SoC02 Utumwa wa Internet na Mitandao ya Kijamii

Stories of Change - 2022 Competition

KALEKU

Member
Feb 23, 2015
8
6
UTUMWA WA INTANETI NA MITANDAO YA KIJAMII
images (14).jpeg

Matumizi ya intaneti yanazidi kukua kila kukicha kulingana na jinsi Sayansi na Teknolojia vinavyozidi kuboreshwa. Kutokana na maendeleo hayo mitandao ya kijamii nayo inazidi kushika kasi na kuzidi kujipatia watumiaji wengi. Maisha yamebadilika sana na si mjini tu bali hata kijijini wanaweza kufurahia matumizi ya intaneti na mitandao ya kijamii.

Changamoto kubwa tuliyonayo katika ukuaji na kupanuka kwa matumizi ya intaneti na mitandao ya kijamii ni matumizi sahihi na yenye tija kwa watumiaji. Mashirika yanayotoa huduma za intaneti na mitandao ya kijamii wote wanajipatia kipato lakini tukimtazama mtumiaji wa huduma hizi sio wote wana matokeo chanya ya matumizi ya intaneti na mitandao ya kijamii.

Katika taifa letu Tanzania kuna watumiaji wengi sana wa intaneti na mitandao ya kijamii lakini wanaotumia kwa manufaa ni wachache walio tambua faida zake. Kuna watu wengi sana na wengi wao wakiangukia katika kundi la vijana ambao ambao wanalipia huduma za intaneti kila siku lakini ukihitaji mrejesho wa nini cha faida kimepatikana sio wengi wanaweza kuonyesha walichokipata.

Mitandao ya kijamii ikitumika vizuri inaweza kuwa njia nzuri ya kujiingizia kipato lakini vijana wengi bado hawajajikita kuitazama mitandao hii kama JUKWAA LA KIBIASHARA. Mitandao ya kijamii inawafanya vijana wengi kuwa watumwa kwa kushindwa kukaa nje ya mitandao hiyo hata kidogo. Wengi wamejiunga kwenye mtandao zaidi ya mmoja na wanaweza kutumia masaa mengi wakihama kutoka mtandao mmoja kwenda mwingine bila kuwa na manufaa makubwa.

Changamoto ni kubwa sana kwa vijana walioshikwa na mitandao hii na wakati mwingi ukifatilia wanachokifanya katika mitandao hii kwa asilimia kubwa sio vitu vya maana. Wengi tunashuhudia mada na mijadala mbalimbali isiyomjenga kijana jinsi gani inapata wafuasi wengi. Ni ukweli usiopingika kwamba wengi wanatumia mitandao ya kijamii kishabiki tu na kufuata mikumbo na mwisho wake wanalewa matumizi yasiyo sahihi ya mitandao hii.

Ni ajabu kuona mijadala na mada zinazohusu mapenzi na mambo ya starehe na anasa mara nyingi ndizo hupata wafuasi wengi na mwisho hakuna chochote kinachomjenga wala kumfaidisha mtumiaji. Kadhalika kutotambua sheria na kanuni ya matumizi yah ii mitandao inapelekea watumiaji wengi kutuma maudhui yasiyofaa kama picha za utupu na wengine kutumia lugha mbaya matusi.

Mitandao ya kijamii inapotumika bila uelewa sahihi inatengeneza uraibu kwa watumiaji na mwisho unakuwa utumwa mbaya ambao watumiaji wanajiingiza wenyewe na kulipa gharama huku wakiathirika katika maeneo mbalimbali kimaisha.

Wapo wengi wanakosa uhuru na amani kabisa wanaposhindwa kununua vifurushi vya intaneti na kutumia mitandao hii ya kijamii. Wengi wanajiona kukosa kitu muhimu sana kuwa nje ya mitandao ya kijamii na kupelekea kuingia gharama zisizo za msingi ili kupata huduma hii. Wengine wanakosa nidhamu hata katika maeneo yasiyostahili kutumia vifaa vya kimtandao na kushindwa kujizuia. UTUMWA WA INTANETI NA MITANDAO YA KIJAMII HAUCHUKULIWI KWA UMAKINI ILA KUNA WATU MAISHA YAO YAMEFUNGWA.

MADHARA YA MATUMIZI MABAYA YA INTANETI NA MITANDAO YA KIJAMII
34748226_446348305829284_1925280748982501376_n.jpg

1. MATUMIZI MABAYA YA KIPATO
Watu wengi wasiojua matumizi sahihi ya intaneti na mitandao ya kijamii wanatumia fedha vibaya. Wapo wanaotumia fedha kununua tu vifurushi vya intaneti ambavyo haviwaingizii kipato chochote na kutumia kufanya mambo yasiyo na tija.

2. MATUMIZI MABAYA YA MUDA
Watu wengi sana hususani vijana hupoteza muda mwingi sana kwenye mitandao ya kijamii kwa kutotambua matumizi yake sahihi. Wapo watu wanachelewa kulala, wanachelewa kazini, wanachelewa kwenye mambo ya msingi kwa sababu ya kupoteza muda kwenye hii mitandao

3. MATATIZO YA KIAFYA
Baadhi ya watu wanaotumia mitandao hii bila kuwa na kiasi wanapata changamoto za kiafya kama kuumwa na kichwa na wakati mwingine macho kupata tatizo, msongo wa mawazo na matatizo mengine ya akili.

4. KUHARIBU SIFA YA MTU
Matumizi yasiyo sahihi ya mitandao hii yanapelekea kuchafua sifa ya mtu pale anaposhindwa kutumia weledi kufikisha baadhi ya mambo katika mitandao. Kwa mfano mtu anapotumia lugha ya matusi au kusambaza picha za utupu hupelekea kuchafua sifa na jina lake.

5. UONGO, UDANGANYIFU NA WIZI
Mambo mengi ya uongo yanaweza kusambaa kwa kutotumia mitandao ipasavyo. Udanganyifu na wizi unaweza pia kutekelezwa kupitia matumizi yasiyo sahihi ya mitandao.

6. MAISHA BANDIA
Baadhi ya watumiaji wa mitandao hii ya kijamii huwa na changamoto ya kuwa na maisha yasiyo halisi kwenye mitandao. Wengi hujionyesha kuwa na viwango fulani vya maisha ambavyo hawana. Lakini pia mitandao inaweza kuondoa uhalisi wa maisha tu na umoja wa kifamilia uliozoeleka. Badala ya familia kukaa pamoja na kushirika mazungumzo ya pamoja kila mtu anakuwa kivyake kwenye mitandao.

7. MAISHA KUKOSA USIRI
Mitandao ya kijamii inapotumika ndivyo sivyo inakuwa chanzo cha watu wengi kukosa usiri katika maisha yao. Sio kila kitu ni cha kuweka kwenye mitandao ila wengi wanashindwa kujizuia na kuanika vitu vya ndani visivyostahili.

20220903_220432.jpg

FAIDA ZA MATUMIZI SAHIHI YA MITANDAO YA KIJAMII
Pamoja na kuwa na athari lukuki za matumizi mabaya ya intaneti na mitandao ya kijamii, kuna faida nyingi na zenye tija kwa wanaoweza kutumia mitandao hii kwa usahihi.

1. NJIA YA KUJIFUNZA
Mitandao ya kijamii ni njia nzuri ya kujifunza mambo mbalimbali yenye faida katika maisha. Badala ya kupoteza muda katika mada na mijadala isiyo na tija ni bora kujifunza vitu kama biashara, ufugaji, kilimo na mengineyo.

2. JUKWAA LA BIASHARA NA MASOKO
Kupitia mitandao yakijamii ni rahisi kufanya biashara ya kimtandao ukauza au kununua bila kuingia gharama ya kuonana ana kwa ana.

3. KUUNGANISHA WATU KIMAWASILIANO
Mitandao ya kijamii ni njia nzuri ya watu kuwa pamoja kwa kuwasiliana. Upweke wa kuwa mbali na wale uwapendao unaweza kuondolewa kupitia mawasiliano katika mitandao hii. Pia mitandao inaweza kumletea mtu watu muhimu wa kumfaa.

4. VYANZO VYA HABARI
Dunia inakuwa kijiji pale unapoweza kutumia vizuri kupata habari toka sehemu mbalimbali.

5. MICHEZO NA BURUDANI
Mitandao ya kijamii ni chanzo kizuri cha michezo na burudani mbalimbali.

6. CHANZO CHA KIPATO
Kupitia matangazo na biashara mtandaoni wengi wanaweza kutengeneza fedha na kuboresha maisha yao.

HITIMISHO: Mitandao ya kijamii ina madhara mengi isipotumika kwa nidhamu ila ikitumika kwa uangalifu ni njia nzuri ya kuboresha maisha ya watu. Ili kuepuka utumwa wa mitandao ya kijamii lazima kuwa na nidhamu binafsi na kutotumia mitandao hii kupita kiasi ili kuepuka madhara yanayoweza kujitokeza.ni vyema kuacha kutumia mara unapoona inakunyima furaha, utulivu na amani.
0746 55 55 44
 
UTUMWA WA INTANETI NA MITANDAO YA KIJAMII
View attachment 2344920

View attachment 2344922

View attachment 2344926

Ni nzuri sana😍sema nimepost na mimi thread ila naona siioni kwenye stories of changes
 
Back
Top Bottom