Uturuki Nayo ni Super Power?!. Meli Zake 4 za Kijeshi Kutia Nanga Dar Konyesha Msuli Ubabe Bahari!.

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
37,366
2,000
Wanabodi,

Kumbe nchi ya Uturuki nayo ni Super Power?!. Meli zake 4 za kijeshi, kutia nanga jijini Salaam hapo Kesho, kuonyesha nguvu ya kijeshi na ubabe wa baharini, ikiwemo kuwasaka maharamia!.

Watanzania tumealikwa kwenda kuzishuhudia bandari ya Dar es Salaam siku ya Alhamisi na Ijumaa kuanzia Saa 3 asubuhi hadi saa 6 mchana! (Sijui huu muda ni kwa ajili tuu ya wasio na kazi) kiingilio ni bure!.
Kwa taarifa zaidi, soma hapa.

Na Pasco wa jf.

Meli Nne za Kijeshi za Uturuki kwa jina la Barbaros Turkish Maritime Task Group (TMTG) zinatarajiwa kutia nanga kwa wakati mmoja katika Bandari ya Dar es Salaam kuanzia leo (kesho) kwa ziara ya kijeshi ya siku 4 ambao itahusisha maonyesho ya zana za kijeshi, mazoezi ya pamoja na jeshi la wanamaji la Tanzania, huduma za kijamii na ushirikiani wa kijeshi baina ya Uturuki na Tanzania.
Hayo yamebainishwa jiji Dar es Salaam na Balozi wa Uturuki nchini, Ali Dovitoglu katika mkutano na waandishi wa habari, uliofanyika Ubalozi wa Uturuki, jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
Balozi Dovitoglu amesema lengo kuu la ziara hiyo ni kukuza ushirikiano wa kijeshe baina ya jeshi la Uturuki na majeshi ya nchi 27 za pwani barani Afrika sio tuu kuonyesha uwepo na uwezo wa kijeshi wa Jeshi la Wanamaji la Uturuki, bali pia kusaidia katika operetions mbalimbali za kijeshi barani Afrika ukiwemo vita dhidi ya uharamia kwa Pwani ya Bahari ya Hindi.
Balozi Dovitoglu amesema meli hizo zitawasili siku ya Jumanne tarehe 27/05/2014, Siku ya Jumatano, tarehe 28/05 2014 waandishi wa habari watakaribishwa kufanya ziara katika meli hizo, baadaye wanamaji hao, watatembelea shule na kituo cha watoto yatima kugawa misaada ya kibinaadamu.
Siku ya Alhamisi na Ijumaa, wananchi wa jiji la Dar es Salaam na vitongoji vyake, wataruhusiwa kutembelea meli hizo kwa muda wa siku 2 kuanzia saa 3 asubuhi mpaka saa 6 mchana kujioneo maonyesho ya zana za kijeshi ya Uturuki ambapo makampuni manane ya vifaa vya kijeshi ya Uturuki wataonyesha vifaa vyao. Makampuni hayo ni Meteksan, Otokar, TAI, Dearsan, Havelsan, Roketsan, Aselsan na STM
Meli hizo nne ni F-495 TCG kwa jina la Gediz, F-245 TCG, Oruçreis, F-511 TCG Heybeliada meli ya usindikizaji ya A-595 TCG Yarbay Kudret Güngör, zitafafiri kwa jumla ya safari ya urefu wa kilometa 30,000 katika ziara itakayochukua siku zaidi ya 100 ambapo itatembelea nchi 28 barani Afrika na kutia nanga katika bandari 40.

Msafara wa meli hizo, unaingia Tanzania ukitokea nchini Afrika ya Kusini, ambapo hii ni mara ya kwanza ndani ya kipindi cha miaka 148 iliyopita ndipo meli ya mwisho ya Uturuki ilitia nanga kwa mara ya mwisha katika Rasi ya Tumaini Jema (Cape of Good Hope) mwaka 1866.

Uturuki ni moja ya mataifa makubwa yenye nguvu kubwa za kijeshi la la majini, tangu enzi za utawala wa kale wa dola la Ottoman ambapo walitawala bandari nyingi barani Afrika ikiwemo miji ya Kilwa, Sofala, na Lamu kwatika Pwani ya Bahari ya Hindi.

Pasco.
 
