gfsonwin
JF-Expert Member
- Apr 12, 2012
- 18,272
- 20,683
=========amina ngalo, post:
TAARIFA ILIOSOMWA MBELE YA WAANDISHI WA HABARI NA MWENYEKITI WA UVCCM MKOA WA MKOA ARUSHA TAREHE 15 JUNE 2016
Ndugu Waandishi wa Habari mtakumbuka vizuri kuwa jana katika kongamano la kumbukizi ya maisha ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere lilofanyiika katika ukumbi wa Nkrumah katila chuo kikuu cha Dar es Salaam kuna mambo kadhaa yamejitokeza na kuteka vichwa vya magazeti hatimaye kufungua mihadala katika vyombo vingine vya habari zikiwemo radio na runinga.
Suala pekee zito ambalo limechukua nafasi pana na kuamsha mijadala ni lile la Jenerali Twaha Ulimwengu kutaka Rais Mstaafu na Mwenyekiti wa CCM Dk Jakaya Mrisho Kikwete ashitakiwe mahakamani kwa kutumia fedha za umma vibaya kwa kuanzisha mchakato wa Katiba unaodaiwa kukwama kufikia tamati yake.
Matamshi ya Jenerali UVCCM Mkoa wa Arusha tumeyapokea kwa mshituko , fazaha na masikitiko makubwa kwa kumuona mwanataaluma huyo akijadili kwa jazba, chuki na kuonyesha kinyingo dhidi ya utawala wa CCM pia akipotoka .
Tumjuavyo Jenerali ni mmoja kati ya vijana waliowahi kufanya kazi za kisiasa na kiutawala kwa karibu sana enzi za utawala wa Mwalimu Julius Nyerere akiwa sanjari na baadhibya vijana wenzake katika TANU Youth League kina Ukiwaona Ditopile Mzuzuri , Jacson Shija.2Andrew Masanje, Mashaka Nindi Chimoto, Jakaya Kikwete , Edward Lowassa,Abdulrahman Kinana, Prince Bagenda, Isdory Shirima na makada wengine kadhaa .
Kwa bahati mbaya sana yaonekana ndoto na malengo ya Jenerali hayakuweza kutimia kisiasa, ghafla mwanataaluma huyo akawa adui na mkosoaji mkubwa wa CCM hasa katika utawala wa Rais Benjamin Mkapa.
Kwa muda mrefu amekuwa akiiandima kuitia kona yake magazetiniviitwayo Rai ya Jenerali Ulimwengu huku akizshambulia tawala za serikali za CCM kwa masuala kadhaa ambayo mengine yakiwa hayana hata msingi, aana, mantikin wala ukweli wowote.
Hata hivyo wakati fulani Jenerali mtakumbuka kuwa alikumbwa na tuhuma tata ya uraia wake na kuonekana akihodhi uraia wa nchi mbili yaani wa Kinyarwanda na Kitanzniia. Akaingia hatiani na kuthibitika hatimae kuvuliwa uraia na kutakiwa kuomba upya uraia wa Tanzania ikiwa atapenda, jambo ambalo amelifanya na kulikamilisha, hivi sasa ni raia halali.
Akiwa na matumaini makubwa kuwa ni mmoja wa viongizi waliostahili kushika madaraka ya juu katika serikali ya Tanzania kutokana na mchango wake, akajikuta akiwekwa kapuni na kusahauliwa.
Wakati Rais Mkapa akiwania urais, Jenerali akawa mtu wa karibu na wa mkono wa kulia kwa wakati wote, cha kustaajabisha na ambacho bado ni siri , Mzee Mlapa aliposhika usukani wa uongozi hakumtazama kwa jicho la huruma wala ahsante kwa kutopewa nafasi yoyote.
Kalamu yake ya uandishi tokanhapo ikaanza kuandamana , kuinanga na kuisakama kila kukicha serikali ya Rais Benjamin Mkapa kwa miaka yote kumi , jambo ambalo wakati fulani Mzee Mkapa katika moja ya majukwaa ya kitaaluma pale chuo kikuu cha Dar es salaam akashindwa kumstahamilia Jenerali na kujikuta akisema wapo ambao huandika kwa chuki dhidi ya serikali yake kwasababu tu watu hao wamenyimwa madaraka na vyeo.
