UTUMISHI: Hakuna nyongeza ya msahahara kwa sasa, tamko la Rais bado linafanyiwa kazi

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Aug 24, 2011
49,195
103,721
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejiment ya Utumishi wa Umma Dr.Ndumbaro amesema nyongeza ya mshahara iliyotangazwa na rais haitaongezwa kwa sasa kwa kuwa bado inafanyiwa kazi.

Katibu Mkuu alizungumza haya wakati anatoa ufafanuzi juu ya kurejeshwa kazini kwa watumishi waliokata rufaa kutokana na vyeti feki.

MY TAKE
Watumishi wa umma muungeni mkono Rais kwa kufanya kazi, kulilia nyongeza ya mshahara ni kumkwamisha Rais kutumikia watanzania masikini (Natania tu)
 
That is too much, he should regards his fellow!!

Post sent using JamiiForums mobile app
 
Watumishi wa umma mnalialia nini? Serikali kwa sasa inajikongoja kutafuta vyanzo vya mapato na kuimarisha uchumi wa ndani. Muungeni mkono rais, bila shaka hapo baadae mtanufaika. Besides, kuongeza mshahara kwa wafanyakazi wote nchini ni mchakato mrefu, si kuamka tu kesho mnajaziwa fedha
 
Fanyeni kazi kwa mshahara huo huo ninyi watumishi wa umma msioweza kujiajiri.
Magufuli usiongezea mshahara peleka fedha kwenye reli ya kisasa na bwawa la umeme la Rufiji.
Usibabaishwe na wafanyakazi wako hata usipoongeza mshahara hawana pa kwenda watabaki kulia lia mpaka wanastaafu.

Post sent using JamiiForums mobile app
 
Ninachofurahia ni kuwa muda unakwenda saana, mapema itakuwa 2020. Kama Watumishi wa Umma siyo Mazombi( Wana Kumbukumbu) hata awadanganyie 2019 kuongeza ni Kumpoteza tu kwenye Usimamizi wa Kura!

NB: Hii inawezekana Labda Kenya kwa Afrika Mashariki hii!
 
Ninachofurahia ni kuwa muda unakwenda saana, mapema itakuwa 2020. Kama Watumishi wa Umma siyo Mazombi( Wana Kumbukumbu) hata awadanganyie 2019 kuongeza ni Kumpoteza tu kwenye Usimamizi wa Kura!

NB: Hii inawezekana Labda Kenya kwa Afrika Mashariki hii!
Shida ni mbadala wa hiki chama mkuu!!!
 
Watu walikuwa na matumaini mwezi huu mambo yatakuwa mazuri, sasa itakuwa balaa zaidi

Post sent using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom