Orodha ya biashara za kujifunzia biashara

andoza

JF-Expert Member
Nov 26, 2018
2,184
2,000
Habari,

Wengi wameenda Business school, wamesoma uchumi, wamesoma marketing na wengine wamefanya mpaka PhD katika maeneo ya biashara lakini bado wanapokuja katika real life situation wanajikuta wakikwama katika biashara nakujikuta wakikata tamaa. Ni ukweli usiopingika kwamba ili uweze kufanya biashara lazima uwe na elimu, ujuzi na uzoefu wa kutosha katika biashara. Lazima uwe na mtandao wa kutosha kwa ajiili ya biashara yako.

Hapa chini ninaelezea aina ya biashara ambazo mtu anaweza kuzifanya kwa kutumia mtaji mdogo kwa ajili ya kujifunza ambapo anaweza kupata uzoefu wa namna kufanya biashara na jinsi yakushughulikia changamoto tofauti. Unaweza kuchagua aina ya biashara kulingana na malengo yako kibiashara. Nimeziweka hapa biashara hizi katika makundi matatu:

  1. Biashara ndogondogo za uchuuzi kama vile, Genge, Duka dogo la rejareja, Biashara ya kutengeneza bidhaa ndogo ndogo kama karanga, sabuni, ubuyu, icecream, mkate, mama ntilie, kuchoma chipsi, kuuza kahawa etc
  2. Biashara za Network Marketing kama vile, AIM, GNLD, FOREVER LIVING etc
  3. BIASHARA ZA MTANDAONI KAMA VILE, DROPSHIPING FREE LANCING, AFFILIATE AND WHITE LABEL RESELLERS
Nimesema hizi ni biashara ambazo mtu unaweza kufanya kujifunzia kwa sababu kuu mbili: Kwanza, ni biashara ambazo mtu yoyote anaweza kuzianza wakati wowote kwa kutumia kiwango kidogo sana cha mtaji.Pili hizi ni biashara ambazo mtu anaweza kuziacha wakati wowote akipata fursa nyingine,akiona hazilipi au hazimudu.

Vile vile biashara hizi hazina complex regulation wala hazihitaji watu wengi kwani unaweza kuanza peke yako na taratibu ukakua kulingana namahitaji.

Kwa kusema hivi simaanishi kwamba hizi biashara sio serious business, hapana. Ni serious business na wako watu wanaishi maisha mazuri kwa kufanya aina hizi za biashara na maisha yanaenda vizuri tu. Kwa hivo basi iwapo utainigia katika biashara hizi kwa lengo la kujifunza na kisha ukaona zinaenda vizuri si vibaya ukaendelea kuifanya na kuweka maisha yako vizuri.

Biashara hizi zote unaweza kuzianza kwa mtaji ulio chini ya TZS milioni moja na laki 5 na hicho ndio kigezo kikubwa nilichokitumia katika kuzichagua. Vile vile biashara hizi zinakupa fursa ya kufahamu mambo ya ndani ya uendeshaji wa biashara kama vile, negotiation, kutafuta location, pricing, customer servcice, hiring, firing, marketing, customer support, change management na mengine mengi ni aina ya biashara ambazo mtu yeyote mabaye anafikiri kupata darasa zaidi kuhusu biashara na ujasiriamali.

Kumbuka kufanikiwa kwa mjasiriamali kunategemea uwezo wake wa kuzitambua changamoto na fursa zilizopo na uwezo wake wa kuzitatua changamoto hizo na kutumia fursa zilizopo.

Katika Biashara za kundi la kwanza ni kwa wale ambao wanafikira kuanzisha biashara ambazo ni local kwani hizi ni aina ya biashara mabzo zinakuwezesha kudeal na watu wa aina tofauti kulingana na mazingira uliyopo. Hivo basi mtu anayefikiria kufanya Biashara kubwa lakini ambazo ni local na sio international anaweza kupata uzoefu mkubwa wa local business katika biashara hzi kwani atafahamu mambo kama vile income level, life style za watu, tamaduni za watu and much more.

Nasisitiza sana kwamba iwapo katika kipindi chako cha amafunzo utagundua kwamba biashara imekukubali hakuna ubaya kama utaendelea nayo kwani cha muhimu ni mafanikio Ili kuhitimu katika eneo hilo unaweza kufanya biashara hii kwa kipindi cha miezi 6 hadi mwaka na iwpo utafanya kwa umakini uzoefu utakaopata katika usimamzi wa biashara ndogo locally ni mkubwa na wa kipekee kuliko ambao ungepata darasani aktika kipindi hicho hicho.

Katika biashara za kundi la pili ni kwa wale ambao wanalenga zaidi big local corporation ambazo zinafanya kazi katika maeneo tofauti na ambazo zinawezakuwa na branches, kuhitaji clear strategy na ambazo zinahitaji continuous innovation.Kaktika kufanya biashara ya network marketing utapata uzoefu katika maeneo hayo na itakujengea uwezo wa kuandaa na kufanya sales pitch, kufanya presentation, kusoma na kuelewa na products na matumizi na faida zake, kujenga brand, both personal and corporate, etc.

Uzoiefu utakaopata utakuwezesha kuendesha a somehow large business with complex operations. Itakuwezesha kufikiri big picture ya biashara, kuset goals na kufanya kazi ya kuzifikia .Kama lengo lako ni kuanzisha biashara kubwa yenye mrengo wa kitaifa basi unaweza pata Darasa zaidi ukifanya Network marketing kwa lengo la kujifunza. Kumbuka Network marketing ikikukubali na kuanza kukupa faida unaweza endelea kuifanya bila shida ila ili darasa likae vizuri inabidi ujipe angalau miezi 18+ hii itakusaidia kupata intensive understanding of the business.

