UVCCM: Hussein Bashe amjibu Nape kiaina


SHALOOOM JAMVINI

Sikupanga kuchangia bali hii Hoja ya NGONGO imenivutia HUWEZI KUBARIKI AFRIKA KWA KUKUMBATIA MAFISADI NA WEZI.
Hoja ya Bashe ni kwamba LOWASA AKITEULIWA NA CHAMA ATAMUUNGA MKONO,kwani hana mashaka juu ya uwezo wa lowasa kufanya kazi,nakubaliana na Bashe kabisa LOWASA ni mchapa kazi,hoja hapa ni kwamba kama lowasa ni mwizi kwanini yupo uraiani?BASHE amewatega wengi amesema akiteuliwa na chama tujiulize je CCM (MAGAMBA) huteua wezi?majambazi?ninachofahamu kila mtu anauhuru wa kusema lakini haki ya kuhumu ni ya mahakama kama el hajafikishwa mahakamani kwa wizi basi hana kosa.

Taifa letu tukufu tanzania limekumbwa na wimbi la kuhukumiana,juzi tumemsikia VUVUZELA akisema DR WA UKWELI ni FISADI eti analipwa hela nyingi au MBOWE KAMANDA MKUU walipoibua zengwe la ufisadi wa NSSF ,je tuwakatae dokta kwa kuwa katuhumiwa na magazeti ya UHURU na Mzalendo na jambo leo yameandika? kama ni wezi wapelekwe mahakamani wahukumiwe hapo tuwakatae sio tuhuma za kisiasa, Ninachokiona hapa kama EL anatuhumiwa kwa kosa la RICHMOND watanzania tusiwe wavivu wa kufikiri je maamuzi yale ni LOWASA NA MAMA REGINA?nani aliamua ? jibu tunajua ni serekali kupitia baraza la mawaziri,nani alikua kiongozi mkuu wa hiyo serekali?tunamjua,nani alikuwa mweneykiti wa kikao hicho?tunamjua mnakumbuka dk mwakiembe alisema wameficha mengine kulinda mamlaka ya URAIS, tumejinga utamaduni wa kupenda kujibu mambo kirahisi na kupelekea kutotatua tatizo la msingi maamuzi ya kifisadi mengi yamefanyika kupita baraza la mawaziri lakini wandugu tumekuwa wakwanza kutuhumu tunawataka na kusahau msingi wa tatizo.

Rada,tunamtuhumu chenge,kwani aliamua kununua rada yeye na mke wake? Richmond tunamtuhumu lowasa kwani aliamua yeye na mke wake? EPA na KAGODA tunawatuhumu kina maranda,rostam,jitu,na wengine kwani mmesahau balali alisema pesa zile zilienda CCM na sisi wote 2005 tukapewa kanga na tshirt na kuimba nyimbo zao na kutoa asilimia zaidi ya 80%

Dogo huyu wa magamba ameongea mambo ya msingi sana lakini nafahamu CCM hawachelewi kumdhibiti muda si mrefu utasikia kapigwa barua ya onyo na hako kacheo walikompa watakakwapua shauri yake CDM tu ndio uhuru wa kutoa maoni unapatikana,mimi sijaona kosa lake kusema anamuunga mkono lowasa ikiwa magamba watampitisha kama wakati huo atakua segerea basi BASHE atatuambia anamuunga mkono nani.ILA UKWELI MSINGI WA HOJA YAKE KUMUUNGA MKONO EL NI UWEZO WA KUFANYA KAZI NA HILO KULE MAGAMBA WAPO WAWILI EL NA MZEE WA MAKILOMITA NA MABARABARA wengine porojo tuuuuuuuuuuuuuuu
 

Ndugu Bashe, hapo nilipo bold are you serious???.... Halafu wanatokea watu humu jamvini kukupongeza kwa kuweka huu upupu wako hapa...
 
