Uvivu wa kufikiri au ujinga tu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uvivu wa kufikiri au ujinga tu?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by LUS0MYA, Aug 10, 2011.

 1. LUS0MYA

  LUS0MYA JF-Expert Member

  #1
  Aug 10, 2011
  Joined: Aug 4, 2011
  Messages: 243
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 60
  Rais wa awamu iliyopita aliwahi kusema watanzania ni wavivu wa kufikiri! Watu wengine walikebehi na kuona kama wametukanwa!

  Hebu angalia watu waliopewa dhamana ya kufikiri badala yetu wanavyochemsha.

  Naanza na hili la nishati ya gesi.

  Nakumbuka nderemo zilitawala nchi hii pale tulipogundua hazina kubwa ya gesi pale songo songo, watanzania tumepata nishati nafuu sasa mkaa bye bye, aaah wapi mjanja kaingia katoa msaada wa kujenga pipeline toka Huko kuja dsm. Kilichotokea gharama za kusafirisha gesi kuja ikawa kubwa hivyo bei yake ikapanda ikawa sasa inalingana na bei ya kuagiza gesi nje!

  Tukifikiri kidogo tukawapa eneo Tanesco huko songo songo wakaweka mitambo inayotumia gesi wakainunua kwa bei nafuu na kusambaza umeme kwa gridi kuna haja ya kununua majenereta yanayotumia mafuta? Hii mitambo ya Tanesco bado yatakiwa kukaa hapa mjini?

  Mtazamo wangu: SONGAS imefanya gesi yetu kuwa ghali labda wangejenga pipeline kwenda nchi jirani kama zinahitaji lakini siyo hapahapa nchini. Sasa viwanda vikubwa vya cementi, Nondo, Usindikaji, Tanesco waende kwenye source wasisubiri kuletewa gesi hapa dar!

  Unajua kwanini nchi zetu zinaingia katika machafuko? Ni pale wananchi wanapoona rasilimali iliyogunduliwa haijabadilisha kitu chochote ktk maisha ya watu.

  Hata tukigundua mafuta hakuna unafuu kama tutakuwa wavivu wa kufikiri na kubaki wajinga.
   
 2. M

  Mr.Right JF-Expert Member

  #2
  Aug 10, 2011
  Joined: Jul 9, 2011
  Messages: 408
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Umefanya makosa kumquote Rais wa awamu iliyopita Mkapa. Kwa sababu huyu jamaa kajitajirisha sana kwa hela za wizi na Rushwa. Huyu Mkapa ni mmoja wa Mafisadi wakubwa hapa nchini.
   
 3. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #3
  Aug 10, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  'Fata maneno yangu, usifate matendo yangu'

  Msemo wa mababu huo.

  Watu wengi huongea ya maana kuliko wanayoyatenda ila haimaanishi kuwa hata wanayoyaongea yadharauliwe kisa hawayatendi.
   
 4. klorokwini

  klorokwini JF-Expert Member

  #4
  Aug 10, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 8,710
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 135
  Hiyo ni mathayo ngapi?
   
 5. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #5
  Aug 10, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  <br />
  <br />
  hiyo ni between the lines kloro.
   
 6. Radhia Sweety

  Radhia Sweety JF-Expert Member

  #6
  Aug 10, 2011
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 4,448
  Likes Received: 345
  Trophy Points: 180
  Kila mtu anahusika kujenga hii nchi, siyo suala la kuachia viongozi tu.
   
 7. doup

  doup JF-Expert Member

  #7
  Aug 10, 2011
  Joined: Feb 26, 2009
  Messages: 1,172
  Likes Received: 335
  Trophy Points: 180
  Wafikiria MAKALIO kumbe wako wengi, Hongera Masaburi kwa kulijua hilo.
   
 8. LUS0MYA

  LUS0MYA JF-Expert Member

  #8
  Jan 26, 2013
  Joined: Aug 4, 2011
  Messages: 243
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 60
  Wadau nilipost hii thread mwaka jana kuhusu mipango ya kifisadi ya kusafirisha gesi kutoka kusini hadi DSM.Kwa wakati huo nilikuwa napinga dhana ya kusafirisha gesi kuja Dsm kwa ajili ya umeme na viwanda hapa dar.Uvivu wa kufikiri ninaousimamia hadi sasa ni kuwa wataalamu wanaposupport wazo la kusafirisha gesi wanaangalia upande mmoja tu yaani availability ya gesi nasiyo available kwa value gani.bomba litafanya gesi kuwa available hapa dar kwa uhakika lakini kwa gharama ya juu kuliko inayoagizwa nje! simple mathematics gesi ikisafirishwa kwa magari mlaji anpata cost moja tu kubwa ya kusafirisha gesi lakini kuwa na bomba maana yake kuna cost ya kusafirisha,cost ya kutunza bomba lenyewe,security ya bomba lenyewe nk baadaye watu wataanza kutumia gesi ya nje ndipo policy za ajabu zitawekwa kuzuia gesi toka nje ya nchi na kuhalalisha mzigo wa gharama kwa mlaji.Watawala waambie Tanesco kuwa ubungo au kinyerezi siyo tena sehemu muafaka ya kuzalishia umeme waende kwenye source!mbona kidatu,mtera wameshindwa kuleta maji mjini wanazalisha huko huko?TUFIKIRI
   
 9. Mwanahisa

  Mwanahisa JF-Expert Member

  #9
  Jan 26, 2013
  Joined: Jun 29, 2012
  Messages: 1,397
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Uvivu wakufikiri ni huu wakusema gesi ibebwe na magari maana kulaza bomba la gesi ni gharama, Gasprom ya Urusi wamelaza bomba la gesi mpaka ulaya wao hawakufikiri naona waliwehuka...! Mbona tuna bomba la mafuta hapa mpaka Zambia na wala sio magari yanabeba hii malighafi? Kama Korosho hazikuwakomboa, wala vinyago ni kitu gani kinawaaminisha kua umeme ukifuliwa Mtwara maisha yatabadilika? Economies of scales zote ziko mjini, skilled labor, na miundombinu iko mjini. Waelewesheni hawa watu haya mambo sio rahisi.
   
 10. NullPointer

  NullPointer JF-Expert Member

  #10
  Jan 26, 2013
  Joined: Feb 7, 2011
  Messages: 3,483
  Likes Received: 708
  Trophy Points: 280
  Hata umeme ukizalishwa kule bei itakua juu hilo naona hujaliona, tena juu kuliko ambavyo bomba lingewekwa hadi Dar, wewe ndio kaa ufikiri upya.
   
 11. NullPointer

  NullPointer JF-Expert Member

  #11
  Jan 26, 2013
  Joined: Feb 7, 2011
  Messages: 3,483
  Likes Received: 708
  Trophy Points: 280
  Hii kitu ni ngumu zaidi ya unavofikiri, ninahakika leo hii upewe nafasi ya kusimamia hili swala hakuna utakalofanya la maana, zaidi itabaki utapigwa fire tu
   
Loading...