Utumbuaji: Tuache Siasa Kwenye Professionalism, Sio Kila Mtumbuliwa ni Jipu!

Brother hapa umenena point ya msingi sana ambayo huwa mara nyingi baada ya maamuzi ya Ikulu huwa ninajiuliza sana, inakuwaje michakato ya kiutendaji imo ndani ya kanuni,sera au scheme of work na watendaji wanaanza mchakato hatua kwa hatua wakati mwingine kwa taarifa na matangazo ya kusudio la utekelezaji wa jambo fulani hatua zote hizi Ikulu inakaa kimya tu mfano suala la sherehe za siku ya ukimwi duniani (kitaifa),sherehe za kuzima mwenge nk matukio yote haya yalikuwa ndani ya kalenda ya utendaji ya serkali lakini maandalizi yalifanywa watu wakatumiwa mialiko na siku moja kabla ya utekelezji ikulu inatoa tamko la kusitisha na hata kuwataka waalikwa wengine kurejesha fedha za ushiriki nk tena katika language inayowaonyesha kama wamezipata fedha hizo kwa hila.Zoezi la kupandisha bei ya umeme hupitia hatua kadhaa ambazo huhusisha mamlaka husika ikiwemo EWURA kutangaza hadharani kusudio la kufanya hivyo haya yote yalizingatiwa na Ikulu ikawa kimya kwa ninI wasingewazuia?zaidi ya yote kwanini Ikulu isitoe MWONGOZO nini inataka na nini hakitakiwi ili watendaji wa serikali nk wajue wazi kuwa yako mambo yakiutendaji ambayo yalikuwa halali (TRADITIONAL) katika serikali zilizopita ila sasa hayatakiwi tena.
 
Acha porojo hii nchi ina watu wengi wasomi watapewa kazi, yeyote atakae leta mazoea lazima aondoke
 
Ninyi hata siwaelewagi....hivi akili zenu zipo wapi...Rais akifanyaga kitu mnakuja humu kua kila kitu anafanya yeye....leo mnakujasema tena alikua wapi...
 
Muhongo kashasema yeye na wizara yake hawakuhusishwa kwa hilo, alafu nyie jamaa mnasema walikuwa wanataarifa before, mbaya zaidi mnaenda mbali zaidi eti na ikulu walikuwa wanataarifa!! Jaribuni kuwa mnaelewa japo kidogo basi.
 

Huu ndiyo ukweli tena ukweli mtupu na huu mwaka nakuombea uwe mzuri sana kwako.
 
Voted as the Best Comment of this Week
 

Nimefurahi sana kumjua moja ya watu wanaovujisha siri za serikali ni mtukufu mwenyewe kwa kuwa "Pascal Mayala" katuthibitishia kuwa mtumbuaji mwenyewe kathibitisha kuea atatumbua hii inatupa mwanga kuwa kumbe hakuna haja ya kuhangaika kushughulika na watu wanaovujisha siri za serikali wakati raisi mwenyewe anaona ni sawa tu kutoa siri zake kwa waandishi

Hakika huu ni udhaifu mkubwa sana kwa mtukufu maana kile kiluchosemwa kama tetesi sasa ni true story kwa 50%
 
Pascal Najua kampuni yako ya ppr ni moja wa wanufaika na menejiment ya mramba. Kwahiyo unatetea maslahi yako. Mbona walipotenguliwa Akina Hosea hakutoa malalamiko Au Mramba Ndiyo professional peke yake?
 
Muhongo kashasema yeye na wizara yake hawakuhusishwa kwa hilo, alafu nyie jamaa mnasema walikuwa wanataarifa before, mbaya zaidi mnaenda mbali zaidi eti na ikulu walikuwa wanataarifa!! Jaribuni kuwa mnaelewa japo kidogo basi.
Sawa mbona walikuwa kimya siku zote?Huku kuviziana ili kupata sifa za kisiasa hakutatusaidi kitu.

Muda utaongea na matokeo mtayaona.
 
Hiyo mikataba haina influence ya wanasiasa?
Usihangaike na mpayukwaji huyo anaongea bora liende,siku shirika likifa hawa hawa wanaibuka na kulaumu.Tanesco yenyewe inabeba mzigo mkubwa sanaaa,ajitokeze Prof muhongo kutueleza gesi imefikia wapi ili tujue imeanza kutumika na tanesco na si kuleta siasa huku shirika likipata hasara zaid na zaid.WAACHE KUCHEZEA PROFESSIONAL sasa.
 