Suala sijui bashe katumwa anamuongelea nani hili si la msingi, la muhimu ni Ujumbe aliousema una mashiko si mchezo. Saa nyingine hata vichaa na wendawazimu huongea ukweli judge the message not the messenger

Bashe kaka acha janja yako ya darasa la kwanza. Speech yako inajionesha wazi kuwa una ajenda ya siri. Sidhani kama kweli una nia ya kuifanya CCM na UV-CCM ibadilike. Lengo lako hapa ni kubadilisha Ajenda ya kuwawajibisha Mapacha watatu. Hasa hasa hapa una lengo la kumsafisha kaka yako RA. Jaribu kuwa mkweli WARIA!!!!!
 

Hili nalo neno!!!
 
Hamna kituhapo zoote hizo ni dalili za mfa maji haachikutapatapa!
Alikuwa waapimuda waaote kumzuia mwenyekiti asiwavue gamba wenzieilhalinayeye analo?...au kwani yeye hajuikuwa mwekiti wake nikiazi wala hana uwezo wakutekeleza ahadizalizozitoa kwa watanzanaia? alikuwa hajui?
Alikuwa waapikuruhusu tena jina JK kugumbea uraisi kwamaraya piliilihali amnajua nikimeo? ALIKWINA?
mfamajihuyo anauma na kupooza anamtaka EL hukuanajifaragua!
 
Except for the Lowassa affiliation, which is a dealbreaker for any serious Tanzanian, bandiko la kwanza lina mantili. Kama kuna a verbatim account ningependa kuiona. Bashe anasound reasonable na genuine ( as far as I can tell, the Lowassa affiliation could prove a costly frankness). Tungependa kuona future ya CCM inakiwa shaped na views hizi bila ya kuwa corrupted na power as is often the case with revolutionaries ( most recently Museveni springs to mind).

Inawezekana hii independency of mind ndiyo iliyomfanya apigwe vita na ugombea ubunge ukaenda kwa yule fraud Kigwangwalla? Not to pick sides or focus on personalities, this Bashe fellow sounds way better than his mostly tarnished ilk. But somehow he manages to shoot himself in the foot by being in the Lowassa camp. A pity, because he may just have a shot at coherency. But how coherent can he be if he is this misguided?

But can he take the monstrous green behemoth? Is CCM as a party redeemable at all? And if not is there a viable alternate? How can a reasonable sounding chap like Bashe embrace a corrupt failure like Lowassa?

At present, IMHO I fear the answer is NO to both questions at least in the short term. But far from discouraging us, this should move us to work even harder to promote a new wave of thinking in both CCM and the opposition.

I am following this fellow closely.
 

- Jamiiforums, baada ya kazi nzito sana tuliyoifanya ya kumng'oa Lowassa, Msabaha, Karamagi, na Athur Mwakapugi, kazi ambayo kuna baadhi ya member wenzetu hapa kidogo iwakoseshe maisha yao, wengine wametishiwa kukamatwa, wengine ametishiwa kupigwa, wengine wametishiwa familia zao, leo hapa mbele yetu tuna kiongozi mtarajiwa anayesema bila aibu wala kutuogopa kwamba Lowassa ni kiongozi safi na kwamba anamuunga mkono kwa 100%, halafu kuna baadhi yetu wanaosema huyu anafaa sana?

- Are you guys out of your mind nini? Sisi hapa tumehangaika kwenda Texas kutafuta ofisi za Richmond na kukuta ni kampuni ya Office Supplies, tumepiga picha ile ofisi na kuwapa wandishi bongo, ndio taifa likaanza kushituka na mbinu chafu za Lowasaa na Msabaha on the ishu, yaani ile kazi yote tuliyoifanya mpaka kumng'oa Lowassa leo hapa anakuja mtu wake anasema wazi tena kwa kujigamba kwamba Lowassa is good, halafu kuna tunaompa heshima?

