Majajusi wa China waonya nchi zinazotengeneza silaha za kibaiolojia kudhuru watu

Mhaya

JF-Expert Member
Aug 20, 2023
1,658
4,866
Baadhi ya nchi "zimejizatiti" kwa silaha mbaya na hatari zinazolenga jeni (Vinasaba) za binadamu, shirika la juu la kijasusi la China lilidai Jumatatu. Ni mara ya kwanza shirika la serikali ya China kutaja tishio kama hilo hadharani.

Katika chapisho kwenye akaunti yake rasmi ya WeChat, Wizara ya Usalama wa Nchi ilionya na kusema baadhi ya mataifa yalilenga idadi ya watu wa China kwa "nia ovu".

Wizara haikutaja nchi hizo wala kutoa ushahidi kuunga mkono madai hayo.

Wizara hiyo ya China, imesema kuwa Nchi hizo hazitengenezi Silaha za kibaiolojia kwa ajili ya kulenga Dunia nzima, bali silaha hizo za kibaiolojia ni mahususi kwa ajili ya watu wa jamii fulani.

Iwapo silaha hiyo itachagua kulenga kundi fulani la watu, basi kuna uwezekano mkubwa wa kusambaa na kuingia pia katika makundi ya jamii nyingine au idadi ya watu waliokaribu na hiyo jamii au wanaingiliana kibaiolojia na hivyo kuvuka hadi kwenye shabaha zisizotarajiwa.

Lakini ripoti ya Kituo cha James Martin inaonya kwamba maendeleo katika matumizi ya mpangilio wa DNA, Akili bandia na ukusanyaji wa seti za data za vinasaba zinaweza "kuwezesha utambuzi wa walengwa wao kwa usahihi kwa ajili ya matumizi ya mfumo wa silaha za kibaiolojia (Genetic Weapon System)".

Mwezi Juni, mgombea urais wa Marekani Robert F Kennedy Jnr alidai kuwa "Wachina wanatengeneza silaha za kibaiolojia zinazolenga jamii za watu fulani", akisema zaidi kwamba Marekani pia imekuwa ikitengeneza teknolojia hiyo.

Maafisa wa Urusi mwaka jana waliishutumu Ukrainia kwa kuzalisha silaha za kibaiolojia katika maabara zinazofadhiliwa na Marekani, huku baadhi ya ripoti za vyombo vya habari zikipendekeza kuwa wanaamini kwamba silaha hizi zinaweza kulenga asili ya watu fulani.

Uwepo wa silaha kama hizo umekataliwa kwa muda mrefu na jumuiya kuu ya wanasayansi na kuchukuliwa tu kama nadharia zisizokuwa na mashiko (Conspiracy theory).

"Hakuna uwezekano mkubwa kwamba silaha inayolenga kundi la watu fulani inaweza kutengenezwa," Richard Parsons, mhadhiri mkuu wa Biochemical Toxicology katika Chuo cha King's College London, aliambia Kituo cha Vyombo vya Habari vya Sayansi kujibu madai ya Urusi.

Ikumbukwe kuna Mkataba wa Silaha za Kibaiolojia, ambao China, Urusi na Marekani zimetia saini, ambao pia ni ulinzi wa kimataifa unaolenga kuzuia utengenezaji na matumizi ya silaha hizo.

Vyanzo: South China Morning Post, Interesting Engineering, Daily Mail
 
Hii ishu naamini ipo kabisa, niliona kwenye muvi moja hivi yaani watu wa kariba (hasa viongozi, watu wenye nyadhfa)Fulani Fulani wanaanzia kudondoka mmoja mmoja na kufariki, watu wakaanza kushangaa na kuogopa na taharuki ikaanza, wamekuwa target wao tu kupitia DNA zao , ni kama vile kiuogonjwa Fulani kinashbulia DNA ambazo zilishasetiwa Kwa watu hao tu,hii ni muvi ya kiingereza au kimarekani kama sijasahau.
 
Hii teknolojia hipo sana tu, ila hawataki kusema... Sasa hivi haupigwi risasi au kombora... Unapigwa kibaiolojia tu
 
Baadhi ya nchi "zimejizatiti" kwa silaha mbaya na hatari zinazolenga jeni (Vinasaba) za binadamu, shirika la juu la kijasusi la China lilidai Jumatatu. Ni mara ya kwanza shirika la serikali ya China kutaja tishio kama hilo hadharani.

Katika chapisho kwenye akaunti yake rasmi ya WeChat, Wizara ya Usalama wa Nchi ilionya na kusema baadhi ya mataifa yalilenga idadi ya watu wa China kwa "nia ovu".

Wizara haikutaja nchi hizo wala kutoa ushahidi kuunga mkono madai hayo.

Wizara hiyo ya China, imesema kuwa Nchi hizo hazitengenezi Silaha za kibaiolojia kwa ajili ya kulenga Dunia nzima, bali silaha hizo za kibaiolojia ni mahususi kwa ajili ya watu wa jamii fulani.

Iwapo silaha hiyo itachagua kulenga kundi fulani la watu, basi kuna uwezekano mkubwa wa kusambaa na kuingia pia katika makundi ya jamii nyingine au idadi ya watu waliokaribu na hiyo jamii au wanaingiliana kibaiolojia na hivyo kuvuka hadi kwenye shabaha zisizotarajiwa.

Lakini ripoti ya Kituo cha James Martin inaonya kwamba maendeleo katika matumizi ya mpangilio wa DNA, Akili bandia na ukusanyaji wa seti za data za vinasaba zinaweza "kuwezesha utambuzi wa walengwa wao kwa usahihi kwa ajili ya matumizi ya mfumo wa silaha za kibaiolojia (Genetic Weapon System)".

Mwezi Juni, mgombea urais wa Marekani Robert F Kennedy Jnr alidai kuwa "Wachina wanatengeneza silaha za kibaiolojia zinazolenga jamii za watu fulani", akisema zaidi kwamba Marekani pia imekuwa ikitengeneza teknolojia hiyo.

Maafisa wa Urusi mwaka jana waliishutumu Ukrainia kwa kuzalisha silaha za kibaiolojia katika maabara zinazofadhiliwa na Marekani, huku baadhi ya ripoti za vyombo vya habari zikipendekeza kuwa wanaamini kwamba silaha hizi zinaweza kulenga asili ya watu fulani.

Uwepo wa silaha kama hizo umekataliwa kwa muda mrefu na jumuiya kuu ya wanasayansi na kuchukuliwa tu kama nadharia zisizokuwa na mashiko (Conspiracy theory).

"Hakuna uwezekano mkubwa kwamba silaha inayolenga kundi la watu fulani inaweza kutengenezwa," Richard Parsons, mhadhiri mkuu wa Biochemical Toxicology katika Chuo cha King's College London, aliambia Kituo cha Vyombo vya Habari vya Sayansi kujibu madai ya Urusi.

Ikumbukwe kuna Mkataba wa Silaha za Kibaiolojia, ambao China, Urusi na Marekani zimetia saini, ambao pia ni ulinzi wa kimataifa unaolenga kuzuia utengenezaji na matumizi ya silaha hizo.

Vyanzo: South China Morning Post, Interesting Engineering, Daily Mail
"I don't know when the third world war, will be faught, but I am sure it will be faught with sticks- Plato
1698838440231.jpg
 
Hii itawahusu wale viongozi wanaopenda kutembea kwenye nchi za watu
 
Kama wali saini mkatababa wa kuto zitengeneza au kuzitumia hizo B.weapons. Basi Kuna uwezekano mkubwa kwamba zipo na technology hiyo ipo
 
Hizi silaha za kibaiolojia wanazifumbia macho tu, na kuvunga kuzikataza kama wanavyosema kwenye utengenezaji wa mabomu ya Nyuklia, lakini nyuma ya pazia silaha hizo zinatengenezwa.
 
Back
Top Bottom