Utumiaji wa makampuni ya consultants katika miradi ya maji ni upigaji na matumizi mabaya ya fedha za Umma

Upepo wa Pesa

JF-Expert Member
Aug 8, 2015
21,253
34,203
Kuna tetesi nimesikia wizara ya maji inataka kusaini mikataba na makampuni ya consultants kwa ajili ya usanifu wa miradi ya maji na usimamizi wake.

Je inakuaje serikali itumie hizi kampuni wakati inaweza tumia wataalam wa ndani (watumishi wa serikali)?

Inakuaje serikali iwe tayari kulipa kampuni ya consultants mabilioni ya pesa wakati kazi hiyo inaweza fanyika kwa gharama ndogo kwa kutumia mainjinia wake?

Yani mradi wa kijiji kimoja unaajiri kampuni isanifu kweli?

NB: Nashauri hiyo mikataba ya consultants mnayotaka kusaini mwaka huu msisaini kama kweli mnajali fedha za umma wa watanzania!!
 
Kuna tetesi nimesikia wizara ya maji inataka kusaini mikataba na makampuni ya consultants kwa ajili ya usanifu wa miradi ya maji na usimamizi wake.

Je inakuaje serikali itumie hizi kampuni wakati inaweza tumia wataalam wa ndani?

Inakuaje serikali iwe tayari kulipa kampuni ya consultants mabilioni ya pesa wakati kazi hiyo inaweza fanyika kwa gharama ndogo kwa kutumia wataalam wa ndani?

NB: Nashauri hiyo mikataba ya consultants mnayotaka kusaini mwaka huu msisaini kama kweli mnajali fedha za umma wa watanzania!!
Mkuu Mzinga wa asali umeanguka wenyewe kutoka mtini,unataka wanakijiji wasilambe asali!!!
 
Sukuma gang mkae kwa kutulia, mmeambiwa kama roho inauma sana nenda kazikwe chato. Kama una akili timamu kaombe na wewe hizo tenda
 
Sasa unataka consultants wakale wapi?... ushauri wa kitaalamu ni muhimu..

Yaani wewe jamaa unataka miradi ifanyike bila ma consultants kisa tu wewe unaona haifai?

Ungeuliza kwanza umuhimu wa hizo consultants tukuambie.

Najua unachowaza ila kuna protocal lazima zifuatwe, or else tubadilishe kabisa utaratibu wa namna ya kutekeleza miradi ya serikali. Na haya mqbadiliko inatakiwa yafanyike kwa mujibu wa sheria, sio kuzibq viraka kama hivi... iwe kwa miradi yote ya serikali.
 
Mkuu embu acha utani basi, hizo protocal unazisemea ni zipi kiasi kwamba hakuna injinia serikali anayezijua?

Au ataka kutuaminisha huko serikalini hakuna professional engineers kiasi kwamba tutumie mabilioni ya pesa kuweka makampuni?

Je unajua miradi ya maji amekua aki design nani kama sio hao professional engineers walioko serikalini?

Je unajua ni miradi mingapi iliyo sanifiwa na hayo makambuni (kabla ya mikataba yao kuvunjwa) ilifeli na mingine mpaka leo haitoi maji?

Swali la msingi ni kwanini utumie mabilioni ya besa kulipa kampuni ifanye kazi ambayo ingefanywa na imekua ikifanywa na mainjinia wa ndani kwa gharama ndogo?
 
Ndugu

yangu, uzoefu ktk nchi kama Tz unaonyesha kazi za serikali, kama zile za 'force account' value for money, mwisho wa siku, in terms of ' quality' product of works yake imekuwa tatizo kubwa, sababu msimamizi anakuwa yuleyule contractor anayejenga, hivyo mwishowe kazi inakuwa chini ya viwango, na muda mfupi baadae, matokeo yake serikali kuingia gharama tena kwa walipa Kodi........ndo maana wanajaribu Sasa kurudi kwenye mfumo wa kawaida kuepuka changamoto kama hizi, zilizotokea kwenye miradi ya 'force account'...
 
Ushamba ni mzigo wa kuni. Wakati mwingine muwe mnaficha ujinga wenu.
Unaposema wataalamu wa ndani una maanisha nini? Kwani hao ma consultant si watanzania?

Wafanyakazi wa serikali wao kazi yao ni kusimamia miradi, consultant na mkandarasi wanapewa tender.

Au unata kuendekeza mambo ya force account ambayo yamesababisha miradi mingi kujengwa chini ya kiwango?

Kwrli Watanzania wengi ni wajinga.
 
Suala La Maji Ni Muhimu Ila Iwapo Watawaacha Washauri Wataalam WaNdani
Na Kukimbilia KwaHao Wa Ughaibuni Ambako Watatozwa PesaTele Na Huenda Kazi Ikawa Hewa. Wao Wanafanya Kazi Ya Kuwasumbua Watanzania Wenye Visima Vidogo Kwenye Nyumba Eti Ndiyo Wanakwenda Kutoza Kodi Halafu Wanawapa Wageni
 
Ndugu

yangu, uzoefu ktk nchi kama Tz unaonyesha kazi za serikali, kama zile za 'force account' value for money, mwisho wa siku, in terms of ' quality' product of works yake imekuwa tatizo kubwa, sababu msimamizi anakuwa yuleyule contractor anayejenga, hivyo mwishowe kazi inakuwa chini ya viwango, na muda mfupi baadae, matokeo yake serikali kuingia gharama tena kwa walipa Kodi........ndo maana wanajaribu Sasa kurudi kwenye mfumo wa kawaida kuepuka changamoto kama hizi, zilizotokea kwenye miradi ya 'force account'...
Sijaongelea force account mkuu.
 
Ushamba ni mzigo wa kuni. Wakati mwingine muwe mnaficha ujinga wenu.
Unaposema wataalamu wa ndani una maanisha nini? Kwani hao ma consultant si watanzania?

Wafanyakazi wa serikali wao kazi yao ni kusimamia miradi, consultant na mkandarasi wanapewa tender.

Au unata kuendekeza mambo ya force account ambayo yamesababisha miradi mingi kujengwa chini ya kiwango?

Kwrli Watanzania wengi ni wajinga.

Hujaelewa hata nilichoandika. Kwanza nani kaongelea mambo ya force account?

Nnaposema wataalam wa ndani naongelea watumishi wa serikali yaani mainjinia.

Sasa unaposema "watumishi wa serikali kazi yao ni kusimamia" katika hii mikataba hata hilo jukumu kapewa consultant?

Swali la msingi ni hili ...

Mitlradi ya maji imekua ikisanifiwa na watumishi wa serikali miaka nenda rudi na inafanya kazi bila shida, sasa kwanini sasa hivi ulipe makampuni wafanye hiyo kazi kwa mabilioni ya pesa wakati inawezekana kutumia mainjinia wa serikali kufanya kazi hiyo hiyo kwa gharama ndogo na matokea yakaonekana?

Umeelewa??
 
Mkuu embu acha utani basi, hizo protocal unazisemea ni zipi kiasi kwamba hakuna injinia serikali anayezijua?

Au ataka kutuaminisha huko serikalini hakuna professional engineers kiasi kwamba tutumie mabilioni ya pesa kuweka makampuni?

Je unajua miradi ya maji amekua aki design nani kama sio hao professional engineers walioko serikalini?

Je unajua ni miradi mingapi iliyo sanifiwa na hayo makambuni (kabla ya mikataba yao kuvunjwa) ilifeli na mingine mpaka leo haitoi maji?

Swali la msingi ni kwanini utumie mabilioni ya besa kulipa kampuni ifanye kazi ambayo ingefanywa na imekua ikifanywa na mainjinia wa ndani kwa gharama ndogo?
Una uwezo mdogo sana wa kufikiria, anyway wazee wa legacy ndivyo mlivyo
 
Miradi wanayotaka kupewa ni ya Ukubwa gani mkuu?
Kama ni ile kijiji kimoja, au kata moja Hiyo ifanywe tu na maengineer wa mamlaka.
Ila Miradi mikubwa ni muhimu kushauriana kuondoa errors.

Miradi ni hii midogo ya vijiji viwili vitatu. Hata hiyo mikubwa mbona imefanywa na mainjinia wa serikali kwa miaka nenda rudi? Why now?

Mbaya zaidi hata kamradi kadogo wanapewa na wanatakiwa kulipwa mabilioni ya pesa kukasanifu kazi ambayo hata mwanafunzi aliyemaliza chuo anaweza fanya tena gharama ndogo kabisa!
 
Back
Top Bottom