UVCCM: Hussein Bashe amjibu Nape kiaina

Nyie nani kawaambia sio raia? mama yake mnyamwezi.Unajua hakuna mtu mbaguzi kama mwaafrika sema tu hakujaliwa
Hata kama waziri amesema Bashe ni raia sisi kama CCM bado tunamuona si raia" - Luteni (mstaafu) Y Makamba......................:heh:
 

You guys dnt personify your arguments...
 
Hawa ni Waarabu wa Pemba wanajuana kwa vilemba. wote ni Magamba a.k.a Mafisadi
 


Hussein M Bashe
 
Nimeona kwa vipindi tofauti, watu wakijajaribu kutumia maoni au mawazo fulani ya mwl Nyerere kujenga hoja zao, ni kweli kabisa kwamba mawazo ya Mwl Nyerere ambaye ndiye muasisi wa taifa letu ni muhimu sana kwenye kuamua mustakabali wa nchi yetu na ndiyo maana maoni yake yametumika kuua ndoto za urais za watu wengi, wakiwamo wakina Mzee Malecela na wengine wengi, akiwemo pia Mark Bomani kwa hoja ya kukataa Rais kutoka sukumaland or kanda hiyo, lakini ikatumiwa hoja ya ujaji wake kumzuia. Tunatakiwa kumuenzi Mwl Nyerere siku zote, lakini tuwe makini tunatumiaje maoni yake. Kwa taarifa ambazo hazipingiki ni kweli kwamba Lowassa alikuwa groomed kiuongozi na Mwl Nyerere kwenye Chama tangu wakati ule akisoma UDSM, na vijana wengine waliokuwa kwenye kundi hilo wakiwemo Kikwete, Kinana, Marehemu Ditoplie na wengineo, na Nyerere huyo huyo alikuwa akimtumia Lowassa kumuwakilisha sehemu nyingi kichama, wakati huo Lowassa akiwa msaidizi wa Marehemu Mzee Kawawa pale Lumumba, lakini baada ya Mwinyi kuingia madarakani 1985 na Mwl Nyerere kurudi butiama, ingawa bado alikuwa anapatikana msasani na safari zake mikutano yake ya kimataifa duniniani, lakini officiially address yake ikawa butiama na tuliona viongozi wengi wakienda huko kwa ushauri wakati ule. Ilianza kuonekana feeling fulani kama Mwl Nyerere amenyangnywa nchi yake aliyokuwa anaipenda, maneno ya mtaani yakawa kwamba Mwinyi alikuwa hamuheshimu tena Nyerere na alikuwa haendi kuomba ushauri wa kila jambo, ghafla uadui ukahamia hadharani na Mwalimu akawa akimtukana Rais mwinyi aliyekuwa Ikulu kwa matusi mengi mengi hadharani. Tutakumbuka alisema unakuwaje Rais ambaye ukifika kitandani nyumbani halafu mkeo anabadilisha maamuzi yako ya nchi - sijui ingekuwa leo tungesemaje?? hehe . Kwahiyo umaarufu wa kisiasa walioupata Lowasa na Lyatonga wakati ule kuelkea 1995 uliasisiwa na kubarikiwa na Mzee Mwinyi, na alichokiona Mwl Nyerere ni kwamba atazidi kupoteza clout yake kwenye maamuzi ya nchi akiruhusu hayo kutokea na ndiyo maana akaanza politcal games zake - hamna anayemzidi hapa Tanzania, akahakikisha anamshawishi Lyatonga kuhamia upinzani NCCR, akijua haiwezekani dola iruhusu nchi ichukueliwe na upinzani kwa wakati ule na Lowasa akaambiwa kwa makusudi kwamba akahukue fomu pamoja na Kikwete - ambaye hakuwa na umaarufu wowote wakati ule, lakini Nyerere akijua kichwani kwake anamtaka nani na hawa wote wakaingia kwenye mstari. Kwa umaarufu wa Lowassa wakati ule, ni ukweli usiopingika kwamba angeenda kwenye mkutano mkuu, angeshinda na angekuwa Rais 1995, kama amabvyo Mzee Malecela angeingia kwenye mkutano mkuu 2005, angesumbua, kwahiyo njia rahisi ya wagombea kama hawa ni kuwakata majina kwenye kamati kuu. Kulikuwa na mvutano mkubwa sana ndani ya kamati kuu kuhusu Lowassa kipindi kile na ikabidi kujenga hoja ya nguvu ili kumzuia, zikaletwa tuhuma za kuchonga ambazio kamati kuu ilitupilia mbali, lakini Mwl Nyerere akatumia VETO kujenga hoja yake na hamna mtu anaweza kumpinga, lakini baada ya pale, kama baba na watoto wake aliowapenda< aliwaita wote mmoja mmoja pale msasani na Lowassa akaambiwa una miaka 42 tu, natambua uwezo wako mkubwa sana, subiri wakati wako utafika, usiwe na papara na siyo hvyo tu, wasaidizi wake wa karibu wanasema Mwalimu alikwenda Geneva na kukutana na kundi la Watanzania waliohoji kutoswa kwa Lowassa, akasema kwenye vijana niliowa-groom, huyu ndiye mwenye uwezo zaidi, ila sasa haikuwa muda wake, niachieni, najua ninachofanya. Kuna mazuri mengi sana na mabaya aliyoyafanya Mwl Nyerere na tunatakiwa kumuheshimu siku zote kwasababu Baba wa Taifa atakuwa mmoja tu kwa Tanzania lakini tusishabikie maoni yake au maamuzi, ni muhimu kuyajadili na kufanya tathmini jinsi ambavyo yatatusaidia kwenda mbele na maendleo ya nchi yetu. Nawasilisha
 