Kwa kipindi kirefu sana mwanataaluma na mwanasiasa huyo akapotea kwenye ramani ya kisiasa baada ya kukosa kupewa nafasi kadhaa wakati akihesabika ni mmoja wa makada wa CCM shupavu na mwaminifu tena akiwa kijana amstari wa mbele lakini kwasababu ambao ni zaidi ya uraia, uslama na hadhi ya kutopewa dhamana ya juu, hakuwa kama wenzake katika medani za kukabishiwa dhamana za utawala aidha kwa yale ambayo alikuwa anayajua na asiyoyajua wakati wenzake na dola wakiwa wanajua na kumjua zaidi ya vile anavyojijua.
Kwa mukhtasar wa maneno kiini cha kutopewa nyadhifa na madaraka ya uongozi kwa kadri alivyojiamini na kutaraji hakuweza kuambulia kwasababu hakuwa akionekana kutosha pia medani za utawala zilijuwa zikijua amepungukiwa sifa kadhaa muhimu na nyeti za kiongozi kipewa kwa medani na viwango alivyotaraji akabidhiwe.
Ghafla akajiengua pole pole na kuanza kuvua joho la uanasiasa akajiingiza na kuwa mwanaharakati ambaye lengo lake apate mwanya wa kuyatumia majukwaa ili kuishambulia serikali kwa kadri atakavyo kama ambavyo alivyowahi huko nyuma kufanya huko nyuma na anavyofanya sasa.
MCHAKATO WA KUUNDA KATIBA MPYA YA TANZANIA
Si watawala wengi ambao huwa wana fikra, ujasiri, mawazo na utamaduni wa kuzungumzia mabadiliko ya Katiba ya Nchi zao wanapokuwa madarakani hususan Barani Afrika na kama alivyothubutu Dk Kikwete .
Uamuzi wa Rais Mstaafu Dk Jakaya Kikwete ulikuwa ni wa aina yake na hata kufikia kuwashamgaza baadhi ya viongozi na wanasiasa wenzake ndani ya CCM wakati wa utawala wake .
Kwa kujiamini kwake akiwa hana woga wala kitete, akasema midhali Taifa letu linaelekea kufikisha miaka 50, ipo haja ya kuandika upya Katiba yake kulingana na mahitaji yaliopo pia matakwa ya wakati huu na ujao kwa miaka mingine 50 na zaidi.
Mchakato wa dhamira ya uundwaji wa mabadiliko ya Katiba MPYA haukuzuka kama uyoga wakati wa masika, uliundiwa sheria yake na bunge, ukapitishwa kisheria na kuanza utekelezaji wake hadi mahali ulipofikia.
UVCCM tunamtaka Jenerali aache kupotosha ukweli ulivyo , mchakato ule haujakwama ila umezingwa na miingiliano ya vipindi vya uuitishaji wa kura ya maoni , muda wa kufanyika uchaguzi mkuu wa oktoba mwaka 2015 na kipindi cha kisheria kwa Rais wa awamu ya nne aliyeanzisha mchakato huobkubaki kwake madarakni kisheria.
Idhini ya matumizi ya fedha za umma kwa mchakato wa Katiba ziliidhinishwa na bunge kwa nia na dhamira njema ya Taifa kuandika Katiba yake MPYA na wala si ubadhirifu au matumizi ya israf kama anvyotaka Jenerali jamii imuamini asemacho .
Kazi kubwa ya uandikaji wa Katiba imekamilika, rasimu ya Katiba imekabidhiwa serikalini, kinachotakiwa sasa ni kuitishwa kura ya maoni ili wana nchi watumie halibyao kidemokraia kwa kuamua waseme ndiyo au hapana.
Alichokionyeaha Jenerali mbele kadamnasi jana ni kejeli na dharau isiyostahili , ameonekana kujawa na nyongo ya hamaki kutokana na kumbukumbu zile zile za kuwekwa kando ya utawala wa Mkapa kisha kuzikwa katika kaburi la sahau na utawala wa Kikwete .
Anaposimama huku mishipa ya shingo ikimkakamaa na kusema Dk Kikwete anastahili kufikishwa mahakamani, anaonyesha kuitapika nyongo iliosheheni mwilini mwake hatimaye ajipe tahfif ya kuona ni vipi atamkomoa Kikwete kwa maneno ya jikoni na uzushi.
Vyovyote vile iwavyo Dk Kikwete hawezi kushitakiwa kwa mujibu wa Katiba na sheria, hana shitaka linaloweza kumkabili kama anavyojaribu kuota njozi za mchana Jenerali na walio nyuma yake.
Ni vyema akajihesabu kuwa aliyoyataraji kwa muda mrefu hakuyapata ,asahau, hakutazamwa kwa jicho lolote jema na hakupewa kama alivyotaka iwe kwasababu husika ambazo dola hawezi kuhojiwa.
Aidha matamshi yake ya jana ni katika juhudi zake za kujifariji , kujiburudisha, kujiliwaza huku UVCCM Arusha tukiwataka wananchi wema kumpuuza kwasababu anaelekea kuzeeka vibaya huku akiwa ametunisha mashavu ya hamaki na wingi wa hasira za mkizi.
HITIMISHO
UUVCCM Mkoa wa Arusha tunawaomba na kuwasihi sana watanzania wenzetu kuwa makini pia kuweka tahadhari kwa aina ya watu wenye matamshi ya hamaki na hasira uchwara kama za Jeneral.
Tungeomba sana mtu huyo apuuzwe na wala wananchi wasikubali kunasa mtegoni kwa ushawishi wa maneno ya kupika yenye ghiliba na hadaa huku Jenerali akisaka umaarufu usioweza kumpatia tija wala faida yoyote.
Tulitegemea sana Jenerali atamke na kuteka Dk Kikwete ashitakiwe mahakamani kwa kutumia fedha za umma katika ujenzi wa shule za msingi, sekondari, zahanati ,vyuo, barabara za lami, madaraja na majengo ambayo hayakuwepo tokea enzi za wakoloni hadi kuanza kwa utawala wa awamu ya kwanza .
Pia tunamfundisha na kumuelisha Jenerali kwamba aache kukurupuka na si kweli asemayo kama CCM ilihofia na haikutaka ujio wa vyama au Mwalimu Nyerere ndiye aliyeshinikiza kuingia vyama hivyo kwani wakati vyama vingi vikiruhusiwa kisheria mwaka 1992 Rais alikuwa Mzee Ali Hassan Mwinyi si Mwalimu Nyerere .
Tume ya kukusanya maoni ya wananchi kuhusu mabadiliko ya mfumo wa kisiasa nchini ilioongozwa na Marehamu Jaji Francis Nayalali iliundwa na Mzee Mwinyi akiwa Rais.
UVCCM Mkoa wa Arusha inalaani vikali matamshi ya upotoshaji yaliofanywa na Jenerali ambaye anaonekana bado anaugulia majeraha ya kisiasa baada ya matarajio na ndoto zake kuvia na kwenda kombo.
Si kweli kama Tanzania haijapata viongozi wenye upeo, dhamira na kusudio la kuleta mabadiliko kama Jenerali binafsi anavyojaribu kuzua na kueneza chuki na maneno ya mifakano.
Tanzania ilioachwa na wakoloni siyo ile liyoichukua na kuiacha Mwalimu Nyerere, aliyoichukua Mzee Mwinyi si ile aliyoikuta Mzee Mkapa na kumwachia Dk Kikwete pia Tanzania ya sasa ni nyingine kabisa na wala si ile ya awamu ya kwanza, pili au ya tatu vile vile haifanani na itakayoachwa na Rais Dk John Pombe Magufuli baada ya kumaliza muda wake madarakani kikatiba.
Mwisho kabisa tunamueleza Jenerali kuwa siku zote ajue kuwa nguo ya kuazima haisriri matako na mambo ya ngoswe nibheri akaawaachie ngoswe wenyewe .
Ahsanteni sana kwa kunisililiza.
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI Martin Munisi mwkt