Utumiaji wa GNLD na Forever Living products ni hatari? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Utumiaji wa GNLD na Forever Living products ni hatari?

Discussion in 'JF Doctor' started by Shapu, Dec 17, 2008.

 1. Shapu

  Shapu JF-Expert Member

  #1
  Dec 17, 2008
  Joined: Jan 17, 2008
  Messages: 1,920
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Nimekuwa nikipata maelezo meengi kuhusiana na hizi bidhaa za GNLD na Forever living Products (FLP). Hasa za forever, jamaa wako mahiri sana katika kuelezea faida utakazo zipata pindi utakapo jiunga na wanayoiita network marketing. Huwa wanafocus zaidi kwenye faida mtu atakayoipata once anajiunga na business.

  Hawaongei sana kuhusu bidhaa zenyewe. Mimi kidogo ni mshamba kwenye hizo bidhaa/suppliments. Napenda kurusha mjadala huu niweze kupata mawazo yakinifu hasa katika utumiaji wa hizo bidha, pia biashara yenyewe kama kweli inalipa na mwisho nataka kujua kama kuna ukweli watu wana oanisha this business na ushetani.

  Swali, kuna haja sana sisi watu wa kijijini kutumia hizi bidha wakati tunazo fresh mboga, matunda etc ambazo zingeweza kutusaidia tu bila ya hizi bidhaa?

  Wanaongelea Alo Vera! What is the big deal na huo mmea? Mbona tunao hapa lakini sijawahi kuona mtu hata akisema autumie kama mboga?

  Au ni kiini macho cha wenzetu walioendelea kutukandamiza kiuchumi kama kawaida wanatudanganya eti zitatusaidia kuondoa magonjwa etc etc?

  Wakuu naomba niwakilishe ili nipate maoni toka kwenu!
   
 2. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #2
  Dec 17, 2008
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Mimi baba yangu yupo hapa Dar na an miaka 85 hatumii GNLD wala nini....piga zoezi kula matunda na vyakula fresh tu ndugu yangu!

  Sina uzoefu na GNLD ila naona kama wako kibiashara zaidi
   
 3. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #3
  Dec 17, 2008
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,594
  Likes Received: 18,589
  Trophy Points: 280
  Suplements ni virutubisho ziada. Sio siri kama unapata mlo kamili, unajitosheleza kabisa hivyo huhitaji hivyo virutubisho ziada. Ili kupata mlo kamili, ni kupota chakula chenye viini lishe vinavyohitajika kwa ajili ya aina ya mwili wako na shughuli unaifanya na mwili huo.

  Mwili ukishafyonza viini lishe vya kutosha, unaweza kufyonza na ziada kidogo halafu kila vilivyosalia vinageuzwa makapi na kutolewa nje kwa njia kuu 4 za kawaida ambazo ni kutoa hewa,jasho na haja K na haja N.

  Chakula bora sio lazima kiwe ni chakula kingi wala huna haja ya kushiba kuvimbisha tumbo kwani sehemu ya mahitaji halisi ni ndogo tuu na nyingine yote ni ziada na makapi.

  Kila mtu ana mwili wa aina yake wenye mahitaji na viango vyake vya virutubisho. Kama una mwili mkubwa mahitaji ni makubwa kuliko mwili mdogo. Kuna watu wana miili ya kunenepa mahitaji yao ni tofauti na vimbau mbau, siku hizi kwa madada zetu vimbambau ni dili. Unene au wembamba sio viwango vya afya, kuna wanene wenye afya mbaya mpaka unene ugonjwa. Na kuna wemba ni fiti kama chuma cha nondo. Mahitaji ya virutubisho pia vitategemeana na shughuli zako. Kama ni mbeba zege/box sio sawa na washika kamu. Nk.

  Baadhi ya hivi virutubisho vya GNLD na Forever ni kama mbolea. Mwili ukipata virutubisho hivi huwa na afya bora, utapendeza, utang'aa na kuwaka. Kwa kifupi utaelezewa kuwa unakula kuku kwa mrija. Walio na miili isiyo na shukrani, utaambiwa una sura ya njaa njaa tuu.

  Kuku wa kizungu ndio wenye kuhitaji hivyo virutubisho zaidi. Kuku wa kienyeji hahitaji virutubisho na bado ana afya njema.

  Kama kawaida ya mmea uliozoea mbolea ukikosa mbolea unasinyaa na kudorora na ndivyo yatawakuta hawa watumiaji wa haya madawa. Lazima uyatumie siku zako zote za maisha yako.

  Ushetani wa matumizi yake ni utumwa wa kuchangamkia pesa. Hata ukipenda sana movies, unakuwa mtumwa wa movies ama wapenda game wanajikuta wanaabudu gemu kuliko chochote, Mungu anawekwa kando. Kitu chochote kinachomuweka Mungu kando ni kazi ya shetani.
   
 4. M

  Mama JF-Expert Member

  #4
  Dec 17, 2008
  Joined: Mar 24, 2008
  Messages: 2,858
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0
  Hizi supplements ni nzuri kwa wanaohitaji kama vile wagonjwa, kina mama wajawazito na wanyonyeshao na pia wazee. Zitumiwe pale inapolazimu tu.

  Kumbuka kila kitu kikizidi mwilini kila madhara. Na hizi supplements mara nyingi ni vitamins na essential metals ambazo huwa hazina mahitaji makubwa sana kwa mtu wa mwenye afya. Zinaweza kupatikana kwa lishe tu isipokuwa kwa makundi yaliyotajwa hapo juu.

  Epuka kuwapa watoto.
   
 5. M

  Mwanjelwa JF-Expert Member

  #5
  Dec 17, 2008
  Joined: Jul 29, 2007
  Messages: 961
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Wakina nani hawa?
   
 6. Nyikanavome

  Nyikanavome JF-Expert Member

  #6
  Dec 20, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 448
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  Pengine inaweza kuwa unfair kuongelea bidhaa za makampuni hayo zote kwa ujumla na kusema ni hatari; nafahamu makampuni hayo yana bidhaa mbalimbali za kula ambazo nyingi zina supply micronutrients mwilini and nyingine wanaclaim kuwa zina therapeutic effect kwa magonjwa mbalimbali.

  Pia wana bidhaa ambazo sio za kula. Kinachofanya uhatari uwepo ni jinzi wavyo zisambaza bidhaa zao na kuwashawishi watu wazitumie kwa vishawishi vya kupata utajiri na afya bila kuwapa ushauri wa kutosha wa kitaalamu wa kwa wateja wao.

  Ninavyo fahamu mie, ulaji wetu wa kitanzania unaweza usiweze kutupatia wengi wetu kiwango cha kutosha cha vitamini na madini nakupelekea kitu kinachoitwa hidden hunger (njaa iliyojificha). Katika hali ya kawada mtu anaweza kuishi akiwa na kiwango cha chini cha vitamini na madini mbali mbali bila kujitambua. Unaweza kutambua kuwa hupati micronutrients za kutosha kwa kupitia ulaji wako a kilasiku kama unakidhi haja na pia unaweza kuwasiliana na mtaalamu wa chakula na lishe aliyeko karibu nawe.

  Mimi
   
 7. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #7
  Dec 20, 2008
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,594
  Likes Received: 18,589
  Trophy Points: 280
  Wabeba zege ama wabeba box ni watumiaji wa more mascular job, manual laboures ambao wanatumia nguvu nyingi na akili kidogo wanamahitaji yao ya viini lishe tofauti na washika kalamu, wafanyakazi maofisini, watumia compyuta ambao wanatumia akili zaidi na nguvu kidogo nao wana mahitaji yao.
   
 8. MwalimuZawadi

  MwalimuZawadi JF-Expert Member

  #8
  Dec 21, 2008
  Joined: Sep 1, 2007
  Messages: 643
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Wajinga ndio wali-wao...werevu pilau-lao!
   
 9. Shapu

  Shapu JF-Expert Member

  #9
  Apr 17, 2009
  Joined: Jan 17, 2008
  Messages: 1,920
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Naomba ufafanuzi hapo.
   
 10. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #10
  Apr 17, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Si mtumiaji wa bidhaa hizo japo nimeshazisikia sana, na hata kuletewa DVD inayoelezea kwa undani products hizo....two me ukiacha kuwa products hizo zina supplements....GNLD na FLP hazinatofauti na DECI or any Pyramid Scheme...so be careful!

  Mimi babu yangu (kafariki 1999..RIP akiwa na miaka 120), alikuwa mganga wa kienyeji, mpaka anakufa ktk maisha yake hakuwahi kutumia hata panadol au modern medicine yoyote ile...mojawapo ya mmea aliokuwa anatumia kutengeneza dawa zake ni huu wa Alo vera aka Litembatemba.....so 2 me hao FLP hawajaleta kitu kipya hapa!

  Hili nakubaliana na wewe...soma hapo juu zaidi!
   
 11. Makonyagi

  Makonyagi Member

  #11
  Apr 17, 2009
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 40
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wizara ya Afya hawajatoa tamko
  Mamlaka ya dawa na vyakula wanahangaika na metakeflin wanasahau hii piramidi scheme kwenye sekta ya afya.
  Nashangaa ktk maelezo yoooote ya hizi tianshi sijui forevago and whateva hakuna side effects.
  Hic!
  Kula kilaji pata afya
   
 12. Makonyagi

  Makonyagi Member

  #12
  Apr 17, 2009
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 40
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Utakuta mpaka maprofesa wamo humo.
  na wachungaji wakisindikizwa na maaskofu wanawahimiza waumini kuingia ktk hizi scheme za madawa ambayo hayajaruhusiwa
   
 13. LazyDog

  LazyDog JF-Expert Member

  #13
  Apr 17, 2009
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 2,478
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135  Mamlaka ya chakula na dawa ungetaka wafanye nini?
  Tizama hii orodha,
  Orodha ya vipodozi vinavyotambuliwa na mamlaka ya chakula na dawa


  Kuna pyramid schemes za aina nyingi, and not all are illegal. Some are illegal only in some countries.
   
 14. REX

  REX JF-Expert Member

  #14
  Apr 30, 2012
  Joined: Mar 24, 2012
  Messages: 330
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Baada ya kusoma kichwa cha habari nimeogopa sana na kujiuliza kulikon?

  Kwa wasiofaham TFDA wamezipisha bidhaa za forever baada ya tafiti zao kukamilika na shirika la sayans ya aloe vera la dunia limethibitisha uhalari wa bidhaa hizo kwa matumiz ya binadam.
   
 15. m

  manasa Member

  #15
  May 1, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 88
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  4 sure wajinga ndo waliwao
   
 16. b

  bebiwilli Member

  #16
  May 5, 2012
  Joined: Mar 4, 2011
  Messages: 70
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sina imani na hizo dawa,nilishawahi kumnunulia mdogo wangu dawa ya meno ya forever kwa ajili ya shule,alianza kuumwa na ganzi ya meno 2lipompeleka hosp doct alimwambia aache kuitumia na tatizo likaisha.ingiwa cjajua kwa hizo dawa zingine
   
 17. a

  amigooo Senior Member

  #17
  Jul 14, 2012
  Joined: Jun 30, 2012
  Messages: 118
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Walo wengi hawajui ila wanaanza kuponda kabla hawafanya chochote kutaka kujua jambo. Hao ndo Wabongo walivyo
   
 18. Lilian Masilago

  Lilian Masilago Verified User

  #18
  Jul 14, 2012
  Joined: Jul 5, 2012
  Messages: 246
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sina imani na hizi dawa. Wapo kibiashara zaidi na sio huduma kwa jamii
   
 19. Bumpkin Billionare

  Bumpkin Billionare JF-Expert Member

  #19
  Jul 15, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 1,336
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Si kwamba hizi ni DAWA. Ni Supplements wakuu. Dawa ni kwa ajili ya mtu anayeumwa ln supplements ni kwa yeyote especially in busy life.

