Utumwa wa Tume ya Uchaguzi Tanzania: Wasemavyo Maaskofu wa TEC

CCM wakishindwa kwenye uchaguzo wowote ule, ni Uzembe usiosemekana, hasa itatokana na kuchagua vilaza wasiojua siasa, mfano hao maprofessor, hata uwe na IQ kubwa kiasi gani usome mpaka umalize masomo yote! km hujui siasa, utapoteza madaraka kirahisi mno!.

Amini nawaambia ''It must be noted that men with bad instincts are more in number than the good, and therefore the best results in governing them are attained by violence and terrorisation, and not by academic discussions, every man aims at power, every one would like to become a Dictator, if only he could and rare indeed are the men who would not be willing to sacrifices the welfare of all for the sake of securing their own welfare!.

Hata maisha nyumbani baba yapasa uwe Dikteta! ili mambo yaende, kusiwe na uhuru wa, kupiltiliza, niliwahi sema ''Uhuru bila nidhamu ni wendawazimu''. ukiendekeza uhuru nyumbani kwako kila mtu atafanya anavotaka, mke hata wageni!

Political Democracy and freedom is an idea but not a fact. this idea one must know how to apply whenever it appears necessary. the ruler who is governed with the moral is not a skilled politician, and is therefore unstable in his own throne. CCM Must have recourse both to cunning and to make believe. thenceforth powerful enemy'

Kina Mbowe na wenzake wanataka nini? si madarakaa? ambayo CCM amekamata, Sasa iwape? kiarahisi tu?
Ogopa sana mtu anatabasamu au kuongea vimeno vya juu vinaonekana kiduuchu km Mbowe! bora mara zote unayeona meno yote! Siasa ni Propaganda na mchezo wa aina flani fulani hivi mbaya sana! usipoujua! utachekesha walio nuna!
Mama Amon! mimi sina chama!
Naamini hujafika unakopaswa kufika ili uwaze sawa na dunia ilivyo.

Maadili pia ni sehemu ya maisha tunayopaswa kuishi kwa adili umewahi kuchunguza kwa ushahidi wenye mashaka na usionamashaka kugundua maadili ni nadharia ngumu ambayo hatuwezi kuishi?

Ukweli kwenye dunia hii unategemea dunia inataka nini kwa wakati huo.
Hata unayemuamini sijui ni mama yako atakwambia ukweli unalingana na mahitaji ya dunia hiyo.

Ukipata nafasi ya kusoma,
Kasome falsafa pure au falsafa na maadili ujue namna ya akili inavyoweza toa majibu ambayo si kweli lkn yanaweza kuaminika ni kweli kwa watakao msikia.

Kasome falsafa utakayofundishwa na walatini then utagundua dunia ndivyo ilivyo.
Hoja yako inaweza kuwa kama hii

Mungu amekufa.

Utalijibu hilo swali?

Mpaka sasa unaona pos or neg unaona kuna majibu na ushahidi _ hivyo ndivyo ilivyo kwa fikra zako juu ya demokrasia, siasa, ukweli , udikteta na maisha kama si malezi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uchaguz hauhairishwi.
Lakini bado kuna nafasi ya kujenga hoja ya kuahirisha uchaguzi ili kuweka mazingira bora zaidi. Swali ni nani ataijenga?
Na hasipeleke hoja hii mtu hata mmoja bungeni wala kwa tume vilevile rais

Tunataka uchaguzi huru na wa haki.

Ban ya shughuli za kisiasa inaendelea chini ya wingu ka corona. Nani anafaidika?

Nec baada ya kukutana kuhairishwa haikuwa hoja labda kwenye mkutano ujao wa wadau lkn litakataliwa.


Tumieni akili ya kuzaliwa kupata majibu ya maswali ambayo hujajiuliza wala kuulizwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naamini hujafika unakopaswa kufika ili uwaze sawa na dunia ilivyo.

Maadili pia ni sehemu ya maisha tunayopaswa kuishi kwa adili umewahi kuchunguza kwa ushahidi wenye mashaka na usionamashaka kugundua maadili ni nadharia ngumu ambayo hatuwezi kuishi?

Ukweli kwenye dunia hii unategemea dunia inataka nini kwa wakati huo.
Hata unayemuamini sijui ni mama yako atakwambia ukweli unalingana na mahitaji ya dunia hiyo.

Ukipata nafasi ya kusoma,
Kasome falsafa pure au falsafa na maadili ujue namna ya akili inavyoweza toa majibu ambayo si kweli lkn yanaweza kuaminika ni kweli kwa watakao msikia.

Kasome falsafa utakayofundishwa na walatini then utagundua dunia ndivyo ilivyo.
Hoja yako inaweza kuwa kama hii

Mungu amekufa.

Utalijibu hilo swali?

Mpaka sasa unaona pos or neg unaona kuna majibu na ushahidi _ hivyo ndivyo ilivyo kwa fikra zako juu ya demokrasia, siasa, ukweli , udikteta na maisha kama si malezi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naamini hujafika unakopaswa kufika ili uwaze sawa na dunia ilivyo.

Maadili pia ni sehemu ya maisha tunayopaswa kuishi kwa adili umewahi kuchunguza kwa ushahidi wenye mashaka na usionamashaka kugundua maadili ni nadharia ngumu ambayo hatuwezi kuishi?

Ukweli kwenye dunia hii unategemea dunia inataka nini kwa wakati huo.
Hata unayemuamini sijui ni mama yako atakwambia ukweli unalingana na mahitaji ya dunia hiyo.

Ukipata nafasi ya kusoma,
Kasome falsafa pure au falsafa na maadili ujue namna ya akili inavyoweza toa majibu ambayo si kweli lkn yanaweza kuaminika ni kweli kwa watakao msikia.

Kasome falsafa utakayofundishwa na walatini then utagundua dunia ndivyo ilivyo.
Hoja yako inaweza kuwa kama hii

Mungu amekufa.

Utalijibu hilo swali?

Mpaka sasa unaona pos or neg unaona kuna majibu na ushahidi _ hivyo ndivyo ilivyo kwa fikra zako juu ya demokrasia, siasa, ukweli , udikteta na maisha kama si malezi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu uko sahihi, unavo amini! But Dunia uionavyo sivo ndivo ilivyo! the vice versa is true! Maadili simply means ''mwenendo mwema'' kile unachoona chema, wengine ni si chema kwao! so for this kind of theme!
Nakataa Maadili siyo nadharia ngumu, kimtazamo na kimatendo, wahusika wakuu wa Maadili ndiyo wagumu!

Dunia ni watu ikiwa ni pamoja na wewe kwa wakati, siyo tufe, Ukweli kwenye Dunia unakutegemea. mwana Dunia, remember ''Life is how you make it''
Hiyo falsafa pure unayosema ni Bado unarudia neno ''Propaganda'' km nilivo bainisha hapo awali! unless other wise hujui maana yake!

Kuhusu Falsafa ya Latin, hizo ni akili zao, mazingira na wakati wao! Mbongo yako inasemaje? siyo usizisome, siyo kwa sababu alisema M-latin basi unaibeba km lilivo, toa changa moto zako dhidi ya mapungufu yao then ibuka na yako! yanayo endana na wewe, ndo tunacho kifanya humu!

Suala la Mungu amekufa? hilo jambo jengine, wakati mwingine, nevertheless, hakika nasema Mimi Nyarusare ni Mungu. narudia! seriously! ''Am God'' Even Jesus knows!. Jibu ni sijafa!

Laa! hasha siyo fikra zangu! bali suala la historia ya fikra za ulimwengu wa siasa, Pos! and Dons!...inategemea muhitaji anataka nini! wapi na kwa wakati gani.
 
Mkuu uko sahihi, unavo amini! But Dunia uionavyo sivo ndivo ilivyo! the vice versa is true! Maadili simply means ''mwenendo mwema'' kile unachoona chema, wengine ni si chema kwao! so for this kind of theme!
Nakataa Maadili siyo nadharia ngumu, kimtazamo na kimatendo, wahusika wakuu wa Maadili ndiyo wagumu!

Dunia ni watu ikiwa ni pamoja na wewe kwa wakati, siyo tufe, Ukweli kwenye Dunia unakutegemea. mwana Dunia, remember ''Life is how you make it''
Hiyo falsafa pure unayosema ni Bado unarudia neno ''Propaganda'' km nilivo bainisha hapo awali! unless other wise hujui maana yake!

