Uwanja wa ndege wa DSM(JNIA) washushwa viwango vya ubora kimataifa,Waziri Mbarawa chukua hatua upesi | Page 4 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uwanja wa ndege wa DSM(JNIA) washushwa viwango vya ubora kimataifa,Waziri Mbarawa chukua hatua upesi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by barafu, May 19, 2017.

 1. barafu

  barafu JF-Expert Member

  #1
  May 19, 2017
  Joined: Apr 28, 2013
  Messages: 6,256
  Likes Received: 25,326
  Trophy Points: 280
  image.jpeg

  Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga(Interantional Civil Aviation Organization-ICAO) ambaye ndio mratibu na muongozaji wa ubora na sheria (standards and regulations) za usafiri wa anga duniani,ambapo Tanzania ni mwanachama,siku kadhaa zilizopita limeushusha viwango (downgraded) uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere baada ya kushindwa kukidhi vigezo vya ubora (standards) vinavyohitajika kimataifa.

  ICAO imeushusha uwanja wa JNIA kwa "Category" mbili chini,yaani kutoka kiwango cha kimataifa cha "Category 9" mpaka kuwa "Category 7".Hii ni aibu kwa serikali na wale waliopewa kusimamia dhamana ya kusimamia ubora wa viwanja Tanzania ambao ni Tanzania Airports Authority.

  Hii "Category" ni nini?

  Kwa mujibu wa ICAO,viwanja vya ndege vyote vimewekwa katika " Aerodrome category" kulingana na ubora wake.Kuna "category 1" mpaka "Category 10".Category 10 ni kiwango cha juu kabisa cha ubora wa kiwanja,hivyo ndege zote kubwa,za kati na zile ndege ndogo, zinaweza kutua kwenye uwanja wenye hadhi hiyo.

  Kwa muda mrefu uwanja wa Dsm,licha ya changamoto zake,ulidumu katika "Category 9" hivyo kuwa nafasi moja kufikia "Category 10" ambayo ndio ubora wa juu wa viwanja duniani.Uzembe,urafi na uwajibikaji mbovu umesababisha kwa siku kadhaa uwanja kuwa "downgraded" hadi kufikia "category 7".

  ICAO hutoa category hizi kulingana na ubora wa uwanja katika mambo mengi,ikiwa ni pamoja na uwezo wa uwanja kuwa na miundombinu ya kupokea ndege za aina tofautitofauti,kuanzia ndege ndogo aina ya ATR-72 mpaka ile Airbus 380 iliyo kubwa zaidi.


  Pia ICAO,hutoa ubora huu kulingana na ugumu wa mazingira ya uwanja kwa ndege kutua.Kuna viwanja vilivyojengwa sehemu yenye tambarare,runway nzuri,hali ya hewa salama na vifaa vya kisasa vya kuongozea ndege,wakati vingine vimejengwa mazingira mabovu,runway fupi,eneo lenye ukungu kila mara,mvua mwaka mzima,barafu na milima na mabonde.

  Kipimo kingine KIKUBWA (kwa umuhimu wa pekee) ni uwezo wa idara ya zima moto yaani Rescue and Fire Fighting Services (RFFS).Zimamoto ndio "roho" ya kiwanja popote duniani.Uwanja usio na zimamoto ya uhakika,basi ndege nyingi na mashirika mengi huondoa safari za ndege zao kwa kuogopa kuwa na usalama mdogo wa ndege zao na abiria wao.Hii ni sababu katika nchi nyingi,mamlaka za viwanja vya ndege huwekeza kwa kiasi kikubwa sana katika idara ya zimamoto.Hapo JNIA,hili limekuwa ni tatizo na hivyo kulazimu ICAO kuushusha viwango uwanja wetu kwa kukosa magari ya zimamoto yenye viwango vya kukidhi hadhi ya "category 9"

  ICAO kupitia Annex 14,Volume 1 (Aerodrome Design and Operations) inahitaji uwanja wa ndege wenye "category 9" uwe na magari ya kisasa ya zimamoto (Fire Tender) walau yapatayo matatu (3) au zaidi,yenye "performance level A" ya lita 36,400 za maji na lita 13,500 za foam.Kitu ambacho wakati wa ukaguzi wa ICAO (ambao hawahongeki),Uwanja wa JNIA umeshindwa kutimiza na hivyo "dunia kutangaziwa" kwa muda kuwa uwanja wa JNIA si bora tena kwa kiwango cha "Category 9".

  Unapoushusha uwanja wa JNIA toka Category 9 mpaka Category 7,na taarifa kuwekwa katika mfumo wa NOTAM (Notice to Airmen),ina maana NOTAM hiyo inasomwa dunia nzima,na hususani kwa mashirika yote makubwa kama KLM,Swiss International,Emirates,Turkish,Oman,Qatar,South Africa,Egypt nk ambayo ndege zake hutua uwanja wa Dsm.

  Hasara ya "downgrading" hiyo kutoka CAT9 to CAT7 ,ni kuwa baadhi ya mashirika ya ndege yanaweza kuanza kusita na kukosa imani ya kuleta aina fulani ya ndege kwa kuhofia kuwa na usalama mdogo wa ndege zao katika uwanja huu.Iwe kwa kuja na kuondoka(Quick Turn) au kwa kulala (Night Stop).Uwanja ukiwa Category 7 maana yake hauwezi kupokea ndege kubwa kama Boeing 787(Dreamliner),B777-200/300,B767,B747(Kama ile Airforce One ya US),Airbus340-500/600,A350 na A333-300.

  Na kwa hapo JNIA,mashirika makubwa kama Emirates huleta B777-200/300,Swiss International A333-300,KLM huleta B777-300 au A333-300.Hivyo jambo hili lina "impacts" kubwa tu katika uso wa usafiri wa anga kimataifa.Jambo hili lisiachwe juujuu tu,serikali ichukue hatua,Waziri husika achukue hatua juu ya management ya TAA bila kuweka aibu na upendeleo.Mwisho wa siku ataondoka yeye kwa kuwabeba watu na huruma zake za kipemba.

  Kwa habari sizizo na majungu ni kuwa Mamalaka ya Viwanja vya ndege,waliposikia wakaguzi wanakuja na hawawezi kuhongeka ili kupika report,waliamua kwenda kuazima gari kutoka uwanja wa KIA na kulileta Dsm usiku kwa usiku,na mkaguzi alipofika akakuta idara ya zimamoto ina gari lenye kufanya kazi kwa ubora.

  Naambiwa hata sasa pale Zimamoto waziri ukienda mapema utakuta gari la Zimamoto limeandikwa "K'njaro International Airport-Rescue and Fire Fighting Service".

  Baada ya ukaguzi,gari lile likarudishwa tena KIA,na bila kutarajia mkaguzi wa nje toka ICAO akarudi kesho yake kwa kustukiza na kukuta gari lile halipo.Hivyo bila hiyana akaamua kuushusha uwanja(downgraded) toka CAT9 mpaka CAT7,sababu aligundua udanganyifu uliofanyika.Maana baada ya ukaguzi walirudisha KIA,baada ya kutupwa CAT7 wamerifuata tena ili wapate tena vigezo vya kurudishwa CAT9.

  Ndugu yangu Prof Makame,hawa watakuponza,tulishakushauri uisafishe management yote pale uanze na mwanzo,mbona unawalea hawa watu?Hujui ipo siku watakuponza?Unajisikiaje chini ya uwaziri wako kiwanja kushushwa hata kwa week moja tu kutoka CAT9 mpaka CAT7 na bado watu wapo ofisini kuanzia kwa DG mpaka Mkurugenzi wa Kiwanja!?Nasikia unataka kumleta yule jamaa aliyekuwa meneja wa Kigoma,hivi huko juu huwa hakuna watu wenye mafaili ya hawa jamaa mkajua madudu yao!?Kama ni huyo,unategemea lipi jipya?

  Uzuri au ubaya,wengine huwa hatuandika majungu hapa,hatuna chuki na watu.Tunaeleza kile tunachokifahamu kwa lengo la kusaidia.Prof Mbarawa utakuwa shahidi kuwa yale yote niliyoyaleta uwe hapa au ofisini kwako kwa njia rasmi ya kimaandishi,ulituma team yako kuchunguza na ukakuta hakuna majungu wala fitna,bali ni ukweli tupu.

