UVCCM wamuonya Anthony Diallo

Kijogoodi

JF-Expert Member
Mar 29, 2021
1,363
2,372
Katibu wa umoja wa vijana wa CCM Khenan Kihongosi amemuonya Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza bwana Diallo kuwa aache upotoshaji mara moja, kitendo cha kusema baadhi ya viongozi waliopita walitakiwa kuwa Mirembe ni cha kipotoshaji kwani Diallo yupo kwenye vikao vyote vya maamuzi kwani ni mjumbe wa kamati kuu.
===

CCM imelaani kauli ya kubeza viongozi wastaafu iliyotolewa na mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Mwanza, Antony Diallo katika mahojiano aliyofanya na kituo kimoja cha televisheni nchini.

Kauli hiyo imetolewa leo Jumamosi Julai 10, 2021 na katibu mkuu wa umoja wa vijana wa chama hicho (UVCCM), Kenani Kihongosi katika kikao cha majumuisho ya ziara ya kuimarisha chama inayofanywa na sekretarieti ya chama hicho ikiongozwa na katibu mkuu wa CCM, Daniel Chongolo.

Kihongosi amesema kauli iliyotolewa na kiongozi huyo ni msimamo wake mwenyewe na si wa CCM na kwamba jumuiya ya vijana inalaani kauli zinazotolewa na kiongozi huyo kuwabeza viongozi walioitumikia nchi, akitaka wastaafu hao kuachwa wapumzike.

"Tangu leo asubuhi tumeona ujumbe ukisambaa kwenye mitandao ya kijamii ikinukuu kauli iliyotolewa na mmoja na kiongozi ambaye anaingia kwenye vikao vya maamuzi lakini leo ameamua kutoa kauli hii ambayo imetuchukiza sana vijana kwani tulitegemea wawe wa kwanza kutuongoza, " amesema.

Kihongozi amesema kiongozi huyo wa CCM ambaye ni mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa amenukuliwa akisema viongozi wengine wanaoteuliwa na CCM wanapaswa kuwa hospitali ya magonjwa ya akili ya Mirembe iliyopo mkoani Dodoma.

MWANANCHI
 
Kwa nini yeye hakumsubiri huko kwenye vikao? Ameamua kutumia njia ileile aliyotumia Diallo.

Diallo amefanya jambo la maana sana kwa mistakabali wa CCM na chi kwa ujumla. Tunahitaji kizazi cha watanzania wanaosema ukweli ili kuweka mambo sawa.

Diallo ameitendea haki ahadi ya mwanaCCM ya kusema kweli daima.
 
Khenan aache kuyagusa majitu yenye nguvu kama Dialo. Hizi siyo enzi za jiwe. Ohooo!
 
Wakakimbia alafu kiwanda bora kabisa Afrika cha kufua zahabu kikajengwa, nchi ikaingia uchumi wa kati , mabilionea kama akina Laizer wakaibuka, mapato ya ccm yakatoka million 5 yakafikia billioni 20 kwa mwaka!

Tunamuonya Diallo yeye amekuwa mbunge na waziri kwa miaka 20 lakini hakuna wananchi wanachomkumbuka nacho ni kama tu hajawahi kuwa kiongozi
 
Hizi takwimu za kiuongozi za ndugu dialo umezitoa wapi?
 
Back
Top Bottom