Uuzaji wa silaha waongezeka kote duniani yasema ripoti mpya ya SIPRI

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,011
9,879
Ripoti mpya ya Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Amani mjini Stockholm SIPRI, inasema uuzaji wa silaha uliongezeka kwa asilimia tano kote duniani mwaka elfu mbili kumi na nane. Ripoti hiyo inasema Marekani ndiyo nchi inayoongoza katika biashara hiyo na kwamba kutokana na soko lake, mapato ya kampuni mia moja kubwa za utengenezaji wa silaha yalifikia dola bilioni 420.

SIPRI inasema kampuni za Marekani zilinufaika kutokana uamuzi wa utawala wa Rais Donald Trump wa kuzifanya huduma za silaha za Marekani kuwa za kisasa ili kuihifadhi nafasi yake ya juu dhidi ya China na Urusi. Katika ripoti hiyo Urusi ndiyo iliyokuwa ya pili katika utengenezaji silaha kisha Uingereza ikaorodheshwa kwenye nafasi ya tatu kisha Ufaransa imewekwa kwenye nafasi ya nne. Utafiti huo haukuijumuisha China kutokana na kile ilichosema ni ukosefu wa data za kutosha. SIPRI lakini inasema kuna kati ya makampuni matatu hadi saba ya China katika kampuni mia moja kuu za utengenezaji silaha duniani.
 
Vita middle East (Syria, Iraq, Afghanistan, Yemen, Saudis vs Iran wako katika tension, Africa (Libya, Congo, Nigeria, Mali, S. Sudan, Somalia, CAR nk) S.America nk lazima mauzo yapae

Back
Top Bottom