Uwanja wa ndege wa DSM(JNIA) washushwa viwango vya ubora kimataifa,Waziri Mbarawa chukua hatua upesi | Page 6 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uwanja wa ndege wa DSM(JNIA) washushwa viwango vya ubora kimataifa,Waziri Mbarawa chukua hatua upesi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by barafu, May 19, 2017.

 1. barafu

  barafu JF-Expert Member

  #1
  May 19, 2017
  Joined: Apr 28, 2013
  Messages: 6,256
  Likes Received: 25,331
  Trophy Points: 280
  image.jpeg

  Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga(Interantional Civil Aviation Organization-ICAO) ambaye ndio mratibu na muongozaji wa ubora na sheria (standards and regulations) za usafiri wa anga duniani,ambapo Tanzania ni mwanachama,siku kadhaa zilizopita limeushusha viwango (downgraded) uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere baada ya kushindwa kukidhi vigezo vya ubora (standards) vinavyohitajika kimataifa.

  ICAO imeushusha uwanja wa JNIA kwa "Category" mbili chini,yaani kutoka kiwango cha kimataifa cha "Category 9" mpaka kuwa "Category 7".Hii ni aibu kwa serikali na wale waliopewa kusimamia dhamana ya kusimamia ubora wa viwanja Tanzania ambao ni Tanzania Airports Authority.

  Hii "Category" ni nini?

  Kwa mujibu wa ICAO,viwanja vya ndege vyote vimewekwa katika " Aerodrome category" kulingana na ubora wake.Kuna "category 1" mpaka "Category 10".Category 10 ni kiwango cha juu kabisa cha ubora wa kiwanja,hivyo ndege zote kubwa,za kati na zile ndege ndogo, zinaweza kutua kwenye uwanja wenye hadhi hiyo.

  Kwa muda mrefu uwanja wa Dsm,licha ya changamoto zake,ulidumu katika "Category 9" hivyo kuwa nafasi moja kufikia "Category 10" ambayo ndio ubora wa juu wa viwanja duniani.Uzembe,urafi na uwajibikaji mbovu umesababisha kwa siku kadhaa uwanja kuwa "downgraded" hadi kufikia "category 7".

  ICAO hutoa category hizi kulingana na ubora wa uwanja katika mambo mengi,ikiwa ni pamoja na uwezo wa uwanja kuwa na miundombinu ya kupokea ndege za aina tofautitofauti,kuanzia ndege ndogo aina ya ATR-72 mpaka ile Airbus 380 iliyo kubwa zaidi.


  Pia ICAO,hutoa ubora huu kulingana na ugumu wa mazingira ya uwanja kwa ndege kutua.Kuna viwanja vilivyojengwa sehemu yenye tambarare,runway nzuri,hali ya hewa salama na vifaa vya kisasa vya kuongozea ndege,wakati vingine vimejengwa mazingira mabovu,runway fupi,eneo lenye ukungu kila mara,mvua mwaka mzima,barafu na milima na mabonde.

  Kipimo kingine KIKUBWA (kwa umuhimu wa pekee) ni uwezo wa idara ya zima moto yaani Rescue and Fire Fighting Services (RFFS).Zimamoto ndio "roho" ya kiwanja popote duniani.Uwanja usio na zimamoto ya uhakika,basi ndege nyingi na mashirika mengi huondoa safari za ndege zao kwa kuogopa kuwa na usalama mdogo wa ndege zao na abiria wao.Hii ni sababu katika nchi nyingi,mamlaka za viwanja vya ndege huwekeza kwa kiasi kikubwa sana katika idara ya zimamoto.Hapo JNIA,hili limekuwa ni tatizo na hivyo kulazimu ICAO kuushusha viwango uwanja wetu kwa kukosa magari ya zimamoto yenye viwango vya kukidhi hadhi ya "category 9"

  ICAO kupitia Annex 14,Volume 1 (Aerodrome Design and Operations) inahitaji uwanja wa ndege wenye "category 9" uwe na magari ya kisasa ya zimamoto (Fire Tender) walau yapatayo matatu (3) au zaidi,yenye "performance level A" ya lita 36,400 za maji na lita 13,500 za foam.Kitu ambacho wakati wa ukaguzi wa ICAO (ambao hawahongeki),Uwanja wa JNIA umeshindwa kutimiza na hivyo "dunia kutangaziwa" kwa muda kuwa uwanja wa JNIA si bora tena kwa kiwango cha "Category 9".