Attachments

 • DSC_0944.JPG
  File size
  1.5 MB
  Views
  1,065
 • DSC_0901.JPG
  File size
  1.4 MB
  Views
  925
 • DSC_0955.JPG
  File size
  1.4 MB
  Views
  871
 • images-1.jpeg
  File size
  6.9 KB
  Views
  1,009
 • images-2.jpeg
  File size
  7.9 KB
  Views
  888
 • (1).jpg
  File size
  50.2 KB
  Views
  2,515
 • TMTG_Las_Palmas_00.jpg
  File size
  225.2 KB
  Views
  2,601

Mwanamutapa

JF-Expert Member
Dec 5, 2011
499
195
Turker ndio former otoman empire kwahiyo siyo nchi ya kitoto kijeshi.
Hao jamaa wanatengeneza hadi ndege za kivita za F-15 na F-16.
Pamoja na silaha mbalimbali

Turkey taifa lenye nguvu za kijeshi lakini kwa sasa si superpower ila lilikuwa superpower kama Marekani na Urusi wakati wa Otoman Empire kuhusu kutengeneza ndege za kijeshi bado uwezo hawana mpaka 2023 iwapo watafanikisha azma kwa sasa wanaassemble ndege za kimarekani kwa teknoloijia ya Mmarekani

[h=1]Turkey to Produce Indigenous Fighter Jets[/h] December 17, 2010 - 12:26pm, by Joshua Kucera

Turkey is going to produce its first entirely indigenous fighter jet, to be fielded by 2023, the country's defense minister Vecdi Gönül announced this week. From Hurriyet Daily News:
Gönül told reporters after a meeting of the Defense Industry Executive Committee that the Undersecretariat for Defense Industries, Turkey's procurement agency, would start talks with Turkish Aerospace Industries, the country's main aerospace company, for a "conceptual design" of a fighter aircraft and a jet trainer to be built after the year 2020.
"This … effectively is a decision for the making of Turkey's first fighter aircraft," he said...
Minister Gönül said Turkey's newly designed fighter aircraft "would be a next-generation type, would replace the [U.S.-made] F-4Es and would function well with the F-16 and the F-35." He therefore confirmed that the new aircraft mostly would be meant for air-to-air fighting.
Unfortunately, Gönül did not explain why Turkey would do such a thing. It's already planning to buy about 100 F-35s, the next-generation U.S.-built fighter, and had been discussing with Eurofighter to buy some Typhoon jets, but not any more. Why would it make sense to build their own instead?
His rhetoric at the announcement of the fighter plan did suggest some national-pride motivation:
The minister said Turkey may cooperate with South Korea, but implied that this is a small possibility. "We can manufacture the new fighter aircraft with them, we don't rule this out. But the decision we have taken now calls for the production of a totally national and original aircraft," he said. 

Elungata

JF-Expert Member
Jan 28, 2011
36,102
2,000
Turkey taifa lenye nguvu za kijeshi lakini kwa sasa si superpower ila lilikuwa superpower kama Marekani na Urusi wakati wa Otoman Empire kuhusu kutengeneza ndege za kijeshi bado uwezo hawana mpaka 2023 iwapo watafanikisha azma kwa sasa wanaassemble ndege za kimarekani kwa teknoloijia ya Mmarekani

[h=1]Turkey to Produce Indigenous Fighter Jets[/h] December 17, 2010 - 12:26pm, by Joshua Kucera

Turkey is going to produce its first entirely indigenous fighter jet, to be fielded by 2023, the country's defense minister Vecdi Gönül announced this week. From Hurriyet Daily News:
Gönül told reporters after a meeting of the Defense Industry Executive Committee that the Undersecretariat for Defense Industries, Turkey's procurement agency, would start talks with Turkish Aerospace Industries, the country's main aerospace company, for a "conceptual design" of a fighter aircraft and a jet trainer to be built after the year 2020.
"This … effectively is a decision for the making of Turkey's first fighter aircraft," he said...
Minister Gönül said Turkey's newly designed fighter aircraft "would be a next-generation type, would replace the [U.S.-made] F-4Es and would function well with the F-16 and the F-35." He therefore confirmed that the new aircraft mostly would be meant for air-to-air fighting.
Unfortunately, Gönül did not explain why Turkey would do such a thing. It's already planning to buy about 100 F-35s, the next-generation U.S.-built fighter, and had been discussing with Eurofighter to buy some Typhoon jets, but not any more. Why would it make sense to build their own instead?
His rhetoric at the announcement of the fighter plan did suggest some national-pride motivation:
The minister said Turkey may cooperate with South Korea, but implied that this is a small possibility. "We can manufacture the new fighter aircraft with them, we don't rule this out. But the decision we have taken now calls for the production of a totally national and original aircraft," he said.ni wazi kuwa F-15 na F-16 ni ndege ya marekani ku assemble ndege ya kivita ya marekani si mchezo hiyo ina maana wana mafundi waliobobea.
 
Mmawia

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
95,840
2,000
Ukiona hayo mameli yanajitia Kuja dar jua Kuna deal kubwa hasa la kutorosha rasilimali zetu,kama lile meli la kichina.Hapo inabidi tuwe macho Sana huenda meno ya tembo ndio yanafuatwa.
 
Ehud

JF-Expert Member
Feb 12, 2008
2,687
0
hakunaga jeshi la NATO,huwa kukitokea operation ndo members wanacontribute vifaa na askari nalo ndo hujulikana kama NATO FORCE.

Nilikuwa namjibu huo aliyesema Uturuki wana jeshi kubwa NATO (Kama NATO member). Point yako sijui ni nn hapa? Unatoa taarifa ambayo ipo obvious ama?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom