Wapendwa wana jf,kwa muda sasa toka mhe.rais amsimamishe kazi mhe. Tibaijuka,kumekuwepo na uvumi na uongo mwingi unao tungwa na kusambazwa kwa kasi sana tokea siku mhe.rais amwajibishe waziri huyo,sijajua msingi hasa wa watu hao kufanya ivyo ni nini,Imefika mahali hadi picha zake za kipindi cha nyuma zinasambazwa kuelezea au kushawishi uongo huo,baadhi ya picha naziambatanisha hapa,ila binafsi nachukizwa sana na hizi siasa za kuendekeza kuchafuana sana,mimi sioni hasa faida yake nini na ni kwa lengo gani??
Tulisha msikia mhe. rais akisema kuhusu mama huo na nashindwa kuelewa kitu gani kinaendelea,hasa wanaofanya hivvo wana lengo gani??
Watanzania tufike mahali tukatae uzushi na uzandiki huu wa watu wachahce,mimi naomba nieleze tu kidogo juu ya picha hizi ambazo huyu mama alikuwa katika kutatua mgogoro wa ardhi huko Pwani na wananchi ndio walizichukua,lakini nashangaa watu wanachukua baadhi ya vipande na kueneza uvumi wa uongo eti huyu mama ameanza kutembea peku kuomba kura jimboni kwake kipindi hiki cha kampeni kitu ambacho sio kweli.
Picha izi zilichukuliwa kabla hajaondoka madarakani na akiwa bado waziri ,na alikuwa katika ziara ya kutatua migogoro,katika njia hiyo gari la waziri lilikwamba katika tope kali na hata ukiangalia kwa makini katika picha hiyo moja ambayo inamwonesha akitembea peku,nyuma yake kuna gari likiwa limezama kwenye tope,gari hili kuzama halikumzuia mhe waziri kuendelea na ziara yake ambayo ilikuwa kuangalia mipaka na kutatua mgogoro husika kitu ambacho tukubari tukatae ni ngumu kukiona kwa viongozi wetu wengi hapa Tanzania na ukiangalia picha zinazofuata kabla unaona kabsa waziri na wananchi husika wakijaribu kusukuma gari la waziri kutoka katika tope hilo lakini ilikuwa ngumu.
Jamani mimi binafsi hata kama siko upande wa huyu mama ila kiukweli watanzania wenzangu tupunguze na tuache kueneza chuki ambazo hazina tija kwa taifa changa kama letu,ni hayo tu.