  Unapoushusha uwanja wa JNIA toka Category 9 mpaka Category 7,na taarifa kuwekwa katika mfumo wa NOTAM (Notice to Airmen),ina maana NOTAM hiyo inasomwa dunia nzima,na hususani kwa mashirika yote makubwa kama KLM,Swiss International,Emirates,Turkish,Oman,Qatar,South Africa,Egypt nk ambayo ndege zake hutua uwanja wa Dsm.

  Hasara ya "downgrading" hiyo kutoka CAT9 to CAT7 ,ni kuwa baadhi ya mashirika ya ndege yanaweza kuanza kusita na kukosa imani ya kuleta aina fulani ya ndege kwa kuhofia kuwa na usalama mdogo wa ndege zao katika uwanja huu.Iwe kwa kuja na kuondoka(Quick Turn) au kwa kulala (Night Stop).Uwanja ukiwa Category 7 maana yake hauwezi kupokea ndege kubwa kama Boeing 787(Dreamliner),B777-200/300,B767,B747(Kama ile Airforce One ya US),Airbus340-500/600,A350 na A333-300.

  Na kwa hapo JNIA,mashirika makubwa kama Emirates huleta B777-200/300,Swiss International A333-300,KLM huleta B777-300 au A333-300.Hivyo jambo hili lina "impacts" kubwa tu katika uso wa usafiri wa anga kimataifa.Jambo hili lisiachwe juujuu tu,serikali ichukue hatua,Waziri husika achukue hatua juu ya management ya TAA bila kuweka aibu na upendeleo.Mwisho wa siku ataondoka yeye kwa kuwabeba watu na huruma zake za kipemba.

  Kwa habari sizizo na majungu ni kuwa Mamalaka ya Viwanja vya ndege,waliposikia wakaguzi wanakuja na hawawezi kuhongeka ili kupika report,waliamua kwenda kuazima gari kutoka uwanja wa KIA na kulileta Dsm usiku kwa usiku,na mkaguzi alipofika akakuta idara ya zimamoto ina gari lenye kufanya kazi kwa ubora.

  Naambiwa hata sasa pale Zimamoto waziri ukienda mapema utakuta gari la Zimamoto limeandikwa "K'njaro International Airport-Rescue and Fire Fighting Service".

  Baada ya ukaguzi,gari lile likarudishwa tena KIA,na bila kutarajia mkaguzi wa nje toka ICAO akarudi kesho yake kwa kustukiza na kukuta gari lile halipo.Hivyo bila hiyana akaamua kuushusha uwanja(downgraded) toka CAT9 mpaka CAT7,sababu aligundua udanganyifu uliofanyika.Maana baada ya ukaguzi walirudisha KIA,baada ya kutupwa CAT7 wamerifuata tena ili wapate tena vigezo vya kurudishwa CAT9.

  Ndugu yangu Prof Makame,hawa watakuponza,tulishakushauri uisafishe management yote pale uanze na mwanzo,mbona unawalea hawa watu?Hujui ipo siku watakuponza?Unajisikiaje chini ya uwaziri wako kiwanja kushushwa hata kwa week moja tu kutoka CAT9 mpaka CAT7 na bado watu wapo ofisini kuanzia kwa DG mpaka Mkurugenzi wa Kiwanja!?Nasikia unataka kumleta yule jamaa aliyekuwa meneja wa Kigoma,hivi huko juu huwa hakuna watu wenye mafaili ya hawa jamaa mkajua madudu yao!?Kama ni huyo,unategemea lipi jipya?

  Uzuri au ubaya,wengine huwa hatuandika majungu hapa,hatuna chuki na watu.Tunaeleza kile tunachokifahamu kwa lengo la kusaidia.Prof Mbarawa utakuwa shahidi kuwa yale yote niliyoyaleta uwe hapa au ofisini kwako kwa njia rasmi ya kimaandishi,ulituma team yako kuchunguza na ukakuta hakuna majungu wala fitna,bali ni ukweli tupu.

