Utupaji masalia ya makaa ya mawe (coal ash) katika Barabara za mitaa kwenye makazi ya watu maeneo ya Kunduchi Salasala

Freiheit

Member
Feb 4, 2021
7
5
Kuna kiwanda kimoja maeneo ya Kunduchi Salasala kinachotumia nishati ya makaa ya mawe (coal) kuzalisha bidhaa za sabuni.

Ni hivi majuzi kimeanzisha utaratibu wa kusambaza, kwa kutumia magari ya kiwanda, masalia ya coal iliyotumika (coal ash) na kuyamwaga katika Barabara za mitaa.

Kabla ya hatua hi ya Sasa, kiwanda hicho kilikuwa na utaratibu wa kusafirisha masalia hayo na kuyaharibu kulingana na matakwa na sheria za mazingira.

Cha kusikitisha, Uchafuzi huu unadhaminiwa na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Salasala.

Wizara ya Mazingira ichukue hatua stahiki za haraka kuzuia unyama huo kwani eneo husika hukumbwa na mafuriko na maji kutuwama kwakipindi kirefu nyakati za mvua.
 
Nitumie hizo namba ili wachukue hatua haraka.

Taka hizi zina masalia ya kemikali mbalimbali ambazo zikiachwa kusambaa katika eneo hilo ambalo maji hujaa na kutuwama KWA kipindi kirefu, ni hatari KWA afya na maisha ya wakazi wa eneo hilo lililopo Salasala nyuma ya KANISA LA NABII FLORA.

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa ndiye anaratibu uhalifu huu.
 
Mitano tena.

Mtamfanya nini mwrnyekiti wetu?
 
Kama wananchi hamtaki kushiriki kwenye kuboresha njia za mitaa yenu. Mwenyekiti afanyeje? Mnakaa na mwenye malori hapo mnashindwa kushirikiana nao wawaletee kifusi salama kwa bei nafuu!?

Mitano tena
Majibu yako yanadhihirisha hujikiti kwenye kutafuta Tiba ya tatizo bali kufanya ili mradi umefunika tatizo huku ulijuwa ni dhahirii litaibukana sura mpya. Yaani kumwaga taka hatarishi Kwako ni bora kuliko kuwa na barabara mbovu?
 
Je umejiridhisha kuwa hayo mabaki yana madhara? Mimi naona mwenyekiti amejiongeza ili kuziba mashimo ya barabara. Ni vyema ungeongea na mwenyekiti kwanza kujua ni namna gani alifikia kubuni huo mradi.
 
Lakini jua hizo chenga zinasaidia kuunguza tope kwenye barabara ambazo hazina lami hasa kipindi hiki cha mvua,nadhani ulitakiwa umpongeza huyo mwenyekiti wa serikali za mitaa wa eneo hilo kwa ubunifu,naona wewe sio mwenda kwa miguu na huziona adha za tope labda tu kwa kuwa unatembelea gari.
 
Tusikumbatie dhana ya ubunifu wa miradi bila kuangalia athari au madhara yatokanayo na uanzishwaji wa miradi ya aina hiyo Kwa afya za binadamu na mazingira.

Lipo tatizo la viwanda kusaka maeneo ya kutupa taka au masalia ya viwandani kwa kuwalipa wahusika ambao hutoa maeneo hayo ili kujineemesha KWA hadaa kwamba wanafanya KWA manufaa ya wananchi au wanyonge. Ni suala linalopaswa kutazamwa kwa jicho la pili.
 
Lakini jua hizo chenga zinasaidia kuunguza tope kwenye barabara ambazo hazina lami hasa kipindi hiki cha mvua,nadhani ulitakiwa umpongeza huyo mwenyekiti wa serikali za mitaa wa eneo hilo kwa ubunifu,naona wewe sio mwenda kwa miguu na huziona adha za tope labda tu kwa kuwa unatembelea gari.
Mimi sijui kama mabaki ya makaa ya mawe yana athari kwenye mazingira. Ni vyema wakati unatoa malalamiko yako ungeainisha ni madhara gani hayo mabaki yanaweza kusababisha.

Otherwise huku mitaani tunanunua vifusi vya taka wakati mwingine kwa bei juu ili kufanya barabara zipitike.

Sisi tumewahi kumuomba jamaa mmoja mfugaji atupe taka za ng'ombe wake ambazo ni kinyesi cha ng'ombe kilicho changanyikana na nyasi atupe kwenye korongo jirani na nyumba yetu.
 
Majibu yako yanadhihirisha hujikiti kwenye kutafuta Tiba ya tatizo bali kufanya ili mradi umefunika tatizo huku ulijuwa ni dhahirii litaibukana sura mpya. Yaani kumwaga taka hatarishi Kwako ni bora kuliko kuwa na barabara mbovu?
Wengi tungefaidika sana kama ungeeleza nini hasa madhara ya hivyo vifusi.
 
Mimi sijui kama mabaki ya makaa ya mawe yana athari kwenye mazingira. Ni vyema wakati unatoa malalamiko yako ungeainisha ni madhara gani hayo mabaki yanaweza kusababisha.

Otherwise huku mitaani tunanunua vifusi vya taka wakati mwingine kwa bei juu ili kufanya barabara zipitike.

Sisi tumewahi kumuomba jamaa mmoja mfugaji atupe taka za ng'ombe wake ambazo ni kinyesi cha ng'ombe kilicho changanyikana na nyasi atupe kwenye korongo jirani na nyumba yetu.
Mabaki hayo yana athari kubwa ila wengi wetu tunapenda kuchukulia vitu kiurahisi Sana bila kujali athari zake kiafya na mazingira. Soma hii bila kuharibu maana:

"Coal ash, also known as coal combustion residuals (CCRs), is the mineral residue that remains from burning coal. Exposure to coal ash and to the toxic substances it contains may pose a health risk to workers in coal-fired power plants and residents living near coal ash disposal sites".
 
Back
Top Bottom