MKWEAMINAZI
JF-Expert Member
- May 28, 2023
- 930
- 1,299
Hakika inaogopesha na kusikitisha sana kuona jinsi fedha za umma ambazo ni kodi za masikini wananchi wanazolipa kwa kukamuliwa na fedha za mikopo tunazokopa toka nje zinavyoliwa na wajanja watendaji wa umma.
Tumemshuhudia Mh. Waziri Mkuu Mzee Majaliwa katika ziara zake akipambana na ufisadi mkubwa unaofanywa katika halmashauri zetu, ufisadi ambao inaonekana unaanzia Hazina unakuja TAMISEMI kisha halmashauri. Hazina wanatuma fedha zisizo na maelezo kwenda halmashauri kupitia TAMISEMI ambao nao hawaulizi hazina kwanini hizi fedha hazina maelezo!
Ushauri kwa serikali
1. Huu mtandao ni mkubwa wahusika wamejipanga mtandao unawahusu Hazina, TAMISEMI na Halmashauri zote.
2. Ajira za kuteua ma-DED na ma-DAS kutoka UVCCM zinachangia sana Halmashauri kushindwa kusimamia fedha na miradi mbalimbali ajira zitangazwe watumishi waliopo popote na wananchi wengine waombe ili kupata watendaji wenye sifa na uwezo wa kusimamia fedha na miradi tukiendelea kuteuana kiitikadi huu upigaji hautakoma.
Vile vile tunauliza ni hatua gani zimekwishachukuliwa kwa waliotajwa katika report ya CAG au sio lazima?