Uvumilivu na Umoja wa kweli Nguzo ya Ndoa ya kudumu

Kichwamoto

JF-Expert Member
Jan 21, 2019
3,353
4,535
Uvumilivu ni tiba na rutuba ya kupitia milima na mabonde ya ndoa.
Umoja ni dawa chanjo ya uimara wa taasisi yaani ndoa. Wengine mtasema upendo mimi natumia umoja, na hii hutokea pale baadhi ya watu huingia kwa ndoa kama daraja la kuvuka shida zao au kufika malengo yao yasiohusiana na mwanandoa mwenza.
Ndoa ni taasisi au chombo ambacho mmiliki wake ni watoto. Yeyote asiejua hilo hatajua thamani ya neno Umoja.

Umoja ni nguvu ya kufikia malengo,huvusha vikwazo, ni nguzo ya kuweza yote magumu.

Sisi sote ni ndugu,pamoja tunaweza, utengano ni udhaifu na hasara ya udhaifu hupata watoto.

Oa Olewa ili ukadumu na kudumu yakupasa utambue kusudi halisi la ndoa na jiulize kwanini naoa au niolewe na huyu na si wengine?

Ananini chema cha kudumu kimfaacho Mungu? Kipi ntajivunia kwake maisha yetu yote, anasifa ya uvumilivu, subra, ni mfuasi wa umoja.

Ni wakati umefika wachunba waulizane maswali mfano Kwanini Tuoane? Ili iweje?na hadi lini? Kwanini nikuoe wewe na si mwingine?msingi au misingi ya ndoa na kudumu kwake ni nini?

Nimeoa/nimeolewa nikiwa mjini kisha nikampeleka mke/mume kwa wazazi pasipo kufahamu misingi ya ndoa, unadhani utavuna nini?

Uvumilivu ni adimu au watu hawajui maana?

Utayari wa kuingia kwenye ndoa maana yake inafahamika?

Mgawanyo wa kiwajibu katika ndoa katika nyakati za sasa, tafsiri kibiblia, kijamii, iko synchronized? Au fursa ya offside nufaishi.?je offside hio inaakisi tafsiri endelevu ya umoja?

"Sustainable marriages at crossroads a contemporary perspective" Somewhere in TZ working on it right now (Galileo_Gaucho, 2022)
 
Back
Top Bottom