Historia ya Utumwa
Wengi wetu tunadhani biashara ya utumwa ilikuwa ni ya waarabu dhidi ya waafrika. Hii dhana siyo ya kweli kwani
biashara ya utumwa ilianza miaka 2000 huko mesopotamia.
Watumwa kwa asili walikuwa ni mateka kwenye vita [ngawira] ambao walitumika kwenye ujenzi wa miundu mbinu hizo pyramids, mahekalu na majengo ya fahari huko syria, ugiriki na kwingineko.
Wakati wa utawala wa ottoman ambapo walitawala sehemu ya ulaya,afrika na mashariki ya kati. Mateka wengi wa nchi zilizoshindwa kwenye vita hivyo walichukuliwa kama watumwa. Kati yao kulikuwa na wasomi, mafundi, wafanyabiashara, wajenzi na watu wakawaida. Hawa walitumika kutokana na hadhi zao kuleta tija kwa mabwana zao.
Huku kwetu afrika ilikuwa vivo hivyo kwani kwenye vita ya makabila wale walioshindwa walichukuliwa kama mateka ambao pia walitumika kwenye kilimo na ulinzi.
Mapinduzi makubwa ya viwanda kwenye karne 16-18 ambapo uvumbuzi wa mashine na uanzishwaji wa viwanda vikubwa vya kuzalisha bidhaa na nguo.
Kutokana na ulaya kuwa na eneo dogo, ilibidi waingereza,waspaniola,wareno watafute maeneo makubwa zaidi ya uzalishaji mali ghafi. Maeneo makubwa ambayo waliyaainisha kwa kilimo [miwa na pamba] ilikuwa ni marekani pamoja na visiwa vya carribean. Mateka wengi ambao machifu na wafalme wa falme mbali mbali afrika ya magharibi ambako biashara hii ilikuwa kubwa kuliko huku kwetu. Machifu na wafalme [waafrika] ndiyo walikuwa wauzaji wakubwa wa watumwa kwa wazungu ambao walikuwa wanaenda kuwachukua kwa meli [siyo kama huku kwetu ambapo yalikuwa yanatumika majahazi]
Watumwa hao wengi walipelekwa marekani na visiwa vya carribean ambapo wali wa visiwani walikuwa wemepelekwa kwenye mashamba ya miwa na wale wa marekani walipelekwa kwenye mashamba ya pamba.
Watumwa hao waliteswa kinyama na mabwana zao na chuki iliyopo sasa baina ya weupe na weusi marekani asili yake ni hii.
Australia walipelekwa wafungwa wa malkia wa uingereza kwenda kufuga na kulima na mwishowe wengi wakafanya makazi yao huko. Cha ajabu hao wafungwa weupe nao wakawafanya wenyeji kuwa watumwa wao.
Huku kwetu machifu wetu kuanzia Goma hadi pwani wote walikuwa wakusanyaji na wauzaji wa watumwa kwa waarabu ambao waliifanya hiyo biashara ya kuwaleta watumwa hao toka bara hadi zanzibar ambapo palikuwa na soko kuu la kuwauzia wazungu watumwa hao.
Utumwa, ingawa umepigwa marufuku duniani umebadilika kimuundo lakini bado unaendelea hadi sasa.
Inasemakana kuwa hadi sasa kuna watu kiasi kati milioni 25-40 wako utumwani na wengi wao wako Asia.
Huku kwetu Africa hali ni hiyo hiyo. Inasemekana kuwa wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe Sudan, hasa watoto walichukuliwa kwenda kufanyishwa kazi kwenye mashamba ya kakao huko afrika ya magharibi.
Mauritania, ingawa ilipiga marufuku 'utumwa' mwaka 2007, lakini bado unaendelea ambapo idadi yao kwa sasa inafika 600,000.
Kwa afrika magharibi makundi kama Boko haram nao pia wanahusika sana kwenye biashara hii ambayo ni kimoja kati chanzo chao cha fedha za kununulia silaha.Hivyo basi tunapozungumzia suala hili kwanza inabidi tufahamu mapana yake ambayo ni Wafalme wa uingereza,ureno, spain na wengineo wamehusika sana na biashara hii.
Jee Kanisa la Rome lilihusika kwenye biashara hii?
Ingawa kanisa lilikuwa halipendi hali hii lakini liliwaomba watumwa wa kikristu kuheshimu mabwana zao na kukubali mateso yao kwa kumuiga yesu kristu. Kanisa liliwekwa kwenye wakati mgumu kwani sehemu kubwa ya sadaka ilikuwa inatokana na matajiri ambao walikuwa na mashamba/viwanda ambavyo vilikuwa vinatumia watumwa.
Makanisa mengi ulaya yalijengwa kwa nguvu kazi za watumwa.
DHAMBI YA UTUMWA INABEBWA NA WENGI SANA NA SIYO WAARABU PEKE YAO.