Tatizo la kudumu:mikataba ya umeme wa dharura ya kufua umeme,imekuwa siyo ya dharura,na imekuwa inaiuzia Tanesco umeme kwa bei ya juu.
Kwa nini Tanesco inunue umeme,badala ya kuzalisha umeme wake yenyewe?,
 
Umeuliza maswali magumu sana namsubiri @pasco mayalla aje na majibu kwa kila swali otherwise JPM alisema Mayalla kwa ki kwao ni Njaa
 
Huyu aliyetumbiliwa profession yake ni Electricall Engineer Kama sikosei, upangaji wa Bei unaweza kufanywa na expert Kama cost accountant au wachumi.
Pili kuna vitu obvious ambavyo wahusika wange weza kufanya kupunguza mzigo kwa walaji yaani customers .
Tatu vikwazo vikubwa kwa Shirika ni nini ?? Mfano mikataba inayo wa kwanza na juhudi ya kujitoa Huko ukoje?? Kwa kushirikiana na wizara husika kwa mikataba iliyo shinikizwa na Watu nje ya Shirika lenyewe iwe ya iptl , nk
Nne rates za umeme karibu dunia nzima Zipo politically motivated kutegemeana na sera ya nchi ni kuchochea uzalishaji Kama viwanda ni kwenye maeneo yenye kutoa ajira au matumizi ya umeme majumba ni .
Tano huwezi kupandishia bei ya umeme bila waziri husika kujua kwamba bei ya umeme uta ongezeko na hata waziri wa fedha kujua ili kuona impact yake ktk budget kuu ya nchi na effect yake kisiasa .
Haja ya Shirika la tanesco kufanyiwa tathmini na makampuni ya kitaalamu ili kuona Kama muundo wake na idadi ya staff unatija kwa taifa na kwa mlaji , hapo ndipo tunapoweza kuweka professionalism
 
What you imply to propose would mean spoon-feeding in the practice of management.
 
Pasco anajaribu kumtisha Rais!!!Hao ma professionals ndio wametufikisha hapa tulipo.
Maprofessionals wamewapa hata watu wa darasa la saba uwezo kuhoji elimu zao.
Mwacheni Rais afanye kazi yake kwa kadiri atakavyoona inafaa,kama mtu anajiona yeye ni mwantaaluma,na hawezi kufanya kazi serikalini aache kazi,wapo watu kibao wana shida ya hizo kazi tena ni wabobezi
 
Nmekuelewa coz nlichelewa sana kuelewa,tusipende kutetea vibovu wakati mwingine 7bu hata yai huoza japo linacover
 
Muhongo kashasema yeye na wizara yake hawakuhusishwa kwa hilo, alafu nyie jamaa mnasema walikuwa wanataarifa before, mbaya zaidi mnaenda mbali zaidi eti na ikulu walikuwa wanataarifa!! Jaribuni kuwa mnaelewa japo kidogo basi.
Mkuu Mkarimani, kupandisha bei ya umeme ni process ambayo inapitia hatua zifuatazo
1.Menejiment ya Tanesco inaomba kibali cha kupandisha gharama za umeme kwenye bodi ya Tenasco na kutoa sababu. Hiyo bodi ina serikali ndani yake, na ina ikulu ndani yake, M/Kiti ni mteule wa rais na anawajibika kwa waziri husika.
2. Bodi inapitia maombi, inajiridhisha, inatoa kibali cha kupeleka naombi Ewura, Waziri husika anajulishwa, ikulu inajulishwa.
3. Service provider ambaye ni Tanesco anatuma maombi ya ombi la kuongeza bei ya umeme kwa Ewura akiambatanisha sababu za msingi na mkokotoo wa gharama.
4. Ewura inapokea maombi, inaitisha kikao cha stakeholders kukusanya maoni yao na kufanya upembuzi yakinifu.
5. Ewura inafikia uamuzi inatangaza kusudio kw la kupandisha bei, inaitisha bodi ya Uwura kubariki ongezeko hilo. Ndani ya bodi ya Ewura, serikali imo na ikulu imo. Bodi inabariki uamuzi huo na kuipa Menejiment ya Ewura kutangaza huku waziri husika akihusishwa na ikulu ikitaarifiwa.
6. Ndipo Ewura wanatangaza Bei Mpya za Umeme.
Kwa mchakato huu, mtu akisema baadhi ya maamuzi ya taasisi za serikali ya Magufuli ni shaghala Baghala, tutakuwa tunawaonea? .

Kwa serikali ilijua kabla, ikulu ilijua kabla, kwa vile vyombo vyote hivyo vilipaswa kujua na kuzuia kabla ya kutangazwa ongezeko.

Kama ni kweli ikulu haikujua na serikali haikujua, hii ni gross negligence na wahusika sio Menejiment za Tanesco na Ewura.

Then wahusika ndio wawajibishwe!.

Paskali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…