  Tena ukakutana na hata mengine makubwa ambayo kwa sbb za kimaadili humu hatuyaweki.Naomba hili la "CAT7" likupe picha ya watu unaofanya nao kazi.Chukua hatua ngumu ili umsaidie Rais na Taifa kwa ujumla.Usionee mtu,tenda kwa haki...Sisi tunakusaidia pa kuanzia,wewe malizia.Tunakusaidia sababu tunakupenda.Kama watu walisafirisha gari la fire usiku kwa usiku toka KIA ili tu kuja "kumpiga changa la macho" mkaguzi wa ICAO,wewe utakua umepigwa "machanga ya macho mara ngapi?"

  Leo naishia hapa,ntakukusanyia taarifa nikuletee...lengo ni kujenga na si kubomoa.Chukua hatua Ami Prof Mbarawa,hawa unaowaendekeza,watakuponza.Naambatanisha "NOTAM" ilyowekwa na kutolewa baada ya kuazima gari tena KIA ili kuziba aibu,ilikua kwenye website ya TCAA iliyoonyesha kushushwa kwa kiwanja toka CAT9 mpaka CAT7 sababu ya ubovu wa idara ya zimamoto.Haya si majungu,dunia nzima imeona.
   
 2. A

  Aleppo JF-Expert Member

  #61
  May 19, 2017
  Joined: Sep 13, 2013
  Messages: 2,593
  Likes Received: 3,213
  Trophy Points: 280
  Naona umekuwa Israel siyo bure mpaka unajua roho za watu zipoje
   
 3. A

  Aleppo JF-Expert Member

  #62
  May 19, 2017
  Joined: Sep 13, 2013
  Messages: 2,593
  Likes Received: 3,213
  Trophy Points: 280
  NIMEKUOLEWA MDAU
   
 4. M

  MC JF-Expert Member

  #63
  May 19, 2017
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 752
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 45
  Aibu !
  Nikiwa na jamaa zangu kutoka nchi nyingine, tunaposafiri safari ndefu na kutua hapa na pele tukiwa wenye furaha, aibu yangu ni pale tunapotangaziwa sasa tunatua katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa JNIA. Kwa jinsi Tanzania ilivyo nchi nzuri huwa wananiambia 'let's see the beauty of Tanzania'

  Kwa anayesema tunakosoa bila kushauri hajielewi kabisa, wajibu wetu tumetimiza kwa kulipa kodi na kuchagua viongozi, hao viongozi ni kazi yao kuufanya uwanja wetu wa Ndege uendane na hadhi ya nchi,
   
 5. Aisatu

  Aisatu JF-Expert Member

  #64
  May 19, 2017
  Joined: Dec 27, 2012
  Messages: 376
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 45
  Pia naunga mkono TAA imeoza kbs,management ya utawala ibadilishwe kbs kuna uozo mkubwa sana pale,kuna mwaka fulani waliwahi waita watu kufanya interview kwenye tangazo lao kiwango cha mshahara kilikuwa cha juu,kuja kusign mikataba wakasema eti tangazo lilikosewa kama ni watu makini kwan nin hawakuwambia watu mapema wakajijua?Tatizo ni umimi tuu ndo ulioja pale.
   
 6. m

  mwasu JF-Expert Member

  #65
  May 19, 2017
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 8,259
  Likes Received: 6,152
  Trophy Points: 280
  Mradi bombadier zitue hapo, hatuna haja na viwango vya kimataifa.
   
 7. Adharusi

  Adharusi JF-Expert Member

  #66
  May 19, 2017
  Joined: Jan 22, 2012
  Messages: 10,988
  Likes Received: 3,204
  Trophy Points: 280
  Ahsante sana brother barafu
   
 8. MAFILILI

  MAFILILI JF-Expert Member

  #67
  May 19, 2017
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 1,945
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  Mkurugenzi mkuu aliyeko hana uzoefu? ama tatizo lake nini?
   
 9. m

  mwasu JF-Expert Member

  #68
  May 19, 2017
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 8,259
  Likes Received: 6,152
  Trophy Points: 280
  Ana uzoefu sana ila anasubiri amri za utekelezaji kutoka juu..
   