Kuhusu Falsafa ya Latin, hizo ni akili zao, mazingira na wakati wao! Mbongo yako inasemaje? siyo usizisome, siyo kwa sababu alisema M-latin basi unaibeba km lilivo, toa changa moto zako dhidi ya mapungufu yao then ibuka na yako! yanayo endana na wewe, ndo tunacho kifanya humu!

Suala la Mungu amekufa? hilo jambo jengine, wakati mwingine, nevertheless, hakika nasema Mimi Nyarusare ni Mungu. narudia! seriously! ''Am God'' Even Jesus knows!. Jibu ni sijafa!

Laa! hasha siyo fikra zangu! bali suala la historia ya fikra za ulimwengu wa siasa, Pos! and Dons!...inategemea muhitaji anataka nini! wapi na kwa wakati gani.
Pole

Maana hujanielewa
 
Ni makala iliyoshiba vema na imesheheni uhalisia wa kinachoelezwa na Watanzania wazalendo!!

Asantee Sana bandiko hili mujarabu

House girl(dada wa kazi) Ni binadamu aheshimiwe, apumzike, apewe Uhuru wa kuabudu pia
Tume ya uchaguzi ni huru kwa maneno lakini si kiutendaji. Karibu viongozi wakuteulewa mara nyingi wanatetea ugali wao. Hawasimamii haki.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tupitie hii pia kufahamu nini nilikuwa namaanisha kwenye michango yangu hapo juu.
Utumwa wa bunge la jmt na wabunge wake
 
Kina Mbowe na wenzake wanataka nini? si madarakaa? ambayo [serikali ya] CCM [w]amekamata, Sasa [CCM] iwape [madaraka kina Mbowe] ... kiarahisi tu? Ogopa sana mtu anatabasamu au kuongea vimeno vya juu vinaonekana kiduuchu km Mbowe! bora mara zote unayeona meno yote! Siasa ni Propaganda na mchezo wa aina flani fulani hivi mbaya sana! usipoujua! utachekesha walio nuna!

Kosa lako ni moja. Unadhani kwamba serikali ya CCM inamiliki madaraka na kwamba wanayo hiari ya kuayaachia au kuyang'ang'ania. Madaraka yako mikononi mwa umma, na serikali ya CCM ni wakala tu. Umma unaamua nani akalie ofisi ya uwakala na yupi asikalie. Badilisha mtazamo wako, halafu tujenge hoja zilizonyooka.
 
View attachment 1392105
Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe (kushoto) na Mwenyekiti wa CCM, John Magufuli (kulia)

USULI

Maaskofu Katoliki Tanzania wametoa waraka wa Kwarezima ya 2020. Katika makala hii nafupisha, kutafsiri na kutumia hoja yao yenye madokezo makuu saba, katika kuonyesha kwamba Tume ya Taifa ya Uchaguzi hapa Tanzania inapaswa kubomolewa na kujengwa upya ndani ya siku tatu.

Hoja ya Maaskofu inayo madokezo muhimu saba yafuatayo:

Maaskofu wanasema kwamba mfumo wa kanuni za maumbile asilia unaonyesha kuwa upo ufalme wa Mungu ambao umejengwa juu ya mawazo makubwa matatu, yaani ukweli badala ya uwongo, malengo mema badala ya malengo mabaya, mbinu adilifu badala ya mbinu za kihalifu. Ndio kusema "the true as opposed to the false, the good as opposed to the bad, the right as opposed to the wrong." (Waefeso 5:9).

Kwamba, kwa mujibu wa mpango asilia wa maadili ulio katika ufalme wa Mungu, kila tunu ya kibinadamu inayofahamika huambatana na majukumu mawili mara zote, yaani, jukumu chanya la kututaka kulinda na kustawisha tunu husika na jukumu hasi la kututaka kujizuia kuhujumu tunu husika kwa makusudi, ambapo, jukumu hasi hukataza kutendeka kwa tendo baya kila mahali, kila wakati na kwa kila mtendaji. (Mathayo 7:12).

Kwamba, kwa sababu mbili zilizotangulia hapo juu, ufalme wa Mungu ni mfumo wa maadili unaopiga marufuku matumizi ya mbinu mbaya kama njia ya kufukuzia lengo jema. (Warumi 3:8).

Kwamba, tendo la kubatilisha kwa makusudi jukumu linalokataza kutendeka kwa tendo baya (intentionally overriding a negative duty), hii ikiwa ni mbinu ya kutimiza haki yoyote, ni matumizi ya mbinu iliyo haramu ili kufanikisha lengo halali.

Kwamba, kwa sababu mbili zilizotanglia hapo juu, jitihada zozote za kubatilisha kwa makusudi jukumu linalokataza kutendeka kwa tendo baya, hii ikiwa ni mbinu ya kutimiza haki yoyote, ni kitendo cha kupinga mpango wa ufalme wa Mungu.

Kwamba, katika jumuiya ya kisiasa vyombo vya dola kama vile Rais, Bunge, Mahakama, Baraza la Mawaziri, wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya, Baraza la Madiwani, Majeshi, watumishi wanumma, na Tume ya uchaguzi, vimetoka kwa Mungu na hivyo vinalo jukumu la kuheshimu mpango wa ufalme wa Mungu aliye chimbuko la vyombo hivyo.

Kwamba, kutokana na sababu mbili zilizotangulia hapo juu, kila chombo cha dola kinachobatilisha kwa makusudi jukumu linalokataza kutendeka kwa tendo baya, hii ikiwa ni njia ya kutimiza haki yoyote, kinakuwa kinapinga mpango wa Ufalme wa Mungu alikiumba, na hivyo kinapaswa kubomolewa na kujengwa upya ili kiendane na mpango wa Mungu.


UTANGULIZI

Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania wametoa Waraka kwa ajili ya Kwaresima ya 2020, na kuuning'iniza katika tovuti ya Vatican tarehe 26 Februari 2020. Waraka huu unaongelea mahusiano yaliyopo kati ya “Ufalme wa Mbinguni,” “Ufalme wa Duniani” na “Ufalme wa Mungu.”

Waraka huu umeandaliwa na kusambazwa katika kipindi mahsusi katika uhai wa Taifa letu—yaani, kipindi cha uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani kwa ajili ya kuunda serikali ya wamu ya sita.

Kwa hiyo, nimeamua kufanya muhtasari wa hoja ya Maaskofu, kuitafsiri, na hatimaye kuonyesha jinsi ya kuitumia hoja hiyo katika ukombozi wa Mtanzania katika sekta mbalimbali za maisha yetu.

Nakusudia kuonyesha matumizi yake kwa njia ya mfano wa mageuzi yanayopaswa kufanyika kwenye Tume ya Taifa ya Uchaguzi ili kuiwezesha kutimiza majukumu yake kwa ufanisi na kasi stahiki.

Muhtasari wa Waraka wa Kwarezima

Ujumbe wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania wenye kuongozwa na kauli mbiu ya "Ufalme wako ufike," unayo maneno 9,661 yaliyogawanywa katika sura sita zifuatazo: utangulizi; ufalme wako ufike; neno la Mungu linakuza ufalme wa mbinguni; ufalme wa Mungu na mamlaka ya watu; aina tofauti za mazoezi ya kiroho na faida zake; na hitimisho.

Waraka huu ni muhtasari wa ukweli kuhusu vitu vinavyoonekana na visivyoonekana, tunu na maadili kulingana na simulizi kuu ya Ukristo (Christian grand narrative). Ni simulizi kuhusu mpango wa Ufalme wa Mungu juu ya uhuru wa mwanadamu unaoongelewa na Maaskofu wa TEC.

"Tunaposali, 'Ufalme wako ufike,' tunasali kwa ajili ya ufalme (utawala) unaolinda daima uhuru kamili wa mwanadamu na unaopinga nguvu zinazoenda kinyume na mapenzi ya Mungu ulimwenguni," wameandika Maaskofu.

Maandiko ya waandishi watano yamenisaidia zaidi kuielewa zaidi kauli hii ambayo itakuwa kikonyo cha makala yangu. Watu hao ni James Sire (2009) aliyenadika kitabu “The Universe Next Door: A Basic Worldview Catalog,”; Gustavo Gutierrez (1988) aliyenadika kitabu “A Theology of Liberation: History, Politics, and Salvation,”; Bebhinn Donnelly(2016) aliyenadika kitabu "A Natural Law Approach to Normativity"; Karol Wojtyla(2013) aliyenadika "Love and Responsibility"; na MacCallum (1967) aliyeandika makala "Positive and Negative Freedom."

Vitabu vyote vinne nimeviambatanisha hapa katika fomati pepe baada ya kuvichota kutoka maktaba moja huko Majuu (cyberspace).

Kwa ujumla, Waraka huu umetumia misamiati kadhaa inayotumiwa na wafuasi wa teolojia ya ukombozi wa kidemokrasia.

Kwa mfano, kuhusu maana ya "uhuru," Maaskofu wanaonekana kukubaliana na mawazo ya Profesa MacCallum (1967) aliyependekeza kwamba, “…freedom is ... always [said] of something [called an agent], [which is liberated] from something [which is called a constraint], [and hence being in a position] to do, not do, become, or not become something [which is called a goal]; it is a triadic relation.” (uk. 314)

Ndio kusema kuwa, “uhuru ni mahusiano kati ya vitu vitatu kwa mpigo, kwani mara zote tunapoongelea uhuru tunamaanisha uhuru wa MTENDAJI, aliyekombolewa dhidi ya VIKWAZO vinavyokuwa vinamkabili mtendaji huyo, na kukwamisha azma yake ya ama kufanya kitendo fulani, kutofanya kitendo fulani, au kuwa katika hali fulani, au kutokuwa katika hali fulani, hili la mwisho likiwa ni LENGO lake.” (Tafsiri yangu).

Katika fasili hii, MacCallum (1967) anasema mambo mawili kwa mpigo, moja likihusu maana ya “uhuru” na jingine likihusu maana ya “utumwa.”

Kuhusu “uhuru,” MacCallum (1967) anasema kuwa, “uhuru” ni hali ya kuwa katika mazingira fulani, ambapo MTENDAJI amekombolewa dhidi ya KIKWAZO kilichokuwa kinamzuia kufukuzia LENGO lake kwa ufanisi.

Na kuhusu “utumwa” MacCallum (1967) anasema kuwa, “utumwa” ni hali ya kuwa katika mazingira fulani, ambapo MTENDAJI anakuwa hajakombolewa dhidi ya KIKWAZO kinachomzuia kufukuzia LENGO lake kwa ufanisi.

Nimejiridhisha kwamba, hoja ya “Ufalme wa Mungu” inayoongelewa na Maaskofu wa TEC inayo anatomia yenye pointi muhimu tisa kama ifuatavyo:

Mosi, Maaskofu wanasema kwamba, mfumo wa kanuni za maumbile asilia unaonyesha kuwa upo ufalme wa Mungu ambao umejengwa juu ya mawazo makubwa matatu, yaani ukweli badala ya uwongo, malengo mema badala ya malengo mabaya, mbinu adilifu badala ya mbinu za kihalifu.

Ndio kusema "the real as opposed to the illusory, the good as opposed to the bad, the right as opposed to the wrong," kama tunavyosoma katika Waefeso 5:9.

Yaani, kuna ukweli kuhusu vitu halisi hapa duniani na huko mbinguni, baadhi vikiwa vinaonekana kwa macho kama vile binadamu na baadhi vikiwa havionekani kwa macho kama vile sauti; kuna tunu za kibinadamu; na kuna mwongozo wa haki na majukumu anwai, ambao ni mfumo wa maadili kwa ajili ya kulinda umoja wa mfumo wa tunu husika.

Tunu zifuatazo zinahusika: uhai, afya, ukweli, elimu, uaminifu, utawala bora, mazingira salama, ustawi wa kijamii, maendeleo ya kiuchumi, amani, uwazi, uhuru, furaha, maridhiano, na tunu za kibinadamu baki. (Dokezo namba 1).

Pili, Maaskofu wanasema kwamba, kwa mujibu wa mpango asilia wa maadili ulio katika ufalme wa Mungu, kila tunu ya kibinadamu inayofahamika huambatana na majukumu mawili mara zote, yaani, jukumu chanya la kututaka kulinda na kustawisha tunu husika na jukumu hasi la kututaka kujizuia kuhujumu tunu husika kwa makusudi, ambapo, jukumu hasi hukataza kutendeka kwa tendo baya kila mahali, kila wakati na kwa kila mtendaji. (Dokezo namba 2). (Mathayo 7:12).

Mifano michache itaweka bayana maana ya dokezo hili. Kama raha ni tunu chanya (kitu chema) na mateso ni tunu hasi (kitu kibaya), basi, tuna majukumu chanya ya kukuza raha na kuzuia maumivu, kama ambavyo tuna jukumu hasi la kujizuia kusababisha maumivu.

Kama ukweli ni kitu kizuri na uwongo ni kitu kibaya, basi tunayo majukumu chanya ya kukuza ukweli na kuzuia uwongo, kama ambavyo tuna jukumu hasi la kujizuia kusema uwongo.

Kama maarifa ni kitu kizuri na ujinga ni kitu kibaya, basi tunayo majukumu chanya ya kukuza maarifa na kuzuia ujinga, kama ambavyo tunalo jukumu hasi la kujizuia kusababisha ujinga kwa njia ya kusema uwongo au vinginevyo.

Kama uhuru ni kitu kizuri na utumwa ni kitu kibaya, basi tunayo majukumu ya kukuza uhuru na kuzuia utumwa, kama ambavyo tuna jukumu la kujizuia kusababisha utumwa kwa njia ya kuwaburuza wengine au vinginevyo.

Kama uhai ni kitu kizuri na kifo ni kitu kibaya, basi tunayo majukumu chanya ya kukuza uhai na kuzuia kifo, kama ambavyo tuna jukumu hasi la kujizuia kusababisha kifo.

Kama afya ni kitu kizuri na maradhi ni kitu kibaya, basi tunayo majukumu chanya ya kukuza afya na kuzuia maradhi, kama ambavyo tuna jukumu hasi la kujizuia kusababisha maradhi.

Kama utajiri ni kitu kizuri na umaskini ni kitu kibaya, basi tunayo majukumu chanya ya kukuza utajiri na kuzuia umaskini, kama ambavyo tuna jukumu hasi la kujizuia kusababisha umaskini kwa kumwibia jirani au vinginevyo.

Kama demokrasia ni kitu kizuri na udikteta ni kitu kibaya, basi tunayo majukumu ya kukuza demokrasia na kuzuia udikteta, kama ambavyo tunalo jukumu la kujizuia kufanya udikteta.

Kama uaminifu katika ndoa ni kitu kizuri na uzinzi ni kitu kibaya, basi wanandoa wanayo majukumu ya kukuza uaminifu na kuzuia uzinzi, kama ambavyo wanalo jukumu hasi la kujizuia kuzini.

Kuna mifano mingi ya tunu chanya na tunu hasi, yaani mifano wa wema na ubaya, inayoweza kutumika kufafanua dokezo la maaskofu. Lakini, mifano hii inatosha kutusaidia kuona umantiki wa hoja ifuatayo:

Kanuni kuu ya maadili asilia inatuagiza kumtendea jirani wema kama tunavyotaka kutendewa wema na jirani huyo.

Ndio maana Manabii wote wanaofahamika walifundisha kuwa,
“[Mema] yote mnayotaka watu wawatendee nyinyi, watendeeni wao vivyo hivyo (Math 7:12)."

Tamko hili linaitwa kanuni ya dhahabu (golden rule) kwa kuwa dhahabu ya kweli haichujuki kamwe.

Katika muundo wa lugha hasi kanuni ya dhahabu inaitwa kanuni kanuni ya fedha (silver rule), ikiwa inasomeka hivi: “[Mabaya] yote mnayotaka watu wasiwatendee nyinyi, msiwatendeeni wao vivyo hivyo (Math 7:12)."


Kimsingi, kanuni ya dhahabu ni kanuni inayopingana na kanuni ya chuma (iron rule), isemayo kwamba "mwenye nguvu ndiye mwenye haki ya kunufaika." (Wayne Jackson, 2020 )

Tunatenda mema kwa kuheshimu vitu vizuri vinavyoitwa tunu chanya za kibinadamu zinazotuunganisha pamoja na majirani zetu kwa ajili ya ustawi wa pamoja. Tunaweza kuheshimu tunu chanya za kibinadamu kupitia njia mbili.

Njia ya kwanza ni kwa kuzikuza na kuzihami tunu hizo. Na njia ya pili ni kwa kujizuia kuziharibu, kuzijeruhi au kuzidumaza kwa namna yoyote ile tunu hizo, hii ikiwa ni mbinu ya kustawisha tunu baki, ambazo katika muktadha huu zinakuwa ni lengo.