  Kuna mtu amesema wetu karoti ni nyingi. Yes, that is true, lkn that is not the issue. Yawezekana karoti ni nyingi sokoni, ln je unaweza kufaidika nazo kwa kuziona zikiwa zimepangwa kwenye stalls?

  Shida yetu ni premature conclusions. Supplements wandugu ni kwa ajili ya wote wasioweza kwa sababu moja au nyingine kupata balanced diet. Na si hivyo tu, yawezekana hata muda wa kula ndio ukawa tatizo kwani chakula hakikufuati, sasa ukipiga hesabu muda wa kukifuata na kula, wengi tunaamua kukacha.

  Kama haitoshi, si kila tunachokula hufyonzwa kwa namna inayotakiwa. FLP wana kitu inaitwa ABSORBENT C. Hii inaasaidia ufyonzwaji wa virutubisho. Upo uwezekano unakula balanced diet, lkn haifyonzwi, then what? Wastage.

  Kuhusu biashara, hii sio pyramid. Humpi mtu fedha zako zaidi ya wewe kumnunulia mtu kwa bidhaa kwa fedha zake mwenyewe na wewe kupata kamisheni fulani, au umtambulisha kwenye network na wewe kupata % fulani katika kila manunuzi ambayo mtu huyo atafanya na wote aliowatambulisha mtambulishwaji wako nao watakupatia faida wewe.

  By the way, ukiwa unasumbuliwa na huu ugonjwa mnaoupata kwa kula nyama za mbuzi (Gout) usisite kuni-PM.

  Najua utakuwa umeshaenda sana hospitali kutibiwa bila mafanikio. Bacteria wameshakwangua urojo wote kwenye joints za mguu na wanachokifanya hospitali ni kukupa dawa ya kuua hao bacteria lkn jeuri ya kurudisha ile rojo mguu hawanayo.

  Basi hii iwe habari njema kwako, na kwa ambao walifanyiwa operation na ule urojo uliotolewa kwenye uti wa mgongo nao umekuwa issue, basi jiteteeni na maumivu ya mifupa inayosuguana.

  Kwa wale wenye unene ulioshindikana, msijitafutie vidonda vya tumbo kwa kushinda na njaa. Life Style 30 ni dozi ya calories kwa siku 30 plus mazoezi mepesi na ndani ya miezi mitatu, kilo 9+ zitakuwa off you.

  Kama UPARA unakuaibisha, basi jua tangu sasa kuwa nywele zaweza kuota. (Hata Wayne Rooney katumia) Hizo hizo karoti mnazosema kwenu zipo nyingi plus some bee products unaretain nywele. Betta Carotene na Forever Bathe Gel lee ndio suluhisho.

  ANTI AGING: Yes, unaweza kurudia ujana kwa mwili wenye afya na ngozi nadhifu. Just some pinches of Royal Jelly utaretain ujana wako. Ni kama kulala ndani ya maparachichi kwa afya
   
 20. nyumba kubwa

  nyumba kubwa JF-Expert Member

  #20
  Jul 15, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 10,280
  Likes Received: 1,720
  Trophy Points: 280
  Mimi sijawahi tumia virutubisho ila niliwahi jaribu vipodozi vyao.. nikaona ni wizi mtupu.

  Kuhusu kama ni biashara inayolipa au la... marafiki zangu waliojiunga kuuza hizo bidhaa wote walichemsha baaba ya muda.

  Sasa sijuhi hawakuwa serious au ndio mambo ya upatu wanaofaidi ni waliowahi. Na inataka moyo maana mtu mzima inabidi ugeuke machinga kusumbua watu wakuungishe maofisini.
   
Loading...