofurahisha madereva na kila kitu kwenye usalama ni cha hovyo hovyo, wahindi wana dharau sana wakiambiwa kuhusu usalama wanawaambia watu waondoke waende wakafanye kazi maeneo salama kwenye viwanda vingine Tanzania, hii yote ni kujaribu kuonyesha kwamba watanzania hawako tayari kufanya kazi. Hakuna maafisa usalama wala mtaalamu wa mazingira hapo, kila kitu kinaendeshwa kienyeji kwa utaratibu wa India.

Nimeandika waraka huu nikiwa na masikitiko makubwa sana kama mtanzania wa kawaida, najua serikali yetu ya awamu ya tano imeanza kushughulikia matatizo haya kwa kasi nzuri, naiunga mkono seriklai na kuipongeza kwa hatua iliyofikia, kwa hapa tulipofikia na kwa jinsi tunavyoendelea nashawishika kuamini kwamba tunaelekea kupata heshima kama binadamu wenye taifa lao. Naiomba serikali iendelee kufanya operations za kuwarudisha hawa wahamiaji haramu makwao, najua ni wabishi sana na wengi wao wanaamini kwamba serikali ya Tanzania haijawahi kuwa na haitakuwa serious kiasi hicho ndiyo maana wengi wanaonekana kugoma goma na kuokuwa na mpango wakuondoka.

Ninamini, watanzania wana uwezo mkubwa wa kufanya mambo makubwa na kuleta maendeleo katika nchi yetu, iwapo taifa likiwekeza katika kuwaendeleza wasomi tulionao, hakuna taifa lililoendelea kwa kutegemea kuendelezwa na watu wa mataifa mengine kama viongozi wavivu wa kufikiri walivyoamini, Serikali iliyopita ililewa madaraka na kuamini katika uzembe, ukarimu wa kijinga pamoja na wizi wa ujanja ujanja, hakuna taifa linaloendelea kwa kujenga msingi wa maendeleo yake katika wizi na ujanja ujanja na matanuzi. Lazima tukubali kuanza kuumia ili kujenga taifa lenye heshima, leo hii ukienda kutafuta Mtanzania anayefanya kazi India humpati, kwanza nani atamruhusu, nenda Kenya, Rwanda na China kama utakuta mtanzania anakalia nafasi ya wazawa, lakini kwetu hapa limekuwa shamba la bibi na sisi tunalia hakuna ajira hata pale tunapopata ajira tunakuwa chini ya raia wa nchi nyingine na tunachekelea tu, Hatuwezi kuwa taifa lenye watu wenye akili timamu tukakubaliana na haya.
 
wahusika tafadhali mliangalie hili ukweli wake, kwa uwing wa wahind hata mimi nathibitisha niliishafanya interview pale, wizara ya kazi muda wa kulala umeisha tunaomba msiwe kama yule mama kabaka sasa hivi muwabane wawekezaji watoto wa kitanzania wapate kazi
 
pale dangote kuna jipu kubwa linaitwa UCC (unique consulting). hao ndiyo wamepewa tenda ya kuajiri kwa niaba ya dangote. asee, utawaonea huruma vijana walioajiriwa pale. tatizo ni kwamba watu walikuwa na matumaini makubwa sana, na siasa zilizopitiliza!
 
Presidential Commendations

Nigeria’s President, Muhammadu Buhari and his Tanzanian counterpart, Dr. Jakaya Mrisho Kikwete commended Dangote for the investment, which is the largest private investment so far made in Tanzania.

According to Kikwete, there was no better way of rejuvenating and sustaining a nation’s economy if not through investment sustain which opens the door of for job creation and opportunity for people to express their creative abilities.

He described the 3 mtpa cement plant as the largest cement plant in the Eastern and Central Africa, noting that the investment is a huge one that would have a huge impact as well as bilateral relation between Tanzania and Nigeria.

Kikwete pointed that the timing of the citing of the cement plant was very auspicious, coming at a time when the demand for cement is on the upsurge and increasing both locally and regionally.

The President disclosed that cement price has been on the increase because of the shortages in supply as opposed to increasing demands, saying Dangote Cement is coming to fill the gap.

On his own part, Buhari, who was represented by the Kaduna State Governor, Mallam Nasir El-Rufai said Dangote is a key role player in the economic development of Africa and his investment model is in tandem with the unfolding economic policy of his government.

He said Dangote by his investment is teaching Africa nations the need to adopt an economic integration policy which will encourage Africans to invest in their continent rather than waiting endlessly for the elusive foreigners to come and help invest and develop Africa.

Buhari pointed out that Dangote has proved a point that though there could be challenges but there are huge returns for African investment in Africa.

“Others should emulate him and partner the government the onerous task of job creation. As our son, we are proud of Dangote. Nigeria is very proud of him,” Buhari said.

Speaking at the inauguration of Tanzanian cement plant, Dangote explained the choice of Tanzania for investment, stating that the existing supply gap had been inadequate in meeting local demands, noting the need to boost export supply in the eastern Africa regional bloc.

“The construction sector is a major emergent component of the Tanzanian economy that has been receiving the attention of investors. This makes it an ideal market for cement production. The existing cement manufacturers have historically been unable to satisfy local demand, which has been filled by imports. As essential economy-driven infrastructure continues to be built to improve electricity supply and the transport network, additional demand for cement can be expected,” he said.

Dangote added that the investment will certainly contribute to Tanzania’s on-going story of infrastructure development, job creation, and broad economic development. (mtizamo wangu ''Bagamoyo'' naongeza maneno yangu hapa a.k.a BRN - MATOKEO MAKUBWA SASA siyo ajira zitakazopatikana Dangote Cement Mtwara tu bali tutizame hata ajira zitakazojitokeza ktk sekta za ujenzi n.k yaani ''nje ya box'' tusijibane kuangalia ni ajira ngapi pekee zinapatikana ndani ya fensi ya kiwanda cha Dangote Cement Mtwara. )

READ MORE: http://www.thisdaylive.com/articles/dangote-cement-consolidates-with-600m-tanzania-plant/223932/
 
Sehemu yoyote Ukiona Wahindi andika maumivu, , Wahindi wawe wa kwanza kufukuzwa nchini tena wahindi waliokuja miaka ya 2000s wanawanyanyasa sana watanzania sanaaaa na hivi watanzania hawawez hata ku shout basi ndo holaaa
 
Wahindi tena!ni bora kiwanda kifungwe,kama wahind wapo hapo,wahind wanyanyasaj mno
 
Dangote Muundo wake kama kiajira ni shida kwa wazawa.Wizara ya kazi bado ina nafasi ya kurekebisha tofauti hizo
 
Sasa hayo ni ya kuangalia upya uwekezaji huu au serikali ihakikishe sheria za kazi zinafuatwa?
 
Last edited by a moderator:
Ajira Tanzania imekuwa ni shida sana. Siyo wahindi tu, watu wanaajiri hadi kwa kujuana kwa makabila. Ati unalizwa na mswahili mwenzio wewe ni kabila flani vile, ukijibu hapana, utasikia sasa utaitwa, ndiyo imetoka hiyo.

Unakuta ofisi nzima wanaongea lugha ya kabila moja.

Kwa wahindi ni kweli wamejazana sana kizembe zembe tu hapa. Hawajui chochote, kazi zote wanafanya wazawa ila mishahara mikubwa wanapokea wao. Nishawahi kuwa na Technical appointment na muhindi mmoja.. dah yani yule mswali aliyekuja nae ndiyo anafanya kila kitu na kutoa majibu sahihi, yule muhindi anayejiita boss, hajui chochote yupo yupo tu.
 
Wageni wote waondoke nadhani kuna haja ya kuitosha maandamano juu ya hili...hata kwenye mahotel nako waondoke...
 