- I mean kina Kubeenea wameishia kumwagiwa Tindikali kwa sababu ya kutusaidia sisi JF kuuelimisha umma kuhusu Richmonduli, leo kuna kiongozi mtarajiwa anayetuambia kwamba eti Lowassa the masterminder wa Richimonduli ni kiongozi safi na kwamba anamuunga mkono 100% na kuna members hapa wanakubali kwamba eti huyu anafaa sana? Hebu someni vizuri sana hiyo hotuba yake ni wale wale mapacha watatu, yaani JF kumkoma nyani inaweza kumpa huyu free pass kirahisi hivi?

- Count me out on that wagon, Bashe we are not fools here man, take that to vikao vya CCM not here, hapa ndipo moto wa kumng'oa Lowassa ulipoanzia, wrong number hapa, kuna watu hapa kidogo wapoteze maisha yao kwa sababu ya kuifuatilia Richimonduli kama wewe hujasahau uliyofanyiwa huko CCM, hapa kuna some of us hatujasahau pia ufisadi wa Lowassa, so take your nonsense huko huko UV-CCM!


Field Marshall Es - Ni Wazee Wa Sauti Ya Umeme!
 

Heshima kwako FMES

Mkuu soma bandiko langu sawa sawa huyu jamaa nimemweleza wazi hafai kabisa katumwa kupima upepo unavumaje !.
 
FMES,

Hiyo Lowassa element iko so concerning, however attractive this fellow may look otherwise. Lowassa ananuka beyond salvation, na kwangu mimi kukubali kujiuzulu kulikuwa kukubali guilt.
 
Heshima kwako FMES

Mkuu soma bandiko langu sawa sawa huyu jamaa nimemweleza wazi hafai kabisa katumwa kupima upepo unavumaje !.

- Mkuu ninaamini sana maana majuzi kuna mjumbe mmoja wa NEC ya CCM, alikuwa ananiambia bila uoga wala aibu kwamba Lowassa is the next President, well over our dead bodies!

- Hivi hapa JF kuna mliowahi kusikia jinsi Lowassa na kundi lake walivyojaribu kila mbinu kuikwamisha ripoti ya Mwekyembe isifike bungeni? Zile Millioni 4 walizokuwa wakipewa wabunge kuikataa ile ripoti zilikua zinatolewa na nani? Kwenye ripoti ya Mwekyembe, alisema wazi jinsi walivyojaribiwa kupewa magari na majumba ili wapindishe ukweli ni nani aliyetaka kuwapa magarii na nyumba?

- Hivi mnajua kwamba at one point Lowassa na kundi lake walitengeneza ripoti ya siri ambayo waliitaka isomwe badala ya ile original ya Mwakyembe, ikabidi Mwakyembe ajfiche usiku wa kuamkia kwenda bungeni maana walikuwa wakijaribu kila njia kumshambulia ili wachukue ile original ripoti, sasa leo hapa tuna mtu anayejisema wazi kwamba ni mtu wake, na kuna some of us tunataka kudanganyika na maneno machache matamu aliyoyaweka kuficha makucha yake ya kweli?

Well, this is JF sio wote hapa wasahaulifu!, na akirudi tena basi tutaenda kufukua archives zote za Richimonduli zipo humu! Halafu atuambie jinsi Lowassa alivyo malaika wa Mungu!

Phweeeeew!


FMes!
 
FMES,

Hiyo Lowassa element iko so concerning, however attractive this fellow may look otherwise. Lowassa ananuka beyond salvation, na kwangu mimi kukubali kujiuzulu kulikuwa kukubali guilt.

- Dataz zipo wazi kwamba Lowassa alimfuata Rais kwa siri kabla ya kwenda Dodoma kwenye kile kikao cha bunge on Richimonduli, Rais akamwambia kama ana utetezi akauote bungeni, he did not akaishia kukimbia wananchi na kuanza kampeni za pembeni pembeni kuwachafua wale wote wasiomkubali, mpaka kutaka kumuondoa U-Spika Sitta na uanachama wa CCM, he almost did it!

- Sasa leo eti Bashe anayetuambia kwamba Lowassa ni msafi sana, anaweza kukusanya maoni ya UV-CCM Tanzania nzima objectively? Halafu kama kawaida yetu wabongo na wepesi wa kusahau, tayari tumeshaanza kumbeba na maneno ya kumpamba kwamba ameongea vizuri sana, people soma vizuri hiyo hotuba yake, uone ilivyotengenezwa kwa ujanja ujanja na kuuma uma maneno, I mean we are not all stupid hapa JF! and not that Fast!


FMeS!
 
Bashe ni wale wale tu na yeye analipiza kisasi tuhuma za uraia wake kwa akina Makamba. Kama anaona kuwa hakuna chama kinafanya si awabwage chini tuuu?? Leo yupo anapiga story zile zile tulizozoea za kuvuana magamba!
 

Big up lampard, nilikuwa nashangazwa sana na uharaka wa wana JF wa kumpongeza bashe kwa hotuba ya kawaida kama hiyo, nilitaka nisome kwanza mawazo ya wana JF ndio nichangie, naona umeniwahi though umezungumzia na mambo mengine amabayo nilikuwa siyajui kama ya UDOM.kwani aliyoyazungumza humo kuna asiyeyajua, hayo si ya kawaida tu, kwani yeye ana nguvu gani CCM ya kwamba akisema hayo yatafatwa. ukiangalia kwa undani wa kawaida tu, utagundua anazungumza kwa nafasi ya mkosaji, kutafuta cheap popularity kwamba he can do better, but he cannot, mtu anaetumia hawezi kufanya chochote zaidi ya anachotaka bwana yake. Guys we need to think before just supporting.
 
Sawa mkuu! umeongea vizuri sana na ninakubaliana na wewe kabisaaa kuhusu Rowassa na Richmondi....lakini je, vipi kuhusu kagoda? Ukitufafanulia na hapa hakika utakuwa umemaliza mchezo mzima. karibu FMeS!
 
FMES,

Nikuombe jaribu kuficha hasira zako kwa Lowassa. Haki na Uhuru wa mimi kumuunga mkono LOWASSA akitangaza NIA, na KUTEULIWA na chama changu ni haki yangu ya Kikatiba kama ilivyokuwa haki yako mwaka 2005 kumuunga mkono Mzee Malecela.

Nikuombe uheshimu haki yangu ya kutoa maoni yangu kama wewe ulivyotoa maoni yako ukitaka wagombea wajitokeze..

Leo mimi nimejitokeza openly na kusema ninachokiamini sijaongelea suala la whether Lowassa ana tuhuma ama hapana, tukianza kufukua tuhuma hata mzee wako ana tuhuma za kupokea fedha za EPA kupitia Jeetu Patel lakini hakuna aliekutuhumu kwa wewe kumuunga Mkono 2005 na pale Morogoro zilipoporwa na wezi wakati mama Anne Malecela akizileta kugawia wapiga kura.

Leo hapa nimesema ninachokiamin, come out sema kama Lowassa hana sifa niliyotaja then utakuwa na hoja ukinipa sababu za yeye kutokuwa na uwezo wa kuchapa kazi na ukajenga hoja nitakuelewa.

Tusipige porojo eti Lowassa alimfata Rais na kubembeleza, go and ask Mr. Malecela and he will give u the facts ambazo wengi hawapendi kusikia. Kama Lowassa anahusika na Richmond apelekwe mahakamani, hakuna anayemtetea na wala hilo halina mjadala; mahakama itaamua, kama Lowassa ni mwizi basi ni udhaifu wa mamlaka kutowakamata wezi na kuwapeleka mahakamani. Kama una ushahidi peleka katika authority uje hapa utueleze umepeleka ushahidi wa wizi wa Lowassa na hata mimi nitakuona hero! Tujadili facts mkuu, tusiingilie uhuru wa mtu kuchagua. Nimesema wazi kama chama kitamteua nitampigia kura na nimetoa sababu yangu, na si Lowassa pekee, same applies kwa CDM, wakisimamisha mgombea hawezi kuwa mkamilifu wa kila kitu lakini kila mmoja atahakikisha anampigia kura.