 10. P

  Pythagoras JF-Expert Member

  #69
  May 19, 2017
  Joined: Feb 24, 2015
  Messages: 2,808
  Likes Received: 2,141
  Trophy Points: 280
  Awamu hii ya tano na bado...kila kukicha hata kilichokuwa kizuri kinakuwa kichafu sijui kuna nini awamu hii.....huu utawala nikama hauna baraka, maana jitihada zinaonekana kama.zinafanyika lakini matokeo ndio haya.
   
 11. barafu

  barafu JF-Expert Member

  #70
  May 19, 2017
  Joined: Apr 28, 2013
  Messages: 6,256
  Likes Received: 25,326
  Trophy Points: 280
  Here we Go!!
   
 12. P

  Pythagoras JF-Expert Member

  #71
  May 19, 2017
  Joined: Feb 24, 2015
  Messages: 2,808
  Likes Received: 2,141
  Trophy Points: 280
  Mimi nawaza tu hiyo speed ya gari la KIA usiku usiku...hahahaaa dereva wake alitamani liruke kama ndege kuja ku counter attack ujio wa ICAO
   
 13. barafu

  barafu JF-Expert Member

  #72
  May 19, 2017
  Joined: Apr 28, 2013
  Messages: 6,256
  Likes Received: 25,326
  Trophy Points: 280
  Bahati mbaya huwezi kuhonga watu wa ICAO
   
 14. MAFILILI

  MAFILILI JF-Expert Member

  #73
  May 19, 2017
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 1,945
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  Ametokea wapi kabla ya kupata cheo hiki? Kwa nini anasubiri amri kutoka juu, atakuwa hana uwezo huyo ama kabebwa tu!!
   
 15. m

  mwasu JF-Expert Member

  #74
  May 19, 2017
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 8,259
  Likes Received: 6,152
  Trophy Points: 280
  Mkuu ndie alie muweka hapo na ni yeye anaesema anajua nani akae wapi kwa wakati gani, na amri zisizokwisha lazima mapungufu yatokee..
   
 16. P

  Pythagoras JF-Expert Member

  #75
  May 19, 2017
  Joined: Feb 24, 2015
  Messages: 2,808
  Likes Received: 2,141
  Trophy Points: 280
  Niliingia siku moja nikakuta hakuna maji kuna tissue paper tu...niliboreka sana
   
 17. F

  Fais12 JF-Expert Member

  #76
  May 19, 2017
  Joined: Jan 31, 2017
  Messages: 274
  Likes Received: 167
  Trophy Points: 60
  Asante saana ndugu kwa taarifa.
  Ss wengine tunasikia habari ya terminal 3 kushindana na ya kenya, sasa kama kiwanja chenyewe kinashushwa grade kweli kitaweza kushindana na cha kenya.
   
 18. marejesho

  marejesho JF-Expert Member

  #77
  May 19, 2017
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 6,584
  Likes Received: 877
  Trophy Points: 280
  Kwa kweli wamechelewa kutoa hayo maamuzi. ..Viongozi wetu ndio wengi wanaongoza kwa kusafiri lakini hawajifunzi toka kwa wenzetu na kutamani kuiga vizuri.

  Embu sasa wahusike wachukulie hii kama changamoto muhimu sana ya kuwabadilisha ikibidi wavuke hata madaraja manne ya ushindi. ....

  Mabadiliko ni lazima
   
 19. P

  Pythagoras JF-Expert Member

  #78
  May 19, 2017
  Joined: Feb 24, 2015
  Messages: 2,808
  Likes Received: 2,141
  Trophy Points: 280
  Hahahaa hawahongeki wale sio waswahili
   
 20. samurai

  samurai JF-Expert Member

  #79
  May 19, 2017
  Joined: Oct 16, 2010
  Messages: 4,367
  Likes Received: 4,382
  Trophy Points: 280
  Kiukweli wakosoaji katika nchi hii ndio Wazalendo na wenye msaada kuliko haya majamaa yasiojielewa... kiukweli hata ukiwa angani tu ukaangalia mji kwa juu utajua unatua kwenye nchi ya namna gani..
   
 21. barafu

  barafu JF-Expert Member

  #80
  May 19, 2017
  Joined: Apr 28, 2013
  Messages: 6,256
  Likes Received: 25,326
  Trophy Points: 280
  Na kila mara wamekuwa wakisafiri kwenda nchi za watu!!Sijui huko huwa wanajifunza nini cha maana?ni aibu sana
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...