Watanzani wenyewe kwa wenyewe tunasalitiana hii habari imeniuma tofauti na tulivyo haminishwa na viongozi matalajio ya kiwanda wahusika wachukue hatua Kali mkoa kwa mkoa kuchunguza mwenendo Wa wawekezaji una maslai kwa taifa na wananchi.chunguzeni hajira za wageni
 
Pale mahala ni shida, ukifika pale mahali ndio utaona tatizo la watendaji wa serikali ya kitanzania na mamlaka zake, sijaona pale kiwandani mahala ambapo mtanzania atajifunza, pili wapo watanzania wengi wenye uwezo wa kufit hasa kwenye kada ya Engineering,logistics,procurement nk,, KAMA KUNA WAZIRI ANASOMA HAPA ANIPM NITAMLETEA HATA WATU 1000 WANAOFIT BILA SHAKA PALE KIWANDANI KWENYE TAALUMA AMBAZO NI VERY PROFFESIONAL, ukweli ni kwamba watanzania hatupendi, mamlaka za mkoa wa mtwara zilitosha sana kulisimamia hili linalozungumzwa, 80% ya wahindi walikuwa pale kiwandani sio speacial kiasi cha watanzania kukosa kazi, KAMA KUNA MH YUPO HAPA TWENDE MIMI na yeye tukawafanyie interview wale wahindi pale engineering na watu 1000 nitakaoleta mimi halafu tuone nani anadeserve, UPUMBAVU,UJINGA,UJUAJI NA UFALA wa baadhi ya viongozi waliopewa mamlaka kwenye taifa hili umeleta matatizo makubwa sana kwa jamii hii, suala dangote cement liko kabisa kwenye uwezo wa mamlaka ndogo kabisa za mtwara pale, kuna hawa watu serikali ikawaangalia na iwapime kama kweli tanzania hatuna watu hao, mfano, MINING MANAGER - BW MANOJI, wapo mining engineers wengi sana tanzania hapa huko kwenye migodi wana explosure,experience,na wanafanya vizuri kiasi cha wengine kupata kazi nje ya nchi mfano, Mali,Congo,Guinea,Eritrea,Burkina faso,Australia,Ghana nk, Mbeya cement,tanga cement na twiga cement mbona hiki cheo kiko kwa waswahili tu watanzania, kule migodini, N/MARA,GEITA GOLD, BUZWAGI nk ambao wanakazi kubwa mara 100 ya hawa mbona hivi vyeo wako watanzania????
KUNA HUYU WORKSHOP MANAGER - ANAITWA MR PRASAD,, yaani ni kichekesho kiukweli, mamlaka ziko wapi? Kama huyu anakuja kuwa workshop manager hapa, workshop manager hakuna tanzania?? Project ile ni ndogo sana ukifananisha mining area kama shanta mining, geita gold,north mara, buzwagi nk ambapo kazi ni kubwa mara 1000 na mashine ni kubwa na nyingi mara 300, lakini hii position inashikiliwa na wabongo au mzungu mwenye experience akikaimiwa na mtanzania na kweli kwa mzungu unakuta kuna cha kujifunza mara wanaexperience na explosure in mining, kwa huyu PRASSAD hakuna chakujifunza aisee maana hata mwenyewe naye ni kama mwanafunzi kwenye hiyo nafasi hapo alipo,, kuna hawa watu pia mpaka inasikitisha NALAN, SANTOSH, nk yaani ni kichekesho aisee...
SERIKALI IKO WAPI,MAMLAKA ZIKO WAPI??? PALE DANGOTE CEMENT KUNA SHIDA JAMANI, watanzania tubadirike sasa jamani kunusuru taifa letu..
 
