Uwanja wa JKT Tanzania pale Mbweni

Simba imepoteza ushawishi ndani na nje ya uwanja ndiyo maana tunaona maamuzi ya kuiumiza yanaweza kufanywa bila wahusika kuogopa. Simba kwa hadhi yake siyo ya kupelekwa kucheza mechi ya mashindano kwenye kiwanja hiki chenye standard ya kiwanja cha mazoezi hasa ukizingatia hao JKT walikuwa na uwezo wa kuipeleka mechi Chamazi ambapo bado ni mazingira rafiki kwao kutokana na timu zinazotumia uwanja huo.

Vigezo vya TFF linapokuja suala la viwanja viangaliwe upya. Kwa tulipofikia uwanja lazima uwe na majukwaa ya kuingiza idadi fulani ya watazamaji na viwanja vyote vipewe deadline majukwaa yawe na viti vinavyohesabika siyo watu wanakaa kwenye sakafu ya cement.

Pia nimewaza kwa nini jeshi haliongezi nguvu katika kuboresha uwanja wa Uhuru ambao pia unamilikiwa na jeshi na badala yake inaenda kuhangaika katika uwanja mpya ambao hauna facilities kabisa?

Screen Shot 2024-02-14 at 11.27.50 AM.png
 
Simba imepoteza ushawishi ndani na nje ya uwanja ndiyo maana tunaona maamuzi ya kuiumiza yanaweza kufanywa bila wahusika kuogopa. Simba kwa hadhi yake siyo...
Naunga Mkono hoja Chamazi sio salama kwà Simba pale kuna Majini hapafai niko Bunju tayari kushuhudia mechi hapo kesho uwanja wa Isamuyo
 
Simba imepoteza ushawishi ndani na nje ya uwanja ndiyo maana tunaona maamuzi ya kuiumiza yanaweza kufanywa bila wahusika kuogopa. Simba kwa hadhi yake siyo ya kupelekwa kucheza mechi ya mashindano kwenye kiwanja hiki chenye standard ya kiwanja cha mazoezi hasa ukizingatia hao JKT walikuwa na uwezo wa kuipeleka mechi Chamazi ambapo bado ni mazingira rafiki kwao kutokana na timu zinazotumia uwanja huo.

Vigezo vya TFF linapokuja suala la viwanja viangaliwe upya. Kwa tulipofikia uwanja lazima uwe na majukwaa ya kuingiza idadi fulani ya watazamaji na viwanja vyote vipewe deadline majukwaa yawe na viti vinavyohesabika siyo watu wanakaa kwenye sakafu ya cement.

Pia nimewaza kwa nini jeshi haliongezi nguvu katika kuboresha uwanja wa Uhuru ambao pia unamilikiwa na jeshi na badala yake inaenda kuhangaika katika uwanja mpya ambao hauna facilities kabisa?

View attachment 2903982
Ni Simba kupoteza hadhi(ambao ni uongo na ujinga wako)au TFF kutoithamini timu?Muulize Mrisho Ngassa.
 
Sijasema hadhi nimesema ushawishi, vitu viwili tofauti. Maamuzi haya yanafanyika kutokana na ama viongozi wa Simba hawana mahusiano ya karibu na watu wa TFF na vilabu vingine au nguvu ya Simba inapigwa vita halafu viongozi wa Simba wanakosa ushawishi wa kisiasa kuwazuia hao wanaoipiga vita.
 
Ushawishi?Uongo mwingine.Twende CAF tuwaulize.Muwe mnathamini mambo yenu.
Kama hauoni, omba fimbo itakusaidia. Sijaongelea huko nje naongelea katika ligi ya ndani na kwa Azam inavyokuja, viongozi wa Simba wakifanya mchezo hata hiyo nafasi ya uwakilishi haitakuwepo.
 
Kumbe unaombea na wala si Simba kukosa mvuto.Mtu anakatazwaje kuwaza?Wewe waza tu.
 
Nasikia simba watacheza apo sasa kama huo uwanja unaweza kuchezewa ligi kuu kwa nini na sisi tusicheze pale bunju upi mzuli kati ya uwanja wao na wetu
uwanja sio mzuri na hata kwenye kutangaza kwa tv ni shida kubwa,na uwanja hauna umeme wa kutosha
 
Sijasema hadhi nimesema ushawishi, vitu viwili tofauti. Maamuzi haya yanafanyika kutokana na ama viongozi wa Simba hawana mahusiano ya karibu na watu wa TFF na vilabu vingine au nguvu ya Simba inapigwa vita halafu viongozi wa Simba wanakosa ushawishi wa kisiasa kuwazuia hao wanaoipiga vita
TFF inaendeshwa kwa rimoti sasa na wanaoiendesha wanajulikana.Tokea Marehemu Hans Pope afariki Simba imekuwa mtoto wa kambo pale TFF.
Baada ya mechi na JKT uwanja utafungiwa.
Ali Hassan ulifungiwa timu pendwa ikachezea Dodoma na ukafunguliwa baada ya siku 2.
Simba bila kuchukua uamuzi mgumu hizi njama zitaendelea.
 
Endeleeni hivyo hivyo mwisho wa msimu mna anza maandamano Mangungu ajihudhuru
 
Viwanja vya Uhuru & Mkapa. Vilifungwa kwa sababu za kutengeneza soko/ mwanya wa kuuza/kulipia kiwanja flani. Haiwezekani viwanja vyote viwili viwe na matengezo kwa muda unaofanana??.
 
  • Kicheko
Reactions: Tui
Back
Top Bottom