Hahahahah sarakasi hizi! Lowassa na ufisadi wote kweli aje kuwa raisi wa nchi? Hebu acheni mazingaobwe of all the peoples Lowassa kabisa? Kwanza huyu avuliwe Gamba na kufukuzwa CCM ni mwizi na Fisadi.....hatutaki maneno le eti alikuwa groomed na Nyerere hahahahaha kituko hiki. Nyerere huyo huyo alimuuliza kijana mdogo kama wewe umetoa wapi huo utajili ....kifupi hafai hafai kabisa.
 

Kwa yote uliyosema wenye akili zao umewapa mwanga zaidi kuliko ilivyokuwa hapo nyuma
 

hehehehe, Rev Masanilo, wewe ni senior kidogo, epuka ushabiki na tujaribu kusaidiana kueliminishana humu kwenye forum, argument yangu wala haikuwa kuhusu Urais wa Lowassa, lakini kuna mtu hmu ndani alisema tunauguzwa homa ya Lowassa, tukisikia jina tu, tunafikiria Urais. Kasheshe nzito

Hoja yangu ni kwamba mawazo au maoni ya Mwl Nyerere siyo msaafu, lakini lazima tuendelee kumuenzi na kumuheshimu siku zote, lakini kufanyia tathmini za kina mambo aliyofanya ili utusaidie kwenda mbele. Hayo mengine nadhani siyo thread yake hii
 

Nimerudia tena ulichoandika ! Sina ushabiki na si tabia yangu huwa naandika ninachofikiri. Hiyo grooming ya Lowassa na Nyerere unaweza iweka wazi kwa evidence? Kwa kuwa saidia huyo Edward Lowassa akisimamishwa na CCM nina wahakikishia wapinzani wanachukua uraisi. Hasafishiki kwa kashfa za ufisadi ndugu yangu.
 
Kwa yote uliyosema wenye akili zao umewapa mwanga zaidi kuliko ilivyokuwa hapo nyuma

Ha ha ha ha ha ha ha ha ha Kaka mpaka leo unakumbuka majibu yangu?na kura alinipa huyo mzee kama unakumbuka maana yake aliridhika na majibu alopata ,usipotoshe sikufura bali nilitabasamu na kuwakumbusha wana nzega jinsi mbunge wetu kaka seleli kamati ilimsaidia angalau akajenga kale kahoteli ketu kazuri kanako itwa RICHMOND pale nyumbani.

Sasa kaka ( S) why hidding ur identity?
 

Hivyo viwili mazee ntavipata wapi kwani napenda na wanangu waje wavisome
 
Kuna mambo ya msingi sana ameeleza na kama Mkabila Nape akisoma haya maelezo ya Bashe anaweza kubadilisha approach anayotumia kufikisha ujumbe ambayo imekuwa na madhara kuliko kujenga shame on you Nape
there you are makupa
 
Jitu lisiloonekana aka invisible naomba kama mnaweza hii tread iwe article kwa ajili ya kumbukumbu
 
Siipendi ccm..but katika hili bashe kanena,suala la kuwa katumika kupresent au vp sio la msingi sana,the issue is katoa hotuba ya kweli ambayo kwa mwana ccm makini nakifuatilia na kuifanyia kazi itawapeleka one step ahead.Hata kama ametumwa basi nawapongeza waliomtuma kwa kuandaa speech nzuri na yenye mashiko.Ni ujumbe mzuri kwa nape kama ana akili atajifunza kitu,ni matumaini yangu ataacha uropokaji na kuongea vitu bila kupima madhara yake baadaye.Hongera bashe kwa kutumia muda wako kuandaa hii speech I am looking at the message and not where it comes from.
 
Ndugu Bashe, naomba nitoke nje ya mada kidogo. Hivi unafanyaje kujua ID nyingine za watu? Kuna ID kama mbili hivi ambazo umeziunganisha na nimezifuatilia mtiririko wa maneno na kuona ni kweli ni mtu huyo huyo. Inaboa kuna watu wanajiuliza na kujijibu wenyewe humu.

Nikirudi kwenye mada, hotuba ulioitoa ni nzuri sana endapo tu hakuna ajenda ya siri nyuma ya hotuba hiyo ila ukitaka uonekane mbaya CCM basi we sema ukweli. Vijana wengi walioko CCM wako pale sio kwa sababu ya kuridhika na sera za chama bali kwa maslahi binafsi kutokana na uwezo mkubwa wa chama. Hii ndio sababu hakuna suala la kujitolea kwa chama kama ilivyo miaka ya nyuma. Hata kwenda tu kwenye mikutano ya chama inabidi yatumike malori kwenda kuwachukua na kuwarudisha na kupata chakula, kanga, fulana au kofia kinyume cha hapo haendi mtu.
 

Jaluo

ID zipi hizo nasisi tuzijue?
 

iShh...Personal attack? for red above try it again!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…