UVCCM Moshi yawaonya viongozi wa dini na wastaafu wanaofanya uchochezi

UVCCM Moshi yawaonya viongozi wa dini na wastaafu wanaofanya uchochezi

Just Pray

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
2,142
Reaction score
4,779
Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Moshi Vijijini umetoa onyo kali kwa viongozi wa Chama, Serikali na Dini watakaobainika kuchezea au kupuuza maslahi ya Vijana, ukisisitiza kuwa hatua za kinidhamu zitachukuliwa kwa maslahi mapana ya Chama na Taifa.

Onyo hilo limetolewa jana Januari 24, 2026 na Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Moshi Vijijini, Yuvenali Shirima, wakati wa kikao cha Baraza la UVCCM Wilaya, ambapo amesema kuwa katika kipindi cha Siku 100 za Uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan, Vijana hawatakubali kuona maslahi yao yakiyumbishwa au kupuuzwa na kiongozi yeyote ndani ya Wilaya au Taifa kwa ujumla.

Amesema UVCCM itaendelea kusimamia kwa karibu Haki na Fursa za Vijana, na haitasita kuchukua hatua dhidi ya Mtu au Kundi lolote litakalojaribu kuathiri Ustawi na Maendeleo ya Vijana kwa maslahi binafsi au ya Kisiasa.Aidha, Baraza hilo limetoa onyo kali kwa baadhi ya Viongozi wa Dini na Viongozi wastaafu wanaokiuka wajibu wao wa msingi wa kuhubiri Amani, Upendo na Mshikamano, na badala yake kujihusisha na Kauli au Vitendo vinavyochochea Migawanyiko na Vurugu katika Jamii.


 
Back
Top Bottom