UVCCM, mbona mmerudia yaleyale ya Masauni?

Bundewe

JF-Expert Member
Jun 14, 2011
400
141
Ninavyoelewa mimi ni kwamba kiongozi wa uvccm anapoingia madarakani asizidi umri wa miaka 30. Kanuni hii ndo iliyomng'oa madarakani Masauni mwaka 2010 akidaiwa alikuwa na umri mkubwa. Juzi uvccm wamefanya uchaguzi na kumchagua Mbunge wa Donge, Z'bar Mh. Sadifa Juma Hamis kuwa mwenyekiti.

Kwa mujibu wa kumbukumbu za Bunge, Mh. Sadifa amezaliwa tarehe 7 Februari 1982. Hivyo mpaka tarehe 7 Oct 2012 alitimiza umri wa miaka 30 na miezi 8. Vipi kanuni imerekebishwa? au naye ana vyeti viwili vya kuzaliwa?
 
Hapo hata mimi nitakujibu, ni kuwa ujana uanishia miaka 35, hivyo katika kipindi cha uongozi umri wake usizoidi miaka 35. Kwa hiyo kwa mtazamo huo atamaliza uongozi akiwa na miaka 35. Hawajakosea
 
aiseeeeee babaangu ilo lisikupe shida ngoja aapishwe akae madarakani kesi zitaanza kufunguliwa kuhusu umri wake,,kwani wewe uwajui magamba
 
Mkuu ni wewe tu hujaelewa vizuri, kanuni inataka mtu asizidi miaka 30, huyo jamaa ana miaka 30. Hivyo angekuwa amevunja kanuni kama wakati anagombea angekuwa na miaka 31 au zaidi.
Kifupi yuko ndani ya muda sahihi.
 
Naona kama Bundewe is right. Au CCM UV Kanuni yao inataka mpaka miaka isomeke 36 ndo atakuwa kazidisha umri wa kuwa kijana? Ukawa na 35yrs, 11 months, 29 days, 23 hrs, 59 min. Kwao katiba inaruhusu. Kiukweli huyo jamaa hakustahili kugombea. Itakuwa ni takrima imetumika kupindisha kanuni
 
Mkuu ni wewe tu hujaelewa vizuri, kanuni inataka mtu asizidi miaka 30, huyo jamaa ana miaka 30. Hivyo angekuwa amevunja kanuni kama wakati anagombea angekuwa na miaka 31 au zaidi.
Kifupi yuko ndani ya muda sahihi.
Mchango wako unafaa kufunga mjadala huu.
 
Mkuu ni wewe tu hujaelewa vizuri, kanuni inataka mtu asizidi miaka 30, huyo jamaa ana miaka 30. Hivyo angekuwa amevunja kanuni kama wakati anagombea angekuwa na miaka 31 au zaidi.
Kifupi yuko ndani ya muda sahihi.

Naona hapa kidogo nawe hujaelewa kanuni. akifikisha miaka 31 maana yake kazidi mwaka mmoja. akifikisha miaka 30 na mwezi mmoja mana yake kazidi mwezi mmoja, akifikisha miaka 30 na siku moja maana yake kazi siku moja. huko kote ni kuzidi tu bila kujadi to what extent. Kikanuni hatakiwi "kuzidi" miaka 30.
 
Ninavyoelewa mimi ni kwamba kiongozi wa uvccm anapoingia madarakani asizidi umri wa miaka 30. Kanuni hii ndo iliyomng'oa madarakani Masauni mwaka 2010 akidaiwa alikuwa na umri mkubwa. Juzi uvccm wamefanya uchaguzi na kumchagua Mbunge wa Donge, Z'bar Mh. Sadifa Juma Hamis kuwa mwenyekiti.

Kwa mujibu wa kumbukumbu za Bunge, Mh. Sadifa amezaliwa tarehe 7 Februari 1982. Hivyo mpaka tarehe 7 Oct 2012 alitimiza umri wa miaka 30 na miezi 8. Vipi kanuni imerekebishwa? au naye ana vyeti viwili vya kuzaliwa?
Ongeza na ile miezi 9 au 8 ya mimba!
 
Yaani mfano mzuri ni kama umri wa kuustafu.ikifikia tu tarehe yako ya kuzaliwa kutimiza umri husika(60/65) unaachia hapo on the date.kanuni zimepindishwa tena kwa wote mwenyekiti na makamu wake.japo wamejitahd kufichaficha kwnye CV ukweli utabaki kuwa umri wao una walakini sana!kila kitu kinawezekana Tanzania
 
Back
Top Bottom