kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 12,310
- 12,607
Nimekuwa nikipata maelezo meengi kuhusiana na hizi bidhaa za GNLD na Forever living Products (FLP). Hasa za forever, jamaa wako mahiri sana katika kuelezea faida utakazo zipata pindi utakapo jiunga na wanayoiita network marketing. Huwa wanafocus zaidi kwenye faida mtu atakayoipata once anajiunga na business.
Hawaongei sana kuhusu bidhaa zenyewe. Mimi kidogo ni mshamba kwenye hizo bidhaa/suppliments. Napenda kurusha mjadala huu niweze kupata mawazo yakinifu hasa katika utumiaji wa hizo bidha, pia biashara yenyewe kama kweli inalipa na mwisho nataka kujua kama kuna ukweli watu wana oanisha this business na ushetani.
Swali, kuna haja sana sisi watu wa kijijini kutumia hizi bidha wakati tunazo fresh mboga, matunda etc ambazo zingeweza kutusaidia tu bila ya hizi bidhaa?
Wanaongelea Alo Vera! What is the big deal na huo mmea? Mbona tunao hapa lakini sijawahi kuona mtu hata akisema autumie kama mboga?
Au ni kiini macho cha wenzetu walioendelea kutukandamiza kiuchumi kama kawaida wanatudanganya eti zitatusaidia kuondoa magonjwa etc etc?
Wakuu naomba niwakilishe ili nipate maoni toka kwenu!
Hizi bidhaa ni ghali sana, kuzitumia ni kuchochea rushwa, ukwepaji kodi na uhalifu mwingine kwenye jamii ili wamudu kuzinunua. Tuwahimize watu wetu wale vyakula fresh na kupiga marufuku kula kwa wingi mafuta, nyama, chumvi, canned foods, juice, nafaka zilizokobolewa, n.k.