FMES na Wana JF,

Tusipoteze muda mwingi kujadili LOWASSA, huyu kama ana madhambi yake mamlaka husika zitachukua hatua zinazostahili. Nchi yetu ina bahati mbaya tumekumbwa na ugonjwa wa unaoitwa ‘LOWASSA', tujadili issues za maendeleo.

Nikutoe shaka juu ya jambo moja: Ssina historia ya kuficha wala kutafuna maneno katika jambo ninaloliamini, kama wewe ulifanya kazi ya kutafuta ushahidi juu ya mkataba mbovu wa Richmond, nikupe hongera ulitekeleza wajibu wako kama RAIA mwema. Kama utaongelea UADILIFU, wewe mwenyewe ni zao la UKOSEFU wa UADILIFU wa Viongozi wetu. Suala la RICHMOND ni udhaifu wa mfumo wetu, jambo ambalo mpaka leo linatugharimu kama Taifa. Tumelalamika, tumetuhumu, tumekosoa lakini hatujajadili ufumbuzi wa tatizo lililoleta RICHMOND. Leo ni mwaka wa sita bado tatizo lipo lakini bado tunajadili RICHMOND na LOWASSA.

FMES, don't fool people here, tunafahamu why unakuwa na hasira when it comes to LOWASSA. Ni tatizo la familia yenu na ni makovu ya 2005. Nimalize kwa kusema LOWASSA akiteuliwa na kupitishwa na chama nitamuunga mkono asipoteuliwa na asipopitishwa na chama pia nitaheshimu na kufanya maamuzi kutokana na wakati na mazingira ya wakati huo, hiyo ni imani yangu. Mimi nimesema msimamo wangu na kwa jina langu, wewe come out and sema msimamo wako. Kila mmoja wetu atakuwa na maamuzi yake tuyaheshimu, akini kwa sasa tujadili masuala ya NCHI yetu na tutimize wajibu wetu. Wewe binafsi huna moral authority kuongelea uadilifu bcs your background inaonyesha, lakini hatukuangalii kwa Background yako tunakuangalia wewe na unachosema kwa sasa.

Hussein
 
hana jipya anataka ajenda ya mapacha watatu anao watumikia ipite tusahau lakini wajue mwaka huu tunao
 
Adui wa kwanz awa Tanzania kwa mazingira ya sasa ni CCM. jithada zote zinazowezekana kukisambaratisha kama si kukifuta hiki chama zifanywe.

I wsih Ningekuwa Director wa TISS ushauri wa kwanza wa rais JK ni kuwa kama unaipenda na uitakia mema nchi nchi yako nirushusu nisambaratishe chama chako...........

Maelezo ya Bashe, Nape, na makada wa CCM wengine yanaonyesha kuwa Hiki chama hakina uchungu na Taifa. na hakiwez kurdi kwenye mstari kamwe........
 
..........
Leo hapa nimesema ninachokiamin, come out sema kama Lowassa hana sifa niliyotaja then utakuwa na hoja ukinipa sababu za yeye kutokuwa na uwezo wa kuchapa kazi na ukajenga hoja nitakuelewa,

Lowasa ana uwezo wa kuchapa kazi kulliko lets say mlevi Makogoro nyerere au Pinda lakini leo tukisema wanachi wa muleba kule kageara wachague nani awe mbunge wao kati ya Lowasa na Mkongoro nyerere na Pinda . Makongoro Nyerere ataibuka kidedea.. Na ni obvoius Lowasa atakuwa wa mwisho. Jiulize kwa nini

Moja ya sifa ya kiongzi ni Kuaminiwa. Si Phd, sio uachapaji kazi tu. So Lowasa kama alivyo Malechela na wana CCM wengine wengi tu imani kwa wananchi ni ndogo sana. Ukishapoteza imani kwa wnanchi huafi kuongoza labda kama ni Jeshini. CCM Inabidi mtumie nguvu za ziada. Simply CCM is not a place to be kwa mtu anayetaka kuleta mabadiliko.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…