Kihongosi: Maamuzi ya vikao yaheshimiwe

Kihongosi: Maamuzi ya vikao yaheshimiwe

Zack Abdul

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2026
Posts
509
Reaction score
489
Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa, Kenani Kihongosi amesema msingi wa uhai na uimara wa chama ni kuheshimu vikao na maamuzi yake.

Akizungumza Tarime, Kihongosi amesisitiza kuwa viongozi na wanachama walioiva kiitikadi hutambua kuwa maamuzi ya mwisho ya vikao ndiyo maamuzi rasmi ya chama, kwani huko ndiko mipango hujadiliwa, hukubaliwa na kupewa mwelekeo wa pamoja.

Ameeleza kuwa CCM itaendelea kujengwa na wanachama watiifu, wazalendo na wanaoweka maslahi ya chama mbele kuliko makundi au maslahi binafsi.

Soma Pia: Kihongosi: CCM haijawahi kukosea, Hakuna aliye Mkubwa kuliko Chama

“Chama kwanza, watu baadaye. Tukipenda chama chetu, tukalinda umoja, mshikamano na nidhamu ya vikao, tutajenga CCM imara na yenye kuendelea kuaminiwa na wananchi,” amesema Kihongosi.

Aidha, amewataka viongozi kuachana na migawanyiko na kuhakikisha Tarime inabaki kuwa mfano wa umoja, upendo na mshikamano ndani ya Chama Cha Mapinduzi.
IMG-20260515-WA0141.jpg
 
Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa, Kenani Kihongosi amesema msingi wa uhai na uimara wa chama ni kuheshimu vikao na maamuzi yake.

Akizungumza Tarime, Kihongosi amesisitiza kuwa viongozi na wanachama walioiva kiitikadi hutambua kuwa maamuzi ya mwisho ya vikao ndiyo maamuzi rasmi ya chama, kwani huko ndiko mipango hujadiliwa, hukubaliwa na kupewa mwelekeo wa pamoja.

Ameeleza kuwa CCM itaendelea kujengwa na wanachama watiifu, wazalendo na wanaoweka maslahi ya chama mbele kuliko makundi au maslahi binafsi.

“Chama kwanza, watu baadaye. Tukipenda chama chetu, tukalinda umoja, mshikamano na nidhamu ya vikao, tutajenga CCM imara na yenye kuendelea kuaminiwa na wananchi,” amesema Kihongosi.

Aidha, amewataka viongozi kuachana na migawanyiko na kuhakikisha Tarime inabaki kuwa mfano wa umoja, upendo na mshikamano ndani ya Chama Cha Mapinduzi.View attachment 3589186
well done muenezi wa CCM taifa, ndugu Kenan Kihongosi,

Michakato mbalimbali ya ndani ya CCM, kiutararibu huhitimishwa kwa vikao vya juu vya Chama. Na huko ndiko hutoka maamuzi ya mwisho yenye uelekeo wa chama kwa wakati huo.

Ni muhimu sana sote kama wana CCM na waTanzania wote kwa ujumla, kua watiifu kwa kuheshimu maamuzi ya mwisho ya vikao vya Chama.

Kidumu Chama Cha Mapinduzi 🔥
 
Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa, Kenani Kihongosi amesema msingi wa uhai na uimara wa chama ni kuheshimu vikao na maamuzi yake.

Akizungumza Tarime, Kihongosi amesisitiza kuwa viongozi na wanachama walioiva kiitikadi hutambua kuwa maamuzi ya mwisho ya vikao ndiyo maamuzi rasmi ya chama, kwani huko ndiko mipango hujadiliwa, hukubaliwa na kupewa mwelekeo wa pamoja.

Ameeleza kuwa CCM itaendelea kujengwa na wanachama watiifu, wazalendo na wanaoweka maslahi ya chama mbele kuliko makundi au maslahi binafsi.

Soma Pia: Kihongosi: CCM haijawahi kukosea, Hakuna aliye Mkubwa kuliko Chama

“Chama kwanza, watu baadaye. Tukipenda chama chetu, tukalinda umoja, mshikamano na nidhamu ya vikao, tutajenga CCM imara na yenye kuendelea kuaminiwa na wananchi,” amesema Kihongosi.

Aidha, amewataka viongozi kuachana na migawanyiko na kuhakikisha Tarime inabaki kuwa mfano wa umoja, upendo na mshikamano ndani ya Chama Cha Mapinduzi.View attachment 3589186
These mazafakas are idiots. Wao wenyewe hawana hata nidhamu ya kuheshimu kura za wanachama!
 
KIHONGOSI: MAAMUZI YA VIKAO YAHESHIMIWE
TARIME: KATIBU wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Kenani Kihongosi amesema msingi wa chama ni vikao, hivyo maamuzi yanayotolewa katika vikao yanapaswa kuheshimiwa.

Kihongosi ameeleza hayo leo Mei 15,2026 alipotembelea na kuhudhuria Shina namba tatu Tawi la Buhemba Kata ya Bomani jimbo la Tarime Mjini ikiwa ni muendelezo wa ziara yake katika Mkoa wa Mara.

Kihongosi alisema watu wanapaswa kuheshimu maamuzi ya vikao kwa sababu ndipo watu wanapokaa kufanya mipango na kukubaliana hivyo maamuzi ya vikao ndiyo maamuzi ya chama.

“Kiongozi aliyeiva itikadi ya CCM maamuzi ya mwisho ya vikao ndiyo maamuzi ya chama na wanachama hao, vyama vyetu au chama chetu tunasema msingi wa chama ni vikao, kwenye vikao tunakaa, tunapanga tunakubaliana tunasonga mbele,” amesema Kihongosi.

Kihongosi ameongeza kuwa kazi ya chama itafanywa na wanachama watiifu na wazalendo wa chama, hivyo ukiona kuna mtu ana mambo yake mengine huyo si mwanachama aliyoiva itikadi ya CCM.

Katika hatua nyingine amewataka viongozi wa CCM walinde chama kwa sababu chama ndicho kimewapa heshima ya uongozi, hivyo waachane na mambo ambayo yanaharibu chama kwahiyo lazima tulinde maslahi yetu mapana yawe ndani ya chama.

“Jambo ninalopenda kulisisitiza hapa katika mkutano wetu huu wa ndani naomba wana CCM tukipende chama kuliko kupenda watu ndani ya chama, maana yake chama kwanza watu baadaye,” amesisitiza Kihongosi.

“Ninacho maanisha hapa Tarime tunahitaji, umoja upendo na mshikamano ili kuwa na CCM imara na madhubuti lazima kama kuna makundi yafe, kama kuna mambo hayaeleweki yamalizwe ili Tarime Chama Cha Mapinduzi kiwe Imara”.
 
Back
Top Bottom