  Tena ukakutana na hata mengine makubwa ambayo kwa sbb za kimaadili humu hatuyaweki.Naomba hili la "CAT7" likupe picha ya watu unaofanya nao kazi.Chukua hatua ngumu ili umsaidie Rais na Taifa kwa ujumla.Usionee mtu,tenda kwa haki...Sisi tunakusaidia pa kuanzia,wewe malizia.Tunakusaidia sababu tunakupenda.Kama watu walisafirisha gari la fire usiku kwa usiku toka KIA ili tu kuja "kumpiga changa la macho" mkaguzi wa ICAO,wewe utakua umepigwa "machanga ya macho mara ngapi?"

  Leo naishia hapa,ntakukusanyia taarifa nikuletee...lengo ni kujenga na si kubomoa.Chukua hatua Ami Prof Mbarawa,hawa unaowaendekeza,watakuponza.Naambatanisha "NOTAM" ilyowekwa na kutolewa baada ya kuazima gari tena KIA ili kuziba aibu,ilikua kwenye website ya TCAA iliyoonyesha kushushwa kwa kiwanja toka CAT9 mpaka CAT7 sababu ya ubovu wa idara ya zimamoto.Haya si majungu,dunia nzima imeona.
   
 2. Negan The Dead

  Negan The Dead JF-Expert Member

  #101
  May 19, 2017
  Joined: Mar 6, 2017
  Messages: 340
  Likes Received: 986
  Trophy Points: 180
  Nchi ilishajifia hii!!
   
 3. w

  wise123 JF-Expert Member

  #102
  May 19, 2017
  Joined: Apr 8, 2017
  Messages: 1,387
  Likes Received: 1,228
  Trophy Points: 280
  ndo maana Kenya wataendelea kuwin kwenye utalii tu mandege makubwa mengi final destination Yao kwa East Africa ni Kenya , nyie mnaosema haiwaausu bora mnyamaze tu coz impact ni kubwa kuliko unavyofikiri
   
 4. darcity

  darcity JF-Expert Member

  #103
  May 20, 2017
  Joined: Jul 20, 2009
  Messages: 3,901
  Likes Received: 5,371
  Trophy Points: 280
  Mambo mengi tutayaona kwenye hizi teuzi mpya
   
 5. j

  joshua_ok JF-Expert Member

  #104
  May 20, 2017
  Joined: Jun 27, 2012
  Messages: 5,317
  Likes Received: 3,154
  Trophy Points: 280
 6. j

  joshua_ok JF-Expert Member

  #105
  May 20, 2017
  Joined: Jun 27, 2012
  Messages: 5,317
  Likes Received: 3,154
  Trophy Points: 280
  Kama baba lao (JNIA-DAR) kaangukia pua itakuaje pale ZANZIBAR na Mwanza? maana huko nako disaster tupu mizigo samtaimz inabebwa na trekta mara mgongoni, departure lounge kama baa ya mtaani tofauti ni kuna feni kuuubwa linazunguka tu kupulizia wasafiri upepo
   
 7. E

  Earthmover JF-Expert Member

  #106
  May 20, 2017
  Joined: Sep 28, 2012
  Messages: 13,973
  Likes Received: 4,012
  Trophy Points: 280
  .....
  .......Mkuu salute Mingi sana ...
   
 8. E

  Earthmover JF-Expert Member

  #107
  May 20, 2017
  Joined: Sep 28, 2012
  Messages: 13,973
  Likes Received: 4,012
  Trophy Points: 280
  .....
  .....Ngalo wangejenga Ikungulyabashashi Wangetia akili kumtweh
   
 9. SDG

  SDG JF-Expert Member

  #108
  May 20, 2017
  Joined: Feb 28, 2017
  Messages: 7,360
  Likes Received: 7,581
  Trophy Points: 280
  Kupanga ni kuchagua.
  Tumeanza na ndege, tutaiweka tunduni ndo tushughulikie uwanja.
  Maana nchi hii hata viongozi wetu huwa hawajui wanataka nini.
  Sasa ile ndege yetu "TT" ikija inakutana na uwanja "TT GROUND"
   
 10. j

  joshua_ok JF-Expert Member

  #109
  May 20, 2017
  Joined: Jun 27, 2012
  Messages: 5,317
  Likes Received: 3,154
  Trophy Points: 280
  Kizazi cha T
   
 11. zee Don

  zee Don JF-Expert Member

  #110
  May 20, 2017
  Joined: Oct 31, 2016
  Messages: 473
  Likes Received: 345
  Trophy Points: 80
  Apa angalau mwandishi umeona mbali
   