Ukitaka kujua hawa watu uwezo wao ni mdogo kwenye hizo kazi, nenda tu pale kaangalie issue ya safety kwa kiwanda kikubwa na modern kama kile, safety ni first priority kwenye eneo kama lile lakini utakachokuta pale ni tatizo aisee,,sijui hata kama OSHA wanaendaga kutembelea pale,, Mamlaka za kitanzania zinahaja ya kusimamia hawa watu aisee ili watanzania aka wazawa wapate haki yao kama ambavyo wahindi wanapata haki yao India, mshahara wa operator pale ni kichekesho, operator anayeendesha mashine ya zaidi ya millioni 400 mpaka bil 1 analipwa take home 400000/=???? Kuna haja ya wahusika kufanya researches ya mishahara kwa kada mbalimbali kulingana na risk ya taaluma husika na uthamani wa kazi kulingana na faida apatayo mhusika, kuna haja pia kwa serikali kuacha kukumbatia wahindi na wachina na baadala yake turudi kwa Wazungu kama tuna nia ya dhati kwa watu wetu kujifunza teknolojia,, sioni kipya ambacho mtanzania atajifunza kwa wale wahindi pale dangote, wao wenye kukosa kwao explosure kunawafanya waishi kama sisi kiteknolojia kwa maana ya poor method or local method in solving the problem, Yule WORKSHOP MANAGER MFANO PALE ATAMFUNDISHA NINI MTANZANIA??? hebu taasisi husika mjifunze namna ya kutatua haya matatizo, inakuaje unatoa kibali kwa watu kama hawa??? muende mkawahoji vijana waliopo pale mtajua pakuanzia, fanyeni upembuzi yakinifu kwenye international companies tofauti muone watanzania walivyoshikilia nyadhifa kubwa na kuperform to the same nature of job but in big mining industries, mkajifunze pale geita gold kwa nini watanzania ni managers,superitendent,supervisors,team leaders, pale buzwagi na north mara tena kazi ni kubwa na more modern kuliko hapo dangote cement, tujifunze kwa nini imewezekana?? na kwanini watanzania wanafanya, mbinu zipi zimetumika?? ..
tuache ubinafsi hili ni taifa na linahitaji kusonga mbele kwa nguvu ya watanzania wote,,
 
Dawa ni moja, wizara ya uhamiaji na ajira, waende pale, wanakagua department to department, najua watakuwa wamejificha au wahindi wamekimbia kwani wanapata taarifa kuwa wakaguzi wanakuja. Kitakachofanya ni kwenda pale na mnakaa na mkurugenzi na HR mnaanza kufanya usahili upya. Yaani uhamiaji na maafisa wa wizara ya ajira waende pale wakae week mbili, waweke help desk yao pale, wakisaidiana na mkurugenzi na HR waanze wao wenyewe kuajiri upya, kazi isimame for two weeks. Baada ya hapo kazi iendelee. Kingine nahsauri wizara ya kazi na uhamiaji hata baada ya kazi kuendelea wasitoke hapo kwenye help desk wakae hadi baada ya miezi sita. Baada ya kuajili, wakikaa pale miezi sita wakikagua kila mfanya kazi anae ingia wana note down kitambulisho chake, hati yake ya kazi, uraia na nk. Hao wageni wote watakimbia, its very simple. Lakini hii wanakwenda kugagua mara moja then wanarudi, hao watu wanataarifa wanazipata kutoka kwa watu wasio waaminifu. Mie nashauri serikali ifanye hivyo. Waende pale wafungue help desk au office ndogo ya watu wa uhamiaji na ajira, ma office kama kumi , watano uhamiaji na watano wizara ya ajira, waanze usaili upya, na hata kumaliza usaili wakae pale miezi sita .
 
Hapa yafanyike kam ya southafrica ndo wataondoka wenyewe ki serikali kicorrupt hiki hakiwezi kitu
 
Mme sahau pia hawa hawa wanaojifanya wazao sana ndo wamejaza wahindi kila kona ,mfano MENGI bonite yote kazi nzur wahindi ndo wameshikilia ,wazawa wao ni vibarua kwa 4000 kwa siku
 
Nimesoma waraka huu nimejikuta nikipandwa na gadhabu natamani akatize mhindi hapa mbele yangu!!! Lakini Watanzania kuna mahali tulikosea kwa hiyo tukitaka kurekebisha mahali hapo basi tukubali kulaumiwa.'Ooh sisi watanzania ni watu wapole' huu ukarimu wetu wa kipuuzi ndo umesababisha yote haya ndio maana nchi yetu imekua shamba la bibi. Nimewahi kwenda Kenya,Uganda na Rwanda kutafuta kazi aiseee hao watu achana nao hawataki kusikia mgeni kabisa.
 
Back
Top Bottom