Kila tunapopindisha haki ya jirani yetu tunakuwa tumehujumu tunu yake mojawapo, na hivyo kumtumia kama daraja au chombo cha kufanikisha malengo yetu kwa kukiuka jukumu letu la kuheshimu haki yake ya kutotumiwa kama nyenzo ya kufanikisha malengo ya mtu baki bila ridhaa yake.

Hivyo, tunapaswa kujizuia kuzihujumu tunu za kibinadamu kwa kuacha kumtumia jirani kama nyenzo ya kufanikisha malengo tuliyoyachagua sisi pasipo kumshirikisha wakati yeye ni kiumbe anayepaswa kujiongoza kwa kutumia urazini na utashi (Karol Wojtyla, 2013:3-28).

Kwa hiyo, tunalo jukumu la kutenda mema na kujizuia kufanya mabaya kila mahali, kila wakati na kwa kila jirani yetu.

Tatu, Maaskofu wanasema kwamba,, kwa sababu mbili zilizotangulia hapo juu, ufalme wa Mungu ni mfumo wa maadili unaopiga marufuku matumizi ya mbinu mbaya kama njia ya kufukuzia lengo jema, kama tunavyosoma katika Warumi 3:8. (Dokezo namba 3).

Nne, Maaskofu wanasema kwamba, tendo la kubatilisha kwa makusudi jukumu linalokataza kutendeka kwa tendo baya (intentionally overriding a negative duty), hii ikiwa ni mbinu ya kutimiza haki yoyote, ni matumizi ya mbinu iliyo haramu ili kufanikisha lengo halali. (Dokezo namba 4).

Tano, Maaskofu wanasema kwamba, kwa sababu mbili zilizotanglia hapo juu, jitihada zozote za kubatilisha kwa makusudi jukumu linalokataza kutendeka kwa tendo baya, hii ikiwa ni mbinu ya kutimiza haki yoyote, ni kitendo cha kupinga mpango wa ufalme wa Mungu. (Dokezo namba 5).

Sita, Maaskofu wanasema kwamba, katika jumuiya ya kisiasa vyombo vya dola kama vile Rais, Bunge, Mahakama, Baraza la Mawaziri, wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya, Baraza la Madiwani, Majeshi, watumishi wanumma, na Tume ya uchaguzi, vimetoka kwa Mungu na hivyo vinalo jukumu la kuheshimu mpango wa ufalme wa Mungu aliye chimbuko la vyombo hivyo. (Dokezo namba 6).

Na saba, Maaskofu wanasema kwamba, kutokana na sababu mbili zilizotangulia hapo juu, kila chombo cha dola kinachobatilisha kwa makusudi jukumu linalokataza kutendeka kwa tendo baya, hii ikiwa ni njia ya kutimiza haki yoyote, kinakuwa kinapinga mpango wa Ufalme wa Mungu alikiumba, na hivyo kinapaswa kubomolewa na kujengwa upya ili kiendane na mpango wa Mungu. (Dokezo namba 7).

Pengo katika Waraka wa Kwarezima


Endapo tutapunguza neno "Tanzania" kutoka katika waraka wa TEC, na kisha kufuta majina ya Maaskofu 33, maelezo yanayobaki hayawezi kuonyesha kwamba waraka huu umeandikwa kwa ajili ya kutoa majibu ya matatizo ya nchi gani.

Hoja yao ni ya jumla bila kujali mipaka ya nchi. Kwa muda mrefu, huu umekuwa ni utaratibu wa kawaida wa Maaskofu wa Kanisa Katoliki.

Kwa mfano, hakuna andiko la Mtaguso wa pili wa Vatican (1963-65) linalojadili moja kwa moja tatizo la ubaguzi wa rangi huko Afrika ya Kusini, japo ilikuwa ni ajenda ya kimataifa enzi hizo. Askofu Dennis Hurley wa Durban aliyekuwa mjumbe wa Mtaguso huo alisumbuliwa sana na dosari hii.

Lakini Askofu Hurley alilazimika kukubaliana na ukimya wa Mtaguso juu ya ubaguzi wa rangi nchini mwake kwa sababu alizoambiwa. Sababu hizo ziliwekwa wazi mwaka 1983.

Kwa mujibu wa ibara ya 285(3) ya sheria za Kanisa Katoliki (1983), Mapadre na Maaskofu Katoliki, ambao ni makuhani wa daraja, wanakatazwa kufanya siasa za moja kwa moja, kwa maana ya kuikosoa serikali kwa lengo la kuingia katika ofisi ya umma (“public office”) na kushiriki katika kutekeleza madaraka ya kisiasa (“civil power”).

Badala yake, sheria hizi zinasema kuwa, ni kazi ya Makuhani Walei kutafsiri nyaraka za Makuhani wa Daraja na kukamilisha hoja zao kwa kuzipa tafsiri mahalia.

Hivyo, kuna njia ya kutokea. Hoja za aina hii zinaweza na zinapaswa kupewa tafsiri mahalia kwa kuonyesha matumizi yake kwenye utatuzi wa matatizo ya kijamii yanayoikabili nchi husika katika sekta za afya, elimu, ikolojia, ofisi za utawala, na kadhalika.

Huko Kenya na Zambia Walei waliwahi kufanya hivyo kwa kuhuisha nyaraka za maaskofu zilizotolewa kabla ya chaguzi zilizoving'oa vyama vya KANU na UNIP.

Waliongeza madokezo mawili muhimu yaliyosaidia kuzifanya nyaraka hizo zimahalishwe na kumulika vizuri matatizo ya kiuchumi, kisiasa, kijamii, kimazingira na kitamaduni katika nchi hizo.

Vivyo hivyo, napendekeza kwamba Walei wa Tanzania tunalo jukumu la aina hiyo pia. Yaani, tunapaswa kusanifu dokezo namba 8 na dokezo namba 9 kwa ajili ya kila sekta ya maisha ya Watanzania.

Kwa njia ya mfano, katika aya zifuatazo, nimeamua kutumia sekta ya siasa za uchaguzi, nikiwa najielekeza kwenye kitendawili cha uhuru wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Tanzania. Yaani, hapa chini nakusudia kutetea madokezo yafuatayo:

Nane, Maaskofu wa TEC "wanaonekana kudai" kwamba, kuna wakati, chombo cha dola kinachoitwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Tanzania, kinakiuka mpango wa “Ufalme wa Mungu,” kwa kukweza maslahi ya wachache na kutweza maslahi ya wengi. (Dokezo namba 8).

Na tisa, Maaskofu wa TEC "wanaonekana kudai" kwamba, kwa hiyo, kutokana na dokeza namba 7 na dokezo namba 8 hapo juu, Tume ya Taifa ya Uchaguzi ni chombo kinachopaswa kubomolewa na kujengwa upya ili kiendane na mpango wa Ufalme wa Mungu. (Dokezo namba 9).

Tatizo la utumwa wa Tume Huru

Hakuna ubishi kuwa, kuna mdahalo unaendelea katika vyombo vya upashanaji habari kuhusu tamko kwamba: Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Tanzania inapaswa kuongezewa uhuru ili iweze kutekeleza kazi zake kwa kasi na ufanisi stahiki.

Kusudi niweze kujua kambi hizi zinasema nini juu ya uhuru wa Tume, niliandaa dodoso lenye maswali kumi, yanayoweza kujibiwa kwa “ndiyo” au “hapana,” na “kulisambaza” kwa wahusika katika kambi mbili kuu zinazonyukana katika mdahalo huu. Yaani, kambi ya Freeman Mbowe (mwenyekiti wa Chadema) na kambi ya John Magufuli (mwenyekiti wa CCM).

Walengwa wa jumla katika utafiti wangu (populatipn) walikwa ni viongozi wote wa taasisi mbalimbali tangu mwaka 1990. Na walengwa mahsusi (sample) walikuwa ni viongozi ambao waliwahi kutamka jambo kuhusu utawala bora katika mfumo wa vyama vingi. Kwa ajili ya kutambua walengwa mahsusi nilitumia mbinu ya kuwanukuu wale waliokuwa ktk tume mbalimbali, viongozi wa vyama vya siasa, viongozi wa asasi za kiraia, viongozi wa serikali waliowahi kusema kitu juu ya uhuru wa Tume ya Uchaguzi. Yaani nilifanya exploratory study kwa msaada wa focused sampling.

Kutokana na majibu niliyoyapokea, ninahitimisha kuwa, Kambi ya Freeman Mbowe wanasema katika Tume kuna uhuru wa 20% na utumwa wa 80% wakati Kambi ya John Magufuli wanasema kuna uhuru wa 100% na utumwa wa 0%.

Katika aya zifuatazo naonyesha kwamba, Kambi ya Freeman Mbowe inasema ukweli na kwamba Kambi ya John Magufuli haisemi ukweli wote.

Hoja za Kambi ya Mbowe

Kwa ujumla, kambi ya Mbowe wanasema kwamba, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (baada ya hapa isomeke Tume) inao uhuru-koko kwa sababu uhuru wake umechanganyikana na utumwa kwa sababu ya vikwazo kutoka upande wa serikali. Majibu ya kambi hili kwenye dodoso langu ni kama ifuatavyo:

Kwanza: Je, Tume inalazimika kikatiba na kisheria kufuata amri au ushauri wa mtu yeyote, idara yoyote ya serikali, au chama chochote cha siasa? Jibu la Kambi ya Mbowe ni “hapana.”

Pili: Je, kuna mahakama yenye mamlaka ya kuhoji jambo lolote lililofanywa na Tume wakati wa kutekeleza majukumu yake, kama vile kumtangaza mgombea Urais, ambaye kwa mujibu wa Tume ameshinda kihalali? Jibu la Kambi ya Mbowe ni “hapana.”

Kuhusu hizi alama mbili za “hapana,” Kambi ya Mbowe inakubali kuwa, kwa mujibu wa ibara za 74(7) na 74(11) za Katiba ya Tanzania, angalau kinadharia, Tume iko huru kwa 20% katika ngazi ya Taifa.

Lakini, kuhusu alama nane za “ndiyo,” Kambi ya Mbowe inadai kuwa, kivitendo, Tume haiku huru kwa 80% katika ngazi ya mikoni na wilayani.

Tatu: Je, Mwenyekiti na Makamishna wa Tume wanateuliwa na Rais, ambaye pia ni mwenyekiti wa chama cha siasa ambacho ni tawala? Jibu la Kambi ya Mbowe ni “ndiyo.”

Nne: Je, kuna ombwe la masharti ya kisheria yanayopaswa kumwongoza Rais katika kuteua baadhi ya watumishi wanaofanya kazi katika Tume? Jibu la Kambi ya Mbowe ni “ndiyo.”

Tano: Je, mikataba ya ajira za wajumbe wanaoteuliwa kufanya kazi katika Tume imo hatarini kwa sababu inaweza kutenguliwa na mwajiri, tena bila mwajiri kuhojiwa na mtu au chombo chochote? Jibu la Kambi ya Mbowe ni “ndiyo.”

Sita: Je, Tume inalalamikia tabia ya serikali kukiuka matakwa ya sheria ya uchaguzi yanayoeleza kwamba, fedha kwa ajili ya bajeti ya Tume zinapaswa kupatikana kwa wakati kutoka katika mfuko mkuu wa serikali? Jibu la Kambi ya Mbowe ni “ndiyo.”

Saba: Je, kuna ombwe la wafanyakazi wa Tume katika ngazi ya mkoa na wilaya, kiasi cha Tume kulazimika kutegemea watumishi wa umma walioko katika serikali za mitaa, ambapo wengi wao wanakuwa ni makada wa chama tawala mpaka siku chache kabla ya kuteuliwa kufanya kazi za Tume? Jibu la Kambi ya Mbowe ni “ndiyo.”

Nane: Je, kuna ombwe la ofisi na magari ya Tume katika ngazi ya mkoa na wilaya, kiasi cha Tume kulazimika kutegemea ofisi na magari ya watumishi wa umma katika serikali za mitaa, ambapo wengi wao wanakuwa ni makada wa chama tawala mpaka siku chache kabla ya kuteuliwa kufanya kazi za Tume? Jibu la Kambi ya Mbowe ni “ndiyo.”

Tisa: Je Mwenyekiti wa Tume aliiambia Tume ya Warioba kwa ajili ya Kuratibu maoni ya wananchi kuhusu Katiba Mpya (2014) kwamba uhuru wa Tume yake umeminywa? Jibu la Kambi ya Mbowe ni “ndiyo.”

Na kumi: Je, Katiba na sheria za nchi vinainyima Tume uhuru wa kujitenga na dhambi ya kuvunja maadili asilia yanayowapa wananchi haki ya kuhoji uhalali wa matokeo ya Rais, baada ya kuwa yametangazwa na Tume? Jibu la Kambi ya Mbowe ni “ndiyo.”

Baada ya Kambi ya Mbowe kujibu maswali haya kumi, wanaipatia Tume alama mbili za “hapana,” sawa na uhuru wa 20%, na wanaipata Tume alama nane za “ndiyo,” sawa na utumwa wa 80%.

Hivyo, Kambi ya Mbowe wanahitimisha hukumu yao dhidi ya Tume kwa kusema kwamba: Tume ya Taifa ya Uchaguzi haiwezi kujitenga na CCM katika mazingira ambamo: kwa sehemu kubwa, sheria hamzuii Rais kuteua baadhi ya watumishi wa Tume ambao ni makada wa chama tawala; utaratibu wa kupatikana kwa wajumbe wa Tume unafanywa na mwenyekiti wa chama tawala cha CCM; upatikananaji wa fedha za bajeti ya Tume unategemea huruma ya serikali ya chama tawala cha CCM; na watumishi wa Tume huko mikoani na wilayani wanaazimwa kutoka serikali ya chama tawala cha CCM, wengi wao wakiwa ni makada wa CCM mpaka siku chache kabla ya kuazimwa na Tume.

Kwa sababu hizi kumi, Kambi ya Mbowe, inadai kwamba, kuna umuhimu, ulazima na uharaka wa kufanyika kwa mageuzi ya kitaasisi katika Tume ya Taifa ya Uchaguzi kabla ya Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 2020.

Ni uelewa wa kambi ya Mbowe kuwa, kimuundo, Tume za Uchaguzi inaweza kuanguka katika modeli mojawapo kati ya modeli tatu zinazojulikana.

Katika modeli ya kwanza, Tume ni chombo kinachojitegemea kwa kila kitu, yaani iko huru dhidi ya maamuzi ya serikali. Katika modeli ya pili, Tume ni chombo kinachotegemea serikali kwa kila kitu, yaani haiko huru dhidi ya maamuzi ya serikali. Na katika modeli ya tatu, Tume ni chombo chenye sifa mseto, kwani inajitegemea kwa kiasi fulani na kutegemea maamuzi ya serikali kwa kiasi baki, yaani Tume inazo chembechembe za uhuru na utumwa chini ya serikali.

Kwa kutumia mgawanyo huu wa Tume za Uchaguzi, ni wazi kwamba, Tume ya Taifa ya Uchaguzi nchini Tanzania inazo chembechembe za uhuru na utumwa.

Hivyo, kambi ya Mbowe inapendekeza kuwa, mwisho wa siku, Tanzania tunapaswa kuongeza uhuru wa Tume kwa kufanya yafuatayo:

Mosi, tunapaswa kukataa Tume ambayo inatumia majengo, magari na watumishi wa serikali na kupigania Tume inayojitosheleza kwa majengo, magari na watumishi tangu Taifani mpaka wilayani.

Pili, tunapaswa kukataa Tume ya wajumbe wanaowajibika kwa Rais aliyevaa kofia ya uenyekiti wa chama tawala na kupigania Tume inayowajibika kwenye Bunge.

Tatu, tunapaswa kukataa Tume yenye wajumbe wanaowakilisha chama kimoja na kupigania Tume inayojumuisha wawakilishi wa vyama vyote.

Na nne, tunapaswa kukataa Tume yenye wajumbe walioteuliwa na Rais, na kupigania Tume yenye wajumbe walitokana na orodha iliyopendekezwa na Rais kwa kushauriana na Bunge, kuhaririwa na vyama vya siasa, na kuthibitishwa na kundi maalum la majaji.

Hoja za Kambi ya Magufuli

Kambi ya John Magufuli, ilifanikiwa “kujibu” maswali machache sana kwenye dodoso “nililolisambaza.” Kimsingi, kuna majawabu mawili pekee yaliyotolewa kwa uwazi mpaka sasa.

Jawabu la kwanza ni kauli ya Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa, akiwa Bungeni hivi karibuni, wakati akijibu swali na Msemaji wa Kambi Rasmi ya Upinzani, Freeman Mbowe.

“Tume hii imeundwa kwa mujibu wa Katiba. Na kwa mujibu wa Katiba ya nchi kipengele cha 7, 11, 12, 78, 74, hiki ni chombo huru. Chombo hiki hakipaswi kuingiliwa na na chombo kingine chochote , iwe rais wa nchi, iwe chama chochote cha siasa au mamlaka nyingine yoyote ile,” alisema Waziri Mkuu Majaliwa.

“Kama ni chombo huru kwa mujibu wa Katiba ndio Tume huru. Sasa kunaweza kuwa na tofauti ya neno uhuru, yaani tunataka itambulike vipi. Chombo kipo, kinajitegemea na kinafanya kazi yake bila kuingiliwa na mtu yeyote kwa mujibu wa Katiba yetu ya mwaka 1977,” aliongeza Waziri Mkuu Majaliwa.

Na jawabu la pili ni kauli ya serikali kupitia Ripoti ya Kamati ya Jaji Kisanga (1999). Baadhi ya wananchi waliojitokeza kwenye Tume hiyo walisema kuwa, kuna mgongano wa maslahi pale Rais wa nchi ambaye amevaa kofia ya uenyekiti wa chama cha siasa kinachotawala anapopewa madaraka ya kuteua watumishi wa Tume inayopaswa kuhudumia vyama vyote.

Kamati ya Kisanga ilitafuta majibu ya serikali kuhusu tuhuma hii, na maoni ya serikali kuhusu hoja hii yalikuwa kama ifuatavyo:

“Kusudi Tume ya Uchaguzi iweze kutekeleza majukumu yake bila woga wala upendeleo, inapaswa kuwa ya kitaalam au yenye wajumbe wenye hadhi, wanaokubalika na ambao uteuzi wao hautazingatia mwelekeo wa siasa wa chama chochote.”

Serikali ikaendelea kusema kwamba, “Muundo wa sasa wa Tume unazingatia sifa hizo na serikali inaona muundo huo uendelee,” na kwamba “kwa upande wa uteuzi wa wajumbe wa Tume ya uchaguzi serikali inaona kwamba Rais ambaye ana dhamana kubwa kikatiba ya kuwateua hata majaji, aendelee kuwateua wajumbe wa Tume.”

Hapa, hoja ya serikali ni kwamba, kwa kuwa Rais huteua Majaji wa Mahakama, ambao ni mhimili mwingine; na kwa kuwa, hakuna ushahidi kuwa, Mhimili wa Mahakama unaathirika kiutendaji kutokana na uteuzi unaofanywa na Rais; basi, inafuata kimantiki kwamba, hakuna sababu nzuri ya kumwondolea Rais madaraka ya kuteua wajumbe wa Tume.

Upekuzi wa kumbukumbu za kimahakama, unaonyesha kuwa, huenda msimamo huu wa serikali unatokana na hukumu ya mahakama iliyotolewa mwaka 1993. Wakati huo, Mabere Nyaucho Marando na Edwin Mtei, walifungua kesi Mahakama Kuu wakidai kuwa, Rais hakuwa na haki ya kuhodhi madaraka yote ya kuunda Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

Marando na Mtei waliiomba Mahakama Kuu itamke kuwa katika kutekeleza jukumu la kuunda Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Rais anakumbana na mgongano wa maslahi yanayotokana na kofia ya urais na kofia ya uenyekiti wa chama anazozivaa pamoja kwa mpigo.

Katika hukumu yake, Mahakama Kuu ilisema: “the mere fact that members of the commission are appointed by the President, who is a leader of a political party, ipso facto, does not imply that the commission cannot act independently.”

Mahakama Kuu inasema kuwa, “taarifa kwamba wajumbe wa Tume wanateuliwa na Rais, ambaye ni kiongozi wa chama cha siasa, pasipo kuangalia ushahidi wa ziada, haziwezi kuhalalisha hitimisho kwamba Tume haina uwezo wa kutekeleza majukumu yake kwa uhuru.”

Wanazuoni kama vile Amon Chaligha na Timothy Mwaikusa waliunga mkono mtazamo huu. Amon Chaligha alidai kwamba, uhuru wa Tume unatokana na uadilifu binafsi wa Makamishna wa Tume. Na Timothy Mwaikusa alidai kwamba katika mfumo wa mahakama kuna wateuliwa wengi wa Rais ambao wanatekeleza majukumu yao vizuri bila kuipendelea serikali inayoongozwa na mamlaka iliyowateua.

Hata hivyo, mawazo haya ya Mahakama Kuu, Amon Chaligha na Timothy Mwaikusa yanakataliwa na wachambuzi huru wa masuala ya kisiasa na kisheria. Kwa mfano, Alexander Makulilo anapinga vikali mtazamo wa Mahakama Kuu.

Makulilo anadai kuwa, kama tukizingatia “mamlaka ya uteuzi kama kigawe kidogo cha shirika chenye kuziunganisha ofisi zote zinazojazwa kwa njia ya uteuzi wa Rais,” tutakubaliana kwamba, “ni kosa kubwa kulingamisha uhuru wa Tume na uhuru wa Mahakama.” Kwa maoni yake, uhuru wa Mahakama ni mkubwa kuliko uhuru wa Tume, kwa sababu kuu nne.

Kwanza, Rais huteua majaji wa Mahakama ya Rufaa baada ya kushauriana na Jaji Mkuu; na huteua Majaji wa Mahakama Kuu baada ya kushauriana na Tume ya Utumishi wa Mahakama.

Pili, uhai wa mkataba wa ajira za majaji umelindwa na Katiba ya nchi kwa sababu kadhaa. Majaji hawawajibiki kwa Rais baada ya kuteuliwa; na hawawezi kuondolewa ofisini kutokana na uamuzi wa Rais pekee, bila kufanyika kwa uchunguzi wa tume maalum ya majaji wa Jumuiya ya Madola, tume ambayo ushauri wake wa mwisho lazima uzingatiwe na Rais.

Tatu, malipo ya majaji wa Mahakama ya Rufaa na Mahakama Kuu yanatoka moja kwa moja katika Mfuko Mkuu wa Serikali, wakati bajeti ya Tume hainufaiki na Mfuko huu, japo sheria ya uchaguzi inasema kuwa Tume inapaswa kunufaika.

Na nne, majukumu ya Tume yanahusu uchaguzi unaoamua nani aunde serikali na yupi asiunde serikali; wakati mahakama ni mhimili mmojawapo kati ya mihimili mitatu ya dola, ambako mhimili huu unayo majukumu mapana ya utoaji haki katika kesi zote za madai na jinai.

Makulilo anasisitiza kuwa, sababu hizi nne kuhusiana na tofauti zilizopo kati ya Tume na Mahakama zinatoa kivutio (“incentive”) kwa Rais ambaye ni mamlaka ya uteuzi iliyovaa kofia ya uenyekiti wa chama tawala kuitumia Tume kama daraja la kukipendelea chama chake tawala na kuvionea vyama vya upinzani. Yaani, huu ni “ushahidi wa ziada” ambao haukuzingatiwa na Mahakama katika kesi ya Marando na Mtei dhidi ya serikali ya mwaka 1993.

Kwa kutumia kanuni za mantiki ya Aristotle, inayotutaka kusanifu hoja yenye dokezo kuu, dokezo dogo na hitimisho, naona kwamba, hoja ya Makulilo inaweza kufupishwa kama ifuatavyo:

Mosi, Makulilo anaonekana kudai kwamba, kwa mujibu wa nadharia ya ubosi na uwakala (“principal-agent theory”), kila mjumbe wa Tume ni wakala aliyeteuliwa kutekeleza kazi kwa mujibu wa mkataba maalum (“agent”), wakati Rais aliyevaa kofia ya uenyekiti wa chama tawala cha CCM ni mamlaka ya uteuzi (“principal”), ambayo pia inafanya kazi kama jukwa la uwajibikaji wanakoripoti wateuliwa (“accounting forum”).

Pili, Makulilo anaonekana kudai kwamba, kwa mujibu wa nadharia ya ubosi na uwakala, mamlaka ya uteuzi wa wajumbe wa Tume na jukwa la uwajibikaji wanakoripoti wateuliwa ni kitovu chenye mamlaka ya veto kuhusu maudhui ya hati ya majukumu na uhai wa mkataba wa ajira ya wateuliwa.

Na tatu, Makulilo anaonekana kuhitimisha kwamba, pale mgongano wa maslahi unapotokea kati ya chama tawala na vyama vya upinzani, rais aliyevaa kofia ya uenyekiti wa chama tawala atakuwa na kivutio (“incentive”) cha kumfanya atumie kofia ya urais kukinufaisha chama chake tawala anachokiongoza.

Yaani, Rais atatoa maagizo haramu kwa wajumbe wa Tume kuwataka wakipendelee chama chake tawala. Katika mazingira haya, wajumbe wa Tume pia watakuwa na kivutio (“incentive”) cha kutekeleza hayo maagizo haramu kwa sababu ya ulazima wa kulinda ajira zao, ambazo hazijalindwa kisheria.

Hatimaye kanuni za kutofungamana na upande wowote, uwazi na uadilifu (“impartiality, transparency and integrity”) zitayeyuka. Hivyo ndivyo nadharia ya ubosi na uwakala (“principal-agent theory”) inavyotufundisha kuhusu haki na majukumu ya bosi, kwa upande mmoja, na haki na majukumu ya wakala wake, kwa upande mwingine. Kwa hiyo, mwanazuoni Makulilo anayo hoja nzito hasa.

Muhtasari na majumuisho

Mpaka sasa tumeona tofauti kati ya uhuru na utumwa, hoja za kambi ya Mbowe, na hoja za kambi ya Magufuli. Ni wazi kwamba, hoja za kambi ya Mbowe zinazipiku hoja za kambi ya Magufuli.

Hivyo, baada ya kuyaona haya yote, mwandishi wa makala hii anakubaliana na kambi ya Mbowe katika raia kwamba: Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Tanzania inapaswa kuongezewa uhuru ili iweze kutekeleza kazi zake kwa kasi na ufanisi stahiki.

Hitimisho na mapendekezo

Mwaka 2020 ni mwaka wa kutumia sanduku la kura, chini ya usimamizi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, kuchagua viongozi wazuri na kubagua viongozi wabaya, kuchagua sera nzuri na kubagua sera mbaya, kuchagua itikadi nzuri na kubagua itikadi mbaya.

Na kama inavyoeleweka, kwa sasa tuko katika kipindi ambacho serikali inatuhumiwa kuminya uhuru wa watu kukusanyika, kufikiri na kueleza wanachokifikiri.

Aidha, hiki ni kipindi ambamo watu wengi wanalalamikia kufungwa na minyororo ya afya duni, minyororo ya elimu duni, minyororo ya ikolojia duni, minyororo ya ofisi-tawala duni, na minyororo ya uchumi duni.

Hawa wanataka kuona afya bora, elimu bora, ikolojia bora, ofisi za utawala bora, na uchumi bora kwa watanzania wengi.

Kunahitajika ushahidi usiokanushika ili kusanifu dokezo namba nane na dokezo namba tisa kwa kila sekta ya maisha ya Watanzania, madokezo haya yakiwa yanatumia hoja ya waraka wa TEC kama egemeo.

Kwa njia hiyo tutakuwa tumeutumia vizuri Waraka wa TEC kwa ajili ya Kwarezima ya 2020.

Naomba kuwasilisha hoja nikiwa natarajia kupata udadavuzi kabambe kuonyesha matatizo katika sekta ya uhai, afya, elimu, ikolojia, ofisi za utawala na uchumi

Bibliografia

1. Alexander Makulilo et al., Election Management Bodies in East Africa: A comparative study of the contribution of electoral commissions to the strengthening of democracy (Johannesburg: Open Society Foundation, 2015).

2. Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania, Ujumbe wa Kwaresima 2020: Ufalme wako Ufike! (Nimeisoma 18 Machi 2020).

3. Bebhinn Donnelly, A Natural Law Approach to Normativity (New York: Routledge, 2016)

4. Gerald C. MacCallum, Negative and Positive Freedom, The Philosophical Review, 76.3(1967): 312-334.

5. Gustavo Gutierrez, A Theology of Liberation: History, Politics, and Salvation (Maryknoll, USA: Orbis Books, 1988).

6. James Sire, The Universe Next Door: A Basic Worldview Catalog (Illinois, USA: InterVarsity Press, 2009).

7. The United Republic of Tanzania (URT), The Constitution of the United Republic of Tanzania (1977).

8. The United Republic of Tanzania (URT), The Political Parties Act No. 5 of 1992.

9.Karol Wojtyla, Love and Responsibility (Boston, USA: Pauline Books and Media, 2013).

10. Wayne Jackson, "
Gold, Silver, and Iron: Three Rules of Human Conduct." ChristianCourier.com. Access date: 18 March 2020.

11. Religious Tolerance Website, The Golden Rule and Ethics of Reciprocity



Mama Amon,
Sumbawanga Rural,
18 Machi 2020.

(Updated 02 Aprili 2020)
Walaka upo biased sana! Maaskofu wanapokubali kutumika kwa maslahi ya kikundi cha siasa hapo ujue tunayo shughuli! Nyuma ya pazia ya haya yote tunamuona Mbowe @et al! Ktk maeneo yote ya kulenga ktk kutoa salamu za pasaka tume ya uchaguzi ndio lililopewa kipaumbele! Tume huru ya uchaguzi inamahusiano gani na mfungo wa pasaka? Sijui huu ujumbe umetoka kwa Mungu na kufikishwa kwa watumishi wake!? Au ni waumini wamefanya 'petition!?
All in all huu siyo ujumbe wa wananchi wa kawaida! Bado hoja yangu ipo palepale, raia wa kawaida hawana shida na tume ambayo kama ilivyo inauhuru! Hawa watumishi wa Mungu, wanapaswa wajitathmini kama wanawakilisha Mungu wa namna gani kwa aina na 'source' ya ujumbe wanaofikisha kwa jamii!
Kwa kuwa sio wananchi wanaotaka hiyo tume, bali ni shinikizo la vikundi vya vinavyo taka ruzuku, ni wazi watatumia kila hila kushawishi vikundi au hata wanachama wao kutimiza agenda yao maana hamna sera wala agenda yenye mashiko ya kuuza kwa wananchi!
Umekurupuka na povu jingi sana kwa kuleta huu walaka/salamu kama ushahidi! Pole kwa kukuangusha maana huu siyo ushahidi unaotakiwa hapa! Hao watumishi walioandika hawatuwakilishi sisi raia wa mtaani! Hatujui nini kiliwakuta mpaka wakaandika hayo walioandika nachoweza kukuhakikishia, hayakuwa mawazo ya waumini wao waliowengi! Wanajua walikoyatoa!
Narudia tena, ni unafiki wa hali ya juu kujidai mnadai tume huru ya uchaguzi wakati ninyi wenyewe mnawanyongea mbali wanachama wenu kwa kutokuwa na uhuru na uwazi ktk vijichaguzi vyenu ktk vijikundi vyenu!
Watu kama hawa ndio wapewe kushika dola ni hatari sana maana kama huna uaminifu kwenye vidogo hatutarajii muujiza ukipewa vingi....mtanyongelea haji Mbowe et al you lack legitimacy!
 
Kosa lako ni moja. Unadhani kwamba serikali ya CCM inamiliki madaraka na kwamba wanayo hiari ya kuayaachia au kuyang'ang'ania. Madaraka yako mikononi mwa umma, na serikali ya CCM ni wakala tu. Umma unaamua nani akalie ofisi ya uwakala na yupi asikalie. Badilisha mtazamo wako, halafu tujenge hoja zilizonyooka.
Huyo umma ni nani vile!? Si ndio huyo ameiweka ccm kunako dola? Au umma maana yake ni wewe na Mbowe? Hayo makelele na mapovu yenu kwa kukosa sera na agenda yanakera:mad::mad::mad::mad::mad::mad:!
 
CCM wanaona upinzani kuingia ikulu ni sawa na uhaini.Suala la kushindwa uchaguzi halipo kwenye agenda zao!
Sasa nyie wapinzani muende ikulu kwa agenda na sera ipi? Mkatuuze au!?
Huko mliko tu mambo yenu yapo shagharabagala...afu mpewe dola ili mtuuze kwa mabeberu!?
 
Huyo umma ni nani vile!? Si ndio huyo ameiweka ccm kunako dola? Au umma maana yake ni wewe na Mbowe? Hayo makelele na mapovu yenu kwa kukosa sera na agenda yanakera:mad::mad::mad::mad::mad::mad:!

Una uhakika kuwa umma ndio umeiweka CCM madarakani? Fanya utafiti tena vide uchaguzi wa 2015 na huu wa 2019. Utakuja hapa kuniomba msamaha.
 
Walaka upo biased sana! Maaskofu wanapokubali kutumika kwa maslahi ya kikundi cha siasa hapo ujue tunayo shughuli! Nyuma ya pazia ya haya yote tunamuona Mbowe @et al! Ktk maeneo yote ya kulenga ktk kutoa salamu za pasaka tume ya uchaguzi ndio lililopewa kipaumbele! Tume huru ya uchaguzi inamahusiano gani na mfungo wa pasaka? Sijui huu ujumbe umetoka kwa Mungu na kufikishwa kwa watumishi wake!? Au ni waumini wamefanya 'petition!?
All in all huu siyo ujumbe wa wananchi wa kawaida! Bado hoja yangu ipo palepale, raia wa kawaida hawana shida na tume ambayo kama ilivyo inauhuru! Hawa watumishi wa Mungu, wanapaswa wajitathmini kama wanawakilisha Mungu wa namna gani kwa aina na 'source' ya ujumbe wanaofikisha kwa jamii!
Kwa kuwa sio wananchi wanaotaka hiyo tume, bali ni shinikizo la vikundi vya vinavyo taka ruzuku, ni wazi watatumia kila hila kushawishi vikundi au hata wanachama wao kutimiza agenda yao maana hama sera wala agenda yenye mashiko ya kuuza kwa wananchi!
Umekurupuka na povu jingi sana kwa kuleta huu walaka kama ushahidi! Pole kwa kukuangusha maana huu siyo ushahidi unaotakiwa hapa! Hao watumishi walioandika hawatuwakilishi sisi raia wa mtaani! Hatujui nini kiliwakuta mpaka wakaandika hayo walioandika nachoweza kukuhakikishia, hayakuwa mawazo ya waumini wao waliowengi! Wanajua walikoyatoa!
Narudia tena, ni unafiki wa hali ya juu kujidai mnadai tume huru ya uchaguzi wakati ninyi wenyewe mnawanyongea mbali wanachama wenu kwa kutokuwa na uhuru na uwazi ktk vijichaguzi vyenu ktk vijikundi vyenu!
Watu kama hawa ndio wapewe kushika dola ni hatari sana maana kama huna uaminifu kwenye vidogo hatutarajii muujiza ukipewa vingi....mtanyongelea haji Mbowe et al you lack legitimacy!

Hero, hakuna mahali nimeongelea "walaka." Kwa hiyo sina la kukujibu.
 
Una uhakika kuwa umma ndio umeiweka CCM madarakani? Fanya utafiti tena vide uchaguzi wa 2015 na huu wa 2019. Utakuja hapa kuniomba msamaha.
Kukuomba msamaha kwa kuwe wewe ndio umma na hukuiweka ccm!?
Mama Amon, are in your right mind?
Ccm ipo madarakani ki katiba kwa kuchagukiwa na watu wengi! Mie mwenyewe nilikuwa kwenye safari ya matumaini...lakini nawashukuru sana walioirudisha Ccm chini ya Magu!
Kipindi hiki sitafanya makosa tena kupoteza kura yangu ukawa wala chadema! Ccm ndio chaguo langu, hayo magenge ya ruzuku siyahitaji!
 
Una uhakika kuwa umma ndio umeiweka CCM madarakani? Fanya utafiti tena vide uchaguzi wa 2015 na huu wa 2019. Utakuja hapa kuniomba msamaha.
Kukuomba msamaha kwa kuwe wewe ndio umma na hukuiweka ccm!?
Mama Amon, are in your right mind?
Ccm ipo madarakani ki katiba kwa kuchagukiwa na watu wengi! Mie mwenyewe nilikuwa kwenye safari ya matumaini...lakini nawashukuru sana walioirudisha Ccm chini ya Magu!
Kipindi hiki sitafanya makosa tena kupoteza kura yangu ukawa wala chadema! Ccm ndio chaguo langu, hayo magenge ya ruzuku siyahitaji!
 
Hero, hakuna mahali nimeongelea "walaka." Kwa hiyo sina la kukujibu.
Hizo salamu zako za pasaka na maaskofu uliotaka uwe uthibitisho wa wananchi kudai tume wakati tayari ipo!
Afu nyie mnadhambi yaani mpaka mnawapuruta watumishi wa Mungu wawasaidie kufanya 'dirty works'! Mungu anawaona, shauri yenu!
 
Madaraka yako mikononi mwa umma, na serikali ya CCM ni wakala tu. Umma unaamua nani akalie ofisi ya uwakala na yupi asikalie. Badilisha mtazamo wako, halafu tujenge hoja zilizonyooka.
Bado ni yaleyale tu! Siasa!! Umma! siyo Umma! but (TPTB) = the power that be, Easy going ba-Tanzania? are walking dead,comfortably asleep and love it, hawajui why? hela zinapotengenezwa? hapo ndiyo umma wenu ulipo! (TPTB), chunguza Duniani kote, Umma wa Dunia uko hapo! mind you; mtizamo wangu kinzani, hau nyookei hapo kwako!

Tanzania/Africa siyo kisiwa, ipe Mapana na marefu yake, ukite kwenye mizizi ya tatizo, huyo wakala wenu, anajua mchezo na ana guts kuliko upinzani, na mizizi ya tatizo, wengi hamlijui, mnatupoteza maksudi kwa faida zenu! haka kajamaa ka Lisu kana jua mengi sana!

Mysterious Global Elites has been there for Decades, Deep state. they rule, and monopolizes all valuable resources on Earth that suit their needs! and no matter what may, they are chosen by blood to control the World Government..if you don't believe me just try to contest!

I think weye u miongoni wao, an expert in propaganda, twisting Languages which come across with the truth, na unakusanya opinion mkazifanyie kazi. Nchi inajengwa na mawazo kinzani, pasi na badili wakala hovyo. mfano, China. TPTB Hana nafasi kwao, yes! walijua kabla.

Sheria ya Historia iko ivi ''ukiruhusu kubadili wakala hovyo nchi haita stabilize'' ukitaka fanya lkn hapatakalika! sasa tufanye?... walevi watakubali! hawa TPTB ni fragile, wakala akikosea tu, wanatumia Umma unaodhania, NGO's pinzani zinaweza tumia mwanya huo! kuwa wakala.

THINK TANK tunajua mna nguvu tele, endapo mtajua umma wa kawaida unataka nin, mtajipachikiamo the same people! kwa hadaa ya ''mtoto wa mkulima'' au ooh! mimi mpinzani nataka mabadiliko!, ili mbakiemo, mfano kina Mabere Marando! Zitto! Mrema, Lowasa nk! km iktokea CCM kushindwa basi ni umma wa TPTB umeamua, kwa kutanguliza wanuka Moshi wa Mafuta ya Mienge!! wasiojua A'' wala B'' pa kuanzia ni Zanzibar!

Leo hii hkn Mwafrica atatumia nguvu ya Umma wao! kwa faida ya Mwafrica na akafanikiwa, mifano ni mingi! km ikitokea not in my watch! ....cause Peace is a battle, it's not won so easily, it demand humility, Sacrifices from every one, it requires strong committeemen and visionary political wills. hapa wapinzani puppets ni kinyume, huta fanya maamuzi ya tija kwa nchi yako bila Breton-wood institutions kukupa go ahead!

NGO's za Mkoloni mweusi, mlio wengi, wali/wana watumia, the so called ''Umma'' ili kupanda na kupata mafanikio kisiasa, kiuchumi, lkn mbinu na Mamlaka viko palepale!. kifupi! ukweli uko wazi ni fursa adimu kwao! na wewe umeona jicho la fursa! Ok! so nibadilishe mtizamo wangu, and you get what you want from me, in turn you will show me how stupid I'am!
 
Siasa ndivyo zilivyo! usipojua siasa, utahanagaika km hivi! ukikataa matokeo hujui siasa, hata kama tungekupa unachotaka kingepotea kirahisi, tungekupa kura zetu usingejua sababu ya wewe kuwapo pale, kifupi ungetusumbua! sasa tuwape wanaojua? au wasio jua?

Tujengee imani! msione aibu kukodi wanasiasa, anakushindisha akimaliza basi anaenda zake! atakuja tena ukimuhitaji
 
Back
Top Bottom