Katika Biashara za kundi la tatu ni wale ambao wanalenga kuwa change makers, innovators, na hata kufikia ngazi ya kimataifa. Hawa ni wale ambao wanafikira kufanya cross border trades, kudeal na international clients, kuleta international solution to local environment, kujenga strong brands na hata kuwa mabilionea.

Sisemi kwamba katika makundi mawili ya kwanza hawawezi kutoka mabilionea, hapana. Ninachosema hapa ni kwamba unachojifunza katika aina hii ya biashara ni skills na knowledge ambazo mabilionea wanazitumia kila siku katika kuendesha biashra zao.Mifumo ya Mawasiliano,Taarifa,takwimu,real time data, etc.

Ni aina ya biashara ambazo zinakutaka utumie teknolojia, utumia data kufanya maamuzi uwe flexible, unaweza kudeal na watu wa kimataifa na kujikuta ukijifunza baadhi ya mambo ambayo kama usingefanya aina hio ya biashara usingekutana nayo mfano, jinsi ya kutuma na kupokea pesa nje ya nchi, jinsi exchange rate zinavofanya kazi, jinsi exchange rate zinavoathiri biashara, jinsi ya Kuimport bidhaa, jinsi ya kuexport bidhaa, jinsi ya kutumia teknolojia na mifumo mbalimbali, jinsi mifumo ya benki na biashara zakimataifa inavyofanya kazi.

Kwa ufupi aina ya biashara ambayo unachagua kujifunzia inategemea na malengo yako, mtaji wako, kiwango cha elimu na uzoefu pamoja na ujasiri wako.

Jambo la muhimu ni kufahamu kwamba katika biashara zote hizo ukiona zinakulioa vizuri sio vibaya ukaendelea kupambana nazo kama biashara zako ila cha muhimu ni kupata uzoefu na utaalamu zaidi ambao utakusaidia katika kufanya biashara ya ndoto yako.


Kila la Heri
 

Chuku chuku

JF-Expert Member
Mar 11, 2015
741
1,000
Mi nimekuelewa sana bro,na nimeona nia njema ya kumsaidia yule ambaye hana kabisa mentality ya kufanya biashara, mi by profession ni muhasibu katika kampuni kubwa tu hapa nchini ila katika ukuaji wangu sikuwahi kufanya biashara yeyote, kwa kujaribu kujifunza kujitegemea huwezi amini nilianza small scale ya kupanda matango uwani kwangu na nikawa nauza kwa wenye magenge sokoni kama ilivyo kwenye kundi la kwanza la post yako.

Pili nimeingia kwenye kundi la pili ili nataka lisapoti kundi la tatu ninalofanya sasa hivi la foreign exchange market, kwa kweli watanzania wengi bado tunayumba sana linapokuja swala la kujitegemea kiuchumi ukiacha kuajiriwa sababu mazingira yametujenga hivyo, unakuta mtu ana hadi masters ya kitu fulani lakini anashindwa kujimarket kuingiza hela anasubiria ajira, mi nakushukuru sana katika hili umeniongezea kitu.
 

andoza

JF-Expert Member
Nov 26, 2018
2,184
2,000
Niliitwa kwenye hizo mishe zenu..jv maisha haya nan anataka kupewa virutibisho jamani!hv virutubisho mbon tunavikuta kwenye matunda na mboga??khaa!mtuache jaman
Naelewa unakotokea,nisisitize zaidi ninaposema ni biashara za kujifunza.Netowrk marketing ziko za aina nyingi sana.Lengo langu si kuhamasisha ila kama ukijishughulisha kikamilifu katika kufanya networking hata kama hutauza uwezo utakaoupata ikiwamo handling rejection,failure,loss pamoja na uzoefu wa kutafuta wateja, kuwaleza kuhusu bidhaa na mfumo wa biashara,kuwashawishi kwa kutumia data na motivational quotes kutakuanda katika kujenga misingi ya biashata ya ndoto yako.Tulia utafakari kwa kina
 

Wangari Maathai

JF-Expert Member
Aug 13, 2018
35,078
2,000
andoza,Nadhani kama huna lugha ya ushawishi ni bora ukasoma sana vitabu au makala za biashara! Mie nimehudhuria sana mikutano ua GNLD, FOREVER, na hii iliyopo benjamin tower mezanine floor nimeisahau jina...Wala sijaona jipya kwakwel!zaidi ya tambo za uzushi!hata hvyo tumetofautiana!wengine tumeumbwa tayari na hizo sifa!
 

andoza

JF-Expert Member
Nov 26, 2018
2,184
2,000
Nadhani km huna lugha ya ushawishi ni bora ukasoma sana vitabu au makala za biashara! Mie nimehudhuria sana mikutano ua GNLD, FOREVER, na hii iliyopo benjamin tower mezanine floor nimeisahau jina...wala sijaona jipya kwakwel!zaidi ya tambo za uzushi!hata hvyo tumetofautiana!wengine tumeumbwa tayari na hizo sifa!
Ila mikutano sio unakuwa unaudhuria tuuu,unatakiwa uandae ya kwako na wewe uende ukaweke tambo zako.Ndivyo kila mtu anavyofanya ukihudhuria tu lazima utapike kwa sababu wengine bado fix ni nyingi.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom