Tindo
Platinum Member
- Sep 28, 2011
- 69,573
- 123,054
Vijana wangu MSALANI Simiyu Yetu na stroke,si mmeona mlivyo watupu? Badala ya kujadili hoja mnaleta kejeli. Nawaonea huruma sana.
Mzee Tupatupa
Bora hata mzee tupatupa umeliona hili. Hali hii naifananisha na wale watoto ambao huwa wazazi wao wanawaona bora kuliko wengine, matokeo yake watoto hao huishia kumtegemea mzazi mpaka wanapokuwa watu wazima. Ngoma inakuja wakati wa kuoa, unatongozaje wakati hukuachwa uweze kujitegemea wewe mwenyewe, ndio hapo unasubiri babayako akakutongezee. Huu mtindo wa vijana wa uvccm kujiona wana dola basi wamebweteka kiasi kwamba hawana hoja bali wamemezeshwa propanda ndio wakitoka nje utasikia wanajenga hoja, cdm ni chama cha wachaga, watu wa kaskazini, nchi hii imeendelea sana, sijui katiba tumeipokea, tumeielewa na tumeikubali. Sasa waambie waitete hiyo katiba mpya hata vifungu viwili utasikia wanakuja na hoja za kizee, nyinyi mnataka kuvunja muungano na mnatumiwa na mataifa ya nje!! Ukiawaambia mbona hayo mataifa ya nje mbona ndio yanayochimba madini tena kwa mikataba ya siri na mibovu, viongozi wao mbona ndio kila siku wanaenda kutibiwa nje ya nchi, hawana hoja wanaishia kusema ccm itatawala milele au wewe umetumwa na Slaa.
Niwaambie vijana wa ccm na watz wote, wangalau cdm katika miaka hii mitano tumeona wakifanya kazi ya siasa kwa ukweli bila kubebwa, huku wakikutana na changomoto kama, watu kuuliwa kwenye mikutano yao, mfano Ali Zona, Mwangosi achia mbali kupigwa mabomu na kunyimwa vibali na polisi. Ndio chama haswa kilichotembelea watanzania wengi, na kilichokwenda sehemu kubwa ya nchi hii kutoa elimu ya uraia kuliko taasisi yoyote hapa nchini. Hii haswa ndio kazi ya siasa. Hao uvccm siasa zao ndio kama zile za kuleta vijana kufanya fujo pale ubongo plaza kuzuia elimu ya uraia, na kuishia kutoa matamko ya kutokutaka rais toka kaskazini, na kwasababu hawajui kazi ya siasa wamebaki wapiga debe wa wasaka urais ambao ni wazee waliofilisika kimitazamo na kimalengo bali wanataka urais kama kinga ya maovu yao na kulipiziana visasi. Hivi katika mazingira haya unategemea uvccm waje hadharani kusema nini wakati wanasubiri kuambiwa cha kutekeleza toka kwa viongozi wao.
Katika hili siwasifii cdm lakini ukweli uko wazi peupe, kama sio jeshi la polisi kusikiliza amri nyingi ambazo si halali kwa chama cha siasa huwezi kuwapambanisha cdm na ccm katika kufanya kazi za siasa nchini. Kwa kiwango kikubwa cdm imekuwa ni taasisi yenye ubunifu hata kama baadhi ya ubinifu wao unakutana na changamoto na mapungufu ya hapa na pale wangalau tunaona kabisa wanafanya kazi ya siasa kama ambavyo inakipasa chama cha siasa kufanya. Hawa ccm ukiachia kushika dola sehemu kubwa ya siasa zao zimebaki za mazoea, fitina, hila, majungu na umafia. Hivi leo kila baya kuanzia kuuza unga, mauaji ya watu wenye mtazamo tofauti na chama chao, ufisadi,uwizi wa mali ya umma ccm ndio vinara. Siasa zao zimebaki kwenda kutoa hela za kulaghai watu makanisani, misikitini, kwenye vikundi hasa wakati wa karibu na uchaguzi ili wapate madaraka. Lakini lini umewaona hao wanaopita makanisani, misikitini wakiitisha mikutano ya hadhara ambayo ni ya kisiasa wangalau kujibu na kutafuta miafaka na jamii? Kama hawafanyi hayo yote wanajiitaje ni chama cha siasa na sio genge la wezi? Watanzania naomba tujitambue ni wakati sasa wa kufanya mabadiliko kupitia njia ya box la kura, ule uzembe na kutokujali wajibu wa kuchagua viongozi sahihi ufikie mwisho.