 12. u

  ushuzi.1 JF-Expert Member

  #111
  May 20, 2017
  Joined: Feb 17, 2015
  Messages: 7,424
  Likes Received: 5,595
  Trophy Points: 280
  Tunapoenda itashuka mpaka ifike zero zero kabsa
   
 13. u

  ushuzi.1 JF-Expert Member

  #112
  May 20, 2017
  Joined: Feb 17, 2015
  Messages: 7,424
  Likes Received: 5,595
  Trophy Points: 280
  Pesa za maendeleo zote anakula Lipumba kwa ajili ya kudhoofisha upinzani zingine zinatumika kimlinda Daud Bashite unategemea kutakuwa na maendeleo tena?
   
 14. Duduwasha

  Duduwasha JF-Expert Member

  #113
  May 20, 2017
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 5,169
  Likes Received: 2,221
  Trophy Points: 280
  Uwanja ni mbaya haswa... picha ya kwanza unatoka main road tu ubaya unaanzia hapo pia mchafu
   
 15. Duduwasha

  Duduwasha JF-Expert Member

  #114
  May 20, 2017
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 5,169
  Likes Received: 2,221
  Trophy Points: 280
  Bora turejee kutua Nairobi kisha tunapanda yale mabus Dar Express maana Akamba bus is no more
   
 16. Duduwasha

  Duduwasha JF-Expert Member

  #115
  May 20, 2017
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 5,169
  Likes Received: 2,221
  Trophy Points: 280
  Chato mkuu au hujawahi fika huko?
   
 17. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #116
  May 20, 2017
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,546
  Likes Received: 1,531
  Trophy Points: 280
  HahaĆ a kiisome namba tena..
   
 18. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #117
  May 20, 2017
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,546
  Likes Received: 1,531
  Trophy Points: 280
  Airport limejaa nzi kama tandale mxxxxx.
   
 19. s

  singojr JF-Expert Member

  #118
  May 20, 2017
  Joined: Oct 28, 2014
  Messages: 3,468
  Likes Received: 3,536
  Trophy Points: 280
  Si Ndonga anataka chattle iwe mji mkuu
   
 20. mbuta likasu

  mbuta likasu Senior Member

  #119
  May 20, 2017
  Joined: Feb 29, 2016
  Messages: 164
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 45
  Povu mubashara..pole kama nawe ni miongoni mwa wale wafilisti wa taa,nendeni mkaungame..udhalimu wa pale ni superb..haya madudu ni kutokana na ubabaishaji sugu..mna workforce ya vijana wazuri tu lkn mnawabania,mnapeana vyeo kwa kujuana,mnawabania kusoma..km wamekutuma waambie huku ni 10 kwa bashite,km hawajakutuma basi wataukuta hapa huu mwandiko..
  Waziri wenye dhamana anatakiwa afumue mamlaka yote,ikiwezekana ata aimerge ktk taasisi nyingine km itaonekana inafaa..taa ya sasa ina ombwe kubwa la uongozi,wanapata tabu sana kujaza nafasi za juu ,wanajikuta wanachagua 'afadhali'baada ya kukosa watu wa uhakika...wakiamua kutoa fursa za mafunzo na promotion kwa wote bila figisu,mamlaka itasonga mbele..pia idara ya utumishi ifanye kazi yake kwa weledi sio kwa utashi wa yule bwana mdini..I do this for the love of my country ,nothing else..outperforming Kenya in aviation industry ain't easy ..u need to change ,get rid of ur chronic nepotism..
   
 21. nra2303

  nra2303 JF-Expert Member

  #120
  May 20, 2017
  Joined: Jul 28, 2015
  Messages: 2,727
  Likes Received: 2,214
  Trophy Points: 280
  Maboresho yanahitajika makubwa sana apo Terminal 2 hats km T3 inakuja sio ndege zote zitatua T3 trust me! Kwa innovations ya T2 ni muhimu sana! Na sio inshu ngumu,pale kunamiss izo fire extinguisher,lagage belt,AC,Rangi,scanner,security procedure,paa lipande juu,cz hmna hewa pale chini,alafu na nje usafi! Ikienda Rwanda terminal yao ni ndogo Ila INA mpangilio mzuri kasoro sehemu ya kuondokea tu basi
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...